Pages

KAPIPI TV

Tuesday, March 7, 2017

MAANDALIZI YA TANZANIA DAY 2017 DALLAS TEXAS



Aprili 29, 2016, Mstahiki Meya wa jiji la Dallas, jimbo la Texas aliitangaza rasmi siku hiyo kuwa SIKU YA TANZANIA
Na mwaka huu, Jumuiya ya waTanzania waishio jimboni humo kwa kushirikiana na Baraza la waTanzania waishio nchini Marekani (Diaspora Council of Tanzanians in America) wanaandaa maadhimisho makubwa ya siku hiyo yatakayofanyika katika jiji la Dallas.
Viongozi Ben Kazora wa Jumuiya ya Dallas na Charles Bishota wa DICOTA wamezungumza na Mubelwa Bandio kuhusu maandalizi ya siku hiyo
KARIBU USIKILIZE

KUTOKA VOA SWAHILI:-ZULIA JEKUNDU

Zulia Jekundu ni kipindi cha televisheni cha kila wiki kinachotayarishwa na kutangazwa na Mkamiti Kibayasi toka Idhaa ya Kiswahili ya Sauti ya America (VOA)
Kipindi hiki hukuletea habari mbalimbali za burudani zinazotamba. Humu utapata kujua juu ya habari za mastaa zinazogonga vichwa vya habari, kujua baadhi ya wanaosherehekea siku zao za kuzaliwa wiki husika na hata filamu 5 zilizoongoza kwa mauzo katika wiki hiyo
Juma hili, video mpya ya Ariana Grande, mzozo mkali kati ya Nicki Minaj na Remy Na unavyoendelea, matatizo ya iPhone 7plus, The Weekend alipokutana na Drake Ujerumani, Obamas ndani ya New York, kuelekea siku ya kimataifa ya wanawake duniani na kadhalika
< br />

ULAJI WA VYAKULA NA KUTOFANYA MAZOEZI WACHANGIA ONGEZEKO LA MAGONJWA YASIYOAMBUKIZWA

 mkuu wa wilaya ya Arusha Gabriel Daqqaro akichukuliwa vipimo  mara baada ya kuzindua wiki ya wanawake duniani ambayo kwa mkoa wa Arusha imeathimishwa katika viwanja vya Sheikh Amri Abeid
 Muuandaaji ya wiki ya wanawake duniani kwa mkoa wa Arusha Phidesia Mwakitalima wa kwanza kulia  akishuhudua jinsi mkuu wa wilaya ya Arusha akiwa anachukuliwa vipimo vya afya yake




Mgeni Rasmi Mkuu wa wilaya ya Arusha Mh Gabriel Fabian Daqarro akiwa anaingia uwanjani tayari kwa  uzinduzi  Rasmi zoezi la kupima Moyo, Cancer, Kisukari, Macho, Magonjwa Sugu ya mfumo wa hewa Bure yanayofanyika Arusha katika Viwanja vya Sheikh Amri Abeid  yaliyoandaliwa na Phide Entertainment kushirikiana na wafadhili mbalimbali ambapo kilele chake ni siku ya wanawake duniani tar 8/3/2017

Habari picha na Woinde Shizza,Arusha
Tatizo la baadhi ya watanzania kula vyakula bila mpangilio na kutofanya mazoezi ili kulinda afya zao limechangia kwa kiasi kikubwa ongezeko la magonjwa ya kisukari ,kansa,na shinikizo la damu.

Hayo yalisemwa na mtaalamu wa magonjwa ya yasiyoambukizwa kutoka hospitali ya mkoa wa Arusha,Mt meru,Dk Beatrice Ngogi wakati wa zoezi la upimaji wa afya bure lililofanyika jana katika uwanja wa michezo wa Sheikh Amri Abeid jijini hapa.

Akihojiwa na waandishi wa habari mtaalamu huyo alisema asilimia kubwa ya kundi la watu walioathirika na magonjwa yasiyoambukizwa ni kati ya umri wa miaka 45-60 na kudai kuwa  mtindo wa maisha ya watu umechangia kwa kiasi kikubwa  ongezeko la magonjwa hayo.

“mtindo wa maisha umekuwa ni tatizo kubwa kwetu ndio maana tunawasihi watanzania tufanye mazoezi  na kuzingatia mlo wenye utaratibu”alisema mtaalamu huyo

Hatahivyo,mtaalamu wa magonjwa ya kisukari katika hospitali ya rufaa ya KCMC mkoani kilimanajro,DK Valeria Matei alisema kwamba  katika siku za karibuni watoto wadogo wanazaliwa wakiwa na ugonjwa wa kisukari mbali na wazee ambao ilikuwa imezoeleka.


Alisema kwamba elimu ya afya ni muhimu sana itolewe katika jamii ya watanzania kwa kuwa wengi wanakumbwa na ugonjwa huo bila kujijua na wakishajitambua ugonjwa huo unakuwa umeshawathiri kwa kiasi kikubwa.

Doroth Kuziwa, ambaye ni mwathirika wa ugonjwa wa kisukari alisema ya kwamba alikuwa kubaini kuathirika na ugonjwa huo kwa muda mrefu huku akisisitiza kwamba vyakula vya wagonjwa wengi wa kisukari vimekuwa ghali hali ambayo inawafanya washindwe kumudu gharama hizo.

Hatahivyo,Hiza Omary ambaye ni mgonjwa wa macho alisema kwamba aliacha kazi ya udereva kutokana na kusumbuliwa na matatizo ya macho huku akisema kwamba vyombo vya habari vina jukumu kubwa la kuhabarisha umma kuhusu elimu ya afya katika jamii.

Mkurugenzi wa kampuni ya Phide Entertainment,Phidesia Mwakitalima alisema kwamba kampuni yake imeingia mkataba na hospitali za KCMC  na Mt Meru kwa lengo la kufadhili  zoezi la upimaji wa afya bure kwa wakazi wa mkoa  wa Arusha  katika kuelekea siku ya wanawake duniani.

Alisema kwamba zoezi hilo litahitimishwa siku ya kilele cha siku ya mwanamke duniani  huku akisisitiza kundi la wanawake kuzingatia mfumo wa ulaji wa vyakula mbalimbali ili kuepuka magonjwa yasiyoambukizwa.

 mmoja wa madaktari wanaotoa huduma akiwa anachukuwa damu salama kutoka kwa mwananchi ambaye amejitolea kuchangia damu
 mmoja wa daktari akimpongeza mamaa mara baada ya kupimwa na kukutwa anaugongwa wa presha
Dokta kutoka katika hospiotali ya kcmc akitoa elimu kwa wamama waliouthuria kupata huduma ya kupimwa bure
Mkuu wa Wilaya ya Arusha Mh Gabriel Fabian Daqarro Akisaini Daftari la Wageni la Phide Entertainment baada ya Uzinduzi wa Zoezi la kupima buree wananchi Moyo, Cancer, Kisukari, Macho na Magonjwa sugu ya mfumo wa Hewa .. Pamoja na changizo la Damu kwa ajili ya Ward za Wazazi Mkoani Arusha

Sunday, March 5, 2017

WANANCHI WA MKOA WA ARUSHA WAJITOKEZA KWA KASI KUPATA UDUMA YA KUPIMA AFYA BURE SIKU YA WANAWAKE

 baadhi ya wananchi  wakichukuliwa vipimo vya afya na madaktari kutoka kcmc pamoja na Mounti meru Hospital ikiwa ni huduma inayotolewa bure katika viwanja vya kumbukumbu ya sheikh Amri Abeid katika wiki ya wanawake duniani  ambayo kwa mkoa wa Arusha imeandaliwa na Phide intantament
 baadhi ya wananchi wakiwa katika mstari wakisubiri kuchukuliwa vipimo vya magonjwa mbalimbali bure yakiwemo ,Kisukari ,Presha,Kansa  ,Ukimwi na mengineyo
mmoja wa madaktari akiendelea kupima mara baada ya kuchukuwa vipimo vya wagonjwa ndani  viwanja vya Sheikh Amri Abeid

 Na Woinde Shizza,Arusha
Maadhimisho ya wiki ya wanawake duniani yameanza rasmi mkoani Arusha  ambapo wananchi wa mkoa wa Arusha pamoja na vitongoji vyake wamepata fursa ya kupata huduma ya kupima magonjwa mbalimbali bure

zoezi hilo ambalo limeanza leo jijini hapa katika kiwanja cha sheikh Amri Abeid limeonekana kuwavuta wananchi wengi kwani zaidi ya wananchi 100 wamejotokeza kupima afya zao   bure katika viwanja hivyo

Akiongea na waandishi wa habari muandaaji wa maathimisho hayo ya wiki ya wananwake duniani kwa mkoa wa Arusha mkurugenzi wa Phide Intantament Phidesia Mwakitalima alisem akuwa muamko ni mzuri na wananchi wameanza kujitokeza kwa wingi 

Alisema kuwa pamoja ni siku ya kwanza tu lakini zaidi ya wananchi 100 wamejitokeza kupima afya zao  hivyo ni jambo zuri mno 

Alisema kumekuwepo na tabia ya wananchi wengi kutokuwa na  tabia ya kupima afya zao hadi pale wanapoumwa kitu ambacho sio kizuri na kuwataka wananchi  kujijengea tabia ya kupima afya zao mara kwa mara
Zoezi hili la kupima afya limeanza leo na linatarajiwa kumalizika march nane na huduma za kupima magonjwa mbalimbali na ushauri wa aina mbalimbali ikiwa ni pamoja na watu kuchangia damu unatolew bure hivyo ni wajibu wa kila mwananchi kutumia fursa hiii ili kujua afya yake

Wednesday, March 1, 2017

KUELEKEA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI,WANAWAKE WATAKIWA KUJIJENGEA TABIA YA KUPIMA AFYA ZAO


 Na  Woinde Shizza,Arusha

Wanawake wote hapa nchini wametakiwa kujijengea tabia ya kupima afya zao mara kwa mara ili kuweza kujua matatizo  ya mwili waliyonayo na kuyatatua  kabla ya madhara makubwa kutokea .

Hayo yamebainishwa leo na  mkurugenzi wa kampuni   ya Phide  entertaiment  Phidesia Mwakitalima wakati alipokuwa akiongea na waandishi wa habari juu ya maandalizi ya wiki   wanawake duniani ambayo inatarajia kuanza March mbili ambapo kwa mkoa wa Arusha maadhimisho hayo yanatarajiwa kufanyika kwa muda wa siku  saba katika viwanja vya kumbukumbu  ya sheikh Amri Abeid  .
Alisema kuwa wanawake wengi wamekuwa awana tabia ya kupima afya zao mara kwa mara  kitu ambacho ni hatari mno kwani maisha ya sasa ukilinganisha na hali ya tabia nchi ilivyo pamoja na vyakula ambavyo vinaliwa kwa kipindi hichi.
Alisema kuwa kutokana na tatizo hilo kuonekana hivyo  kampuni ya Phide entertaiment wameamua kuandaa kuandaa maadhimisho haya kwa kuwapa fursa wanawake kujitokeza kupima afya zao bure ambapo alisema  tukio zima litafanyika katika viwanja vya kumbukumbu ya Sheikh Amri Abeid  kwa muda wa siku saba  ambapo alisema kuwa maadhimisho haya yataanza rasmi  March 2 hadi March  nane.
" tamasha hili kubwa linawapa  fursa  wanawake kuweza  kupima Afya yako bure na magonjwa ambayo yatapimwa katika wiki hii ni pamoja na Moyo, Kisukari, Macho, na figo hivyo napenda kuwasihi wanawake wenzangu wote wajitokeze kwa wingi waje wapime afya zao  na wajijue vizuri "alisema Phide

Aidha alisema kuwa mbali  na kupima afya pia wiki hiyo itatumika kwa ajili ya kuwapa wanawake ushauri juu ya kupima afya zao mara kwa mara  ambapo watawapa elimu ya kutosha .

"unajua kipindi hichi wanawake wamekuwa wanapata magonjwa ya haina mbalimbali na wingine wamekuwa wanapuuzia kwenda hospitali kupima afya zao mara kwa mara hivyo tamasha hili la wiki nzima litatumika kuwaelimisha wanawake faida za kupima afya zao mara kwa mara"alisema Phide

Alimalizia kwa kuwataka wanawake wote kutopuuzia wiki hiii kwani ni muhimu sana kwa kujotokeza kupima afya zao na wajue mfumo mzima wa miiili yao ilivyo pamoja na kupata ushauri kutoka kwa wataalamu  wa afya .



AZANIA GROUP KUWAKILISHA TANZANIA KATIKA MASHINDANO YA A.MASHARIKI YA STANDARD CHARTERED

Timu ya Azania Group, ndiyo itakayowakilisha Tanzania katika mashindano ya kikanda ya Afrika Mashariki, ya Benki ya “Standard Chartered-Road to Anfield” yatakaofanyika uwanja wa Jakaya Kikwete Youth Park Jumamosi, Machi 4. 

Azania walipata ushindi huo kwa kuichakaza timu ya H&R Consultancy mabao ya 6-5 kwa penati dhidi ya katika mchezo wa kukata na shoka uliofanyika mwishoni mwa wiki na kufanikiwa kuipeperusha bendera ya Tanzania. 

Kwa maana hiyo, Azania Group wanatarajia kumenyana uso kwa uso na washindi wa michuano hiyo kutoka nchi za Kenya na Uganda. Washindi wa michuano hiyo nchini Uganda ni timu ya Cocacola wakati kidedea wa kombe hilo nchini Kenya ni Radio ya Capital FM.

Mtendaji Mkuu wa Benki ya Standard Chartered, Tanzania Sanjay Rughani (kushoto) na Mkuu wa Mahusiano na Masoko wa Benki hiyo, Juanita Mramba wakikabidhi kikombe kwa Bw Sikaba Hamisi ambaye ni Nahodha wa timu Azania Group, Mshindi wa kitaifa wa mashindano ya Kombe la Standard Chartered 2017 (Road to Anfield), mashindano yaliyofanyika mwishoni mwa wiki kwenye viwanja vya JK Youth Park, Gerezani jijini Dar es Salaam.
Akiongea na waandishi wa habari muda mfupi baada ya kutwaa ushindi huo, Nahodha wa Azania Group, Bw. Shabaka Hamisi alisema maandalizi yao mazuri ndiyo siri ya ushindi wao na kuongeza kwamba wapo tayari kuwanyoa hao wageni asubuhi kabisa. “Katika jambo lolote kama unataka kufanya vyema, maandalizi mazuri yanasaidia sana. 
Kwa upande wetu, tulifanya mazoezi yakutosha na ndiyo maana leo tumeibuka washindi.” Alisema. Aliongeza, “Siyo kwamba wenzetu walikua wabovu, ila umakini na utulivu kwa upande wa wachezaji wangu ndiyo kilichotusababishia kupata matokeo mazuri.” 

Alisema mazoezi ya kujipanga kwa ajili ya mechi tayari yameshaanza kwa ari na nguvu mpya, akiongeza kuwa ushindi kwao ni lazima. Kwa upande wake, Phillip David, nahodha wa H&R Consultancy alisema kukosekana kwa ukosefu wa umakini katika ushambuliaji ndiyo uliosababisha timu yake kupoteza mechi hiyo, hata hivyo alishukuru kwa kuibuka mshindi wa pili wa mashindano hayo.

Mtendaji Mkuu wa Benki ya Standard Chartered, Tanzania Sanjay Rughani (kushoto) na Mkuu wa Mahusiano na Masoko wa Benki hiyo, Juanita Mramba (kulia) wakifurahi katika picha ya pamoja na timu ya Azania Group wakikabidhi kikombe kwa timu Azania Group,Mshindi wa kitaifa wa mashindano ya Kombe la Standard Chartered 2017(Road to Anfield), mashindano yaliyofanyika mwishoni mwa wiki kwenye viwanja vya JK Youth Park,Gerezani jijini Dar es Salaam.
“Kama ulivyoona, mechi ilikuwa moja moja hadi tukaingia kwenye matuta. Wenzetu walipata penati sita wakati sisi tulifunga tano. Nafasi ya kushinda ilikuwa upande wetu lakini Mungu hakupenda iwe ivyo,” alisema. 

Mtendaji Mkuu wa Benki ya Standard Chartered Tanzania Limited, Sanjay Rughani aliwaasa wachezaji wa Azania Group kuwa wajiandae kikamilifu ili waubakishe ubingwa nchini Tanzania. “Sisi hakuna zawadi nzuri ambayo tunaitaka kutoka kwenu zaidi ushindi. 

Fanyeni mazoezi ya kutosha ili Jumamosi inayokuja muweze kushinda mechi zenu zote dhidi ya hizo timu kutoka Kenya na Uganda. Na sisi kama wadhamini tutakua pamoja nanyi ili kuhakikisha kwamba mnapata ushindi hapa nyumbani,” alisema Sanjay. Naye Mkuu wa Masoko na Uhusiano wa Benki hiyo, Juanita Mramba, aliwapongeza kwa ushindi huo lakini akiwatahadharisha kuwa safari yao ndiyo kwanza imeanza. 

“Leo mmeshinda mashindano haya, Jumamosi kazi yenu ni kubwa zaidi kwani mtacheza na wageni wawili, hivyo jipangeni vizuri zaidi mkiutumia vyema uwanja wa nyumbani,” alisema. 

Ukiachia mbali Azania ambao waliondoka na kombe za dhahabu, washindi wa pili H&R Consultancy walijitwalia kombe la shaba, huku washindi wa tatu PWC wakitwaa kombe la Bronze.

Mtendaji Mkuu wa Benki ya Standard Chartered, Tanzania Sanjay Rughani (kushoto) akikabidhi kombe kwa Nahodha wa timu ya HR Consultants, Phillip David ambao ni washindi wa pili wa mashindano ya Kombe la Standard Chartered 2017 (Road to Anfield), yaliyofanyika mwishoni mwa wiki kwenye viwanja vya JK Youth Park, Gerezani jijini Dar es Salaam. Anayeshuhudia tukio hilo ni Mkuu wa Wateja Binafsi wa Benki ya Standard Chartered, Michael Shio (kulia).

UNESCO KUENDELEA KUSAIDIA REDIO JAMII KUKUZA DEMOKRASIA

Shirika la Kimataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) limeahidi kuendelea kuzisaidia redio jamii kwa lengo la kuhakikisha sauti za wanyonge zinapazwa na kusikika ili kukuza demokrasia nchini. Akizungumza katika Mkutano Mkuu wa Mtandao wa Vyombo vya Habari Jamii Tanzania (COMNETA), 

Mkuu wa Ofisi na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), Zulmira Rodrigues alisema UNESCO alisema kuwa wakati umefika kwa wadau wa sekta ya habari kufikiri kwa kina namna ya kuhabarisha umma kwa kuangalia namna ya uwasilishaji ambapo kwa sasa changamoto kubwa ni kasi ya ukuaji wa teknolojia ya habari na namna ambapo redio zinaweza kushindana na vyombo vingine. 

Alisema kwa wanahabari wanapaswa kuwa makini na taarifa wazitoazo kwa jamii kwani kumekuwa na mazoea ya baadhi yao kuripoti habari bila kufanya uchuinguzi wa kina huku wakitumia chanzo kimoja cha habari badala ya kujiuliza maswali mengi ili kupata taarifa sahihi.
Mkuu wa Idara ya Mawasiliano na Habari wa UNESCO, Ofisi za Tanzania, Christophe Legay akizungumza machache wakati wa mkutano mkuu wa wajumbe wa Bodi ya Mtandao wa Vyombo vya Habari Jamii Tanzania (COMNETA) unaoendelea katika ukumbi wa Chuo Kikuu Huria (OUT) jijini Dar es Salaam.

Aliwashauri wanachama wa COMNETA, wawe na umoja, mshikamano na kupendana ili kuepuka migogoro inayoweza kuyumbisha ustawi wa mtandao huo. “Ninawaomba sana, COMNETA, muwe mfano wa kuigwa kwa kuepuka migongano ya wenyewe kwa wenyewe ikiwamo kugombea madaraka ili kuwa umoja wa mfano kwa katika tasnia ya vyombo vya habari hapa nchini’.

‘Vipindi mbalimbali vya kuhamasisha maendeleo vinavyorushwa na redio hii vimesaidia sana kuhamasisha wananchi na sasa mwamko wa maendeleo umekuwa mkubwa hapo Micheweni” alisema Zulmira Rodrigues
Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya COMNETA, Mohamed Tibanyendera akizungumza na wadau mbalimbali wa vyombo vya habari jamii waliokutana kwenye mkutano mkuu ili kujadili changamoto na kufanya uchaguzi wa viongozi wapya uliodhaminiwa na Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO).

Mwenyekiti wa Mtandao wa Vyombo vya Habari Jamii Tanzania-COMNETA, Prosper Kwigize alisema kuwa ipo changamoto kwa baadhi ya maafisa habari mikoani na wilayani kuleta urasimu mkubwa katika utoaji wa taarifa zinazohitajika kwa waandishi wa habari hivyo kukwamisha upatikanaji wa habri kwa umma. Pia kuna changamoto mbalimbali kwenye chama hicho hivyo ni vyema kuzitafutia suluhiso la msingi ili mtandao huwe imara.

Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya COMNETA, Mohamed Tibanyendera alisema kuwa kwa siku za nyuma redio ilikuwa ni chombo cha kuaminika katika utoaji wa habari hivyo kujijengea umaarufu na kuaminika zaidi tofauti na ilivyo sasa ambapo kuna upotoshaji mkubwa. Pia aliweza kuyatolea majibu maswali yaliyoulizwa na wajumbe wa bodi ya COMNETA ili kuimarisha uwajibikaji katika Mtandao wa Vyombo vya Habari Jamii Tanzania-COMNETA.
Mwenyekiti wa Bodi ya Mtandao wa Vyombo vya Habari Jamii Tanzania (COMNETA), Prosper Kwigize akizungumza na viongozi wa vyombo vya habari jamii wakati wa mkutano mkuu wa COMNETA unaondelea katika ukumbi wa Chuo Kikuu Huria (OUT) jijini Dar es Salaam.
Mjumbe wa Bodi ya Udhamini ya COMNETA, Balozi Christopher Liundi akizungumza jambo wakati wa mkutano mkuu Mtandao wa Vyombo vya Habari Jamii Tanzania (COMNETA) unaofanyika katika ukumbi wa Chuo Kikuu Huria (OUT) jijini Dar es Salaam chini ya udhamini wa UNESCO.
Katibu wa Bodi ya Mtandao wa Vyombo vya Habari Jamii Tanzania (COMNETA), Marco Mipawa akisoma marejesho kwenye mkutano mkuu unaondelea OUT jijini Dar es Salaam. Pichani juu na chini ni Baadhi ya Wajumbe wa Bodi ya COMNETA ambao pia ni Mameneja na wawakilishi wa vituo vya redio jamii nchini wakishiriki kutoa maoni kwenye mkutano mkuu wa COMNETA unaoendelea katika ukumbi wa Chuo Kikuu Huria (OUT) jijini Dar es Salaam.
Kutoka kushoto ni Afisa Programu wa Mawasiliano na Habari wa UNESCO, Nancy Kaizilege na Mkufunzi wa Redio Jamii UNESCO, Rose Haji Mwalimu wakirekodi mambo muhimu katika mkutano mkuu wa COMNETA unaoendelea jijini Dar es Salaam.
Mkutano ukiendelea.

BOHARI YA DAWA (MSD) YAPIGA HATUA KUWEZESHA UZALISHAJI DAWA KWA NJIA YA UBIA NA SEKTA BINAFSI (PPP)

 Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya Dawa (MSD), Bwana, Laurean Bwanakunu (kushoto) na Mkurugenzi wa Halmashauri  ya Mji wa Kibaha Bi.Jenifa Omolo wakibadilishana hati baada ya kusaini makubaliano ya umilikishwaji wa eneo la ardhi, lenye ukubwa wa mita za mraba 400,000 Dar es Salaam leo, ambayo itatumika kwa ajili ya ujenzi wa Kiwanda cha kuzalishia dawa na vifaa tiba Kibaha mkoani Pwani.

RHINO CEMENT TANGA YAKABIDHI MADAWATI 350 SHULE MSINGI KANGE TANGA



Tanga, MKUU wa  Wilaya ya Tanga, Thobias Mwalapwa, amekishukuru kiwanda cha Saruji cha Rhino  cha Tanga kwa msaada wake wa madawati 350 kwa shule ya Msingi ya Kange na mabenchi 10 kwa Zahanati iliyopo ndani ya kata hiyo.
Akizungumza wakati wa hafla fupi ya makabidhiano, Mwalapwa alisema msaada huo utaondosha kero ya wanafunzi darasani kukaa chini hivyo kutaka makampuni mengine kufuata nyayo za kiwanda hicho cha Rhino.
Amesema mabenchi 10 kwa Zahanati pia itaondosha kero kwa wagonjwa wanaofika kituoni na kuondosha kero ya foleni ya kukaa chini kusubiri huduma.
“Niseme kutoka moyoni nimepata faraja kubwa kwa ndugu zetu kutukumbuka jiwe moja kwa ndege wawili, madawati 350 kwa shule na mabenchi 10 kwa Zahanati, hili ni tukio jema la faraja” alisema Mwailapwa
Kwa upande wake Mkuu wa Kiwanda cha Saruji cha Rhino, Girish Gumar, amesema msaada huo wa madawati 350 na mabenchi kwa Zahanati uko na thamani zaidi ya milioni 45.
Alisema kiwanda cha Rhino kimekuwa kikisaidia katika Nyanja mbalimbali zikiwemo za Elimu, Afya, Mazingira na huduma nyengine za kijamii.  



Meneja Mkuu wa Kiwanda cha Saruji cha Rinho, Girish Kumar akimkabidhi Mkuu wa Wilaya ya Tanga, Thobias Mwalapwa moja ya madawati 350 kwa shule ya msingi ya Kange  kupunguza kero ya uhaba wa madawati kwa shule hiyo ambayo awali wanafunzi walikuwa wakisomea chini.









 Wanafunzi wa shule ya msingi ya Kange  Tanga wakipeleka madawati madarasani kati ya madawati  350 yaliyotolewa  na kiwanda cha Saruji cha Rinho jana. Shule hiyo ilikuwa ikikabiliwa na uhaba wa madawati na baadhi ya wanafunzi kulazimika kukaa chini
Habari kwa Hisani ya Blog ya Kijamii ya Tangakumekucha

Tuesday, February 7, 2017

WALIOGOMEA MAITI HOSPITALI YA AMANA JIJINI DAR ES SALAAM KWENDA KWA WAZIRI WA AFYA


Mama wa mtoto huyo, Julieth Daudi
Na Dotto Mwaibale

SAKATA la Julieth Daudi (19) mkazi wa Tabata Relini pamoja na ndugu zake kususia kuchukua mwili wa mtoto aliyejifungua kwa madai kuwa mtoto huyo hakuwa wake baada  ya kubadilishiwa na wauguzi wa Hospitali ya Amana katika Manispaa ya Ilala  jijini Dar es Salaam baada ya kujifungua limechua sura mpya kufuatia wazazi hao kutaka kwenda kumuona Waziri wa Afya kufikisha kilio chao.

Akizungumza na Jambo Leo nyumbani kwao  Dar es Salaam jana, Daudi alisema tunahitaji kwenda kumuona  Waziri waAfya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na 
Watoto, Ummy Mwalimu  kwa hatua zaidi kutokana na kitendo hicho walichofanyiwa na wauuguzi hao.

"Mimi pamoja na ndugu zangu tutakwenda kumuona waziri ili kumpelekea malalamiko yetu" alisema Daudi.

Akizungumzia mkasa huo Daudi alisema  alifika Hospitalini hapo Februari 2 jioni akiwa amesindikizwa na mama yake Veronica Lucas na shangazi yake Judith 
Christopher.

"Nilipofika daktari aliponipima aliniambia kuwa hasikii mapigo ya mtoto isipokuwa ya kwangu hivyo alishauri siku iliyofuata nipate kipimo cha utrasaund lakini kabla ya
kipimo hicho nilijisia uchungu na kujifungua" alisema Daudi.

Daudi alisema baada ya kupita muda kidogo muuguzi aliyemzalisha alimfuata na kumueleza kuwa mtoto wake alikuwa amefariki na alipomuuliza alikuwa wa jinsia 
gani muuguzi huyo alimweleza kuwa alikuwa hajui kama alikuwa wa kiume au wa kike.

Aliongeza kuwa wakati yupo wodini alimuona kijana mmoja aliyevalia koti la hospitali akiwa amembeba mtoto ambaye hakujua alikokuwa amempeleka.

Alisema baada ya kuambiwa mtoto wake amefariki aliomba aonyeshwe lakini hakuoneshwa tangu saa tatu asubuhi ambapo alilazimika kwenda kuomba simu kwa mlinzi wa hospitali hiyo na kuwajulisha ndugu zake walipofika nao waliomba kuonyeshwa mwili wa mtoto huyo bila mafanikio.

Shangazi wa Julieth Judith Christopher alisema baada ya kutokea tukio hilo walikwenda kumuona Mganga Mkuu wa Hospitali hiyo ambaye aliitisha kikao baina 
ya ndugu pamoja na maofisa wengine wa hospitali hiyo ambacho hakikufikia muafaka baada ya ndugu hao kukataa kuuchukua mwili wa mtoto huyo wakidai si wa kwao.

Aliongeza kuwa mganga mkuu huyo aliwaeleza kuwa mtoto huyo alikuwa amefia tumboni baada ya mimba hiyo kuharibika na ndiyo sababu mtoto huyo alizaliwa akiwa 
mfu.

"Wanafamilia tumegoma kuuchukua mwili wa mtoto huyo na maamuzi yaliyofikiwa ni kufanyika kipimo cha DNA"  alisema Christopher.

Alipopigiwa simu Muuguzi Mkuu wa Hospitali hiyo, Beauty Mwambebule alisema hawezi kulizungumzia tukio hilo kwenye simu njia ya simu badala yake alimtaka mwandishi wetu kwenda hospitali kupata undani wa jambo hilo.

(Imeandaliwa na mtandao wa www.habari za jamii.com-simu namba 0712-727062)

KAMPENI YA KUINUA MAADILI KITAIFA 2017,MARYLAND MAREKANI

Mtaalam wa Maendeleo ya Watu Mayrose Kavura Majinge akieleza umuhimu wa Kanuni ya Dhahabu "The Golden Rule" Katika kuondoa Ufisadi na maovu mbalimbali katika jamii yetu. Fuatilia Habari kamili: maadilikitaifa.blogspot.com
Profesa Nicholls Boas wa Chuo Kikuu Maryland Marekani akiwa miongoni mwa wadau Watanzania waishio Marekani akifurahia jambo wakati wa Siku Maalum ya Kuwezesha Kampeni ya Kuinua Maadili Kitaifa iliyofanyika Katika ukumbi wa Quality One Care, Maryland Marekani.
Baadhi ya wadau wa Kampeni ya Kuinua Maadili Kitaifa kutoka maeneo mbalimbali nchini Marekani wakifuatilia kwa makini Maudhui ya Siku Maalum ya Kuwezesha Kampeni ya Kuinua Maadili Kitaifa iliyofanyika Katika ukumbi wa Quality One Care Silver Spring, Maryland Nchini Marekani
Baadhi ya wadau wa Kampeni ya Kuinua Maadili Kitaifa kutoka maeneo mbalimbali nchini Marekani wakifuatilia kwa makini Maudhui ya Siku Maalum ya Kuwezesha Kampeni ya Kuinua Maadili Kitaifa iliyofanyika Katika ukumbi wa Quality One Care Silver Spring, Maryland Nchini Marekani.