Pages

KAPIPI TV

Monday, April 30, 2012

BARABARA URAMBO VIJIJINI ZATELEKEZWA"Kinamama wajawazito wapata taabu wakati wakipelekwa hospitalini kujifungua"

Na Paul Kagenzi -Urambo
Barabara nyingi za vijijini hazipitiki kutoka na ubovu ama kukatisha mito kama ilivyo kwa njia inayounganisha vijini vya Ichemba na Ng'wande yenye urefu wa zaidi ya kilometa 10, katika kata ya Ichemba wilaya ya Urambo mkoa wa Tabora.
Hali ya njia hiyo uwa mbaya zaidi wakati wa mvua za masika na unaweza kujiuliza inakuwaje pale inapohitajika kumpeleka hospitali mama mjamzito kwa huduma ya kujifungua au kupata huduma nyingine muhimu ambazo zinapatikana makao makuu ya kata yaliyopo katika kijiji cha Ichemba.

No comments: