''Nawahakikishia tukiwa na programu maalum ya utoaji elimu kuhusu
utendaji na faida ya NHIF/CHF kwenye ngazi ya kata,mwitikio wa wananchi
wengi kujiunga na mifuko hii hautakuwa wa kusuasua hapa Mkoan Mara
,kwani mahitaji ya huduma bora za matibabu ni makubwa zaidi hususani
vijijini na CHF imejikita huko''..Pichani ni Mkuu wa Wilaya ya Bunda bwn. Francis Mtinga ambaye alikuwa mgeni rasmi wakati ufunguzi wa kongamano la siku ya wadau wa NHF kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa Mara.
Mama Leticia Nyaboke akiwa amemaliza kumfunika mtoto Neema kwenye
hospitali ya mkoa wa mara ambapo NHIF ilitoa msaada wa mashuka 400 kwa
hospital hiyo,ikiwa ni maadhimisho ya miaka 10 ya mfuko iliyoambatana na
siku ya wadau wa mkoa huo.
NA.Paul Marenga-Mara
Watendaji
wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya na Mifuko ya Afya ya Jamii
wametakiwa kuhamasisha
wananchi kujiunga na mifuko hiyo kwani uelewa mdogo wa utendaji wa
Mifuko hii kwenye mkoa Mara ndiyo chanzo cha kuwa na Idadi ndogo ya
wanachama wachangiaji,kwani hadi disemba mwaka jana ni kati ya kaya
237,071 zilizopo ni kaya 1,460 tu zilizojiunga na CHF sawa na 0.6
%asilimia.
Akizungumza
Kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Mara ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Bunda
bwn. Francis Mtinga alisema ‘Pamoja na agizo na maombi ya bodi ya
wakurugenzi wa NHIF, nawataka muandae utaratibu na kuwa na program
maalum za kuwashirikisha watendaji kuanzia ngazi ya kata,kutoa elimu
stahiki kuhusu utendaji wa mifuko hii,sanjari na maboresho ya huduma za
afya hapa mkoani kwetu kwani wananchi wana uwezo wa kuchangia kutokana
na vyanzo mbalimbali vya mapato walivyo navyo lakini elimu ndiyo
kikwazo.
Pia
amewaomba wananchi kuwa walinzi wa huduma za matibabu hususani
wanapokutana na dawa zinazotolewa na serikali zinauzwa katika maduka ya
watu binafsi,toeni taarifa kwa wahusika ili hatua stahili
zichukuliwe,.bwn Francis Mtinga alisema.
Naye
mjumbe wa bodi ya wakurugenzi NHIF ambaye pia ni Rais wa CWT bwn.
Gratian Mukoba amewataka wakuu wa wilaya,waheshimiwa wabunge, makatibu
tawala na watendaji kuanzia ngazi ya kata na Halmashauri, kuunganisha
nguvu ya pamoja katika kusimamia fedha za NHIF/CHF ,sambamba na
uhamasishaji wa wananchi kuchangia Mifuko ya Afya ya Jamii,Mikopo ya
Vifaa Tiba na Ukarabati wa Majengo.
Bodi
imeidhinisha mikopo hii zaidi ya miaka mitatu (3) lakini watoa huduma
wengi hawajachangamkia fursa hii,hivyo nitumie nafasi hii kuwahamasisha
ili kuboresha huduma za matibabu kwa wanachama na wananchi kwa ujumla
kwenye hospitali,zahanati na vituo vya afya vilivyopo mkoani kwenu.
Wakichangia
katika kongamano hilo bwn Alfonce Mwita mtoa huduma wa kata ya
kyabakari kutoka Tarime alisema watoa huduma wachache wasio na maadili
wamekuwa wakidhoofisha,nia njema ya serikali kupitia mifuko hii ya
NHIF/CHF katika kuboresha huduma za matibabu nchini.
Mfuko
wa Taifa wa Bima ya Afya umeendelea kuwa na makongamano ya siku za
wadau kwenye mikoa yote nchini sanjari na maadhimisho ya miaka 10, kama
ambavyo umefanyika Mkoani Mara ,lengo likiwa ni kufanya mrejesho na
kukusanya maoni na ushauri kwa wadau wake,ili kuboresha utendaji wake.
No comments:
Post a Comment