Pages

KAPIPI TV

Saturday, June 24, 2017

MUFTI MKUU WA TANZANIA AWASILI MKOANI KILIMANJARO KWA AJILI YA SWALA YA EID-ELFITRI

Mufti wa Tanzania,Sheakh Abubakary Zubery akiwa katika lango la kutokea eneo la watu mashuhuri katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) alipowasili jana mkoani Kilimanjaro kwa ajili ya Swala ya Idd El- Fitr inayotaraji kufanika kitaifa mkoani humo.
Mufti wa Tanzania ,Sheakh Abubakary Zubery akitia aini katika kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili katika uwanja wa Ndege wa Kilimajaro (KIA).
Mufti Mkuu wa Tanzania ,Sheakh Abubary Zubery akiteta jambo na Sheakh Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro mara baada ya kuwasili katika uwanja wa Ndege wa kimataifa wa Kilimanjaro (KIA).
Msafara wa Mufti ukitoka katika uwanja wa Ndege wa Kilimanjaro (KIA) .
Mufti wa Tanzania ,Sheakh Abubary Zubery akiwa na viongozi pamoja na waumini wa Dini ya Kiislamu mara baada ya kuwasili mkoani Kilimanjaro.
Baadhi ya wanawake wa Dini ya Kiislamu walipofika kwa ajili ya kumpokea Mufti wa Tanzania,Sheakh Abubakary Zubery.
Mufti wa Tanzania ,Abubakary Zubery akiwasili katika mmoja wa miskiti iliyopo wilayani Hai kwa ajili ya uwekaji wa jiwe la Msingi. 
Mufti wa Tanzania,Sheakh Abubakary Zubery akifungua kitambaa katika jiwe la Msini kuashiria kuendelea kwa ujenzi wa jingo hilo litakalo tumika kama Madrasa.
Jengo la Ofisi za BAKWATA wilaya ya Hai ambalo Mufti wa Tanzania ,Sheakh Abubakary Zubery amefika kwa ajili ya uzinduzi wake.
Mufti wa Tanzania,Sheakh Abubakary Zubery akisalimiana na waumini wa Dini ya Kiislamu mara baada ya kuwasili katika ofisi za Bakwata wilaya ya Hai ka ajili ya ufunguzi wake.
Mufti wa Tanzania,Sheakh Abubakary Zubery akizindua rasmi ofisi za BAKWATA wilaya ya Hai.
Mufti wa Tanzania ,Abubakary Zubery akitia saini katika kitabu cha ageni mara baada ya kufungua rasmi ofisi za BAKWATA wilaya ya Hai.
Msikiti wa Masjid Shafi uliopo wilayani Hai
Mufti Mkuu wa Tanzania ,Abubakar Zubery akitia saini katika kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili katika mskiti wa masjid Shafi kwa ajili ya uzinduzi.
Mufti wa Tanzania ,Abubakary Zubery akizindua rasmi Msikiti wa Masjid Shafi uliopo wilayani Hai mkoani Kilimanjaro.
Katibu wa Bakwata wilaya ya Hai,Mwl Mohamed Mbowe akisoma risala wakati wa uzinduzi rasmi wa msikiti wa Masjid Shafi uliopo wilayani Hai.
Mufti wa Tanzania ,Abubakary Zubery akizungumza mara baada ya kuzindua Msikiti wa Masjid Shafi uliopo wilayani Hai.

Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii,Kanda ya Kaskazini.

