Rais Jakaya Kikwete akitoa heshima za mwisho kwa Marehemu Brigedia Jenerali Mstaafu
Adam
Mwakanjuki mapema asubuhi leo April 22, 2012 katika kambi ya JWTZ ya
Kikosi cha Anga kabla ya kupelekwa Zanzibar kwa mazishi.
PICHA NA IKULU
-----------------
Marehemu amewahi kushika nafasi mbalimbali za uongozi visiwani Zanzibar zikiwemo za Uwaziri katika Wizara mbalimbali na pia kuwahi kuwa Mjumbe wa Baraza la Wawakilishi.
"Pokea rambirambi zangu za dhati kwa kuondokewa na mzee wetu, kiongozi shupavu na mwanamapinduzi imara, ni pengo kubwa kwetu kwani Marehemu amekuwa mshauri wetu mkweli na muwazi, upendo na ucheshi wake pia ilikuwa faraja kwetu wakati wa vipindi vigumu na vyepesi" Rais ameeleza,
"Tutaukosa ushauri wake, upendo wake na mchango wake katika kila hali" Rais amesema na kumuomba Rais Dk. Ali Mohamed Shein kufikisha salamu zake za rambirambi kwa familia, wananchi wote na viongozi wenzake ambao marehemu amefanya nao kazi katika idara zote serikalini, jeshini, na pia katika Baraza la Wawakilishi.
Marehemu Mwakanjuki alianza Siasa kabla ya Mapinduzi ya Zanzibar ya Januari 12, 1964 akianzia katika Chama Cha Afro Shiraz (ASP) na baadae Chama cha Mapinduzi.
"hatuna budi kumshukuru mwenyezi Mungu kwa mchango wa marehemu wakati wa uhai wake nasi twamuombea mapumziko mema ya milele, Amina" Rais amemuombea Dua na kuiomba familia ya marehemu kuwa na subira wakati huu wakuondokewa na mpendwa wao.
No comments:
Post a Comment