Pages

KAPIPI TV

Monday, April 25, 2016

WAZAZI WAPONGEZA MAFANIKIO NEW ERA SEKONDARI

Na Allan Ntana, Tabora

WAZAZI Mkoani Tabora wamepongeza walimu na wafanyakazi wa shule ya Sekondari New Era iliyopo katika Manispaa ya Tabora kwa jitihada zao kubwa zilizowezesha shule hiyo kuwa na mafanikio makubwa kitaaluma tangu kuanzishwa kwake.

Pongezi hizo zimetolewa juzi katika mahafali ya 7 ya kidato cha sita yaliyofanyika shuleni hapo.

Walisema jitihada za walimu na watumishi wa shule hiyo zimewezesha watoto wao kuwa na nidhamu nzuri ikiwa ni pamoja na maendeleo mazuri kitaaluma.

'Kwa kweli nawapongeza sana walimu, mtoto wangu alikuwa na nidhamu mbovu sana lakini tokea ajiunge na shule hii tabia yake imebadilika, amekuwa mtoto mzuri hata nyumbani anafanya kazi kwa kujituma na hata maendeleo yake kitaaluma yamekuwa mazuri tofauti na alivyokuwa awali', alisema mzazi mmojawapo.

Mzazi mwingine aliyejitambulika kwa jina la mama Mary alisema shule hiyo sasa ina mazingira mazuri ya kusomea yanayowafanya watoto wasome kwa bidii, na kitendo cha kuanzisha shule ya awali na msingi katika shule hiyo kinawarahisishia wazazi hao, kwani mtoto anaweza kuanza chekechea hapo hapo na kuendelea hadi kidato cha sita tena kwa gharama nafuu.

Akitoa taarifa ya shule hiyo Mkuu wa shule Efel
Mbata alisema mafanikio makubwa ya shule hiyo ilianzishwa mwaka 2004
yamechochewa na ushirikiano mzuri wanaopata toka kwa wazazi wa watoto
wanaosoma shuleni hapo.

Alisema shule hiyo ilianzishwa mwaka 2004 ikiwa na kidato cha kwanza
lakini baada ya kupata mwitikio mkubwa wa wanafunzi kutokana na
ufundishaji mzuri wa walimu shuleni hapo walilazimika kuanzisha kidato
cha tano huku msukumo mkubwa ukitoka kwa wazazi wa watoto hao.

Alifafanua kuwa chachu kubwa ya mafanikio ya shule hiyo katika kipindi
hicho kifupi yanatokana na ushirikiano mzuri uliopo baina ya walimu na
wafanyakazi wengineo hali inayowafanya wanafunzi kujituma zaidi katika
masomo yao.

 Aidha alisema shule hiyo imekuwa na ongezeko kubwa la wanafunzi wa
kidato cha kwanza hadi cha sita kwa kipindi kifupi kutokana na huduma
bora za kitaaluma zinazotolewa shuleni hapo sambamba na uwepo wa
maabara za masomo yote ya sayansi tofauti na shule zingine.

Mbali na masomo yanayofundishwa kwa wanafunzi wa kidato cha kwanza
hadi cha nne, alitaja michepuo ya masomo inayofundishwa shuleni hapo
kwa wanafunzi wa kidato cha tano na sita kuwa ni PCB, PCM, ECA, CBG,
EGM, HE, CBM, HGL, HGK na HKL masomo ambayo yamewavuti wanafunzi wengi
zaidi.

Ili kuendelea kutoa huduma nzuri na taaluma bora kwa wanafunzi shuleni
hapo aliwataka wazazi wenye watoto katika shule hiyo kulipa ada kwa
wakati ili kufanikisha malengo mbalimbali ya shule hiyo.