MBOWE AFUTURISHA MISIKITI MINNEJIMBONI KWAKE,WAISLAMU WILAYA YA HAI WAMTUNUKU CHETI

Mbunge wa Jimbo la Hai,Freeman Mbowe akiwa na Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya hiyo Helga Mchomvu wakati wa Futari ya pamoja iliyoandaliwa na Mbunge huyo katika miskiti minne tofauti.
Baadhi ya Waumini wa Dini ya Kiislamu wakipata Futari katika msikiti wa Kibaoni wilayani Hai.
Sheakh Mkuu wa wilaya ya Hai,Omar Mohamoud akizungumza wakati wa hafla ya kupata Futari iliyoandaliwa na Mbunge wa Jimbo la Hai,Freeman Mbowe.
Imamu wa Msikiti wa Kambi ya Nyuki ,Fahad Lema akisoma Risala kwa Mbunge wa jimbo la Hai,Freeman Mbowe mara baada ya kumalizika hafa ya kupaa futari kwa pamoja katika msikit wa Kibaoni wilayani humo.
Mbunge wa Jimbo la Hai,Freeman Mbowe akisalimiana na Imamu wa Msikiti wa Kambi ya Nyuki Fahad Lema mara baada ya kuwasilisha ombi la kusaidiwa ujenzi wa vyumba vya madrasa ambapo Mh Mbowe alichangia kiasi cha Sh Mil,2 kwa ajili ya kununua mbao za kuezekea Paa.  
Mbunge wa jimbo la Hai,Freeman Mbowe akisalimana na Waumini katika Msikiti wa Kibaoni uliopo Bomang'ombe wilayani Hai ,mara baada ya kumalizika kwa hafla ya kupata futari iliyoandaliwa na Mbunge huyo katika miskiti minne tofauti katika jimbo hilo.
Mbunge wa jimbo la Hai,Freeman Mbowe akipata Futari na waumini wengine katika Msikiti wa Lambo uliopo Machame wilayani Hai baada ya kushiriki pia katika miskiti mingine mitatu .
Mmoja wa viongozi wa Dini ya Kiislamu Mwl Mohamed Mbowe akizungumza wakati akimkaribisha Mbunge wa jimbo la Hai,Freeman Mbowe katika Msikiti wa Lambo .
Mjumbe wa Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) Alhaji ,Habib Nasiwa akikabidhi Cheti cha Heshima kwa Mbunge wa jimbo la Hai,Freeman Mbowe kwa jitihada zake za kuleta umoja katika Dini na Madhehebu mbalimbali katika wilaya hiyo.
Mbunge wa jimbo la Hai,Freeman Mbowe akionesha zawadi ya Cheti alichokabidhiwa na Waislamu katika wilaya ya Hai.
Mbunge wa jimbo la Hai,Freeman Mbowe akikabidhi zawadi ya Cheti kwa Diwani wa kata ya Machame Kaskazini,Clement Kwayu ili afungue na kusoma kilichoandikwa ndani.
Diwani wa kata ya Machame Kaskazini,Clement Kwayu (Mwenye suti) akisoma maneno yaliyoandikwa katika Cheti kilichotolewa na Waislamu wa wilaya ya Hai,kwa Mbunge wa jimbo hilo Freeman Mbowe. 
Mbunge wa jimbo la Hai,Freeman Mbowe akishiriki Dua mara baada ya kumalizika kwa hafla ya Futari iliyoandaliwa katika misikiti minne tofauti ukiwemo msikiti wa Lambo uliopo Machame wilayani Hai.
Baadhi ya wauimini wa Dini ya Kiislamu wakiwasiliza viongozi mara bada ya kushiriki hafla ya Futari iliyoandaliwa na Mbunge wa jimbo la Hai,Freeman Mbowe.
Msikiti wa Lambo uliopo Machame ambao Mbunge wa jimbo la Hai,Freeman Mbowe amechangia kwa kiasi kikubwa ujenzi wake.

Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii,Kanda ya Kaskazini.
MBUNGE wa Jimbo la Hai na Kionozi wa Kambi rasmi Bungeni,Mh ,Freeman Mbowe ametunukiwa cheti cha heshima na jamii ya Waislamu katika wilaya ya Hai kutokana na jitihada zake zisizo na ukomo katika kuleta umoja katika Dini na Madhehebu mbalimbali.
“Tunaamini katka Uhuru wa kuabudu na kujieleza ,malumbano ya hoja na mijadala ,Kuvumiliana na kusamehe, Vitisho ,ugandamizaji  na uonevu wa aina yoyote vinaweza kuendelea lakini havitaweza kushinda jamii yetu. Uhuru ni tunu ya sili tuliyopewa na Mwenyezi Mungu Mtukufu” yalieleza maeno yaliyopo katika Cheti hiycho.
Mh Mbowe alikabidhiwa cheti hicho na Mjumbe wa Baraza Kuu la Waisalmu (BAKWATA) Alhaji Habib Nasiwa , katika msikiti wa Lambo uliopo Machame wilayani muda mfupi baada ya kumalizika kwa hafla ya kushiriki futari iliyoandaliwa na mbunge huyo katika misikiti minne tofauti ya Modio ,Rundugai,Kibaoni na Lambo.
Cheti hicho kilichosainiwa na Sheakh Mkuu wa wilaya ya Hai,Sheakh ,Omary Mahmoud ambaye pia ni katibu wa msikiti wa Kibaboni Bomangombe kimetolewa ikiwa ni ni ishara ya kutambua mchango mkubwa unatolewa na Mbunge huo kwa Waislamu.
AkIzinunguza mara baada ya kukabidi cheti hMjumbe wa Baraza kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) Alhaji Habib Nasiwa alitoa shukrani kwa niaba ya waislamu wa jimbo la Hai kwa namna ambavyo ameendelea kujitoa pamoja na kuchangia ujenzi wa msikiti wa Lambo.
“Nimehemewa sana ,sidhani kama naweza kusema kiasi cha kutoshereza ,nimehemewa na kujaaa furaha ya kufikiwa na Mh Mbowe,halikua jambo rahisi la kumpata leo ,kwanza tukijua Bunge linaendelea kadharika tukijua kwamba ana majukumu mengine mengi lakini akaona ashiriki na sisi wilaya ya Hai.”alisema Nasiwa.
“Jambo fupi la kukushirikisha jioni ya leo,mheshimwa tunakupongeza kwa kujua umuhimu wa ramadhan kwa kuacha shughuli zako na kuja kushiriki nasi katika kutufuturisha,tunakupa asante sana na mungu akubariki sana,”aliongeza Alhaji Nasiwa.
Katika hafla hiyo ya kufuturisha ,Mh Mbwe alishiriki katika misikiti yote minne ambapokatika msikiti wa Mudio alitoa mifuko 100 ya Saruji kwa ajili ya ujenzi wa Shule ya msingi inayomilikiwa na msikiti huo na pia alikabidhi kiasi cha sh Mil moja kwa msikiti wa Rundugai kwa ajili ya mwalimu anayefundisha masomo ya dini katika shule ya Msingi na Sekondari za Rundugai .

RAIS MAGUFULI ATOA MSAADA WA VITANDA,MAGODORO NA MASHUKA KATIKA HOSPITALI YA LEVOLOSI

 Mbunge wa viti maalumu ccm Mkoa wa Arusha  Catherine Magige akitoa nasaha mara tu baada ya kukabidhi msaada huo wa vitanda,magodoro na mashuka yaliyotolewa na Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania
 Picha ikionyesha  wa kwanza kulia Mbunge wa viti maalum(CCM) Catherine Magige akikabidhi kwa niaba ya Rais  John Magufuli    msaada wa magodoro 25,mashuka 25 pamoja na vitanda  25 katika  kituo cha afya cha Levolosi  ,ambapo msaada wa vitu hivi umetolewa na Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania ikiwa ni moja wapo ya ahadi zake alizozitoa katika kipindi cha kampeni  ,katikati ni Mganga  mkuu wa kituo cha Afya cha Levolosi  Feksi Edward ,wa kwanza kushoto ni Mganga mkuu wa Halmashauri ya jiji la Arusha Saimoni Chacha
                                                     (picha na Woinde Shizza,Arusha)
 Katibu wa UWT mkoa wa Arusha Fatuma Hassan akiwasalimia wananchi wakati wa hafla hiyo
 Mkuu  wa wilaya ya Arusha  Gabriel Fabian Daqarro akiongea na wananchi  wa jiji la Arusha 


