Pages

KAPIPI TV

Tuesday, June 5, 2018

WANAKIJIJI 772 WA KIJIJI CHA MLANDA WAPATA HATI MILIKI ZA KIMILA 1,777

 Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa, Robert Masunya na naibu mkurugenzi wa Mradi wa Urasimishaji Ardhi (LTA) unaofanywa chini ya mpango wa Feed The Future kwa ufadhili wa Shirika la Misaada la Marekani (USAID) Malaki Msigwa wakimkabidhi hati ya kimila mmoja ya wananchi wa kijiji cha Mlanda ambaye ni mlemavu 


 Naibu mkurugenzi wa Mradi wa Urasimishaji Ardhi (LTA) unaofanywa chini ya mpango wa Feed The Future kwa ufadhili wa Shirika la Misaada la Marekani (USAID) Malaki Msigwa akitoa neo kwa wananchi wa kijiji cha Mlanda wakati wa kutoa hati za kimila 
 Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa, Robert Masunya na naibu mkurugenzi wa Mradi wa Urasimishaji Ardhi (LTA) unaofanywa chini ya mpango wa Feed The Future kwa ufadhili wa Shirika la Misaada la Marekani (USAID) Malaki Msigwa wakimkabidhi hati ya kimila mmoja ya wananchi wa kijiji cha Mlanda ambaye alikuwa anawakilisha kundi la wazee
Baadhi ya wananchi waliojitokeza kushirikia zoezi la utoaji wa hati miliki za kimila zilizotolewa na Mradi wa Urasimishaji Ardhi (LTA) unaofanywa chini ya mpango wa Feed The Future kwa ufadhili wa Shirika la Misaada la Marekani (USAID)

Picha ya pamoja baina ya viongozi wa Mradi wa Urasimishaji Ardhi (LTA) unaofanywa chini ya mpango wa Feed The Future kwa ufadhili wa Shirika la Misaada la Marekani (USAID),viongozi wa halmashauri ya wilaya ya Iringa pamoja na baadhi ya wananchi walikuwa tayari wamepokea hati za kimila


NA FREDY MGUNDA.IRINGA.


JUMLA ya wanakijiji 772 kati ya 1890 wa kijiji cha Mlanda kata ya Magulilwa wilaya ya Iringa mkoani Iringa wamepimiwa maeneo na mashamba yao na kukukabidhiwa hati miliki za kimila zinazotolewa kupitia Mradi wa Urasimishaji Ardhi (LTA) unaofanywa chini ya mpango wa Feed The Future kwa ufadhili wa Shirika la Misaada la Marekani (USAID).


Hati hizo zilikabidhiwa na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa, Robert Masunya wakati wa sherehe fupi za kuwakabidhi hati hizo zilizofanyika kijijini hapo na kuhudhuriwa na umati mkubwa wa wananchi na wageni mbalimbali walikuwepo katika tukio hilo.

Akizungumza na wanakijiji hao baada ya kukabidhi hati hizo Masunya alisema kuwa hati hizo zitawasaidia kutenga maeneo kwa ajili ya matumizi mbalimbali kwa kuzingatia uwezo wa ardhi kuhimili idadi hiyo na kasi ya ongezeko la watu na mifugo kwa miaka mingi ijayo.

Masunya aliongezea kuwa,hatua hiyo itasaidia kupunguza migogoro ya ardhi kwa kuimarisha usalama wa miliki za ardhi na kuongeza thamani ambayo itawawezesha hata kukopesheka katika taasisi za kifedha zikiwemo benki.

“Usajili wa ardhi ni muhimu kwasababu unaongeza ulinzi wa umiliki wa ardhi, unawezesha uwekezaji, unaongeza thamani ya ardhi na unapunguza migogoro ya ardhi,” alisema Masunya

Masunya aliupongeza mpango huo akisema utasaidia kupunguza eneo kubwa la ardhi ya Halmashauri ya Wilaya ya Iringa ambayo haijapimwa.

Aidha Masunya aliwaomba Feed The Future wautanue mradi huo angalau ufike umalize kupima vijiji vyote vya Halmashauri ya Wilaya ya Iringa  huku akivikumbusha vijiji vyote vya wilaya hiyo kuendelea kutoa ushirikiano kwenye miradi ambayo inasaidia kukuza maendeleo ya nchi. 

“Tunataka katika kipindi ambacho Mradi wa Urasimishaji Ardhi (LTA) unaofanywa chini ya mpango wa Feed The Future kwa ufadhili wa Shirika la Misaada la Marekani (USAID) tuhakikishe tunapima ardhi na mipango ya matumizi bora na ipimwe ili kila mwenye kipande chake cha ardhi awe na hati yake,” alisema Masunya.

Alisema kwa kupitia sera hiyo, kutakuwa na usimamizi zaidi wa ulinzi wa ardhi ya watu masikini ili kupunguza uporaji wa rasilimali hiyo unaofanywa na matajiri.

“Marekebisho ya sera hiyo ya ardhi yatawezesha pia kufanyika kwa mrekebisho ya sheria mbalimbali za ardhi ili ziendane na sera na mazingira ya sasa,” alisema Masunya.


Masunya aliwataka wanakijiji wa kijiji hicho ambao hawajapimiwa maeneo yao kwa sababu mbalimbali ikiwemo ubishi na migogoro ya kifamilia kutumia vizuri muda ambao bado mradi huo upo katika wilaya hiyo na kuhakikisha nao wananufaika na zoezi hilo.

Wanakijiji ambao hawajapimiwa maeneo yao wanaweza kuendeleoa kuzalisha migogoro ambayo haina tija kwa maendeleo yao na kusababisha waendelee kuwa masikini kwa kuwa hawatakuwa na dhamana ya kwenda kukopa.

Awali naibu mkurugenzi wa Mradi wa LTA, Malaki Msigwa alisema kuwa kijiji cha Mlanda kinajumla ya wananchi 1890 na walio nufaika na Mradi wa Urasimishaji Ardhi (LTA) unaofanywa chini ya mpango wa Feed The Future kwa ufadhili wa Shirika la Misaada la Marekani (USAID) ni wananchi 772 na kufanikiwa kutoa jumla ya hati miliki za kimila 1777 ambapo wanaume walikuwa 409 na wanawake 363. 

Msigwa aliwapongeza wataalamu wa mradi huo kwa kuhakikisha wanawasaidia wananchi wa kijiji cha Mlanda kupima maeneo yao na kupata hati miliki za kimila ambazo zitakuwa msaada mkubwa kwenye maendeleo ya kiuchumi.

“Baadhi ya miradi imeibuliwa wakati wa upimaji wa ardhi hivyo ni fursa sasa kwa wananchi wenyewe kuitumia vizuri ardhi waliyopimiwa na kupewa hati miliki za kimila na kwa kuwa asilimia fulani kijiji hiki kimepimwa hivyo wanaweza kuwa kijiji cha mfano kwa kuwapa maendeleo hata wawekezaji wazuri kwa faida yao” alisema Msigwa

Msigwa alisema kati ya vijiji hivyo 41 vitakavyotayarishiwa mipango ya matumizi bora ya ardhi na kila mwenye ardhi kupimiwa na kupewa hati miliki za kimila, vijiji 36 vipo wilayani Iringa na vitano vipo wilayani Mbeya.

“Baada ya kukamilisha zoezi la upimaji mashamba na urasimishaji wa kijiji chote cha Mlanda, hivi sasa mradi unaendelea na upimaji mashamba katika vijiji vya mradi ambavyo vipo wilayani Iringa” alisema Msigwa

Naye diwani wa kata ya Magulilwa Jane Mhangala aliupongeza Mradi wa Urasimishaji Ardhi (LTA) unaofanywa chini ya mpango wa Feed The Future kwa ufadhili wa Shirika la Misaada la Marekani (USAID) kwa kuzingatia jinsia wakati walipokuwa wanaendesha zoezi la upimaji ardhi katika kijiji hicho.

“Hongera sana LTA kwa kuwapa elimu wanawake na wanaume na kuhakikisha kuwa wanapa haki zao sawa bila kuwa na mgogoro wowote tofauti na ilivyokuwa hapo awali,maana miaka ya nyuma mwanamke alikuwa anabaguliwa kwenye kila kitu wala alikuwa haruhusiwi hata kumili ardhi” alisema Mhangala

Mhangala aliongeza kwa kusema kuwa wanakijiji wa kijiji cha Mlanda baada ya kupata elimu ya kumiliki ardhi kumepunguza sana migogoro ambayo ilikuwa inaleta chuki kwenye familia.

“Kwa sasa ardhi ya kijiji hiki imepanda dhamani kwa kiasi kikubwa na tayari ishapimwa na mmepata hati miliki za kimila ambazo zitawasaidia katika maendeleo yenu ya kiuchumi” alisema Mhangala

Tuesday, May 29, 2018

AMREF YAISHUKURU SERIKALI KUAMINI UTENDAJI WAO


 Mkurugenzi wa Amref Tanzania, Florence Temu (aliyekaa kushoto), akisaini mkataba wa kufanya kazi pamoja na Tayoa. Kulia ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa Tayoa, Peter Masika. Anayeshuhudia katikati ni Mkurugenzi wa Bodi ya Uratibu ya Miradi ya Ukimwi, Malaria na Kifua Kikuu inayofadhiliwa na mfuko wa dunia Dr. Rachae Makunde.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Tanzania Health Promotion Services (THPS), Redemputa Mbatia, akipeana mkono na Mkurugenzi wa Amref Tanzania, Florence Temu baada ya kusaini mkataba huo.
 Wadau wa masuala ya Afya wakiwa kwenye uzinduzi huo.
 Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.Faustine Ndugulile, akihutubia kwenye uzinduzi huo.
 Emiliani Busara kutoka MDH, akizungumza kwenye uzinduzi huo.
 Mchungaji Basilisa Ndonde akizungumza kwenye uzinduzi huo.
 Mkurugenzi wa Amref Tanzania, Florence Temu (aliyekaa kushoto), akisaini mkataba wa kufanya kazi pamoja na MDH. Kulia ni Emiliani Busara kutoka MDH.
 Mkurugenzi wa Amref Tanzania, Florence Temu, akihutubia kwenye uzinduzi huo.
  Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.Faustine Ndugulile (wa pili kushoto), akiwa na viongozi wengine katika uzinduzi huo.
 Ofisa Mtendaji Mkuu wa Tayoa, Peter Masika (kulia), akipeana mkono na Mkurugenzi wa Amref Tanzania, Florence Temu baada ya kusaini mkataba huo.
 Ofisa Mtendaji Mkuu wa Tayoa,, Peter Masika, akihutubia.
 Mkurugenzi wa Bodi ya Uratibu ya Miradi ya Ukimwi, Malaria na Kifua Kikuu inayofadhiliwa na mfuko wa dunia Dr. Rachae Makunde ,  akizungumza kwenye uzinduzi huo.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Mkapa Foundition, Rahel Sheiza (kulia),  akipeana mkono na Mkurugenzi wa Amref Tanzania Florence Temu baada ya kuisaini makubaliano ya kufanya kazi pamoja.

Na Dotto Mwaibale

MKURUGENZI Mkazi wa Amref nchini Tanzania, Florence Temu ameishukuru serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais Dkt. John Pombe Magufuli na zilizopita kwa ushirikiano inayotoa kwao.

Temu alitoa shukurani hizo kwenye uzinduzi wa mradi wa Amref Health Africa wa kupambana na Ukimwi na Kifua Kikuu unaofadhiliwa na Mfuko wa Dunia (Global Fund) uliofanyika leo jijini Dar es Salaam.

Kwenye uzinduzi huo ambao mgeni rasmi alikuwa Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Wazee na Watoto, Dr.  Faustine Ndugulile walihudhuria pia Mwenyekiti wa Baraza la Ushauri  wa Amref Tanzania, Dr. Eric Van Praag, Mwakilishi kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa linalojishughulisha na Ukimwi (UNAIDS), Dr. Leo Zekeng  na viongozi na wawakilishi wa mashirika mbalimbali  yaliyopewa dhamana ya kusimamia mpango wa mapambano dhidi ya ugonjwa wa Ukimwi ili kufikia asilimia 90 ya  waishiyo na   VVU kupatiwa tiba na asilimia 90 ya walio kwenye tiba za VVU 90 wafanikiwe kufubaza VVU.

Temu alisema kuwa, baada ya kupitia michakato ya kutambua asasi itakayochukua jukumu la 'Principle Recipient' katika mkondo wa taasisi zisizokuwa za serikali, mwanzoni mwa mwaka jana, Amref Health Africa Tanzania ilihidhinishwa rasmi na hatimaye Februari 21 walisaini kama Principle Recipient wa mkondo wa taasisi zisizo za serikali Mfuko wa Dunia wa Fedha zenye thamani ya Bilioni 55 na milioni 256 na laki 7 (yaani $24,969,174) kwa ajili ya kuibua na kutibia VVU na Kifua Kikuu, wakikabidhiwa jukumu la kusimamia na kuratibu afua za kwenye jamii zihusuzo Ukimwi na Kifua Kikuu kwa kupitia asasi ya kijamii, takriban asilimia 10% ya fedha hizo zitaelekezwa katika afua za kukabiliana na Kifua Kikuu katika jamii.

Aliongeza kuwa, kwenye mapambano ya maradhi hayo wataifikia mikoa 15 ambayo ni Arusha, Dodoma, Kilimanjaro, Manyara, Mara, Mbeya, Morogoro, Mtwara, Mwanza, Pwani, Shinyanga, Simiyu, Singida,Tanga na Ruvuma.

"Tunatarajia kupitia mfuko huu jumla ya watu 546,880 watafikiwa na huduma ya kupima VVU na kujua majibu, pia wasichana wa umri rika/ balehe na wanawake 162,064. Lakini pia kuibua na kuwapa rufaa wenye maambukizi ya kifua kikuu wapatao 16,465 watapata uchambuzi zaidi kwenye uwakilishi utakaofuata," alisema Temu.

Aliongeza kuwa, Amref inathamini kwa dhati jukumu walilopewa la kuratibu na kuongoza mradi huo uliofadhiliwa na Global Fund kwa miaka mitatu ijayo na kuahidi kufuata muongozo stahiki uliopo katika kutekeleza mradi huo, kwa dhana hiyo wanaahidi kuendelea kushirikiana kwa karibu na wadau husika kadiri watakavyoweza.

"Tutashirikiana moja kwa moja kama Amref lakini pia kwa kuwatumia sub recipients wetu ambao ningependa muwatambue," alisema Temu na kuwataja kuwa ni Tanzania Health Promotion Services (THPS), Management and Development fo Health (MDH), Benjamin Mkapa Foundition (BMF) na Tanzania Youth Alliance (TAYOA).
Aliongeza kuwa, wanatambua changamoto zilizopo katika kufikia jamii  hasa kwenye malengo ya kuwafikia wanaopaswa kujua hali yao ya maambukizi, ambapo kulingana na takwimu za Tanzania HIV Impact Survey ambao ni asilimia 52.2% ya walio na umri wa miaka 15-64 tu ndiyo wamepima na kujua hali zao za maambukizi; na uhaba wa wanaume kufikia huduma hizo, pia kuwepo kwa makundi yenye mazingira hatarishi zaidi ya kuambukizwa na kuambukiza VVU, pia haja ya kuibua wenye kifua kikuu na kuhudumia wenye TB sugu katika jamii, hizo ni baadhi tu!

Temu alisema wanatambua juhudi za Serikali ya Muungano wa Tanzania katika kuhakikisha anafikia asilimia hizo 90 tatu na nia ya kutokomeza kifua kikuu na kudhibiti maambukizi na kupeleka huduma hizo katika ngazi za jamii kuimarisha mifumo ya usambazi dawa na vifaa tiba, kusomesha wataalam, kuboresha vituo vya afya na hospitali na mifumo ya rufaa ni juhudi za wazi na wanaipongeza wizara ya afya inayoongozwa na Waziri Ummy Mwalimu akishirikiana kwa karibu na naibu wake Dr. Faustine Ndugulile.

"Mfano nichomekee kidogo hapo jinsi Amref kwa kupitia brand ya Angaza tulivyoweza kuleta huduma rafiki za upimaji wa VVU ulivyoweza kuifikia jamii ya rika zote na jinsi zote na hata kuwa huduma rafiki kwa jinsi za kiume yaani wanaume, tunashauri serikali iendelee kutumia hiyo brand kwani tunaamini neno Angaza ni rafiki na linaondoa hofu na linaleta ujasiri hata kwa wanaokuwa na VVU," alisema Temu.

Mkurugenzi huyo aliongeza kuwa, wanashukuru uthubutu wa wataalam wa wizara ya afya kuweza kuongeza wapimaji wa VVU kutoka kwa wataalam wa maabara hadi wahudumu wa afya walio wa maabara.

Alimalizia kwa kusema, wao Amref na wadau  wakiwemo SRs, wataendelea kufanya kazi kwa karibu na kufuata miongozo ya Global Fund, Sera na mitakati ya kitaifa, maelekezo ya vikao mbalimbali vya TNCM na hata kusimamia matumizi ya fedha za ufadhili huo na kutumia vyombo vilivyopo katika kutafuta ushauri ikiwemo wizara ya afya na vitengo vyake ambavyo ni Sekretariet ya TNCM,lfa PR-1 (Wizara ya Fedha) na Programme za NACP na NTLP pamoja na GF Office ya Wizara ya Afya.

Naye Dr. Ndugulile akizungumza katika uzinduzi huo, aliishukuru Amref na wadau wengine waliopewa jukumu la kupambana na maradhi ya kifua kikuu pamoja na Ukimwi ambao ni THPS, MDH, BMF na TAYOA.

Naibu waziri huyo aliwataka wote kuwa wabunifu na wenye mikakati ili kufikia malengo ya  kupambana na maradhi hayo kama walivyoyaanisha kwenye mchanganuo wa bajeti waliyoomba.

Alisema milango ipo wazi kwa wao kufika ofisini kwao kwa lengo la kuhitaji ushauri wowote watakaouhitaji.


Monday, May 28, 2018

KINANA, MBUYU KWENYE MSITU WA SIASA

Image may contain: 2 people, people smiling, people standing

Na Emmanuel J. Shilatu

Kanali Mstaafu wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ), Abdulrahman Omar Kinana anatajwa kuwa katika orodha ya safu za viongozi mibuyu na migude kwenye misitu minene ya siasa yenye kuhimili tufani za kila aina pia Mwanasiasa anayependa kuheshimu utamaduni, utaratibu na mwenye kuishi kwa misingi ya nidhamu .

Kinana anatajwa kama zao miongoni mwa kunga zitokanazo na mazao katika medani za siasa, utawala, uongozi na aliyeshiba ujuzi toshelezi wa masuala ya diplomasia ya siasa pia anayejua mahusiano yatokanayo na historia, harakati za ukombozi na umoja wa Afrika.

Sauti yake aghalabu huwa na mvumo wa mawimbi ya busara, fikara njema na hekima zenye wito pele aamuapo kusema, kukosoa, kutetea, kukumbusha, kushauri au kuonya kutokana na tabia yake ya kufanya yote hayo kwa hali ya kujiamini akiwa na nguvu ya hoja.

Ukimya wa Mwanasiasa huyo siku zote ni kama mfano wa Simba hodari awindae nyikani au mbugani akiwa hana pupa wala kiherehere. Huyafanya yote kwa utulivu na umakini mkubwa ambao baadae haumletei majuto, athari wala taathira.

Ni Mwanasiasa wa aina yake aliyewahi kuhitajiwa na Marais (Wenyeviti) watatu awe katibu mkuu wa CCM akakataa huku akitoa madai mazito yenye msingi, nguvu ya hoja na maana.

Amewahi kutakiwa na Rais Ali Hassan Mwinyi awe Katibu Mkuu wa CCM akakataa huku akitoa hoja. Akasema alikuwa na mchakato wa kazi nyeti na muhimu akishirikiana na wenzake kufanya mabadiliko ya mfumo mpya wa Jeshi utakaokwenda sanjari na mahitaji ya wakati; hivyo asingekuwa tayari kuiacha kabla kazi hiyo kukamilika.

Akatakiwa tena na Rais Benjamin Mkapa ashike nafasi hiyo akasita kukubali huku akitoa hoja za msingi na zenye mashiko yasio na shaka wala utata.

Kinana mara ya kwanza alitakiwa na Mwenyekiti Mstaafu Kikwete akakataa kubeba jukumu hilo kwa sababu kadhaa alizoona ni ngumu kwake kukitumikia chama kwa wakati huo. Hata hivyo mbinu za ushawishi zikafanyika akaafiki kuwa Katibu Mkuu.

Bila shaka Kinana aliteuliwa kuwa Katibu Mkuu wakati CCM ikiwa katika mgawanyiko mkubwa uliohatarisha uhai na mustakabali wa chama hicho kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka 2010.

Kwa busara zake, pengine na ziada ya maarifa au mbinu za kijeshi, uzoefu wa kisiasa, uongozi na utawala, Chama Cha Mapinduzi na viongozi wake ghafla wakashikamana tena na kuzika yaliopita.

Amewahi kusema mbele ya Mzee Mkapa kwa wakati ule amejiona mbele yake bado ipo hazina ya Viongozi wajuzi wa muda mrefu ndani ya chama, vingunge wenye weledi na maarifa ya kisiasa kuliko yake hivyo muda wa yeye kushika wadhifa si wakati huo.

Akaachwa na kuendelea kuwa Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM akiwa Meneja wa kampeni za wagombea urais Mzee Mkapa na Dk. Jakaya Kikwete.

Katika safu ya Vijana wa TANU Youth League na baadae UVCCM waliolelewa kwenye mikono ya Wanasiasa kama kina Mwalimu Julius Nyerere, Sheikh Aboud Jumbe Mwinyi, Sheikh Thabit Kombo Jecha, Mzee Rashid Kawawa, Mzee Saadan Abdul Kandoro na Mzee Rajab Diwani, Kinana anaweza kusimama kati yao.

Ameshiriki pamoja nao katika mbio za siasa, akichuma uzoefu huku mbele yake kukiwa na Wanasiasa kama Mzee Pius Msekwa, Marehemu Kingunge Ngombare Mwiru, Mzee John Malecela, Hayati Daudi Mwakawago, Hayati Moses Nnuye, Balozi Chrispher Liundi, Ali Ameir Mohamed na wengine kadhaa.

Vijana wanasiasia wa rika lake na wanaopishana kwa umri kiasi kidogo ni kina Dk Kikwete , Dk Mohamed Seif Khatib, Dk Salmin Amour, Yusuf Makamba, Jaka Mwambi, John Chiligati, Marehenu Ukiwaona Ditope Mzuzuri na wengine wengi .

Kanali Mstaafu Kinana kama atajigamba amezaliwa na kulelewa ndani ya TANU/ASP na maisha yake yote amekulia CCM na serikali zake, hoja hiyo itajuzu na kuyakinika.

Kwa ufupi ni Mwanasiasa asiyebahatisha katika utambuzi wa mizungu ya siasa, mbinu za utendaji, uelewa na upimaji kwenye viwango vya usemaji, ushauri au anapofanya shambulizi la kisiasa dhidi ya hasimu wake.

Niliposikia tetesi za kujiuzulu kwake kwa siku nzima ya jana nilikuwa nikitafakari bila kupata majibu ya haraka na kuona haikuwa wakati sahihi na muafaka sana kwa kiongozi huyo wa CCM kuachia ngazi na kujiweka kando.

Hata hivyo CCM ni chama kikongwe chenye hazina kubwa ya Wanasiasa hodari hivyo lolote linaweza kuwa ila muhimu ni kutega mingo na kusubiri wakati kwa kutega vyema masikio yetu.

