Kamanda
wa Polisi mkoani Kigoma Kamishna Msaidizi ACP Frasser Kashai.
POLISI KIGOMA WAANZA UCHUNGUZI WA MAUAJI HOLELA
Na Pardon Mbwate na Felister Elias wa Jeshi la Polisi Kigoma
Jeshi la Polisi Mkoani Kigoma limeanza
uchunguzi mauaji ya watu wanne yakiwemo ya mkazi mmoja wa kijiji cha Muhange
Wilaya ya Kibondo mkoani humo Bw. Misigalo Kamoli(53), aliyekutwa juzi
saa 2.00 asubuhi akiwa ameuawa kwenye shambani la mkazi mmoja wa kijiji
hicho baada ya kushambuliwa na watu wasiojulikana.
Kamanda
wa Polisi mkoani Kigoma Kamishna Msaidizi ACP Frasser Kashai, amesema
kuwa marehemu alikutwa wakati wa ukaguzi wa eneo la tukio kufuatia
mauaji hayo, Makachro wake waliukuta mwili wa marehemu ukiwa na jeraha
la kuchomwa na kitu chenye ncha kali sehemu ya kwapa la mkono wa
kushoto.
Kamanda
Kashai amesema kuwa ingawa Polisi wanaendelea na uchunguzi juu ya tukio
hilo, lakini huenda marehemu alishambuliwa na watu baada ya
kukurupushwa wakati alipokuwa kwenye harakati za kutaka kuiba nyakati za
usiku kijijini hapo.
Alisema
kumbukumbu za Polisi zinaonyesha kuwa mwaka 2009 marehemu Misigalo
aliwahi kuhukumiwa kifungo cha mwaka mmoja gerezani kwa kosa la kuvunja
nyumba usiku na kuiba.
Hata
hivyo Kamanda Kashai amewaonya vikali wananchi mkoani humo kuacha
kuchukua sheria mkononi za kuwashambulia na hata kuwaua watuhumiwa
wanaodaiwa kutenda makosa na badalayake watuhumiwa wakamatwe na
kufikishwa Polisi ili hatua zichukuliwe dhidi yao.
Kamanda
Kashai amesema kamwe Jeshi la Polisi halitaweza kukaa kimya huku
likiona kwamba kuna baadhi ya watu wakijichukulia sheria mkononi kwa
kuwahukumu watuhumiwa hata kabla ya kufikishwa mahakamani.
Wiki
iliyopita Jeshi la Polisi mkoani Kigoma liliwakamata watu wanane kwa
tuhuma za kuhusika na mauaji ya watu watatu kwa kisingizio cha hasira
kali.
Watu wawili waliuawa kwa kutuhumiwaa kuwa ni wachawi na mmoja kwa tuhuma za wizi wa kuku.
Taarifa hii imehaririwa na kusambazwa na Inspekta Mohammed Mhina, Afisa Habari Mkuu wa Jeshi la Polisi Zanzibar.
No comments:
Post a Comment