Pages

KAPIPI TV

Wednesday, March 1, 2017

BOHARI YA DAWA (MSD) YAPIGA HATUA KUWEZESHA UZALISHAJI DAWA KWA NJIA YA UBIA NA SEKTA BINAFSI (PPP)

 Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya Dawa (MSD), Bwana, Laurean Bwanakunu (kushoto) na Mkurugenzi wa Halmashauri  ya Mji wa Kibaha Bi.Jenifa Omolo wakibadilishana hati baada ya kusaini makubaliano ya umilikishwaji wa eneo la ardhi, lenye ukubwa wa mita za mraba 400,000 Dar es Salaam leo, ambayo itatumika kwa ajili ya ujenzi wa Kiwanda cha kuzalishia dawa na vifaa tiba Kibaha mkoani Pwani.

RHINO CEMENT TANGA YAKABIDHI MADAWATI 350 SHULE MSINGI KANGE TANGA



Tanga, MKUU wa  Wilaya ya Tanga, Thobias Mwalapwa, amekishukuru kiwanda cha Saruji cha Rhino  cha Tanga kwa msaada wake wa madawati 350 kwa shule ya Msingi ya Kange na mabenchi 10 kwa Zahanati iliyopo ndani ya kata hiyo.
Akizungumza wakati wa hafla fupi ya makabidhiano, Mwalapwa alisema msaada huo utaondosha kero ya wanafunzi darasani kukaa chini hivyo kutaka makampuni mengine kufuata nyayo za kiwanda hicho cha Rhino.
Amesema mabenchi 10 kwa Zahanati pia itaondosha kero kwa wagonjwa wanaofika kituoni na kuondosha kero ya foleni ya kukaa chini kusubiri huduma.
“Niseme kutoka moyoni nimepata faraja kubwa kwa ndugu zetu kutukumbuka jiwe moja kwa ndege wawili, madawati 350 kwa shule na mabenchi 10 kwa Zahanati, hili ni tukio jema la faraja” alisema Mwailapwa
Kwa upande wake Mkuu wa Kiwanda cha Saruji cha Rhino, Girish Gumar, amesema msaada huo wa madawati 350 na mabenchi kwa Zahanati uko na thamani zaidi ya milioni 45.
Alisema kiwanda cha Rhino kimekuwa kikisaidia katika Nyanja mbalimbali zikiwemo za Elimu, Afya, Mazingira na huduma nyengine za kijamii.  



Meneja Mkuu wa Kiwanda cha Saruji cha Rinho, Girish Kumar akimkabidhi Mkuu wa Wilaya ya Tanga, Thobias Mwalapwa moja ya madawati 350 kwa shule ya msingi ya Kange  kupunguza kero ya uhaba wa madawati kwa shule hiyo ambayo awali wanafunzi walikuwa wakisomea chini.









 Wanafunzi wa shule ya msingi ya Kange  Tanga wakipeleka madawati madarasani kati ya madawati  350 yaliyotolewa  na kiwanda cha Saruji cha Rinho jana. Shule hiyo ilikuwa ikikabiliwa na uhaba wa madawati na baadhi ya wanafunzi kulazimika kukaa chini
Habari kwa Hisani ya Blog ya Kijamii ya Tangakumekucha

Tuesday, February 7, 2017

WALIOGOMEA MAITI HOSPITALI YA AMANA JIJINI DAR ES SALAAM KWENDA KWA WAZIRI WA AFYA


Mama wa mtoto huyo, Julieth Daudi
Na Dotto Mwaibale

SAKATA la Julieth Daudi (19) mkazi wa Tabata Relini pamoja na ndugu zake kususia kuchukua mwili wa mtoto aliyejifungua kwa madai kuwa mtoto huyo hakuwa wake baada  ya kubadilishiwa na wauguzi wa Hospitali ya Amana katika Manispaa ya Ilala  jijini Dar es Salaam baada ya kujifungua limechua sura mpya kufuatia wazazi hao kutaka kwenda kumuona Waziri wa Afya kufikisha kilio chao.

Akizungumza na Jambo Leo nyumbani kwao  Dar es Salaam jana, Daudi alisema tunahitaji kwenda kumuona  Waziri waAfya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na 
Watoto, Ummy Mwalimu  kwa hatua zaidi kutokana na kitendo hicho walichofanyiwa na wauuguzi hao.

"Mimi pamoja na ndugu zangu tutakwenda kumuona waziri ili kumpelekea malalamiko yetu" alisema Daudi.

Akizungumzia mkasa huo Daudi alisema  alifika Hospitalini hapo Februari 2 jioni akiwa amesindikizwa na mama yake Veronica Lucas na shangazi yake Judith 
Christopher.

"Nilipofika daktari aliponipima aliniambia kuwa hasikii mapigo ya mtoto isipokuwa ya kwangu hivyo alishauri siku iliyofuata nipate kipimo cha utrasaund lakini kabla ya
kipimo hicho nilijisia uchungu na kujifungua" alisema Daudi.

Daudi alisema baada ya kupita muda kidogo muuguzi aliyemzalisha alimfuata na kumueleza kuwa mtoto wake alikuwa amefariki na alipomuuliza alikuwa wa jinsia 
gani muuguzi huyo alimweleza kuwa alikuwa hajui kama alikuwa wa kiume au wa kike.

Aliongeza kuwa wakati yupo wodini alimuona kijana mmoja aliyevalia koti la hospitali akiwa amembeba mtoto ambaye hakujua alikokuwa amempeleka.

Alisema baada ya kuambiwa mtoto wake amefariki aliomba aonyeshwe lakini hakuoneshwa tangu saa tatu asubuhi ambapo alilazimika kwenda kuomba simu kwa mlinzi wa hospitali hiyo na kuwajulisha ndugu zake walipofika nao waliomba kuonyeshwa mwili wa mtoto huyo bila mafanikio.

Shangazi wa Julieth Judith Christopher alisema baada ya kutokea tukio hilo walikwenda kumuona Mganga Mkuu wa Hospitali hiyo ambaye aliitisha kikao baina 
ya ndugu pamoja na maofisa wengine wa hospitali hiyo ambacho hakikufikia muafaka baada ya ndugu hao kukataa kuuchukua mwili wa mtoto huyo wakidai si wa kwao.

Aliongeza kuwa mganga mkuu huyo aliwaeleza kuwa mtoto huyo alikuwa amefia tumboni baada ya mimba hiyo kuharibika na ndiyo sababu mtoto huyo alizaliwa akiwa 
mfu.

"Wanafamilia tumegoma kuuchukua mwili wa mtoto huyo na maamuzi yaliyofikiwa ni kufanyika kipimo cha DNA"  alisema Christopher.

Alipopigiwa simu Muuguzi Mkuu wa Hospitali hiyo, Beauty Mwambebule alisema hawezi kulizungumzia tukio hilo kwenye simu njia ya simu badala yake alimtaka mwandishi wetu kwenda hospitali kupata undani wa jambo hilo.

(Imeandaliwa na mtandao wa www.habari za jamii.com-simu namba 0712-727062)

KAMPENI YA KUINUA MAADILI KITAIFA 2017,MARYLAND MAREKANI

Mtaalam wa Maendeleo ya Watu Mayrose Kavura Majinge akieleza umuhimu wa Kanuni ya Dhahabu "The Golden Rule" Katika kuondoa Ufisadi na maovu mbalimbali katika jamii yetu. Fuatilia Habari kamili: maadilikitaifa.blogspot.com
Profesa Nicholls Boas wa Chuo Kikuu Maryland Marekani akiwa miongoni mwa wadau Watanzania waishio Marekani akifurahia jambo wakati wa Siku Maalum ya Kuwezesha Kampeni ya Kuinua Maadili Kitaifa iliyofanyika Katika ukumbi wa Quality One Care, Maryland Marekani.
Baadhi ya wadau wa Kampeni ya Kuinua Maadili Kitaifa kutoka maeneo mbalimbali nchini Marekani wakifuatilia kwa makini Maudhui ya Siku Maalum ya Kuwezesha Kampeni ya Kuinua Maadili Kitaifa iliyofanyika Katika ukumbi wa Quality One Care Silver Spring, Maryland Nchini Marekani
Baadhi ya wadau wa Kampeni ya Kuinua Maadili Kitaifa kutoka maeneo mbalimbali nchini Marekani wakifuatilia kwa makini Maudhui ya Siku Maalum ya Kuwezesha Kampeni ya Kuinua Maadili Kitaifa iliyofanyika Katika ukumbi wa Quality One Care Silver Spring, Maryland Nchini Marekani.

Thursday, January 26, 2017

DC UYUI AACHIA NGAZI,

Aliyekuwa mkuu wa wilaya ya Uyui Bw.Gabriel Mnyele akizungumza na Mwandishi wa habari wa Azam tv Juma Kapipi wakati akiwa ofisi za CCM Wilaya ya Uyui ikielezwa kuwa alikuwa ameitwa na Uongozi wa chama hicho kufuatia kuwepo kwa taarifa kwamba ameamua kuachia ngazi nafasi ya Ukuu wa wilaya hiyo ya Uyui jambo ambalo alilithibitisha kwa Katibu wa CCM wilaya ya Uyui kwamba ni kweli amemwandikia barua Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Bw.Gabriel Mnyele hakuwa tayari kuelezea maamuzi aliyochukua na kuwataka  Waandishi  waliokuwa wakihoji hatua ya maamuzi yake wasubiri tamko kutoka juu."Mimi sina la kusema kuhusu hilo nimeamua mwenyewe,kwani mmesikia kuwa nimetumbuliwa?Aliwahoji waandishi.


Monday, January 23, 2017

TAASISI YA AGRI-BUSNESS MEDIA INNITIATIVE YA JIJINI MWANZA YAWAHIMIZA VIJANA KUHUSU KILIMO

Mkurugenzi wa Taasisi ya Agri-Busness Media Innitiative In Tanzania (AMI-TZ) ya Jijini Mwanza, Deborah Mallaba, akikagua shamba la hekari mbili la taasisi hiyo ambalo lina mkusanyiko wa matunda na mbogamboga za aina mbalimbali, lililopo Igombe Ziwani, Manispaa ya Ilemela Jijini Mwanza.

Na Binagi Media Group
Taasisi ya AMI-TZ inajihusika na kilimo cha matunda na mbogamboga kama vile matikiti maji, nyanya, bamia, nyanya, pilipili mbuzi na aina nyinginezo nyingi.

Baada ya mavuno, taasisi hiyo hufanya usindikaji wa mazao kwa ajili ya kuwafikishia wateja wake majumbani, maofisini na mengine huuzwa moja kwa moja shambani.

"Baadhi ya vijana ukiwaeleza suala la kilimo wanakuona kama vile umepitwa na wakati lakini wale wanaojitambua wameingia kwenye kilimo na kinawalipa. Hivyo niwahamasishe watumie muda wao vizuri kwa kujishughulisha kwenye kilimo hivyo wasisubiri tu kazi za maofisini". Anasisitiza Deborah Mallaba, Mwanahabari na Mkurugenzi wa Taasisi ya AMI-TZ.

Mallaba anawasisitiza viongozi wa serikali kuanzia ngazi ya Kata hadi Wilaya, kuongeza jitihasa za kuwakusanya vijana pamoja na kuwapatia mitaji ikiwemo pembejeo ili wajikite kwenye kilimo maana kilimo ni biashara na kinalipa ambapo pia hatua hio itasaidia kupunguza vijana mitaani.

"Napenda kuwaambia akina dada waamuke maana si vyema kuzurura tu wakisema hakuna ajira. Mfano mimi nimeanza kujiwekea kipato changu kupitia kilimo na nataka kuwa mafano bora kwa vijana wengine". Anasisitiza < i>Aneth Shosha ambaye ni Afisa Masoko wa taasisi ya AMI-TZ huku akiwakaribisha vijana wengine kwenye taasisi hiyo ili wajifunze zaidi kuhusu kilimo.
Aneth Shosha ambaye ni Mratibu/ Afisa Masoko wa Taasisi ya Agri-Busness Media Innitiative In Tanzania (AMI-TZ), akimwagilia maji kwenye shamba la bamia
Wachapa kazi wakichakarika
Kilimo cha nyanya
Mfumo wa umwagiliaji kwa kutumia mashine kutoka Ziwa Victoria ndio hutumika kwenye shamba hili. 
Kwa msaada na ushauri, piga simu nambari 0754 99 66 13

KAMATI YA TAIFA YA MATUMIZI YA BIOTEKNOLOJIA SALAMA YARIDHISHWA NA UTAFITI WA MAHINDI KATIKA KITUO CHA MAKUTUPORA MKOANI DODOMA


Wajumbe wa Kamati ya Taifa ya Matumizi Salama ya Bioteknolojia (NBC), waandishi wa habari na watafiti wakielekea ukumbuni walipowasili Kituo cha Utafiti wa Kilimo cha Kanda ya Kati Makutupora mkoani Dodoma leo asubuhi kuangalia shamba la majaribio la mahindi yaliyotokana na teknolojia ya uhandisi jeni (GMO)
 Mkurugenzi wa Utafiti na Maendeleo wa Wizara ya Kilimo Mifugo na Uvuvi, Hussein Mansour akizungumza katika mkutano huo wakati akiwakaribisha wajumbe wa NBC katika kituo hicho cha utafiti wa kilimo cha Makutupora cha mkoani Dodoma.
Mshauri wa mradi wa Wema, Dk. Alois Kullaya (kkushoto), akitoa maelezo mafupi kwa wajumbe wa Kamati ya Taifa ya Matumizi Salama ya Bioteknolojia (NBC), kabla ya kuingia katika shamba la majaribio la mahindi yaliyoboreshwa kwa kutumia Teknolojia ya uhandisi jeni (GMO) chini ya mradi wa Wema katika Kituo cha Utafiti wa Kilimo cha Makutupora mjini Dodoma leo.
Waandishi wa habari, Lucy Ngowi wa gazeti la Habari Leo (kushoto), Dotto Mwaibale wa Jambo Leo (katikati) na Fatma Abdu wa Daily News wakijadiliana jambo katika shamba hilo la majaribio.
Mwonekano wa shamba hilo.
Mjumbe wa Kamati hiyo, Mhandisi Kissina kutoka Wizara ya Maji na Umwagiliaji, akiangalia hindi lililotokana na teknolojia hiyo.
Mshauri wa mradi wa Wema, Dk. Alois Kullaya (kulia), akitoa maelezo kwa wajumbe wa Kamati ya Taifa ya Matumizi Salama ya Bioteknolojia (NBC), kuhusu matumizi ya Teknolojia ya Uhandisi Jeni (GMO) walipotembelea shamba la majaribio la mahindi yaliyoboreshwa kwa kutumia Teknolojia ya uhandisi jeni (GMO) chini ya mradi wa Wema katika Kituo cha Utafiti wa Kilimo cha Makutupora mjini Dodoma leo.
Meneja wa shamba hilo, Bakar Mohamed akielezea kuhusu 
shamba hilo.

Safari ya kuelekea kuangalia shimo la kuchomea uchafu mbalimbali baada ya kufanya utafiti ikiendelea.
Wajumbe wa kamati hiyo na watafiti wa kilimo wakiangalia shimo la kuchomea uchafu mbalimbali baada ya kufanya utafiti huo.
Wajumbe wa kamati hiyo na watafiti wa kilimo wakiangalia shimo la kuchomea uchafu mbalimbali baada ya kufanya utafiti huo.
Mlinzi wa shamba hilo, Mbisi Masinga akiwa kazini.
Watafiti wa Kilimo na Wajumbe wa Kamati ya NBC wakiwa katika picha ya pamoja mbele ya shamba hilo.


Na Dotto Mwaibale, Dodoma

KAMATI ya Taifa ya Matumizi Salama ya Bioteknolojia (NBC) imeridhishwa na  matumizi ya Teknolojia ya Uhandisi Jeni (GMO) yenye lengo la kuwakwamua wakulima nchini.

Wajumbe wa kamati hiyo wakizungumza kwa nyakati tofauti na waandishi wa habari wakati walipotembelea shamba la majaribio la mahindi yaliyoboreshwa kwa kutumia Teknolojia ya uhandisi jeni (GMO) chini ya mradi wa Wema katika Kituo cha Utafiti wa Kilimo cha Makutupora mjini Dodoma leo walisema hatua iliyofikiwa na watafiti hao ni kubwa hivyo haipaswi kuachwa ikapotea bure. 

Elisa Moses kutoka Taasisi ya Chakula na Lishe ambaye ni mjumbe wa NBC alisema teknolojia hii ya bioteknolojia ni nzuri na inaonesha uhalisia halisi na inaweza kusaidia changamoto za ukosefu wa chakula iliyopo nchi.

"Binafsi nimefurahi kujionea hali halisi ya teknolojia hii hasa ninapoyaona mahindi haya ya GMO yalivyomakubwa kwani ni muhimu sana katika kukabiliana na ukame uliopo sehemu kubwa nchini" alisema Moses.

Mjumbe mwingine wa kamati hiyo kutoka Chemba ya Wanyabiashara Wenye Viwanda na Kilimo, Magdalene Mkocha alisema wamefurahi kuona jambo walilolipitisha linafanyiwa kazi vizuri na linaleta matumaini makubwa kutokana na matokeo ya jaribio hilo.

Alisema wadau wa sekta binafsi wanasubiri kwa hamu kuhusu matokeo hayo baada ya kuthibitishwa na takwimu za kisayansi kwani kwa kuangalia kwa macho mahindi yanaonekana ni bora zaidi.

Ofisa Habari na Mawasiliano wa Wizara ya Kilimo Mifugo na Uvuvi Kanda ya Kati Dodoma, Sebastian Kandira alisema hapo awali tafiti hizo zilikuwa hazifikishwi kwa wakulima ndio maana zilikuwa hazieleweki vizuri lakini hivi sasa wameanza kuzielewa kupitia vyombo mbalimbali vya habari.

Mkurugenzi wa Utafiti na Maendeleo Kanda ya Kati, Leon Mroso alisema wakati wanaanza majaribio hayo kulikuwa na changamoto nyingi kutokana na wadau kutokuwa na uelewa hasa kwa mahindi yaliyobadilishwa vinasaba kikubwa ni mshukuru Waziri wa Kilimo Mifugo na Uvuvi, Charles Tizeba  kwa kufika katika shamba hili la majaribio ambalo tulipanda mahindi Oktoba 5, mwaka jana na kutupa faraja kuwa kuna kila sababu ya kuharakisha matumizi ya teknolojia hiyo ili iweze kutumika kama zinazofanya nchi zingine zinazofanya tafiti za namna hiyo. 

TTCL YATOA MSAADA WA VIFAA VYA MAABARA KWA SHULE ZA SEKONDARI TABORA VYENYE THAMANI YA SHILINGI MILIONI SABA

Baadhi ya maafisa wa Kampuni ya Simu  Tanzania TTCL katika picha ya pamoja na wanafunzi wa Shule za Sekondari ya Tabora Wavulana na Wasichana nje ya Ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Tabora baada ya hafla fupi ya  TTCL kukabidhi msaada wa vifaa vya Maabara ya Sayansi kwa Shule za Sekondari za mkoa wa Tabora.
Mkuu wa mkoa wa Tabora Bw.Aggrey Mwanry akipokea msaada wa vifaa hivyo vya maabara ya Sayansi kutoka kwa Meneja wa TTCL tawi la Tabora Bw.James Mlaguzi,vifaa hivyo vinathamani ya shilingi milioni saba.
Meneja wa TTCL tawi la Tabora Bw.James Mlaguzi akisoma taarifa fupi ya kukabidhi msaada huo wa vifaa vya maabara vilivyogharimu jumla ya shilingi milioni saba.
Meneja wa TTCL tawi la Tabora Bw.James Mlaguzi akikabidhi taarifa aliyoisoma wakati wa kukabidhi vifaa hivyo vya maabara ya Sayansi kwa Shule za Sekondari kwa Mkuu wa mkoa wa Tabora Bw.Aggrey Mwanry.
Baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Tabora Wasichana wakiwa wamebeba masanduku ya vifaa vya maabara vilivyotolewa msaada na Kampuni ya Simu Tanzania TTCL

Baadhi ya maafisa wa TTCL wakati wa hafla fupi ya kukabidhi vifaa vya maabara ya sayansi vilivyokabidhiwa na Kampuni hiyo ya simu Tanzania.












Thursday, January 19, 2017

SERIKALI YAONYA WAWEKEZAJI WANAOCHOCHEA MIGOGORO

Na Woinde Shizza,Arusha.
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo amesema kuwa serikali haitasita
kuwachukulia hatua wawekezaji wanaochochea migogoro katika wilaya ya
Ngorongoro na kusababisha uvunjifu wa amani hivyo kuchangia kuzorota kwa
shughuli za maendeleo.



Gambo ameyasema hayo katika ziara yake wilayani Ngorongoro inayolenga
kutatua migogoro wa pori tengefu lenye ukumbwa wa kilomita za mraba elfu
kumi na tano ambapo amekutana na wadau mbalimbali ikiwemo
wawekezaji,wafugaji pamoja na viongozi wa kiserikali.



Amesema kuwa serikali itawaondoa wawekezaji wanaochochea migogoro na
kuwagombanisha wananchi na serikali yao jambo ambalo halitafumbiwa
macho



Mkuu wa Wilaya ya Ngorongoro Rashid Taka amesema kuwa wako baadhi ya watu
wanaonufaika na migogoro hiyo hivyo kumalizika kwa migogoro hiyo kutaleta
manufaa kwa wananchi wengi kuliko kunufaisha kundi la watu
wachache



Kwa upande wake Naibu Waziri wa Wizara ya Mifugo,Kilimo na Uvuvi  ambaye
pia ni Mbunge wa Ngorongoro Wiliam Ole Nasha na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa
Arusha  Lekule Laizer wamesema kuwa utatuzi wa mgogoro huo utasaidia
kuepusha migongano ya kimaslahi na kuchochea shughuli za kimaendeleo badala
ya kutumia muda mwingi katika usuluhishi wa miigogoro hiyo




Mkuu wa Mkoa ameanza Ziara yake leo Wilayani Ngorongo na kesho atatembelea
katika vijiji mbalimbali ikiwa ni katika juhudi za kutatua mgogoro wa pori
tengefu katika wilaya hiyo.

WAKUU WA MASHIRIKA YA UMEME KUTOKA NCHI KUMI ZA EASTERN AFRICA WAKUTANA ARUSHA


Na Woinde Shizza,Arusha

Wakuu wa  mashirika umeme kutoka katika nchi kumi za Afrika zinazozalisha
umeme(Eastern Africa Power pool(EAPP)          zimekutana  jijini arusha
kwa malengo ya kujadili mfumo wa usafirishaji wa umeme ikiwa ni pamoja na
namna wananchi wao watakavyoweza pata nishati ya umeme kwa uraisi tofauti na sasa

 

Hayo yalisemwa na naibu katibu mkuu wizara ya nishati na madini Dkt.Juliana palangyo alipokuwa akizungumza katika ufunguzi wa mkutano wa wakuu wa mashirika ya umeme katika nchi hizo za eastern Africa power
pool(eapp)mapema leo

 

Palangyo alisema kuwa lengo halisi ni kuweza kujadili mambo mbalimbali
yahusuyo nishati ya umeme kwa watumiaji wake kwani  kuna uwezekano  mkubwa wa nchi zote zilizo kwenye umoja huo.

 

Alisema kwa sasa yapo baadhi ya makampuni ambayo yalikuwa yanauza umeme kwa gharama kubwa hasa kwa wananchi ambao hawajapata huduma hiyo ya umeme lakini kupitia umoja huo wataweza kupata nishati hiyo kwa gharama nafuu.
 

"Hizi nchi za eastern tumekutana hapa ili tujadili namna ambayo tunaayo
wanayoweza kutafuta namna ya kuzalisha umeme kwa bei nafuu na kisha nchi
hiyo itaweza kuuza umeme  kwa bei ndogo"aliongeza palangyo.

 

Hata  hivyo kwa upande  kaimu meneja uhusiano wa shirika la tanesco  Leila
Muhaji alisema kuwa katika mkutano huo pia watajadili namna ambavyo
tanzania itajenga njia ya usafirishaji wa umeme wa njia ya maji ambayo
itatoka nchi ya tanzania kwenda kenya,zambia,pamoja na nchi nyingine

Muhaji alisema kuwa tanzania itanufaika na ujenzi wa njia hizo hivyo jamiii
itanufaika kwa kiwango kikubwa sana kama ilivyo kwenye nchi ambazo
zimeeendelea duniani.

 

"Hataivyo mara baada ya huu mkutano wa wakuu wa nchi zinazolisha umeme
tunatarajia pia kuwepo na wadau wengine ambao ni mawaziri kutoka nchi zote ambao nao sasa wataweza kuweka mambo sawa ili huduma iweze kumfikia mlengwa"aliongeza Muhaji

Alimalizia kwa kutaja nchi ambazo zina unda umoja huo kuwa ni  Tanzania ,Kenya,Uganda ,Rwanda ,Burundi ,Sudan , Dr congo, Ethiopia ,Djbout, Libya pamoja na Egypt.

SEMINA YA KUPEANA TAARIFA KUHUSU UTOAJI MIMBA USIO SALAMA

1
Mkurugenzi Mtendaji wa Chama Cha wanasheria wanawake TAWLA Bi Tike Mwambipile akifungua semina ya kuhamasisha wadau wa Kutetea haki za wanawake na kujadili madhara ya utoaji mimba usio salama hapa Tanzania kwa kushirikishana matokeo ya utafiti uliofanyika hivi karibuni wa matukio ya utoaji mimba usio salama pamoja na huduma za baada ya utoaji mimba usio salama hapa Tanzania.
2
Baadhi ya washiriki wa semina hiyo wakifuatilia mada kadhaa zilizokuwa zikitolewa katika semina hiyo.
3
Dk. Pensiens Mapunda Mhadhiri Mwandamizi wa Chuo Kikuu cha Afya na Tiba Hurbert Kairuki HKMU akielezea jambo wakati wa semina hiyo.
4
Baadhi ya washiriki wakisikiliza kwa makini mambo mbalimbali yaliyokuwa yakijadiliwa katika semina hiyo.
7
5
Washiriki wa semina hiyo wakiwa katika picha ya pamoja.
...........................................................................
Lengo la semina hii ni kujadili swala nyeti linaloigusa jamii yetu ya Kitanzania na wadau muhimu katika kutetea haki za wanawake katika kuhakikisha ustawi wa mwanamke unaendelea vizuri katika jamii yetu
Pamoja na kazi tunazofanya za kutoa huduma ya msaada na ushauri wa kisheria kwa wanawake na watoto, TAWLA imejikita pia katika kupigania haki za wanawake na usawa wa kijinsia hapa nchini ikiwemo Haki ya Afya ya Uzazi. Hii ni kwa sababu, TAWLA inatambua umuhimu wa haki za kijinsia na Afya ya Uzazi katika kuleta maendeleo ya kiuchumi na kijamii na zaidi sana kuondoa imani potofu kuhusu afya ya uzazi.
TAWLA kupitia vituo vyake vya msaada wa kisheria na mijadala ya kijamii (Community Conversation) tulipata taarifa za madhara na vifo vitokanavyo na utoaji mimba usio salama ambazo zilitushtusha na kutugusa sana na ndio maana tukaonelea kuwa ni vyema takafanya utafiti juu ya suala hili ili kuona ni kwa namna gani tunaweza kuisaidia jamii yetu kwa kushirikiana na wadau muhimu katika swala hili, ili kupunguza au kuondoa kabisa vifo vya akina mama na wasichana vitokanavyo na utoaji mimba usio salama.
Takwimu za tafiti ya Guttmacher zinaonyesha kwamba utoaji mimba usio salama ni sababu ya pili ya vifo vya akina mama na wasichana hapa nchini kwa maana kwamba:
(1) Kila mwaka wanawake wa Kitanzania 405,000 hutoa mimba kwa usiri karibu wote na kwamba 40% hupata matatizo ambayo yanahitaji matibabu:
(2) Kila mwaka wanawake wa Kitanzania milioni moja hupata mimba zisizotarajiwa ambazo 39% ya wanawake hao huishia kwenye utoaji mimba:
(3) 60% ya wanawake wa Tanzania wenye matatizo ya utoaji mimba hawapati huduma ya matibabu wanayoihitaji:
(4) Kila mwanamke 1 kati ya wanawake 5 nchini Tanzania ana mahitaji yasiyofikiwa ya uzazi wa mpango
Ni kwa misingi hiyo basi kongamano hili lina malengo makuu yafuatayo:
(1) kuhamasisha washiriki na kujadili madhara ya utoaji mimba usio salama hapa Tanzania kwa kushirikishana matokeo ya utafiti uliofanyika hivi karibuni wa matukio ya utoaji mimba usio salama pamoja na huduma za baada ya utoaji mimba usio salama hapa Tanzania:
(2) Kushirikishana matokeo ya utafiti uliofanyika hivi karibuni wa matukio ya utoaji mimba usio salama pamoja na huduma za baada ya utoaji mimba usio salama hapa Tanzania:
(3) Kubadilishana uzoefu:
(4) Kufanya uchechemuzi wa kuingizwa kwenye Sheria za Tanzania vipengele vinavyohusu haki ya Afya ya Uzazi vilivyopo kwenye Mkataba wa Nyongeza wa Afrika (Maputo Protocol) juu ya Haki za Wanawake:
(5) Kuwakutanisha wadau muhimu juu ya swala hili ili kujadili kuhusu Sheria na Sera zinazohusu Haki ya Afya ya Uzazi na utoaji mimba ulio salama hapa Tanzania.
Pamoja na madhumuni yaliyoiainisha hapo juu, semina hii inakusudia kutambua aina ya michango ambayo wadau mbali mbali waliopo hapa leo wanaweza kutoa katika kupunguza vifo vya akina mama vinavyotokana na utoaji mimba usio salama na madhara yake hapa Tanzania
Chama Cha Wanasheria Wanawake Tanzania kinaamini kwamba, kutambua Haki ya Afya ya Uzazi ni muhimu katika kufikia lengo la kupigania haki za wanawake na usawa wa kijinsia hapa nchini.. Lengo hili linaweza kukamilika endapo tu kila mmoja wetu katika ukumbi huu atajitoa katika kuhakikisha kuwa, wototo wetu wa kike, dada zetu, mama zetu na wanawake wote hapa nchini hawafi kwa sababu ya utoaji mimba usio salama.
Tunatambua kazi za Taasisi/ofisi zenu katika kuletea haki za binadamu, haki za wanawake na usawa wa kijinsia hapa Tanzania, ndio maana tumeomba ushiriki wenu ili kufanikisha lengo hili la kuleta haki katika jamii yetu.
Washiriki wa semina hii ni Baadhi ya wadau kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Wizara ya Katiba na Sheria na baadhi ya Asasi zisizo za kiraia zinazoshughulikia maswala ya haki za wanawake Nchini Tanzania.