Waziri mkuu mstaafu Mh.Edward Lowassa akisalimiana na Mc Charles Mwakipesile(mwandishi wa gazeti la Majira mkoani Mbeya)
Na Mwandishi Wetu,Mbeya.
Na Mwandishi Wetu,Mbeya.
WAZIRI
mkuu mstaafu,Edward Lowassa ametoa Shilingi Milioni 10 taslimu kwa
ajili ya ujenzi wa kanisa la EAGT lililopo mjini Tunduma wilaya ya
Mbozi mkoani Mbeya.
Fedha
hizo amezitoa wakati wa harambee ya kuchagia ujenzi wa kanisa hilo
ililofanyika katika viwanja vya Hoteli ya High Class mjini hapa.
Lowassa
ambaye alitumia takribani dakika 28 pekee kuwepo katika viwanja hivyo,
alisema kuwa watanzania ni vema wakawa na wito wa kujenga nyumba za
kuabudia kuliko kujenga nyumba za starehe zikiwemo Bar.
‘’Nafurahi
kualikwa katika tafrija hii na niwaombe kwa pamoja tuwe na tabia za
kujenga nyumba za Mungu ambazo zitakusanya waumini kuabudia na kuomba
kwa pamoja kuliko hivi ilivyo wengi wanajenga Bar’’ alisema Lowassa.
Aliongeza
kuwa kwa sasa nchi ipo katika kipindi kigumu cha uchumi na masuala ya
katiba mpya hivyo aliwaomba wakristo kupanga ratiba ya kuiombea nchi
ili iendelee kuwa na amani na watanzania kuendelea kuimarisha
ushirikiano na umoja uliopo.
Alisema
kuwa jambo hilo ni muhimu kwa kila mtanzania ambapo kila mmoja
aliombee taifa,ili lisikumbwe naghasia na mambo kama yale yanayotokea
katika nchi zingine ikiwemo Nigeria ambako kikundi cha Boko Haramu
hakiwataki Wakristo.
‘’Mimi
,familia yangu na marafiki zangu tumeguswa na ujenzi wa nyumba ya
Mungu na tunatoa Shilingi Milioni 10 na huu ni mwanzo tu’’ alisema
Lowassa.
Sanjari
na kutoa fedha hizo, pia alimuomba askofu wa kanisa hilo aandae tamasha
la kuchagia ujenzi huo kwa kwaya zote ambazo zilihudhuria harambee
hiyo na kwamba kwaya tatu zitakazoshinda zitachagua mwakilishi mmoja
ambao atawagharamia kwenda nchini Israel kuona historia ya kikristo.
Alisema
amefanya hivyo kwasababu anapenda sana uimbaji na kwamba alibarikiwa
zaidi alipoimba pamoja na wanakwaya hao wimbo usemao ‘’Bwana Mungu
nashangaa kabisa nikitazama jinsi ulivyo……..
Kwa
upande wake Askofu mkuu wa Kanisa hilo,Keneth Kasunga alimshukuru
Waziri Mkuu huyo mstaafu ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Monduli kuwa
amejenga nyumba ya Mungu na wala si ya Mtu binafsi hivyo Mungu hawezi
kumuacha katika mambo yake yote na mahitaji pia.
Kanisa
hilo lilisema kuwa katika ujenzi wa kanisa hilo lenye waumini 750,
walipungukiwa kiasi cha Shilingi Milioni 750, kanisa litakaloweza
kuwaondolea adha waumini ambao wanasali wakiwa nje kutokana na kanisa
lililopo kwa sasa kuwa dogo.
No comments:
Post a Comment