ROZA MASANJA:
''JAMANI NAOMBA KAMA KUNA MTU AU WATU WANISAIDIE KUPATA CHEREHANI TU NIWEZE KUOKOA MAISHA YA WATOTO WANGU"
Ni Mwanamke ambaye bado anaishi katika kijiji cha Amani cha wazee wasiojiweza kilichopo Ipuli manispaa ya Tabora, baada ya wazazi wake kufariki ambao walikuwa wakilelewa katika kijiji hicho kutokana na kutokuwa na uwezo kufuatia ulemavu waliokuwa nao.
Roza amemaliza darasa la saba akiwa katika kambi hiyo ya kijiji cha Amani,kwakuwa hakukuwa na msaada wa kumwezesha kuendelea na masomo alikaa hivyo akiwasaidia wazazi wake kazi ndogo ndogo za nyumbani kwakuwa walikuwa hawajiwezi.
Mazingira magumu aliyokuwa nayo kwa wakati wote,Roza kama walivyo mabinti wengine kutokana na shida alizokuwa nazo akajikuta amerubuniwa na kubebeshwa ujauzito,hali iliyosababisha ugumu wa maisha kushika hatamu.
Mara baada ya kujifungua alipata wazo la kujifundisha ufundi wa kushona nguo,hiyo ikawa na ahueni kwake na mtoto aliyekuwa naye.
Kabla ya kujiweka sawa wazazi walifariki,na hapa sasa ndipo maisha yake yakachukua sura mpya na kuzidi kuwa magumu.
Muda wa kujifundisha na hata kufikia kuwa ni fundi wa kuaminika ukawa umewadia na akaanza kutafuta eneo la kufanyia kazi zake ingawa uongozi wa kijiji cha Amani ukamtaka aendelee kuishi hapo kutokana na ukweli kwamba aliishi vizuri na wazee wa kambi hiyo.
"Nilipata cherehani kwa mama mmoja akawa ananikodisha,nikawa nashona lakini baadaye aliiuza kutokana na matatizo aliyokuwa nayo,kwahiyo mimi nikalazimika kukaa tena bila kazi ndipo nikapata ujauzito wa mtoto huyu mwingine"alisema Roza
Aliongeza kuwa "Nimekuwa naishi kwa shida kubwa,nimefanya kazi za ndani kwenye majumba ya watu lakini watoto wanakaa muda mwingi peke yao,hali hii inanitia uchungu sana"
WANAUME ALIOZAA NAO WALIKUWA WANATUMIA FURSA ZA SHIDA ZAKE KUJISTAREHESHA
Amekiri kutorubuniwa tena kwa kuzalishwa kiholela....!!!

No comments:
Post a Comment