Pages

KAPIPI TV

Tuesday, April 24, 2012

UKIUKWAJI WA SHERIA NDOGONDOGO NA MAPATO DUNI KWA HALMASHAURI


 Pamoja na kuwepo kwa sheria ndogondogo zinazotungwa na halmashauri katika maeneo mbalimbali ya mkoa wa Tabora lakini sheria hizo zimekuwa zikikiukwa mara kwa mara na kuzua hoja kwa baadhi ya watu mjini hapa.


Ingawa wapo baadhi ya watu wamefikia hata kulalamikia watendaji wa halmashauri kwa kuonesha kushindwa kusimamia sheria hizo au kwa upande mwingine wamefika mbali zaidi na kufikia hata hatua ya  kuwahusisha watendaji hao na vitendo vya kula rushwa kwa watu wanaodaiwa kukiuka sheria hizo.


Hapa upo mfano mdogo tu katika soko kuu la Tabora mjini ambapo lipo Tangazo la kupigwa marufuku kwa kuegesha magari ya mizigo eneo hilo lakini cha kushangaza magari yamekuwa ndio sehemu kubwa ya maegesho na kufanya eneo hilo kuwa na muonekano kama Gereji.


Inashangaza pia kuona marufuku ya kuegesha magari hapo eneo la Stendi ya zamani mjini Tabora,faini yake ni kiasi cha shilingi elfu hamsini,lakini je madereva wa magari hayo wameridhia kuendelea kutoa hizo faini?na kama wanatoa halmashauri inaendelea kuongeza pato lisilokuwa?au kuna wajanja wachache ambao wanafaidika na pato hilo?


Manispaa ambayo hadi sasa bado haijafikia hata robo ya makusanyo ya mapato yake kwa wakati huu inaelekea kumaliza mwaka wa fedha kwa hesabu za serikali,...kwakweli ni ajabu sana!!!!    

No comments: