Pages

KAPIPI TV

Wednesday, December 7, 2016

WAHARIRI WAKUTANA KUPITIA SHERIA YA HUDUMA YA VYOMBO VYA HABARI ILIYOPITISHWA NA BUNGE

 Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) Theophil Makunga (kulia), akizungumza Dar es Salaam leo wakati akifungua mkutano wa siku mbili wa wahariri  kupitia sheria ya huduma ya vyombo vya habari uliyopitishwa na Bunge pamoja na kujadili mpango mkakati wa TEF wa kuendeleza tasnia ya habari nchini. Kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa TEF, Deodatus Balile na Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko wa Habari Tanzania (TMF), Ernest Sungura.

NAPE NAUYE AWAPONGEZA TBN KWA UPASHAJI WA HABARI




Dar es Salaam, WAZIRI wa habari na Uenezi, Nape Nauye, amesema siri ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), kuingia madarakani ni mitandao ya kijamii.

Akifunga kongamano la mkutano mkuu wa Umoja wa Wanachama wa mitandao ya kijamii (blogeers), Nape alisema CCM imeingia madarakani baada ya kuandikwa kwa upana mkubwa katika mitandao ya kijamii.

Alisema mitandao ya kijamii iko na nafasi kubwa katika jamii ambapo asilimia kubwa ya Watanzania wanatumia mitandao ya kijamii ambapo habari nyingi wakati wa kampeni walikuwa wakisoma katika mitandao hiyo.

“Leo nitoe siri kwenu kuwa CCM kuingia madarakani ni ninyi mabloggers, hivyo nawapongezeni na niko nanyi bega kwa bega” alisema Nauye
Aliitaka mitandao hiyo kufuata maadili ya upashaji habari na kuepuka upotoshaji jambo ambalo linaweza kuwa hatari kwa jamii hivyo kuwataka kuzingatia taaluma hiyo.

                                          





Waendeshaji wamitandao ya kijamii (bloggers) wakipiga picha ya Selfie na Waziri wa habari na Uenezi mara baada ya kufunga kongamano la mkutano mkuu wa mwaka wa Tanzania Network (TBN) jijini Dar es Salaam.

MSD YAZINDUA HUDUMA MAALUMU KWA WATEJA WAKUBWA JIJINI DAR ES SALAAM


Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee naWatoto Dk. Mpoki Ulisubisya (kulia), akizungumza na viongozi mbalimbali wa sekta ya afya wakati akizindua mpango wa huduma maalumu kwa wateja wakubwa Dar es Salaam.

Wednesday, November 16, 2016

WAKALA WA HUDUMA ZA MISITU TANZANIA (TFS) WILAYA YA TEMEKE YATOA MADAWATI 80 KWA SHULE ZA MSINGI JIJINI DAR ES SALAAM

 Katibu Tawala wa Wilaya ya Temeke, Hashimu Komba (katikati), akikata utepe kwa niaba ya mkuu wa wilaya hiyo, kuashiria kupokea madawati 80 yaliyotolewa na Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) kwa Shule ya Msingi ya Kibasila Dar es Salaam jana. Wanaoshuhudia kutoka kulia ni Msaidizi wa Mkuu wa wilaya hiyo, Betha Minga, Meneja wa TFS Wilaya ya Temeke, Francis Kiondo na Mwakilishi wa Meneja wa TFS Kanda ya Mashariki, Mohamed Lyandama
Ofisa Mistu wa Wilaya ya Temeke, Fredrick Umilla (kulia), akizungumza katika hafla hiyo ya kukabidhi madawati.
Meneja wa TFS Wilaya ya Temeke, Francis Kiondo (kulia), akitoa taarifa kwa mgeni rasmi.
Meneja wa TFS Wilaya ya Temeke, Francis Kiondo (wa pili kulia), akimkabidhi mgeni rasmi, Hashim Komba  hati ya makabidhiano wa madawati hayo. Kutoka kushoto ni Msaidizi wa Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Betha Minga na Mwakilishi wa Meneja wa Kanda ya Mashariki wa TFS, Mohamed Lyandama.
Mgeni rasmi Hashim Komba akipanda mti wa kumbukumbu mbele ya ofisi ya TFS Wilaya ya Temeke iliyopo Chang'ombe Veta jijini Dar es Salaam.
Ofisa Elimu Vifaa na Takwimu wa Wilaya ya Temeke, Bakari Mrondwa akipanda mti.
Msaidizi wa Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Betha Minga 
akishiriki kupanda mti.
Wanafunzi wa Shule ya Msingi Wailes wakishiriki kupanda mti. Kulia ni Masha Hassan na Yahaya Hamza.
Mgeni rasmi akiwa katika picha ya pamoja na maofisa wa TFS Wilaya ya Temeke pamoja na wanafunzi wa Shule ya Msingi Wailes waliopokea madawati hayo kwa niaba ya wenzao.

Na Dotto Mwaibale

WAFANYAKAZI wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) Wilaya ya Temeke wametakiwa kuendelea kuwa waadilifu katika kazi zao za kila siku ili kujiepusha na vitendo vya rushwa kutoka kwa watu wanaojihusisha na uharamia wa mali asili ya nchi.

Mwito huo ulitolewa Dar es Salaam jana na Katibu Tawala wa Wilaya ya Temeke, Hashim Komba kwa niaba ya mkuu wa wilaya hiyo wakati akipokea madawati 80 yenye thamani ya sh.  6,370, 000 yaliyotolewa na TFS wilaya ya Temeke kwa ajili ya kukabiliana na uhaba wa madawati wilayani humo.

"Kwa hali halisi ninayoiona hapa ofisini kwenu najua ninyi ni waadilifu mnaviepuka vitendo vya rushwa endeleeni kusimamia kazi yenu ili kulinda mali asili ya taifa" alisema Komba.

Komba alisema kuwepo kwa magunia ya mkaa na mbao katika ofisi hiyo zilizokamatwa na kielelezo tosha kuwa hakuna vitendo vya rushwa vinavyofanywa na maofisa wa ofisi hiyo.

Komba amewaomba TFS kuendelea kuchangia madawati ili kumuunga mkono 
Rais Dk. John Magufuli ya kuhakikisha wanafunzi wanasoma bure na katika mazingira bora ikiwemo kukaa kwenye madawati.

Akitoa taarifa fupi wakati wa kukabidhi madawati hayo Meneja Wakala wa Huduma za Misitu Wilaya Tanzania (TFS) Wilaya ya Temeke, Francis Kiondo alisema wakala tangu kuanzishwa kwake wamepata mafanikio makubwa kupitia utekelezaji wa mpango mkakati wa kwanza wa miaka mitatu 2011 -2014 ambapo sasa wanaelekeza nguvu katika kutekeleza mpango mkakati wa pili wa miaka mitatu 2014 hadi 2016.

Alisema katika kutekeleza majukumu yake wakala imepata changamoto za uvamizi wa maeneo ya misitu kwa ajili ya kilimo, ufugaji, makazi, ukataji miti, uchimbaji madini na uchomaji moto misitu.

Alisema ili kukabiliana na changamoto hizo inatakiwa kuongeza watumishi na vitendea kazi na kujenga vituo katika kila msitu wa hifadhi na  kuweka mabango ya tahadhari.

Kiondo alisema kuwa wakala umetayarisha mpango bora wa usimamizi wa uhifadhi wa misitu na moja ya mikakati iliyopo kwenye mpango huo ni kupanda hekta 185,000 za miti kwa mwaka kwa kushirikiana na wadau ili kuziba pengo la mita za ujazo 19.5 milioni kwa mwaka za timbao hadi kufikia miaka 2030.


WATUMISHI WA UMMA WATAKIWA KUCHANGAMKIA NYUMBA ZA BEI NAFUU ZINAZOJENGWA NA SERIKALI

 Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Ujenzi  wa Nyumba za Watumishi wa Umma (WHC) Fredy Msemwa (katikati), akitoa taarifa kwa Waziri  wa Nchi, Ofisi ya Rais, Utumishi na Utawala Bora, Angella Kairuki (kushoto), kuhusu mradi wa ujenzi wa nyumba za watumishi wa Umma zinazojengwa Gezaulole Kigamboni jijini Dar es Salaam. Waziri Kairuki alikuwa katika ziara ya siku moja kutembelea miradi ya ujenzi ya Taasisi hiyo iliyopo Dar es Salaam. Kulia ni Mjumbe wa Bodi ya WHC, Daud Msangi.
 Mjumbe wa Bodi ya WHC, Daud Msangi akitoa taarifa kwa 
Waziri Kairuki.
 Waziri  wa Nchi, Ofisi ya Rais, Utumishi na Utawala Bora, Angella Kairuki (kushoto), akizungumza na watendaji wa mradi huo. Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni, Hashim Mgandilwa.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Ujenzi  wa Nyumba za Watumishi wa Umma (WHC) Fredy Msemwa (kushoto), akimuelekeza Waziri Kairuki jinsi ujenzi wa magorofa unavyoendelea katika mradi huo wa Gezaulole. Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni, Hashim Mgandilwa, Mjumbe wa Bodi ya WHC, Daud Msangi na Kaimu Meneja Miradi wa NSSF, Mhandisi Robert Wambura.
 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Utumishi na Utawala Bora, Angella Kairuki (katikati), akikagua nyumba zinazojengwa na Taasisi ya Ujenzi  wa Nyumba za Watumishi wa Umma (WHC) katika mradi ya Gezaulole Kigamboni Dar es Salaam leo asubuhi. Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa WHC, Fredy Msemwa na kulia kwake ni Mjumbe wa Bodi ya WHC, Agnes Meena.
 Waziri Kairuki (kushoto), akimuelekeza jambo Meneja Miradi wa NSSF, Mhandisi Robert Wambura wakati wa ziara hiyo.
 Wafanyakazi wa WHC, wakijadiliana jambo kwenye ziara hiyo.
 Ukaguzi wa mradi huo ukiendelea.

Msanifu Majengo kutoka Onspace Consult. Co.Ltd, Edmund Kahabuka (kulia), akitoa taarifa fupi ya mradi wa ujenzi wa Magomeni kwa Waziri Kairuki.
 Mwonekano wa ujenzi wa magorofa yanayo jengwa katika mradi huo wa Gezaulole Kigamboni.
 Mwonekano wa nyumba za chini zinazojengwa katika mradi huo.
 Mwonekano wa jengo la ghorofa la mradi huo baada ya kukamilika ujenzi wake.

Na Dotto Mwaibale

WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais, Utumishi na Utawala Bora, Angella Kairuki amewataka watumishi wa Umma kuchangamkia nyumba za bei nafuu zinazojengwa na Serikali ili kuondokana na changamoto ya makazi.

Katika hatua nyingine Kairuki ameiagiza Taasisi ya Ujenzi  wa Nyumba za Watumishi wa Umma (WHC), kuzingatia ujenzi utakaokidhi mahitaji ya watumishi wenye mishahara ya kima cha chini wakiwemo walinzi, wahudumu, madereva na makatibu muhtasi.

Kairuki aliyasema hayo Dar es Salaam jana alipofanya ziara kwenye mradi wa nyumba za WHC, zilizopo Kigamboni, Magomeni na Bunju jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kuangalia ujenzi unavyoendelea.

Alisema asilimia 80 ya watumishi wa serikali wana mishahara midogo hivyo endapo nyumba hizo zitauzwa kwa gharama kubwa hawataweza kuzinunua, na azma ya serikali ni kuwa na nyumba bora zenye gharama nafuu kwa watumishi wake.

"Kwa asilimia 80 ya watumishi wa umma kiwango watakachoweza kumudu kununua nyumba hizo hakiwezi kuzidi sh. milioni 20 kwa miaka 18, Tujitahidi kupunguza gharama kwa kadiri inavyowezekana ili kutoa fursa kwa watumishi wa umma wa kipato cha chini kuweza kupata nyumba za bei nafuu za kuishi" alisema.

Waziri huyo alisema azma ya serikali ni kuhakikisha wanaboresha na kujenga nyumba kwa ajili ya watumishi wa umma ambazo zinatakiwa ziwe sio chini ya nyumba 10,000.

Aliwataka WHC, kuwa na mpango mkakati wa kuweza kujenga nyumba zaidi ya 10,000 kwa mwaka ili kuwafikia watumishi wengi zaidi hasa waliopo vijijini.

Alisema katika manunuzi ya nyumba hizo serikali inaangalia jinsi ya kupunguza kodi ya ongezeko la thamani (VAT), ili kumpunguzia mtumishi gharama.

Nyumba hizo zinazojengwa kwa mkopo kutoka Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Mifuko ya Hifadhi ya Jamii na Pensheni zitauzwa kulingana na ukubwa wa nyumba husika kwani ile ya chumba kimoja itauzwa kwa sh.milioni 35, vyumba viwili milioni 75 na vyumba vitatu itauzwa sh.milioni 91.

Mkurugenzi Mtendaji wa WHC, Fredy Msemwa alisema katika eneo la Kigamboni lenye ekari 24 wanatarajia kujenga nyumba 790, mradi unaotekelezwa kwa awamu mbili.

Alisema katika nyumba za awamu ya kwanza wapo katika hatua ya umaliziaji ambapo nyumba hizo zinatarajia kukamilia Februari mwakani.

Nyumba hizo pia zinajengwa katika maeneo mbalimbali nchini, ambazo gharama zake ni kati ya sh. milioni 33 mpaka sh. milioni 190 pamoja na VAT.

Mwenyekiti wa Bodi ya WHC, Daud Msangi alielezea changamoto za mradi huo kuwa waliomba nyumba hizo zisiwe na vat, kupata viwanja bure na vya bei rahisi pamoja na serikali kuangalia huduma za maji, umeme na barabara.

Nyumba nyingine zimeanza kujengwa katika mikoa ya Morogoro, Mwanza, Dodoma, Mtwara, Lindi, Mbeya, Shinyanga, Singida na Arusha huku katika baadhi ya mikoa hiyo kukiwa na viwanja vya ujenzi huo.


WASAIDIZI WA KISHERIA WA SHIRIKA LA EfG WAUNGA JITIHADA ZA RAIS MAGUFULI KATIKA KUFANYA USAFI

Ofisa Ufuatiliaji na Tathmini wa Shirika la Equality for Growth (EfG), Shaban Rulimbiye (kushoto), akiwaongoza kufanya usafi Soko la Temeke Sterio Dar es Salaam mwishoni mwa wiki iliwa ni kuunga mkono jitihada za Rais Dk.John Magufuli katika suala zima la usafi wa mazingira.

WAJUMBE BARAZA LA WAWAKILISHI ZANZIBAR WATEMBELEA BANDARI YA TANGA

Tanga
WAJUMBE 14 wa Kamati ya Mawasiliano na Ujenzi Baraza la Uwakilishi  la Zanzibar wamesema  ujio wa  Mradi wa Bomba la Mafuta Tanga  litaongeza ajira kwa vijana wakiwemo Wanzanzibar waishio Tanga.
 
Wajumbe hao wakiongozwa na Mwenyekiti wa kamati hiyo, Hamza Hassan Juma walitembelea  bandari ya Tanga eneo la upakuzi wa shehena ya mizigo na eneo itakapojengwa bandari mpya ya Mwambani.
 
Akizungumza mara baada ya ziara hiyo,  Hassan alisema Serikali ya Zanzibar imejipanga kuimarisha bandari zake ikiwemo ya Wete na Mkoani Kisiwani Pemba ikiwa ni maandalizi ya ujio wa Bomba la Mafuta.
 
Akizungumzia  kilio cha wafanyabiashara na wasafiri wa Pemba na Tanga kwa kutumia usafiri wa baharini, Hassan alisema kero hiyo Serikali inaitambua na jitihada za kuwa na meli ya uhakika inafanywa.
 
Alisema kuna baadhi ya wafanyabiashara wa Pemba ambao walikuwa wakichukua bidhaa Tanga wamekatisha na baadhi yao mitaji kufa kutokana na kutokuwepo kwa usafiri wa uhakika wa baharini.
 
Awali akizungumza na wajumbe hao wa Baraza la Wawakilishi, Kaimu Meneja wa Badari Tanga, Henry Arika, alisema mchakato wa mradi wa bomba la mafuta unaenda kwa kasi na kuwataka wawekezaji kutoka Zanzibar kuja kuwekeza.
 
Alisema Tanga ziko fursa nyingi za uwekezaji  na yako maeneo mengi hivyo kupitia ujio wa mradi wa Bomba la mafuta amewataka wawekezaji wa ndani kuchangamkia.
                                       
Kaimu Meneja wa Bandari ya Tanga, Henry Arika (katikati) akitoa maelezo kwa wajumbe 14 wa Baraza la Wawakilishi kutoka Zanzibar walipotembelea bandari ya Tanga kujifunza


  Afisa Mtekelezaji Mkuu Bandari ya Tanga, Donald Kaire, akitoa maelezo kwa wajumbe wa Baraza la Wawakilishi wa Zanzibar walipofanya ziara bandari hiyo juzi. Katikati ni Kaimu Meneja wa Bandari ya Tanga, Henry Arika.

blog ya kijamii ya tangakumekuchablog 0655 902929

SERIKALI KUBORESHA MITAMBO YA KUCHAPISHA NYARAKA YA KIWANDA CHA UHAMIAJI KIJICHI JIJINI DAR ES SALAAM

 Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba, akizungumza na baadhi ya wananchi waliokuja kupata huduma Makao Makuu ya Idaya ya Uhamiaji wakati wa ziara yake ya siku moja aliyoifanya leo Kurasini jijini Dar es Salaam.

THBUB YASHUKURU UN KWA KUSAIDIA PROGRAMU ZA SHERIA

TUME ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB) imeshukuru Umoja wa Mataifa kwa msaada wake mkubwa inaotoa kwa taasisi zisizo za kiserikali za kujengea uwezo wa kuweza kutetea haki za binadamu nchini Tanzania.

Kauli hiyo imetolewa na Katibu Mtendaji wa THBUB, Mary Massay wakati wajumbe wa nchi za Nordic ambao ni wafadhili wakubwa wa programu za Umoja wa Mataifa zinazotekelezwa nchini Tanzania walipozuru katika ofisi hizo kwa mazungumzo.

“Kuna ongezeko kubwa la ufahamu kuhusu haki za binadamu, upatikanaji wa haki kwa makundi maalumu, uandishi wa habari kuhusu haki za binadamu na kuboreshwa kwa huduma za kisheria na ukaribu wa serikali wa kufanyakazi na wadau wa haki za binadamu,” alisema Massay akifafanua zaidi kuhusu manufaa ya ufadhili wa Umoja wa Mataifa katika kuboresha haki za binadamu nchini.
Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB), Mhe. Bahame Tom Nyanduga (wa pili kushoto) akitoa neno la ukaribisho kwa wajumbe kutoka nchi za Nordic walioambatana na wataalam kutoka mashirika ya Umoja wa Mataifa (hawapo pichani) ulipotembelea tume hiyo jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez (kushoto), Katibu Mtendaji wa THBUB, Mary Massay (wa pili kulia), Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Awa Dabo (kulia).(Picha zote na Zainul Mzige wa Modewjiblog)

Katika mazungumzo yao na ujumbe wa nchi za Nordic ambazo ni Sweden, Denmark, Norway Finland na Iceland kulikuwepo pia asasi mbalimbali zisizo za kiserikali kama Women’s Legal Aid Center, Tanzania Women Lawyers Association, Tanzania Women Judges Association, Legal Aid and Human Rights Center, Human Rights Defenders Coalition, na Tanganyika Law Society.

Katika mazungumzo hayo asasi hizo zilielezea ufanyaji kazi wao mafanikio na changamoto wanazokumbana nazo na umuhimu wa ufadhili wa mashirika ya Umoja wa Mataifa.

Akizungumzia changamoto zinazokabili Umoja wa Mataifa, serikali na asasi Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez alisema ipo haja ya kuwa na muono wa muda mrefu wa kuratibu shughuli zinazohusiana na maendeleo endelevu.

Katibu Mtendaji wa THBUB, Mary Massay akizungumzia shughuli mbalimbali zinazofanywa na tume hiyo kwa ujumbe kutoka nchi za Nordic ulioambatana na wataalam kutoka mashirika ya Umoja wa Mataifa (hawapo pichani) ulipotembelea tume hiyo.

Alisema kwamba mabadiliko ya kitabia kwa binadamu huchukua muda mrefu kukubalika hivyo ni wajibu wa kila mmoja kufanya bidii ya kuhakikisha kwamba maisha yanabadilika na watu wanakumbatia mambo ya kisasa yanayochochea maendeleo yao na jamii

Akizungumza kwa niaba ya wajumbe kutoka nchi hizo za Nordic, Anders Rönquist, ambaye ni kiongozi wa ushirikiano wa kimataifa wa Shirika la Misaada la Sweden (SIDA), alisema pamoja na changamoto zilizopo kitaasisi, kisiasa, kifedha na kitamaduni maendeleo yaliyopo katika sheria na haki za binadamu nchini Tanzania yanatia moyo sana.

Alisema ipo haja ya serikali kuendelea kuhimiza mabadiliko na kwamba wao wapo tayari kusaidia mkakati wa kuboresha masuala ya sheria na haki za binadamu.

Kiongozi wa ushirikiano wa kimataifa wa Shirika la Misaada la Sweden (SIDA), Anders Rönquist (kulia) akizungumza kwa niaba ya wajumbe kutoka nchi hizo za Nordic ulipotembelea ofisi za Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB) jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi mkazi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) Awa Dabo (kulia), akizungumza katika mkutano huo ambapo alishukuru mataifa hayo kwa kuendelea kusaidia programu za haki a binadamu nchini Tanzania. Alisema kwamba haki za binadamu ni kitu cha msingi katika maendeleo kwa kuwa hakuna maendeleo ya kweli bila kuwapo na haki za binadamu. Alisema kwamba maendeleo na haki za binadamu ni mambo yanayoshabihiana na kuimarika kwake kunasaidia kuimarisha ustawi wa jamii. Alishukuru pia serikali ya Tanzania kwa kuhakikisha kwamna masuala ya utawala bora na haki za binadamu yamo katika mpango wa miaka mitano wa maendeleo ambao unasaidiwa pia na UNDAP ll.
Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB), Mhe. Bahame Tom Nyanduga akisisitiza jambo kwenye mkutano na wajumbe kutoka nchi za Nordic walioambatana na wataalam kutoka mashirika ya Umoja wa Mataifa walipotembelea ofisi za Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB) jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Msaada wa Sheria kwa Wanawake na Watoto (WLAC), Theodosia Muhulo akielezea shughuli mbalimbali zinazofanywa na kituo chake katika kuhakikishwa wanawake na watoto wapata msaada wa kisheria wakati wa ziara ya wajumbe kutoka nchi za Nordic walioambatana na wataalam kutoka mashirika ya Umoja wa Mataifa walipotembelea ofisi za Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB) jijini Dar es Salaam.
Mwansheria kutoka Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC), Benedict Ishabakaki akizungumzia shughuli mbalimbali wanazofanya za msaada wa kisheria wakati wa ziara ya wajumbe kutoka nchi za Nordic walioambatana na wataalam kutoka mashirika ya Umoja wa Mataifa walipotembelea ofisi za Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB) jijini Dar es Salaam.
Jaji wa Mahakama Kuu na Makamu Mwenyekiti wa TAWLA, Sophia Wambura aki-'share' uzoefu wake katika masuala ya sheria wakati wa ziara ya wajumbe kutoka nchi za Nordic walioambatana na wataalam kutoka mashirika ya Umoja wa Mataifa walipotembelea ofisi za Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB) jijini Dar es Salaam.
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez akitoa neno la shukrani kwa Mwenyekiti wa THBUB wakati wa ziara ya wajumbe kutoka nchi za Nordic walioambatana na wataalam kutoka mashirika ya Umoja wa Mataifa walipotembelea ofisi za Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB) jijini Dar es Salaam.
Jaji wa Mahakama Kuu na Makamu Mwenyekiti wa TAWLA, Sophia Wambura akikabidhi zawadi kwa Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez (kulia) baada ya kumalizika mkutano wa wajumbe kutoka nchi za Nordic walioambatana na wataalam kutoka mashirika ya Umoja wa Mataifa walipotembelea ofisi za Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB) jijini Dar es Salaam.
Jaji Mstaafu wa Mahakama ya Rufaa, Eusebia Munuo akikabidhi zawadi kwa Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB), Mhe. Bahame Tom Nyanduga wakati wa ziara ya wajumbe kutoka nchi za Nordic walioambatana na wataalam kutoka mashirika ya Umoja wa Mataifa walipokutana na uongozi wa ofisi za Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB) jijini Dar es Salaam.
Picha juu na chini ni wajumbe kutoka nchi za Nordic walioambatana na wataalam kutoka mashirika ya Umoja wa Mataifa walipotembelea ofisi za Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB).



Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB), Mhe. Bahame Tom Nyanduga katika picha ya pamoja na wajumbe kutoka nchi za Nordic walioambatana na wataalam kutoka mashirika ya Umoja wa Mataifa walipotembelea ofisi za Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB) jijini Dar es Salaam.