*Shilatu E.J*

0767488622

VIJANA WASHAURIWA KUWA WASHIRIKI WA MAENDELEO SIO WANAOSUBIRI

 Rais wa AIESEC Tanzania, Amani Shayo akizungumza kuhusu AIESEC na kazi zake ambapo alisema jukwaa hilo lengo lake ni kuwasaidia vijana kujitambua katika masuala ya uongozi, anaamini kwamba jukwaa ni sehemu kubwa ya kufanikisha vijana kujitambua na kujiipanga kushiriki maisha yanayotakiwa katika jamii wakati wa jukwaa la vijana la AIESEC lililofanyika katika ukumbi wa Makumbusho ya Taifa jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Jukwaa hilo lilifadhiliwa na Umoja wa Mataifa, Benki ya CRDB, Tanzania Breweries Limited (TBL) pamoja na Empower Ltd.
 Mgeni rasmi Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini, Alvaro Rodriguez akizungumza na vijana wa kutoka vyuo mbalimbali walioshiriki kwenye jukwaa la vijana la AIESEC lililofanyika katika ukumbi wa Makumbusho ya Taifa jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Jukwaa hilo lilifadhiliwa na Umoja wa Mataifa, Benki ya CRDB, Tanzania Breweries Limited (TBL) pamoja na Empower Ltd.
 Msimamizi wa mazungumzo ambaye pia ni Mkuu wa Mafunzo na Miradi wa Empower Ltd, Ella Naiman (kushoto) akizungumza na kuwatambulisha wazungumzaji wakati wa jukwaa la vijana la AIESEC lililofanyika katika ukumbi wa Makumbusho ya Taifa jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Jukwaa hilo lilifadhiliwa na Umoja wa Mataifa, Benki ya CRDB, Tanzania Breweries Limited (TBL) pamoja na Empower Ltd. Kutoka kulia ni Allen Kimambo, Miranda Naiman, Mkurugenzi Mkazi wa Trade Mark East Africa, John Ulanga pamoja na Petrider Paul.
 Mkurugenzi Mkazi wa Trade Mark East Africa, John Ulanga (katikati) akizungumza kwenye jukwaa la vijana la AIESEC  ambapo alisema vijana wanatakiwa kutoa mchango mkubwa katika kuhakikisha nchi inafikia malengo ya maendeleo endelevu ambayo utekelezaji wake unaishia mwaka 2030 wakati wa jukwaa hilo lililofanyika katika ukumbi wa Makumbusho ya Taifa jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Jukwaa hilo lilifadhiliwa na Umoja wa Mataifa, Benki ya CRDB, Tanzania Breweries Limited (TBL) pamoja na Empower Ltd.
 Mzungumzaji katika jukwaa la vijana la AIESEC, Mkurugenzi Mtendaji wa Empower Ltd, Miranda Naiman (wa pili kulia) akizungumza wakati wa jukwaa hilo lililofanyika katika ukumbi wa Makumbusho ya Taifa jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Jukwaa hilo lilifadhiliwa na Umoja wa Mataifa, Benki ya CRDB, Tanzania Breweries Limited (TBL) pamoja na Empower Ltd.
 Meneja wa Masuala Endelevu wa TBL Group, Irene Mutiganzi akiwasilisha mada kuhusu mitandao ya kijamii ambapo alisema matumizi ya mitandao ya kijamii yakitumika sahihi yatasaidia kufanikisha malengo ya maendeleo endelevu (SDGs) wakati wa jukwaa la vijana la AIESEC lililofanyika katika ukumbi wa Makumbusho ya Taifa jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Jukwaa hilo lilifadhiliwa na Umoja wa Mataifa, Benki ya CRDB, Tanzania Breweries Limited (TBL) pamoja na Empower Ltd.
 Mshehereshaji wa jukwaa la vijana la AIESEC, Walter Odemba akiendesha shemsha bongo kuhusu uelewa wa malengo ya maendeleo endelevu (SDGs) kwa vijana kutoka vyuo mbalimbali walioshiriki jukwaa hilo lililofanyika katika ukumbi wa Makumbusho ya Taifa jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Jukwaa hilo lilifadhiliwa na Umoja wa Mataifa, Benki ya CRDB, Tanzania Breweries Limited (TBL) pamoja na Empower Ltd.
 Mgeni rasmi Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini, Alvaro Rodriguez akijibu maswali kwa washiriki wa jukwaa la vijana la AIESEC kuhusu malengo ya maendeleo endelevu na umuhimu wa vijana kushiriki moja kwa moja ambalo limefanyika katika ukumbi wa Makumbusho ya Taifa jijini Dar es Salaam. Jukwaa hilo lilifadhiliwa na Umoja wa Mataifa, Benki ya CRDB, Tanzania Breweries Limited (TBL) pamoja na Empower Ltd.
Baadhi ya vijana kutoka vyuo mbalimbali wakichangia maoni wakati wa jukwaa la vijana la AIESEC lililofanyika katika ukumbi wa Makumbusho ya Taifa jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Jukwaa hilo lilifadhiliwa na Umoja wa Mataifa, Benki ya CRDB, Tanzania Breweries Limited (TBL) pamoja na Empower.
Baadhi ya vijana kutoka vyuo mbalimbali walioshiriki jukwaa la vijana la AIESEC lililofanyika katika ukumbi wa Makumbusho ya Taifa jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Jukwaa hilo lilifadhiliwa na Umoja wa Mataifa, Benki ya CRDB, Tanzania Breweries Limited (TBL) pamoja na Empower Ltd.
Sekretarieti ya maandalizi ya jukwaa la vijana la AIESEC lililofanyika katika ukumbi wa Makumbusho ya Taifa jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Jukwaa hilo lilifadhiliwa na Umoja wa Mataifa, Benki ya CRDB, Tanzania Breweries Limited (TBL) pamoja na Empower Ltd.


Na Mwandishi wetu
MRATIBU Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini Alvaro Rodriguez amewataka vijana wa Tanzania kuwa washiriki katika mipango ya maendeleo na sio kusubiri kufanyiwa.

Aidha ameshauri vijana kuacha kuilalamikia serikali na jumuiya ya kimataifa kuhusu ajira na badala yake wajiulize wamelifanyia nini taifa na jumuiya hiyo.

Alisema katika kipindi ambacho theluthi mbili ya watu nchini ni vijana, wasitarajie kuajiriwa au kupatiwa kazi kirahisi kwa kuwa idadi ni kubwa kuliko hata yeye alipokuwa akisoma.

Alisema tatizo la ajira kwa sasa haliwezi kusubiri serikali au wahisani ni tatizo linalokuwa kibinafsi zaidi na kuhitaji vijana katika uwingi wao kuamka na kubuni vitu vitakavyoleta maendeleo yao binafsi na pia ya kitaifa.

Akizungumza katika jukwaa la vijana la AIESEC mwishoni mwa wiki katika ukumbi wa Makumbusho ya Taifa, Dar es salaam Mratibu huyo alisema kwamba  vijana  wanatakiwa kushiriki katika kila kitu na kuacha kushutumu serikali au jumuiya ya kimataifa katika kipindi ambacho dunia imebarikiwa na vijana  kama nguvu kazi yake kubwa.

Aliwataka vijana kujadili kuhusu malengo ya dunia, fursa zake, utekelezaji wake na changamoto zake.

“Malengo ya Dunia ni ajenga muhimu sana kwa Tanzania, Afrika na ulimwenguni  kote. Ajenda hii imelenga kuleta mabadiliko chanya kwa kuhakikisha hakuna anayeachwa nyuma katika utekelezaji wake” alisema Alvaro na kuongeza kuwa malengo hayo 17 ni lazima yajulikane ili kil kijana ashiriki katika utekelezaji wake.

Alisema vijana wakiwa ndio viongozi wa baadae ni lazima waelewe malengo hayo ya dunia na namna ya kuyatekeleza kwa kuyafungamanisha na mpango wa maendeleo wa miaka mitano wa taifa.

Alisema kwa vijana kuangalia na kutambua wataweza pia kuona ni kwa namna gani wao ni watekelezaji wa malengo hayo na wala si wasindikizaji.

Aidha aliwataka wakiwa kama vijana wanatakiwa kuwa wbaunifu katika eneo  walilipoo na kuhakikisha kwamba linapata mafanikio makubwa.

“Kwa wale wanaonifuatilia katika twita mtakumbuka  niliposti  habari za kijana wa miaka kumi na minane ambaye alitengeneza mkono wa roboti unaofanyakazi kutoka katika mabaki ya vifaa vya matumizi ya nyumbani. Huu ndio ubunifu tunaoutaka, wa kutambua changamoto na suluhu zake” alisema Alavaro katika jukwaa hilo lililofanyika Makumbusho jijini Dar es salaam.

Alisema anaamini kuwa Mpango wa dunia wa maendeleo endelevu sio Biblia wala Kurani na kuwataka vijana kuuangalia, kuutafakari kuujadili na kujua namna ya kuendesha utekelezaji wake kwani imebaki miaka 12 kumalizika kwa utekelezaji.

Alisema ili kufikia adhima ya kuutokomeza umaskini  ifikapo mwaka 2030 ni vyema vijana wakatumia wakati kwa makini kuangalia malengo hayo 17 na kuona namna ya wao kuwa washirika.

Aidha katika hotuba yake hiyo alihimiza vijana kufanya mambo kwa wakati:” Vijana tufanye ya wakati, wakati tuna wakati, kwani utafikia wakati tunataka kufanya ya wakati, wakati hatuna wakati”

Akizungumzia nguvu ya mtandao , Alvaro aliwataka vijana kuwa smati katika kuchagua mambo yanayofaa kwa maendeleo yao na sio kuchukua mambo ambayo yatawaangamiza au kuleta vurugu.

Katika jukwaa hilo ambalo liliongozwa na Mratibu huyo kulikuwa na wasemaji wengine wakiwemo Rais wa AIESEC Tanzania, Amani Shayo; Mkurugenzi Mkazi wa Trade Mark East Africa, John Ulanga na Mkurugenzi Mtendaji wa Empower, Miranda Naiman wote hao waliwataka vijana kuwa sehemu ya mafanikio.

Mmoja wa wa shiriki Debora Kaluzi kutoka Chuo cha Diplomasia ambaye pia ni championi wa malengo endelevu ya dunia alisema kama champion amefarijika kuwepo katika jukwaa hilo kujadili mambo mbalimbali yanayosukuma maendeleo ya nchi na vijana.

Alisema akiwa championi yeye anajikita zaidi katika lengo la nne na la tano ambalo linahakikisha kwamba wasichana wanakuwa na uwezo huku wakijua thamani yao katika jamii.

Alisema utekelezaji wa malengo hayo yatasaidia wanawake kujitambua na kufikia lengo la wao kushiriki kikamilifu katika masuala yanayohusu mambo mbalimbali ya kidunia yakiwemo ujasirimali na madaraka.

Alisema wanawake wakipewa fursa na kukawepo na haki sawa ya jinsia wanaweza kubadilisha mambo mbalimbali yanayohusu dunia wanayoishi.

Naye Amani Shayo katika mahojiano pamoja na kuzungumza na vijana alisema kwamba akiwa Rais wa AIESEC, Shirika la vijana lililoanzishwa mwaka 2000 Chuo Kikuu kwa lengo la kuwasaidia vijana kujitambua katika masuala ya uongozi, anaamini kwamba jukwaa ni sehemu kubwa ya kufanikisha vijana kujitambua na kujiipanga kushiriki maisha yanayotakiwa katika jamii.

Alisema kupitia kazi za kujitolea vijana wanazungumza kuhusu malengo ya maendeleo endelevu 17 yaliyopangwa na dunia na kuhakikisha kwamba wanafanikisha adhima ya dunia.

Alisema utafiti uliofanywa kwa takaribani vijana 2000 umewapa wazo la nini wanatakiwa kufanya na moja ya mambo ambayo yalijadiliwa katika Jukwaa ni namna ambavyo vijana wanaweza kuwezeshwa kujiajiri kuajiriwa na pia kushiriki kikamilifu katika miradi mbalimbali ya utoaji huduma na kadhalika.

Alisema shirika hilo lina mradi wa kuwezesha vijana kushiriki katika kazi za kujitolea ndani na nje ya nchi na pia kutoa elimu ya kuongeza ujuzi.

Alisema kazi kubwa ya jukwaa ni kuwaleta pamoja watawala na viongozi na wadau wa maendeleo ambao watashirikiana na vijana kudadavua malengo hayo ya dunia na kuyawezesha kufanyakazi katika maeneo ambapo vijana wenyewe wapo.

Sunday, May 27, 2018

MAJALIWA AHUTUBIA NA KUKABIDHI ZAWADI KWA WASHINDI WA MASHINDANO YA KUHIFADHI QUR-AAN TUKUFU AFRIKA KWENYE UWANJA WA TAIFA DAR ES SALAAM

PMO_2215
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana wakati alipowasili kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam kuwa mgeni rasmi katika Mashindano ya 19 ya Kuhifadhi Qur- aan Tukufu  Afrika yaliyoandaliwa na  Taasisi ya Al – Hikima, Mei 27, 2018. Katikati ni Waziri wa Mambo ya Dini wa Saud Arabia, Dkt. Saleh  Alashiek.
PMO_2222
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana wakati alipowasili kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam kuwa mgeni rasmi katika Mashindano ya 19 ya Kuhifadhi Qur- aan Tukufu  Afrika yaliyoandaliwa na  Taasisi ya Al – Hikima, Mei 27, 2018.
PMO_2284
Mufti Mkuu wa Tanzania, Sheikh Abubakary Zubeir akizungumza katika Mashindano ya 19 ya Kuhifadhi Qur-aan Tukufu Afrika yaliyoandaliwa na Taasisi ya Al-Hikima kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam, Mei 27, 2018.
PMO_2253
Baadhi ya waalikwa waliohudhuria katika Mashindano ya 19 ya Kuhifadhi Qur-aan Tukufu Afrika yaliyoandaliwa na Taasisi ya Al-Hikima wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipohutubia kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam, Mei 27, 2018.
PMO_2290
Waziri wa Mambo ya Dini wa Saudi Arabia, Dr. Saleh  Alashiek  akizungumza katika Mashindano ya 19 ya Kuhifadhi Qur-aan Tukufu Afrika yaliyoandaliwa na Taasisi ya Al-Hikima kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam, Mei 27, 2018.
PMO_2348
Waziri Mkuu,  Kassim Majaliwa akihutubia katika Mashindano ya 19 ya Kuhifadhi Qur-aan Tukufu Afrika  yaliyoandaliwa na Taasisi ya Al-Hikima kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam, Mei 27, 2018.
PMO_2669
Waziri Mkuu, Kassim Majliwa akimkabidhi Shujaa Suleiman Shujaa zawadi ya shilling milioni 15 baada ya kutangazwa kuwa mshindi wa kwanza wa Mashindano ya Kuhifadhi Qur-aan Tukufu Afrika yaliyoandaliwa na Taasisi ya Al-Hikima kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam, Mei 17, 2018. Kulia ni Mufti Mkuu wa Tanzania, Sheikh Abubakary Zubeir na watatu kulia ni Rais wa Taasisi ya Al- Hikima, Sheikh Shariff Abdukadir.
Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)