 Baadhi ya manesi na madaktari wa jiji la Arusha wakiwa wamelibeba moja ya godoro mara baada ya kukabidhiwa hii leo
   Mkurugenzi wa Jiji la Arusha Mh: Athuman Kihamia akitoa neno la shukrani kwa niaba ya jiji  mara baada ya kupokea msaada huo na kuhadi kuvitunza vifaa hivyo walivyokabidhiwa
 Mbunge wa viti maalumu Catherine Magige akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wananchi wa jiji la Arusha mara baada ya kukabidhi vifaa hivyo



Baadhi ya madaktari na manesi wakiwa wanashuhudia makabidhiano ya msaada huo wa vitanda ,mashuka na magodoro (habari picha na Woinde Shizza,Arusha)

 Na Woinde Shizza,Arusha
Wananchi wametakiwa kuwapiga vita na kutokubaliana na wale wote ambao wanapinga jitiada za maendeleo ambazo zinafanywa na Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kwani jitiada hizo zinamanufaa makubwa kwa wananchi.

Aidha  kumekuwa na baadhi ya watu wamekuwa wakiziponda kazi ambazo anazifanya   Rasi kitu  ambacho sio kizuri kwani Rais amekuwa akijitaidi kufanya kazi vizuri ya kuwaletea maendeleo wananchi kama ilani ya chama cha mapinduzi inavyosema</ span>

 Hayo yamesemwa   leo jijini hapa  na mbunge wa viti maalumu kupitia chama cha mapinduzi mkoa wa Arusha  Catherine Magige  wakati akikiabidhi kwa niaba ya Raisi  vitanda 25 ,mashuka 25 na magodoro 25 viliyotolewa na Rais wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania ikiwa ni moja ya utekelezaji wa ilani ya chama cha mapinduzi</ span>

</ span>
Alisema k uwa  kumekuwa na baadhi ya viongozi wamekuwa wakiponda kazi  za Rais na kusema kuwa  afanyikitu chochote </ b>

"Rais  wetu anafanyakazi mtu anaesema afanyikazi kweli ni wakupuunzwa kabisa au naweza sema ana akili angalieni jinsi alivyozuia makontena  ya madini,angalieni jinsi alivyowakamata waujumu uchumi wa Escrow na sasa ivi ameunda tume ya kwenda kuchunguza Tanzanite one mbali na apo ata leo ametambua umuimu wawananchi wa mkoa wa Arusha na  ameamua kutoa msaada wa  magodoro ,mashuka pamoja na vitanda "alisema Magige

Aidha alitoa wito kwa wananchi kuunga mkono kazi ziazofanywa na Rais  ,pia alitumia muda huho kuwasihi madaktari kutunza vifaa ambavyo vinatolewa na serikali kwani vifaa hivyo vinanunuliwa kwa kodi za wananchi ,huku akisisitiza iwapo vitatunzwa vizuri vinaweza kukaa kwa muda mrefu na kuwahudumia wananchi wengi zaidi

Akitoa shukrani kwa vifaa hivyo mkurugenzi wa jiji la Arusha Mh: Athuman Kihamia aliishukuru serikali kwa kutoa misaada hii kwa jiji la Arusha na kuahidi kuvitunza vifaa hivyo vilivyotolewa  huku akiiomba serikali iendelee kuwapa misaada ya aina mbalimbali.

Msaada huu wa magodoro 25 ,mashuka 25 pamoja na vitanda 25  uliogaiwa leo katika hospitali ya Levolosi jijini Arusha umetolewa na Rais wa Jamuhuri ya muungano wa Tanzania  ikiwani moja ya utekelezaji wa ilani ya chama cha mapinduzi