Alitaja baadhi ya changamoto zinazoikabili shule yake kuwa ni upungufu
wa vitabu kwa baadhi ya masomo na vifaa vya maabara.</div>

BENKI YA CRDB YATANGAZA AJIRA KWA KIDATO CHA SITA JITEGEMEE JKT SHULE YA SEKONDARIBENKI

 Meneja wa Huduma Mbadala wa Benki ya CRDB,  Joseph Wite (katikati), akimkabidhi Mwenyekiti wa Bodi ya Shule ya Sekondari ya Jitegemee JKT, Brigedia Jenerali mstaafu Lawrence Magere (kushoto), hundi yenye thamani ya sh.milioni 2.5 kwa ajili ya kusaidia kujenga mifumo ya maji shuleni hapo katika Mahafali ya 22 ya kidato cha sita yaliyofanyika Dar es Salaam leo. Kulia ni Mkuu wa Shule hiyo, Luteni Kanali Robert Kessy.
 Wazazi na walezi wa wanafunzi hao wakiwa kwenye mahafali hayo.
Viongozi mbalimbali wakiwa na mgeni rasmi wakielekea ukumbini.
Maandamano ya wanafunzi hao yakielekea ukumbini.
Wimbo wa Taifa ukiimbwa.
Bendi  ya JKT ikitumbuiza.
Wimbo maalumu wa shule ukiimbwa.
Wanafunzi wa kidato cha sita wakiwa kwenye mahafali hayo.
Burudani zikiwa zimepamba moto.
Mkuu wa Shule, Luteni Kanali, Robert Kessy akizungumza kwenye mahafali hayo.
Mwenyekiti wa Bodi ya Shule ya Sekondari ya Jitegemee JKT, Brigedia Jenerali mstaafu Lawrence Magere akizungumza kwenye mahafali hayo.
 Meneja wa Huduma Mbadala wa Benki ya CRDB,  Joseph Wite (katikati), akizungumza katika mahafali hayo.
Mwenyekiti wa Bodi ya Shule, Brigedia Jenerali mstaafu Lawrence Magere (kushoto), akimkabidhi hundi iliyotolewa na CRDB, Mkuu wa shule hiyo, Luteni Kanali Robert Kessy.
Mkuu wa Shule akimkabishi cheki hiyo, Meja Rehema  Wanjara Msarifu wa Shule. Wengine kutoka kulia ni Makamu Mkuu wa Shule hiyo na Utawala, Kapteni Benitho na Mjumbe wa Bodi ya Shule, Sebastian Inosh.
Kwaito likiwa limepamba moto.
Hapa mwanafunzi Khalifa Chege aliyekuwa namba moja katika masomo akikabidhiwa zawadi.
Mwanafunzi Ibrahim Pazi aliyeshika nafasi ya pili katika masomo akikabidhiwa zawadi.



Dotto Mwaibale

BENKI ya CRDB imetangaza ajira kwa wanafunzi wa kidato cha sita katika Shule ya Sekondari ya Jitegemee JKT watakao pata divisheni one ya pointi tatu baada ya kufanya mtihani wa taifa.

Ofa hiyo ilitolewa na Meneja wa huduma mbadala wa Benki ya CRDB Joseph Wite kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa benki hiyo Dk. Charles Kimei katika mahafali ya 22 yaliyofanyika shuleni hapo Dar es Salaam jana.

Katika hatua nyingine Wite amewataka wanafunzi hao kutumia fursa ya ajira katika Jumuiya ya Afrika Mashariki kwani uwezekano upo endapo watafanya bidii katika masomo yao.

Alisema ni wakati wa vijana kuchangamkia fursa za ajira katika jumuiya ya Afrika Mashariki ili kuweza kufikia malengo na kuondokana na dhana ya kwamba hakuna ajira nchini.

"Pamoja na kwamba vijana wengi wanahofia kuajiriwa nje ya nchini kutokana na mambo mbalimbali ikiwemo kuogopa kwamba hawawezi kukidhi vigezo lakini mimi napenda kuwatoa hofu hiyo kwamba hata kama kiingereza huwezi kiswahili utashindwa kufundisha,"alisema Wite.

Aliwataka wanafunzi hao kuhakikisha kwamba wanajiepusha na matendo mabaya  ambayo yatapelekea kujiunga na madawa ya kulevya na kuhatarisha maisha yao.

Alisema mtu anapojiunga na madawa ya kulevya ana uwezekano mkubwa wa kupata magonjwa ya kuambukiza ikiwemo ukimwi.

"Janga la ukimwi halichagui mwenye nacho au asiye nacho ukicheza unahatarisha maisha hivyo ni vyena mjihadhari nalo ili muweze kufikia malengo,"alisema.

Hata hivyo aliendelea kusema kuwa benki hiyo inachangia  kwa kutambua asilimia moja ya faida wanayoipata kwa mwaka kwa sekta zinazopewa ikiwemo elimu na afya.

Pia alisema benki hiyo itaisaidia shule hiyo milioni 2.5 kwa ajili ya kuboresha mfumo wa maji safi.
 Mkuu wa Shule hiyo Luteni Kanali Robert Kessy alisema wanafunzi wanaohitimu katika mahafali hayo ya 22 ni 558.

Alisema wamewalea wanafunzi hao  katika maadili mazuri pamoja na kuwafundisha nyezo zote hivyo wanatarajia kwamba watafanya vizuri na kuwa mabalozi wazuri katika jamii.


Mmoja ya wazazi waliohudhuria mahafali hayo Hamisa Athumani aliipongeza shule hiyo kwa kufundisha masomo ya ukakamavu kwani yamewajengea uwezo wa kujiamini na kuwa na nidhamu. 

CHAMA CHA UDP CHAPATA PIGO VIGOGO WAKE WAWILI WAKIMBILIA CCK

 Katibu Mkuu wa Chama cha Kijamii (CCK), Renatus Muabhi (katikati), akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam leo wakati akiwapokea waliokuwa viongozi wa Chama cha UDP, waliokihama chama ambao ni  Salum Makunganya aliyekuwa Mwenyekiti wa UDP Mkoa wa Mtwara na Mkurugenzi wa Uchaguzi  Taifa na Mjumbe wa Halmshauri Kuu na Mwenyekiti wa UDP Mkoa wa Dar es Salaam na aliyekuwa Mjumbe wa Halmshauri Kuu ya chama hicho , Joachim Mwakitiga waliotangaza kujiondoa katika chama hicho na kujiunga CCK jijini Dar es Salaam leo asubuhi mbele ya waandishi wa habari.
 Mwenyekiti wa Wanawake CCK Taifa, Salama Juma (kulia), akizungumza wakati wa kuwapokea viongozi hao. Kushoto Salum Makunganya aliyekuwa Mwenyekiti wa UDP Mkoa wa Mtwara aliye hamia CCK. 
 Katibu Mkuu wa Chama cha Kijamii (CCK), Renatus Muabhi (kulia), akimkabidhi kadi ya chama hicho aliyekuwa Mwenyekiti wa UDP Mkoa wa Dar es Salaam, Joachim Mwakitiga aliyejiunga na chama hicho na aliyekuwa Mwenyekiti wa chama hicho Mkoa wa Mtwara, Salum Makunganya Dar es Salaam.
Katibu Mkuu wa Chama cha Kijamii (CCK), Renatus Muabhi (kulia), akimkabidhi kadi ya chama hicho aliyekuwa Mwenyekiti wa UDP Mkoa wa Mtwara, Salum Makunganya aliyehamia chama hicho.


Na Dotto Mwaibale


CHAMA cha United Democratic Party (UDP) kinachoongozwa na Mwenyekiti wake wa Taifa, John Momose Cheyo, kimepata pigo baada ya wenyeviti wawili wa mikoa ya Mtwara na Dar es 
Salaam kukihama na kujiunga na Chama Cha Kijamii (CCK).

Viongozi waliokihama chama hicho ni  Salum Makunganya ambaye alikuwa Mwenyekiti wa UDP Mkoa wa Mtwara,  Mkurugenzi wa Uchaguzi  Taifa na Mjumbe wa Halmshauri Kuu ya chama hicho na Mwenyekiti wa UDP Mkoa wa Dar es Salaam na Mjumbe wa Halmshauri Kuu, Joachim Mwakitiga waliotangaza kujiondoa katika chama hicho na kujiunga CCK leo jijini Dar es Salaam mbele ya waandishi wa 
habari.

Wenyeviti hao baada ya kujitoa walikabidhi kadi zao za UDP kwa Katibu Mkuu wa CCK, Renatus Muabhi ambaye naye aliwakabidi kadi ya CCK na kuwatangaza rasmi  kuwa wanachama wa chama hicho.

Makunganya alikabidi kadi yake ya UDP yenye namba 4544 na kukabidhiwa ya CCK namba 1597 huku Mwakitiga akibidhi kadi yake ya UDP namba 2852 na kukabidhi ya CCK yenye namba 01599 katika tukio lililofanyika ofisi za CCK.

Wakizungumzia sababu zilizowafanya wajitoe UDP walisema ni kutokana na chama hicho kutokuwa na mwelekeo wa kimaendeleo ambacho kwa zaidi ya miaka sita viongozi wake wa kitaifa hawajaitisha mikutano ukiwamo wa Halmashauri Kuu ya Taifa na Kamati Kuu.

Walisema sababu nyingine ni kwamba viongozi wa kitaifa wa UDP wamekigeuza chama hicho kama kampuni binafsi ambapo wamekuwa wakitoa maamuzi mbalimbali ambayo hayajaamuliwa na wanachama kwenye vikao .

“Nyie waandishi si mnaishi Dar es Salaam tangu lini mlishaona Mwenyekiti wa Taifa wa UDP, John Cheyo akiitisha hata mkutano wa hadhara hapa Dar es Salaam kuzungumzia mambo mbalimbali ya chama na taifa kwa ujumla kama vinavyofanya vyama vingine…jibu ni hakuna, UDP inabuka tu wakati wa uchaguzi na tena kwenye eneo moja tu,”alisema Mwakitiga.

Muabhi akizungumza baadhi baada ya kuwakabidhi kadi wenyeviti hao alisema CCK inawapokea kwa mikono miwili viongozi hao na kwamba wakiwa ndani ya chama hicho wataona utofauti na vyama vingine kwa kuwa chama kimejiwekea misingi ya kusikiliza kero za wananchi na kuzipatia ufumbuzi.

Muabhi aliitaka serikali kulitazama upya suala la vikao vya Bunge kutotangazwa kwenye vyombo vya habari kwa kuwa kufanya hivyo kunawanyima haki wananchi ya kupata habari na hivyo kushindwa kujua nini kinaendelea Bungeni.

“Serikali ijitathimini, wananchi wasipojua nini kinaendelea Bungeni kuna haja gani kwa wabunge ambao ndio wawakilishi wa wananchi kwenda Bungeni, wananchi watajuaje kama wawakilishi wao wamezifikisha kero zao serikalini,”alisema.

Mwenyekiti wa Wanawake CCK Taifa, Salama Juma, alisema ujio wa wanachama hao wapya ambao ni wakongwe katika siasa na hivyo CCK itajifunza mambo mengi kutoka kwao.

Sunday, April 24, 2016

MPANGO WA KUSAIDIA KAYA MASIKINI (PSSN) WABADILISHA MAISHA YA WANANCHI VIKUGE,KIBAHA

Natalia Kanem -TASAF Beneficiaries Kibaha
Mkurugenzi Mkazi Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Idadi ya Watu (UNFPA), Natalia Kanem (kulia) akifanya manunuzi ya bidhaa zinazotengenezwa na wanakijiji wa Vikuge ambao wamewezeshwa na mpango wa PSSN wa TASAF. (Picha na Modewjiblog)
Washirika wa maendeleo nchini wametembelea vijiji viwili Vikuge na Mwanabwito vilivyopo Wilayani Kibaha kwa ajili ya kutazama miradi ya kusaidia kaya masikini ambayo imeanzishwa kwa msaada wa fedha ambazo zinatolewa na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) ambapo washirika hao wamekuwa wakitoa fedha ili kusaidia miradi hiyo.
Washirika hao wa maendeleo kutoka UN Tanzania, Idara ya Maendeleo ya Kimataifa ya Serikali ya Uingereza (DFID), Irish Aid, USAID na Shirika la Kimataifa la Misaada la Sweden (SIDA) ambao wamekuwa wakishirikiana na TASAF katika Mpango wa Kusaidia Kaya Masikini (PSSN).
Wakitoa taarifa mbele ya washirika wa maendeleo, wanavikundi kutoka Kijiji cha Vikuge wamesema kuwa kupitia mpango huo wameweza kuboresha maisha yao tofauti na jinsi ilivyokuwa awali.
Walisema kuwa maisha yao ya awali yalikuwa magumu lakini kutokana na msaada walioupata kutoka TASAF wameweza kuanzisha vikundi ambavyo vinawasaidia kuboresha maisha kwa kufanya biashara za mazao, nguo na chakula.
“Kuna mafanikio tumeyapata darasani mahudhurio yameongezeka, klini wamama wanakwenda na hata utapiamlo haupo tena kwa watoto kwa sababu ya TASAF kutusaidia,” alisema mwakilishi wa wanavikundi kutoka Vikuge.
TASAF Kibaha
Mratibu TASAF Kibaha, Goodson Hare, akitoa neno la ukaribisho kwa ujumbe wa washirika wa maendeleo nchini waliotembelea vijiji viwili Vikuge na Mwanabwito vilivyopo Wilayani Kibaha kwa ajili ya kutazama miradi ya kusaidia kaya masikini ambayo imeanzishwa kwa msaada wa fedha ambazo zinatolewa na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF).
Akizungumzia ziara hiyo, Mratibu Mkazi wa Umoja wa MATAIFA NCHINI, Alvaro Rodriguez alisema wamefanya ziara hiyo ili kuona ni hatua gani imefikiwa na wanufaikaji na kuona ni changamoto gani bado zinawakabili.
“Tunaangalia changamoto zilizopo ili kuona ni jisni gani tunaweza kuwasaidia kama Mpango wa Kusaidia Kaya masikini ulivyo nab ado kuna wahitaji zaidi licha ya kuwa tumeshasaidia kaya Milioni1.1 kwa nchi nzima,
“Mpango huu ni mzuri na kawa wasaidiwa wakiwa kama wajasiliamali na kutengeneza kipato inaweza kusaidia Tanzania kuondokana na umasikini kuelekea katika uchumi wa kati kama jinsi ilivyojiwekea malengo,” alisema Rodriguez.
UN Resident Coordinator and UNDP Resident Representative in Tanzania, Mr. Alvaro Rodriguez
Kiongozi wa msafara wa washirika wa maendeleo nchini, Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez akizungumzia madhumuni ya ziara yao kwa wanakijiji.
DSC_0311
Mkurugenzi wa Programu Jamii wa TASAF, Amadeus Kamagenge akizungumza jambo wakati wa utambulisho wa ujumbe huo.
DSC_0183
Wanufaikaji wa mpango wa PSSN wakisoma risala kwa wageni.
DSC_0299
Mmoja wa wanufaikaji wa mpango wa PSSN akitoa maoni wakati wa mkutano na washirika wa maendeleo waliotembelea kijiji chao.
DSC_0321
Mwenyekiti kijiji cha Vikuge, Vitus Mchami akitoa salamu kwa niaba ya wanakijiji kwa ugeni huo.
DSC_0173
Baadhi ya wanakijiji cha Vikuge wanaonufaika na mradi wa PSSN waliohudhuria mkutano huo.
DSC_0145
Zoe Glorious (kulia) kutoka ofisi ya Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini akifanya mahojiano na Mnufaikaji wa kijiji cha Vikuge, Bi. Halima ambaye aliwezeshwa na mpango wa PSSN na kuanzisha biashara ya kufuga bata ambayo imemuwezesha kuendesha maisha yake na kumuingizia kipato.
DSC_0170
Bi Halima akiwa katika picha ya pamoja na mtoto wake wakati wa ziara ya washirika wa maendeleo nchini walipomtembelea nyumbani kwake.
DSC_0388
Mwakilishi wa Ubalozi wa Finland nchini, Milma Kettunen (kulia) akinunua moja ya bidhaa iliyotengenezwa na ukili kutoka kwa wakinamama wa kijiji cha Vikuge walionufaika na mpango wa PSSN na kujikwamua kiuchumi.
Natalia Kanem -TASAF Beneficiaries Kibaha
Mkurugenzi Mkazi Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Idadi ya Watu (UNFPA), Natalia Kanem (kulia) akifanya manunuzi ya bidhaa zinazotengenezwa na wanakijiji wa Vikuge ambao wamewezeshwa na mpango wa PSSN wa TASAF.
DSC_0413
Mwakilishi wa USAID, Daniel Moore akinunua kitamba cha Batiki kutoka kwa wanufaikaji wa mpango wa PSSN unaoendeshwa na TASAF wakati wa ziara ya kukagua miradi mbalimbali ya TASAF mkoa wa Pwani.
DSC_0375
Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo (UNDP) nchini, Awa Dabo (wa pili kushoto) na Mwakilishi wa Umoja wa Ulaya (EU), Eric Beaume wakimsikiliza mmoja wa wanakijiji cha Vikuge aliwezeshwa na mpango wa PSSN na kufanya biashara ya kilimo cha matunda na mazao mbalimbali. Wa kwanza kulia ni Mwenyekiti wa Vikuge,Vitus Mchami, anayefatia Mratibu TASAF Kibaha, Goodson Hare
DSC_0379
Baadhi ya Biashara za wananchi wa Vikuge walionufaika na mpanngo wa PSSN wa TASAF.
DSC_0717
DSC_0556
Baadhi ya wanakijiji wa Mwanabwito, Kibaha mkoa wa Pwani waliohudhuria mkutano wa washirika wa maendeleo.
DSC_0367
Mratibu TASAF wa wilaya ya Kibaha, Goodson Hare akizungumza jambo wakati wa kutizama biashara zinazofanywa na wajasiriamali walionufaika na mpango wa PSSN wa TASAF kutoka kijiji cha Vikuge, Kibaha.
DSC_0553
Ujumbe wa washirika wa maendeleo nchini akiwemo Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo (UNDP) nchini, Awa Dabo (kulia) wakiwasili kwenye kijiji cha Mwanabwito.
DSC_0518
Ujumbe wa washirika wa maendeleo nchini na viongozi wa TASAF katika picha ya pamoja walipotembelea shamba la miti katika kijiji cha Mwanabwito mkoani Pwani.
Usia Nkhoma Ledama
Afisa Habari wa kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC), Bi. Usia Nkhoma- Ledama (katikati) akifafanua jambo kwa baadhi ya wajumbe wa msafara wa washirika wa maendeleo nchini wakati wa ziara hiyo.

CLOUDS MEDIA GROUP IKIONGOZWA NA MD JOE KUSAGA YATEMBELEA NYUMBANI KWA BALOZI MANONGI,NEW YORK

Mwakilishi wa kudumu wa Ubalozi wa Tanzania Umoja wa Mataifa Mhe. Balozi Tovako Manongi akimkaribisha Mkurugenzi wa Clouds Media Group Joseph Kusaga nyumbani kwake siku ya Jumamosi April 23, 2016.
Mkurugenzi huyo alitembelea nyumbani kwa Balozi jijini New York akiongozana na baadhi ya wafanyakzi wake ambao walikuja nchini Marekani kwa ajili ya tamasha la Radio lililofanyika jijini Las Vegas. Picha na Vijimambo New York.
Mhe. Balozi Tuvako Manongi akiwatambulisha maafisa na wafanyakazi wa Ubalozi wa Tanzania Umoja wa Mataifa kwa Mkurugenzi wa Clouds Media Group, Bwn, Joseph Kusaga (hayupo pichani) siku ya Jumamosi April 23, 2016.
Mkurugenzi wa Clouds Media Group Bwn. Joseph Kusaga akitambulisha timu yake kwa Mhe. Balozi Tuvako Manongi.
Mhe. Balozi Tuvako Manongi, mwakilishi wa kudumu wa Ubalozi wa Tanzania Umoja wa Mataifa, New York akibadilishana mawazo na Mkurugenzi wa Clouds Media Group, Bwn. Joseph Kusaga.
Mkurugenzi wa Clouds Medea Group, Bwn. Joseph Kusaga akiwa katika picha ya pamoja na Mhe. Balozi Tuvako Manongi na mkewe.
Timu nzima ya Clouds Media Group iliyohudhuria Tamasha la Radio nchini Marekani ikiwa katika picha ya pamoja na Balozi Tuvako Manongi na mkewe.
Kutoka kushoto ni Saleh Mohammed, Daudu Lembuya, Dj Venture, Mhe. Balozi Tuvako Manongi, Mkurugenzi Joseph Kusaga, Mama Manongi, Dj Peter Moe na Jackson Joseph.
Kushoto ni Brightus Titus, Getrude Clement na NY Ebra wakiwa katika picha ya pamoja.

Siku hiyo pia lilifanyika kusanyiko la maDJ mbalimbali wa zamani waishio nchini Marekani ambao walikutana kwa nyama choma na kubadilishana mawazo. MaDj hawa ni wachache miongoni mwa wengi wanaounda kundi la Tanzania Djs Worldwide ambalo limeanza miezi mitatu iliyopita, na mpaka sasa lina wanachama wapatao 70. Kusanyiko lao la kwanza lilifanyika Escape One March 24 (lirejee hapa)

UZINDUZI WA TAMASHA LA KIMATAIFA LA FILAM LA TANZANITE MKOANI ARUSHA


 Waziri wa Habari,Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye akizungumza wakati wa uzinduzi wa tamasha la Kimataifa la Filamu la Tanzanite mkoani Arusha .

 Waziri Nape aliwaambia wadau na waigizaji wa Filamu waliohudhuria uzinduzi wa Tamasha hilo kuwa hii ni moja ya hatua kubwa kwenye historia ya filamu nchini na kuahidi Wizara yake itaendelea kutoa ushirikiano mkubwa na kuhakikisha haki za wasanii hazipotei wala haziliwi na wajanja.

 
 Mkurugenzi wa Tanzanite One ambao ndio wadhamini wakuu wa Tamasha, Ndugu Faisal Juma akizungumza wakati wa uzinduzi wa Tamasha la Kimataifa la Filamu la Tanzanite mjini Arusha kwenye hotel ya Mt. Meru
  Waziri wa Habari,Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye akifunua pazia kuashiria uzinduzi wa Tamasha la kimataifa la filamu la Tanzanite mjini Arusha.
  Waziri wa Habari,Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye (mwenye kaunda suti ya kijivu) akiwa pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Ndugu Felix Ntibenda  kwenye picha ya pamoja na viongozi pamoja na wadhamini kwenye uzinduzi wa Tamasha la Kimataifa la Filamu la Tanzanite.
 Viongozi wa Arusha wakiwa
 Baadhi ya watu waliohudhuria uzinduzi huo wa Tamasha la Filamu la Kimataifa la Tanzanite.
Yvonne Cherry 'Monalisa' pamoja na mama yake, Suzan Lewis 'Natasha' (katikati) wakifuatilia sherehe uzinduzi wa Tamasha la Filamu la Kimataifa la Tanzanite kwenye hotel ya Mt. Meru

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI