Pages

KAPIPI TV

Saturday, June 24, 2017

RAIS MAGUFULI ATOA MSAADA WA VITANDA,MAGODORO NA MASHUKA KATIKA HOSPITALI YA LEVOLOSI

 Mbunge wa viti maalumu ccm Mkoa wa Arusha  Catherine Magige akitoa nasaha mara tu baada ya kukabidhi msaada huo wa vitanda,magodoro na mashuka yaliyotolewa na Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania
 Picha ikionyesha  wa kwanza kulia Mbunge wa viti maalum(CCM) Catherine Magige akikabidhi kwa niaba ya Rais  John Magufuli    msaada wa magodoro 25,mashuka 25 pamoja na vitanda  25 katika  kituo cha afya cha Levolosi  ,ambapo msaada wa vitu hivi umetolewa na Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania ikiwa ni moja wapo ya ahadi zake alizozitoa katika kipindi cha kampeni  ,katikati ni Mganga  mkuu wa kituo cha Afya cha Levolosi  Feksi Edward ,wa kwanza kushoto ni Mganga mkuu wa Halmashauri ya jiji la Arusha Saimoni Chacha
                                                     (picha na Woinde Shizza,Arusha)
 Katibu wa UWT mkoa wa Arusha Fatuma Hassan akiwasalimia wananchi wakati wa hafla hiyo
 Mkuu  wa wilaya ya Arusha  Gabriel Fabian Daqarro akiongea na wananchi  wa jiji la Arusha 


 Baadhi ya manesi na madaktari wa jiji la Arusha wakiwa wamelibeba moja ya godoro mara baada ya kukabidhiwa hii leo
   Mkurugenzi wa Jiji la Arusha Mh: Athuman Kihamia akitoa neno la shukrani kwa niaba ya jiji  mara baada ya kupokea msaada huo na kuhadi kuvitunza vifaa hivyo walivyokabidhiwa
 Mbunge wa viti maalumu Catherine Magige akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wananchi wa jiji la Arusha mara baada ya kukabidhi vifaa hivyoBaadhi ya madaktari na manesi wakiwa wanashuhudia makabidhiano ya msaada huo wa vitanda ,mashuka na magodoro (habari picha na Woinde Shizza,Arusha)

 Na Woinde Shizza,Arusha
Wananchi wametakiwa kuwapiga vita na kutokubaliana na wale wote ambao wanapinga jitiada za maendeleo ambazo zinafanywa na Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kwani jitiada hizo zinamanufaa makubwa kwa wananchi.

Aidha  kumekuwa na baadhi ya watu wamekuwa wakiziponda kazi ambazo anazifanya   Rasi kitu  ambacho sio kizuri kwani Rais amekuwa akijitaidi kufanya kazi vizuri ya kuwaletea maendeleo wananchi kama ilani ya chama cha mapinduzi inavyosema</ span>

 Hayo yamesemwa   leo jijini hapa  na mbunge wa viti maalumu kupitia chama cha mapinduzi mkoa wa Arusha  Catherine Magige  wakati akikiabidhi kwa niaba ya Raisi  vitanda 25 ,mashuka 25 na magodoro 25 viliyotolewa na Rais wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania ikiwa ni moja ya utekelezaji wa ilani ya chama cha mapinduzi</ span>

</ span>
Alisema k uwa  kumekuwa na baadhi ya viongozi wamekuwa wakiponda kazi  za Rais na kusema kuwa  afanyikitu chochote </ b>

"Rais  wetu anafanyakazi mtu anaesema afanyikazi kweli ni wakupuunzwa kabisa au naweza sema ana akili angalieni jinsi alivyozuia makontena  ya madini,angalieni jinsi alivyowakamata waujumu uchumi wa Escrow na sasa ivi ameunda tume ya kwenda kuchunguza Tanzanite one mbali na apo ata leo ametambua umuimu wawananchi wa mkoa wa Arusha na  ameamua kutoa msaada wa  magodoro ,mashuka pamoja na vitanda "alisema Magige

Aidha alitoa wito kwa wananchi kuunga mkono kazi ziazofanywa na Rais  ,pia alitumia muda huho kuwasihi madaktari kutunza vifaa ambavyo vinatolewa na serikali kwani vifaa hivyo vinanunuliwa kwa kodi za wananchi ,huku akisisitiza iwapo vitatunzwa vizuri vinaweza kukaa kwa muda mrefu na kuwahudumia wananchi wengi zaidi

Akitoa shukrani kwa vifaa hivyo mkurugenzi wa jiji la Arusha Mh: Athuman Kihamia aliishukuru serikali kwa kutoa misaada hii kwa jiji la Arusha na kuahidi kuvitunza vifaa hivyo vilivyotolewa  huku akiiomba serikali iendelee kuwapa misaada ya aina mbalimbali.

Msaada huu wa magodoro 25 ,mashuka 25 pamoja na vitanda 25  uliogaiwa leo katika hospitali ya Levolosi jijini Arusha umetolewa na Rais wa Jamuhuri ya muungano wa Tanzania  ikiwani moja ya utekelezaji wa ilani ya chama cha mapinduzi

Friday, June 23, 2017

AKINAMAMA WALIMA NYANYA KINYEREZI DAR WAJIFUNZA KILIMO CHA UYOGA

Mafunzo kwa vitendo. Akinamama wa Kinyerezi Green Voices wakiweka udongo kwenye mifuko kama maandalizi ya kilimo cha uyoga.

MRITHI WA DKT. MDEGELA KKKT DAYOSISI YA IRINGA, MCHUNGAJI BLASTON GAVILE, KUWEKWA WAKFU JUMAPILIAskofu Mteule Mchungaji Blastone Tuluwene Gavile (kushoto) akiwa na Msaidizi wa Askofu Mteule Mchungaji Himid  John Sagga.

IBADA ya kuwekwa wakfu kwa Askofu Mteule wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Iringa, Mchungaji Blaston Tuluwene Gavile, inatarajiwa kufanyika Jumapili Juni 25, 2017 mjini Iringa.

Monday, March 27, 2017

WAZIRI MWIGULU AWAASA ASKARI KUTOWABAMBIKIZIA WATU KESI

Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi Mhe Mwigulu Lameck Nchemba akizungumza wakati wa ufunguzi wa kikao cha kazi cha Mwaka 2017 cha Maafisa waandamizi wa Polisi na Makamanda wa Mikoa/Vikosi
Mzee John Samwel Malecela akizungumza wakati wa kikao cha kazi cha Mwaka 2017 cha Maafisa waandamizi wa Polisi na Makamanda wa Mikoa/Vikosi
 Maafisa waandamizi wa Polisi na Makamanda wa Mikoa/Vikosi
Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi Mhe Mwigulu Lameck Nchemba akizungumza wakati wa ufunguzi wa kikao cha kazi cha Mwaka 2017 cha Maafisa waandamizi wa Polisi na Makamanda wa Mikoa/Vikosi
SACP Ramadhani Mungi Msimamizi wa bandari Tanzania na Kamanda wa polisi mkoa wa Lindi Renata Mzinga wakifatilia kwa makini kikao cha kazi cha Mwaka 2017 cha Maafisa waandamizi wa Polisi na Makamanda wa Mikoa/Vikosi
Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi Mhe Mwigulu Lameck Nchemba akisalimiana na Makamu wa kwanza wa Rais na Waziri Mkuu Mstaafu Mzee John Samwel Malecela mara baada ya kuwasili katika ufunguzi wa kikao cha kazi cha Mwaka 2017 cha Maafisa waandamizi wa Polisi na Makamanda wa Mikoa/Vikosi
Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi Mhe Mwigulu Lameck Nchemba akisalimiana na baadhi ya Maafisa wa jeshi la Polisi mara baada ya kuwasili katika ufunguzi wa kikao cha kazi cha Mwaka 2017 cha Maafisa waandamizi wa Polisi na Makamanda wa Mikoa/Vikosi
Kamanda wa Jeshi la Polisi nchini Ernest Mangu Akisisitiza jambo wakati wa kikao cha kazi cha Mwaka 2017 cha Maafisa waandamizi wa Polisi na Makamanda wa Mikoa/Vikosi
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe Jordan Lugimbana akitoa salamu za Mkoa wa Dodoma wakati wa kikao cha kazi cha Mwaka 2017 cha Maafisa waandamizi wa Polisi na Makamanda wa Mikoa/Vikosi

