Mbunge wa Arusha Mjini (Chadema),
Godbless Lema avuliwa ubunge na Mahakama kufuatia kilichoelezwa na
Mahakama kwamba ni ukiukaji wa taratibu za uchaguzi, ikiwemo matumizi
ya Lugha za matusi.
Na Dixon Busagaga,Arusha.
Na Dixon Busagaga,Arusha.
MAHAKAMA Kuu Kanda ya arusha leo imemvua Ubunge aliyekuwa Mbunge wa
jimbo la Arusha mjini Godbless Lema kwa tiketi ya CHADEMA.
Uamuzi huo umefikiwa Aprili 5, 2012 mbele ya Jaji Mfawidhi wa Kanda ya
Sumbawanga, Gabriel Rwakibarila katika hukumu ya kesi ya kupinga
matokeo ya Ubunge Jimbo la Arusha hilo yaliyo wasilishwa na wanachama
watatu wa CCM waliotaka Mahakama Kuu Kanda ya Arusha kutengua ushindi
wa Mbunge huyo.
Wana CCM hao waliofungua kesi hiyo ni pamoja na Mussa Mkanga (55),
Happy Kivuyo (49) na Agnes Molle (44).
Wanachama hao wanadai kuwa taratibu za maadili ya uchaguzi zilikiukwa
wa kuwa mshindi alitumia lugha za kashfa, matusi na kejeli katika
mikutano ya kampeni aliyofanya jimboni Arusha.
Katika kesi hiyo wadai walileta mashahidi 14 kwenda kutoa ushahidi wao
katika mahakama hiyo nawadaiwa walifanikiwa kuwaleta mashahidi 5
kujitetea.
Kuvuliwa Ubunge kwa Lema, kuna kuja siku chache wakati bado cham hicho
kipo katika shamra shamra za ushindi wa Ubunge jimbo la Arumeru
Mashariki mkoani humo.
Tutaendelea kufahamishana zaidi

No comments:
Post a Comment