Steven Kanumba enzi ya uhai wake akiwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr.Jakaya Mrisho Kikwete |
KUHUSU MAREHEMU KANUMBA:
Steven Charles Kanumba:
Alizaliwa
mnamo Januari 8, mwaka 1984 huko mkoani Shinyanga.
Alipata elimu ya msingi katika shule ya Bugoyi, na baadaye alijiunga na sekondari ya Mwadui, kabla ya kuhamia Dar Christian Seminary.
Kanumba baada ya kumaliza elimu ya Kidato cha Nne Dar Christian, alijiunga na sekondari ya Jitegemee jijini Dar es Salaam ikiwa ni pamoja muendelezo kwa elimu ya Kidato cha Tano na Sita.
Akiwa Jitegemee sekondari ilikuwa ni chanzo kwa Kanumba kuanza shughuli za sanaa katika Kundi la Kaole Sanaa Group la Magomeni jijini Dar es Salaam.
Baada ya kukomaa katika kundi la Kaole, Kanumba aliamua kuanzisha kampuni yake mwenyewe ya filamu na hadi anakutwa na umauti alikuwa mwigizaji anayefahamika Afrika nzima na pengine nje ya bara la Afrika kwa ujumla.
Alishirikiana na wasanii wakubwa duniani kama Ramsey Nouah wa Nigeria na amefanya kazi na mastaa wengine kadhaa wa Nigeria.
Miongoni mwa filamu ambazo alifanya ni Dar To Lagos, She is My Sister, Ancle JJ, Oprah, Tufani, Johari, Gharika, Baragumu, Sikitiko Langu, Dangerous Desire, Cross My Sin, Village Pastor, Family Tears na nyinginezo akamalizia kwa filamu yake mpya ya Kijiji cha tambua Haki ambayo pia iligonga hisia za wengi.
Hivi karibuni, alikaririwa akisema atagombea Ubunge katika uchaguzi mkuu ujao wa mwaka 2015.
Kanumba atakumbukwa na wengi sana kwa ucheshi wake- upole na ushirikiano mzuri na wenzake katika kazi.
Kifo cha Kanumba ni pigo katika tasniya ya filamu Tanzania. Taifa limempoteza mtu ambaye alikwishaanza kuitangaza vema nchi kupitia sanaa hiyo na ambaye angetarajiwa kuitangaza zaidi katika anga za kimataifa zaidi kupitia sanaa hii.
Mwenyewe aliwahi kukaririwa
alifika hadi Hollywood, Marekani, ambayo ni ‘makka’ ya wacheza filamu.
Kana kwamba sifa na umaaarufu wa Kanumba unapoteza duru ya makaosa yake katika hali ya ukamilifu wa binadamu lakini kwa wakati huu hatuna budi kueleza kuhusu alivyojiimarisha katika kulinda heshima yake na umaarufu aliokuwa nao nyota huyu wa filam nchini Tanzania.
Katika kazi zake amemgusa kila binadamu aliyehai kuanzia kwa watoto ambao sasa wanamkumbuka kama Ancle JJ,huku kwa upande wa watu wazima katika maisha ya vijijini ni katika filamu ya Kijiji cha Tambua haki,ambapo kwa maisha ya vijana kwenye dimbwi la mapenzi aliwagusa katika filamu za Oprah,Johari na She is my Sister.
Na kwa upande wa watu wa dini aliwagusa katika filam za Cross My Sin na Village Pastor,na huku kwa upande wa ngazi ya familia Kanumba alizikusanya hisia za wanafamilia katika filam ya Family Tears.
Kwa muda huu nalazimika kuishia hapo kwani hata nieleze yepi na mangapi lakini kusimama kwa moyo na roho ya nguli huyu aliyeitangaza Tanzania kupitia filam kwa muda mfupi na kujipatia umaarufu mkubwa inazidisha majonzi makubwa.
Mungu aiweke pema peponi roho ya marehemu. Amin.
No comments:
Post a Comment