Na Mathias Canal, Dodoma

Askari na Maafisa wa jeshi la Polisi nchini wameaswa kutotumia madaraka yao vibaya kwa kuwabambikizia wananchi kesi kwani kufanya hivyo ni kushindwa kusimamia dhamira njema ya Mhe Rais ya kuwapatia wananchi wanyonge haki zao stahiki.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Mambo ya ndani ya nchi Mhe Mwigulu Nchemba wakati akifungua kikao cha kazi cha Siku tatu cha mwaka 2017 kwa maafisa waandamizi wa Polisi na Makamanda wa Mikoa/Vikosi kilichofanyika katika ukumbi wa Mikutano wa LAPF Mjini Dodoma.

Mhe Mwigulu amesema kuwa kumekuwa na malalamiko kutoka kwa wananchi juu ya kuwabambikizia kesi, Kuwabadilishia watu kesi zao za msingi kwa sababu ya kushindwa kutoa rushwa hivyo kikao hicho kinapaswa kuwa na maamuzi na maadhimio yenye dira na taswira njema kwa jamii na Taifa kwa ujumla.

Amesisitiza pia Askari na Maafisa wa Polisi kutotumia taarifa za watu wanaohasiana kuwa ndio chanzo pekee cha msingi wa shtaka badala yake kufanya uchunguzi kwa kina na kujiridhisha vyema ili kufikia hukumu yenye tija Na haki kwa mtuhumiwa kwani kufanya hivyo kutaimarisha amani na jeshi la Polisi kupata taarifa nyingi za uhalifu kutoka kwa wananchi endapo watajikita katika haki.

Akizungumzia Vita dhidi ya Dawa za Kulevya Mhe Nchemba alisema kuwa serikali imefanikiwa kwa kiasi kikubwa kukamata na kuziteketeza Dawa za kulevya zilizopo mashambani ambapo ametilia msisitizo zaidi kwa Askari na Maafisa wa Jeshi la Polisi kuendelea kupambana ili kuzikamata Dawa za kulevya zilizopo katika viwanda.

Amesisitiza pia Jeshi la Polisi kuendelea kupambana na kubaini uhalifu sambamba na kushirikiana na vyombo vingine ili kuhakikisha lengo mahususi la serikali ambalo ni kuzuia uhalifu linafanikiwa kwa kiasi kikubwa.

Mhe Mwigulu amesema kuwa kauli mbiu ya Mwaka 2017 inayosema "ZINGATIA MAADILI TUNAPOPAMBANA NA UADILIFU ILI KUIMARISHA USALAMA KWA MAENDELEO YA TAIFA" endapo kama itatekelezwa kwa vitendo itaijenga nchi na kuzidi kudumisha zaidi amani iliyopo kwa wananchi.

Naye Kamanda wa Jeshi la Polisi nchini Ernest Mangu alisema kuwa kikao hicho cha kazi kwa Maafisa wa Jeshi la Polisi kina dhamira kubwa ya kufanya Tathmini ya utendaji wa mwaka 2016 na kuandaa mikakati mizuri ya mwaka 2017 na kupata fursa ya kubadilika kiutendaji kwa kuzingatia dhamira ya serikali ya awamu ya Tano inayoongozwa na Mhe Rais Dkt John Pombe Magufuli.

Hata hivyo amesisitiza zaidi askari wote nchini kutofanya kazi kwa mazoea, Kuacha Urasimu na kujenga uaminifu na weledi katika kazi.

Mangu amesema matendo ya Askari Polisi nchini yanapaswa kuwa mfano bora wa kuigwa katika jamii hivyo askari Polisi hapaswi kuwa chanzo cha vurugu au kujihusisha na matendo ovu yasiyostahili katika jamii.

Ameongeza kuwa miongoni mwa mambo yatakayopewa kipaombele kwa kujadiliwa katika Kikao hicho itakuwa ni pamoja na Vita dhidi ya Dawa za Kulevya, Vita dhidi ya Magendo, Vita dhidi ya ujangili na Uvuvi sambamba na Vita dhidi ya Ubambikizaji wa kesi kwa wananchi.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe Jordan Lugimbana akitoa salamu za Mkoa wa Dodoma kabla ya kumkaribisha Waziri Mwigulu Nchemba kuzungumza na askari hao amelipongeza jeshi la Polisi kwa kazi kubwa linayofanya ambapo pia ameeleza mpango wa Mkoa katika kupambana na migogoro ya ardhi kwa kuanzisha kamati maalumu ya wataalamu wa sheria kutoka chuo kikuu cha Dodoma (UDOM) Kupitia na kushauri ili kuweza kumaliza haraka migogoro hiyo.

Naye Makamu wa kwanza wa Rais na Waziri Mkuu Mstaafu Mzee John Samwel Malecela alisema kuwa jambo la msingi ambalo askari Polisi wanapaswa kulifanya ni pamoja na kuhakikisha kila mwananchi anapata Uhuru wake na kama jambo hilo likitekelezwa ipasavyo Fikra za Hayati Mwalimu J.K Nyerere zitakuwa zimeenziwa kwa weledi.

AGPAHI YAADHIMISHA KILELE CHA SIKU YA KIFUA KIKUU – MERERANI, MKOA WA MANYARA


 
Picha ya pamoja katika maadhimisho ya kifua kikuu -  Mererani.

Shirika lisilo la kiserikali la Ariel Glaser Pediatric AIDS Healthcare Initiative (AGPAHI) linalojishughulisha na mapambano dhidi ya Virusi Vya Ukimwi (VVU) na UKIMWI limeungana na wadau wote duniani katika maadhimisho ya siku ya kifua kikuu duniani, 24 March 2017.

Maadhimisho hayo yalifanyika katika mji mdogo wa Mererani, wilaya ya Simanjiro katika Mkoa wa Manyara, eneo ambalo Shirika la AGPAHI linatekeleza mradi wa kutoa huduma shirikishi za kifua kikuu na UKIMWI sehemu za migodini kwa hisani ya shirika la ADPP la Msumbiji.

Katika maadhimisho hayo, shirika la AGPAHI kwa kushirikiana na timu ya afya ya wilaya walifanya zoezi la kutoa huduma mbalimbali kwa jamiii inayozonguka mji mdogo wa Marerani kuanzia tarehe 23 – 25 Machi, 2017.

Huduma zilizotolewa ni uchunguzi wa kifua kikuu, kupima Virusi vya Ukimwi na kutoa elimu kwa umma kuhusu kifua kikuu na VVU/UKIMWI.

Zoezi hilo lilisimamiwa na afisa mradi wa kifua kikuu na UKIMWI, kutoka AGPAHI, mratibu wa kifua kikuu na ukoma wa wilaya ya Simanjiro, wataalamu wa maabara, watoa huduma wa Afya kutoka kituo cha Afya Mererani na wahudumu wa afya ngazi ya jamii.

Kauli mbiu ya mwaka huu katika maadhimisho ya siku ya kifua kikuu duniani ni; “TUUNGANE PAMOJA KUTOKOMEZA KIFUA KIKUU”.

