RAIS BINGU WA-MUTHARIKA
Rais
wa Malawi Bingu amefariki dunia baada ya kupatwa na mshtuko wa moyo,
akiwa na miaka 78.
Duru kutoka kwa serikali zimethibitisha kifo hicho kwa BBC ambapo Mwili wa kiongozi huyo umepelekwa Afrika Kusini.
Hata hivyo serikali haijatoa taarifa rasmi kuhusu kifo cha Wa-Mutharika huku Mmoja wa madaktari waliokuwa wakimhudumia kiongozi huyo ameliambia BBC, Wa-Mutharika alikufa baada ya moyo wake kusimama ghafla.
Duru kutoka kwa serikali zimethibitisha kifo hicho kwa BBC ambapo Mwili wa kiongozi huyo umepelekwa Afrika Kusini.
Hata hivyo serikali haijatoa taarifa rasmi kuhusu kifo cha Wa-Mutharika huku Mmoja wa madaktari waliokuwa wakimhudumia kiongozi huyo ameliambia BBC, Wa-Mutharika alikufa baada ya moyo wake kusimama ghafla.
Wadadisi wa mambo wameonya kifo cha rais huyo huenda
kikazua mgogoro wa uongozi.
Katiba ya nchi inampa nafasi Makamu wa Rais
kuongoza nchi endapo Rais atafariki au kuugua kiasi cha kushindwa
kuongoza taifa.
Hata hivyo Makamu wa Rais nchini Malawi, Joyce Banda
alitofautiana na Wa-Mutharika kufuatia mzozo wa urithi wa uongozi ambapo
alifukuzwa kutoka chama tawala cha Democratic People's Party (DPP).
Kaka yake na Rais ambaye ni Waziri wa mambo ya nje Bw.Peter Mutharika aliteuliwa kugombea urais hapo mwaka wa 2014.Mwandishi
wa BBC mjini Blantyre Raphale Tenthani amesema mawaziri wamekuwa na
kikao usiku mzima kujadili hali ya sasa.
Rubaa za serikali zimenukuliwa
zikisema kwamba maiti ya Rais imesafirishwa Afrika Kusini huku maafisa
wakitafakari hali ya sasa.
Bingu wa Mutharika aliingia madarakani mwaka wa
2004. Baadaye alikihama chama chake cha United Democratic Front (UDF)
kwa tuhuma za wanachama kuhujumu harakati za kupambana na ufisadi uliokuwa ukifanyika nchini humo.
Alichaguliwa tena mwaka 2009, lakini katika siku za karibuni wakosoaji
wake wamemlaumu kwa kuegemea sera za kiimla.
Rais huyo alikumbwa na shinikizo la kuachia
madaraka kwa tuhuma za kupendelea ukoo wake, na kuharibu madaraka.
Wa
Mutharika aliwakera wafadhili wa kigeni hasa baada ya kumfukuza balozi
wa Uingereza Fergus Cochrane-Dyet, na kufanya utawala wa Uingereza
kusimamisha msaada kwa Malawi.
No comments:
Post a Comment