Msanii Steven kanumba enzi za uhai wake.
Habari
zilizotufikia hivi sasa zinasema msanii maarufu nchini, Steven Kanumba
amefariki dunia ghafla baada ya kudondoka na kujingonga sehemu ya kisogo
akiwa nyumbani kwake Vatican, Sinza jijini Dar es Salaam.
Tukio hilo lidaiwa kutokea majira ya kati ya saa tano na nusu na saa 7 usiku wa kuamkia leo na taarifa za kudondoka
kwa Kanumba zilitolewa na kijana anayeishi nae hapo nyumbani ajulikanaye
kwa jina la Seti aliyemwita daktari kujaribu kuokoa maisha yake lakini
alipofikishwa hospitali ya Muhimbili tayari alikuwa amekata roho.
Kwa
sasa mwili wa marehemu umeifadhiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti
hospitali ya Taifa Muhimbili.
Hata hivyo kifo cha nguli huyo wa filamu nchini kimegusa hisia za wengi licha ya kuwa ni msanii mwenye umri wa mdogo na aliyejipatia umaarufu kwa muda mfupi ukiringanisha na maisha halisi ya kitanzania na tasnia ya filam nchini.
Steven Kanumba leo hii umuhimu na umaarufu wake unajidhihirisha mbele ya watanzania na wasiokuwa wa watanzania baada ya kupata taarifa za kifo chake ambacho hakuna binadam aliyewaza wala kuota kuwa kijana huyo mtanashati jina lake litabadilika katika ulimwengu huu na kuitwa MAREHEMU STEVEN KANUMBA badala ya THE GREAT KANUMBA.
Ingawa hii ni taswira ya kawaida na ni hatua muhimu kwa kila kiumbe kupitia baada ya kuzaliwa lakini ni mshtuko mkubwa kwa mtu yeyote mwenye akili timamu kufikiria hilo kwani mbali na kuguswa bali pia ni kumbukumbu muhimu ya kuwa kila nafsi itaonja kifo pindi wakati unapowadia.
Yatazuka mengi kufuatia kifo chake lakini hakuna haja ya kuyapokea kwa mikono miwili na kuyakumbatia,yatatupotezea muda bure,tubaki na machungu na kuamini kuwa kazi ya MUNGU HAINA MAKOSA na wala hakuna aliyeandikiwa kuishi milele.
Steven Charles Kanumba ni ndugu yetu sote tulimpenda lakini aliyemuumba amempenda zaidi na kumwita kwake.
TAARIFA KUTOKA SINZA;
STEVEN KANUMBA mazishi yake huenda yakafanyika siku ya Jumanne baada ya kukamilika taratibu za mazishi.
No comments:
Post a Comment