Diwani wa kata ya Ipuli Bw.Waziri Mlenda ameahidi kuendelea kutoa shilingi laki moja kwa kila mwanafunzi atakayefaulu katika mitihani ya kidato cha nne katika kata yake.
Bw.Waziri ametoa ahadi hiyo wakati akikabidhi fedha hizo ambazo alitoa ahadi kwa wanafunzi waliofaulu mtihani wa Taifa wa mwaka jana ikiwa ni mkakati aliojiwekea katika kuinua kiwango cha elimu kwa shule zilizopo kwenye kata yake.
Aidha diwani huyo ametoa kiasi cha shilingi laki moja kwa kila mwanafunzi kwa wanafunzi wawili wa shule ya sekondari ya Ipuli iliyopo manispaa ya Tabora.
No comments:
Post a Comment