Shirika la AGPAHI linafanya kazi katika mikoa sita ambayo ni Mwanza, Geita, Mara, Tanga Shinyanga na Simiyu. Huduma zitolewazo na shirika la AGPAHI ni kusaidia serikali kupitia vituo vya kutolea huduma za afya katika:

   1.Kutoa huduma za tiba na matunzo kwa watu
      wanaoishi na virusi vya UKIMWI;

   2.Kutoa huduma za kuzuia maambukizi ya virusi vya
      UKIMWI kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto;

   3.Kutoa huduma ya uchunguzi wa dalili za awali na
      huduma za awali za saratani ya mlango wa kizazi
      na

    4.Kutoa huduma shirikishi za kifua kikuu na UKIMWI
     sehemu za migodini.

Vilevile, shirika linafanya kazi katika mji mdogo wa mererani katika kutekeleza mradi wa kifua kikuu sehemu za migodini.

Matukio katika picha.

Afisa mradi wa Kifua kikuu na UKIMWI kutoka AGPAHI, Bi Alio Hussein akiwaelimisha na kugawa vipeperushi kwa wakazi wa Mererani kuhusu Kifua kikuu na VVU/UKIMWI.


Mhudumu wa afya ngazi ya jamii akiwaelezea wakazi wa Mererani dalili za Kifua Kikuu na namna ya kuweza kujikinga na maambukizi kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mwingine.


Wahudumu wa Afya ngazi ya jamii wakichukua maelezo ya baadhi wakazi wa Mererani waliokua tayari kuchunguzwa kama wana maambukizi ya vijidudu vya Kifua Kikuu.


Msanii wa Muziki wa Kizazi Kipya, Kajolii Maasai akitoa burudani na kuendelea kuwahimiza wakazi wa Mererani kuja kupata Elimu kuhusu Kifua Kikuu.


Elimu kwa wachimbaji wa madini ya Tanzanite kuhusu Kifua kikuu na VVU/UKIMWI ikiendelea.


Wachimbaji wa madini ya Tanzanite katika Kitalu D, wakiwa wamekusanyika kwa wingi wakielimishwa kuhusu Kifua kikuu na VVU/UKIMWI.


Bi. Alio Hussein akiwaonesha kwenye picha namna ambavyo vijidudu vya Kifua Kikuu vinaweza kusambaa kama mgonjwa atakohoa bila kuziba mdomo.


Wachimbaji wakielimishwa kuhusu aina za Kifua
Kikuu kwa njia ya bango.
Maswali mbalimbali yakiulizwa kwa wachimbaji juu ya kifua kikuu na UKIMWI.


Msanii wa Muziki wa Kizazi Kipya Kajolii Maasai akitoa burudani kwa wachimbaji wa Kitalu D waliokusanyika kwa wingi kuja kupata Elimu kuhusu Kifua Kikuu.


Mchimbaji wa madini ya Tanzanite akijibu swali lililoulizwa ikiwa ni mwendelezo wa kutoa elimu na uhamasishaji kuhusu Kifua kikuu na Ukimwi.


Wa kwanza kushoto ni Kajolii Maasai msanii wa muziki wa kizazi kipya, wa pili kushoto ni mchimbaji wa madini ya Tanzanite ambaye alijishindia Tishirt baada ya kujibu vizuri swali kuhusu Kifua kikuu na watatu kutoka kushoto ni Afisa mradi wa Kifua kikuu na UKIMWI, Bi Alio Hussein, na mwisho ni Mratibu wa Kifua kikuu na Ukoma Wilaya ya Simanjairo, Bi Selestina Rosai.


Na Joshua Fanuel wa Kilimanjaro Official blog,

Thursday, March 9, 2017

EfG YAADHIMISHA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI SOKO LA TEMEKE STERIO JIJINI DAR ES SALAAM


 Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Equality for Growth (EfG), Jane Magigita akizungumza na waandishi wa habari katika maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani yaliyofanyika Viwanja vya Soko la Temeke Sterio Dar es Salaam. Maadhimisho hayo yaliandaliwa na shirika hilo na kuhudhuriwa na wadau mbalimbali.
 Mjumbe wa Bodi ya EfG, akizungumza katika maadhimisho hayo.
 Balozi wa Ireland nchini Tanzania, Niall Morris akitoa hutuba 
yake kwenye maadhimisho hayo.
 Mkuu wa Dawati la Jinsia Kituo cha Polisi Chang'ombe, Mkaguzi wa Polisi, Meshack Mpwage, akihutubia kwa niaba ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Temeke ambaye alikuwa mgeni rasmi kwenye maadhimisho hayo. Kushoto ni Mwenyekiti wa muda wa muda wa wanawake wajasiriamali masokoni, Betty Mtewele na Balozi wa Ireland nchini Tanzania, Niall Morris.
 Kikundi cha Sanaa cha Machozi kikitoa burudani.
 Waananchi wakiwa kwenye maadhimisho hayo.
 Maadhimisho yakiendelea. wanawake wakiwa na mabango yenye maneno ya nafaa kuwa kiongozi.
 Meza kuu.
 Wafanyabiashara katika soko la Temeke Sterio wakifuatilia maadhimisho hayo.
 Burudani za sarakasi zikiendelea.

 Nifuraha tupu katika maadhimisho hayo.
 Hapa ni kuserebuka kwa kwenda mbele 'kweli ni wanawake na maendeleo'
 Vipeperushi juu.


Wasaidizi wa kisheria katika soko la Tabata Muslim jijini Dar es Salaam, Aisha Juma (kushoto) na Irene Daniel wakiwa kwenye maadhimisho hayo.
Picha ya pamoja na mgeni rasmi.

Na Dotto Mwaibale

TANZANIA ya Viwanda haitawezekana bila ya kuwepo wanawake wachapa kazi.

Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Equality for Growth (EfG), Jane Magigita wakati akizungumza 
na waandisi wa habari kwenye maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani yaliyofanyika viwanja vya Soko la 
Temeke Sterio Dar es Salaam.

Magigita alisema wanawake waliowengi ndio wanaoinua uchumi wa nchi kutokana na kujikita katika ujasiriamali hivyo bila ya 
kuwepo mpango mzima wa Tanzania ya Viwanda hautakuwepo. 

Alisema wanawake wanapaswa kuendelea na sera yao ya kuhamasishana na kuunda vikundi ili iwe rahisi kwao kupata mikopo yenye riba nafuu kutoka katika Taasisi za 
kifedha ili waweze kusonga mbele katika shughuli zao za ujasiriamali.

"Tunaiomba serikali katika bajeti zake itenge fungu maalumu kwa ajili ya wanawake" alisema Magigita.

Alisema kauli mbiu ya siku ya wanawake mwaka huu ni Tanzania ya Viwanda Wanawake ni Msingi wa Mabadiliko ya Uchumi.


Akizungumza kwa niaba ya Kamnada wa Polisi Mkoa wa Temeke, Mkuu wa Dawati la Jinsia wa Kituo hicho, Mkaguzi wa Polisi, 
Meshack Mpwage alisema jeshi la polisi litaendelea kushirikiana na wadau mbalimbali ili kukabiliana na vitendo vya ukati wa kijinsia masokoni na maeneo mengine.

"Jeshi la polisi kupitia dawati la jinsia tutaendelea kutoa ushirikiano na masuala yote yanyohusu ukatili wa kijinsia na hatutasita kumchukua hatua mkosaji" alisma Mpwage.

Balozi wa Ireland nchini Tanzania, Niall Morris alisema ukatili wa kijinsia upo duniani kote na si Tanzania pekee na umekuwa ukipingwa kwa nguvu zote.

"Matukio ya ukatili wa kijinsia yapo karibu duniani kote na yamekuwa yakipgiwa kelele kutoka na ukubwa wake hivyo ni wajibu wa kila mmoja wetu kuwa katika mapambano 

hayo" alisema Morris. 

(Imeandaliwa na mtandao wa www.habari za jamii.com-simu namba 0712-727062)