Pages

KAPIPI TV

Friday, February 12, 2016

MAWAZIRI WA ZAMANI MRAMBA, YONA WAENDELEA KUTUMIKIA ADHABU YA USAFI WA MAZINGIRA HOSPITALI YA PALESTINA SINZA JIJINI DAR ES SALAAM

 Waziri wa Fedha wa zamani, Basil Pesambili Mramba (kushoto), akijipangusa jasho wakati akienda kusaini fomu kwa Ofisa Afya Mazingira wa Hospitali ya Serikali ya Sinza Palestina, Miriam  Mong (kulia), baada ya kufanya usafi katika maeneo kadhaa ya hospitali hiyo Dar es Salaam leo asubuhi, ikiwa ni adhabu ya kutumikia kifungo cha nje hadi Novemba 5 mwaka huu.

Mawaziri wa Fedha wa zamani, Basil Mramba (kushoto) na Daniel Yona wakienda kusaini fomu kwa Ofisa Afya Mazingira wa Hospitali ya Serikali ya Sinza Palestina, Miriam  Mong baada ya kufanya usafi katika maeneo kadhaa ya hospitali hiyo Dar es Salaam leo asubuhi, ikiwa ni adhabu ya kutumikia kifungo cha nje hadi Novemba 5 mwaka huu.

Na Dotto Mwaibale

ALIYEKUWA Waziri wa Fedha, Basil Mramba na aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini Daniel Yona wanaendelea kutumikia kifungo cha nje kwa kufanya usafi katika Hospitali ya Sinza Palestina.

Yona na Mramba wanaendelea na hatua hiyo baada ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisuu kuridhia kutumikia kifungo hicho baada ya Magereza kuwasilisha orodha ya majina ya wafungwa ambapo wao ni miongoni mwa watu ambao walionekana kuweza kutumikia kifungo hicho cha nje  kitakachoisha Novemba 5 mwaka.

Akizungumza Dar es Salaam leo asubuhi, Ofisa Afya Mazingira wa Hospitali hiyo Miriam Mong ambaye pia anawasimamia alisema wamekuwa wakionesha ushirikiano katika kutimiza majuku waliyopatiwa.

"Wanaanza saa mbili asubuhi hadi saa nne, lakini wamekuwa wakionesha ushirikiano kila wanapofika katika kutimiza majukumu yao," alisema.

Alisema leo walifanya usafi katika maeneo mbalimbali ikiwemo ya kupigadeki katika makorido ya wodi ya wazazi na maeneo ya nje na kesho watafanya katika wodi ambayo wanatibiwa wagonjwa wa kuja na kuondoka OPD na wanafanya usafi kwa awamu," alisema.

Alisema endapo ikitokea wakafanya usafi katika eneo fulani ambalo halikung'aa  watalazimika kurudia.


WAZAZI KISARAWE WAFUNGUKA KUHUSU ADHABU KWA WATOTO

 Joseph Olowa akiiomba kampuni ya True Vision kusaidia kuelimisha watu wenye lugha za matusi hadharani  hivi karibuni wakati wa mdahalo maalum kuhusu adhabu kwa watoto ulioandaliwa na kampuni ya True Vision production kwa ajili ya kipindi cha redio cha Walinde Watoto wilayani kisarawe Mkoani Pwani
  Mtoto akionesha jeraha alilopata baada ya kuchapwa na baba yake alipokuwa mdogo hivi karibuni wakati wa mdahalo maalum kuhusu adhabu kwa watoto ulioandaliwa na kampuni ya True Vision production kwa ajili ya kipindi cha redio cha Walinde Watoto wilayani kisarawe Mkoani Pwani
Mkazi wa kisarawe  Juma Athumani akitoa ushuhuda wa adhabu ya kufukuza watoto nyumbani  hivi karibuni wakati wa mdahalo maalum kuhusu adhabu kwa watoto ulioandaliwa na kampuni ya True Vision production kwa ajili ya kipindi cha redio cha Walinde Watoto.
Cornel Anatory akielezea alivyomwagiwa maji ya ugali utotoni   hivi karibuni wakati wa mdahalo maalum kuhusu adhabu kwa watoto ulioandaliwa na kampuni ya True Vision production kwa ajili ya kipindi cha redio cha Walinde Watoto wilayani kisarawe Mkoani Pwani

Hamisi Idd akihamamisha wazazi kuwapa watoto elimu ya dini tangu utotoni ili kuepuka tabia mbaya hivi karibuni wakati wa mdahalo maalum kuhusu adhabu kwa watoto ulioandaliwa na kampuni ya True Vision production kwa ajili ya kipindi cha redio cha Walinde Watoto wilayani kisarawe Mkoani Pwani


Jamila Shabani akisema kuwa moja ya adhabu wanayopewa watoto ni kuchapwa fimbo    hivi karibuni wakati wa mdahalo maalum kuhusu adhabu kwa watoto ulioandaliwa na kampuni ya True Vision production kwa ajili ya kipindi cha redio cha Walinde Watoto wilayani kisarawe Mkoani Pwani

Kimela Billa Mtayarishaji wa vipindi vya Walinde Watoto akikabidhi Redio kwa Bi. Mwashamba Mrisho ambae ni mtendaji kata wa kata ya Kibo   hivi karibuni wakati wa mdahalo maalum kuhusu adhabu kwa watoto ulioandaliwa na kampuni ya True Vision production kwa ajili ya kipindi cha redio cha Walinde Watoto wilayani kisarawe Mkoani Pwani
Kikundi cha Kisarawe Bomani maarufu kama Kibo katika picha ya pamoja baada ya kupata redio kutoka True Vision hivi karibuni wakati wa mdahalo maalum kuhusu adhabu kwa watoto ulioandaliwa na kampuni ya True Vision production kwa ajili ya kipindi cha redio cha Walinde Watoto wilayani kisarawe Mkoani Pwani
Kikundi cha Tushirikiane cha Kisarawe wakijadiliana baada ya kupewa Redio na True Vision ili kufuatilia vipindi vya Walinde Watoto hivi karibuni wakati wa mdahalo maalum kuhusu adhabu kwa watoto ulioandaliwa na kampuni ya True Vision production kwa ajili ya kipindi cha redio cha Walinde Watoto wilayani kisarawe Mkoani Pwani

Na Krantz Mwantepele , Kisarawe 


Watanzania wametakiwa kuwa karibu na watoto wao na kujenga urafiki nao ili kuwawekea misingi bora ya nidhamu na upendo. Rai hiyo imetolewa na baadhi ya wazazi na walezi kutoka wilaya ya Kisarawe mkoani Pwani hivi karibuni wakati wa mdahalo maalum kuhusu adhabu kwa watoto ulioandaliwa na kampuni ya True Vision production kwa ajili ya kipindi cha redio cha Walinde Watoto.

Katika mdahalo huo mada mbalimbali zilijadiliwa zikiwemo athari za kuchapa watoto, matusi pamoja na adhabu kali kwa watoto mfano kuwafukuza watoto nyumbani.

Aidha washiriki wa mdahalo huo walionyesha kusikitishwa na vitendo vya kuchapa watoto fimbo kupita kiasi na wengine wakikemea tabia ya baadhi ya wazazi na walezi kutukana watoto pasipo kuzingatia maadili huku wakiiomba serikali kuwawajibisha wale wote wanaotukana hadharani bila kujali uwepo wa watoto.

Katika hatua nyingine, washiriki hao walikemea tabia ya kuwafukuza watoto nyumbani na kudai kuwa huo ni mwanzo wa kuwaingiza watoto katika matatizo makubwa na kuongeza idadi ya watoto wa mitaani aidha wamependekeza kuwa ni vyema watoto wafanyiwe maombi mara kwa mara na kuwashirikisha katika Ibada ili kuwaepusha kuwa na utovu wa nidhamu.

Kwa upande wao wanafunzi wa shule ya msingi Kibasila Kisarawe ambao walipata nafasi ya kuongea na timu ya Walinde Watoto walionyesha kuchukizwa na tabia ya kupewa adhabu kupita kiasi pamoja na kutukanwa tabia ambayo hufanywa na baadhi ya walimu na wazazi.


Naye mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi ya Kibasila Kisarawe Debora Mbalilaki alipendekeza kuangalia uwezekano wa kuwepo na adhabu mbadala badala ya fimbo kwa wanafunzi.




CHAMA CHA MPIRA WA MIGUU IRINGA (IRFA) KUJENGA UWANJA WA KISASA


kulia  ni mwenyekiti wa chama cha mpira wa miguu  mkoa wa Iringa Cyprian Kuyava akiwa na baadhi ya viongozi wa uwanja wa samora.


na fredy mgunda,iringa

Chama cha mpira wa miguu mkoa wa Iringa (IRFA) kiko mbioni kujenga uwanja wake wa kisasa utakaosaidia kuendeshea ligi mbalimbali zikiwemo ligi za kimataifa  hali itakayosaidia  kuinua soka la mkoa huo .

DK. KIGWANGALLA ASEMA ATAENDELEA KUMSAIDIA RAIS MAGUFULI KUTUMBUA MAJIPU YANAYOKWAMISHA UPATIKANAJI WA HUDUMA ZA AFYA

kigwa111

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Watoto na Wazee Dk. Hamisi Kigwangalla (aliyekaa) akiwa katika ibada maalum ya kuombea wagonjwa duniani iliyofanyika leo katika Hospitali ya Ndala,Nzega Mkoani Tabora. Wengine kulia ni Rudrovic Mwananzila na kushoto kwake ni Mkuu wa Wilaya ya Nzega, Jacqueline Liana.

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Watoto na Wazee Dk. Hamisi Kigwangalla amesema kwamba wao kama viongozi wataendelea kumsaidia Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Dkt. John Pombe Magufuli kutumbua majibu yanayokwamisha kutokupatikana kwa huduma bora za afya, bila kuogopa wala kumwonea mtu kwa ajili ya maslahi ya taifa.
Aidha Dkt. Kigwangalla alisema watafanya hivyo kwa kufuata sheria, kanuni na taratibu ili kuhakikisha kila mtu anatimiza wajibu ipasavyo.
Dk.Kigwangalla ameyasema hayo leo 11 Februari wakati wa maadhimisho ya 24 ya ibada maalum ya kuwaombea wagonjwa Duniani ambayo Kitaifa yamefanyika katika jimbo kuu la Tabora na baadae kwenye Hospitali ya Ndala, iliyopo Kata ya Ndala, Wilaya ya Nzega, mkoani Tabora.
“Tutaendelea kutumbua majibu bila ya kmwonea mtu kwa kuwa tunafanya hivyo kwa kuangalia sheria, kanuni na taratibu. Haiwezekani mtu akaiba dawa ambazo zinawasaidia wananchi masikini, halafu sisi tukamwaangalia tu,” alisema Dkt.Kigwangalla.
Alisema majipu hayo yatatumbuliwa kwa watendaji ambao watakaozembea, wasio waadilifu na wasiowajibika katika sekta hiyo ya afya.
Aliongeza kwamba Serikali ya Awamu ya Tano itakuwa inafanya kazi kwa kuwafuata wananchi hususani wanyonge (masikini) mahali walipo ili kuhakikisha baada ya miaka kumi ijayo Tanzania itakuwa na maendeleo ya kiwango cha juu.
Naibu Waziri huyo aliwaomba viongozi wa dini kuendelea kuwaombea kwa kuwa kazi ya kutumbua majibu si rahisi.
Aliuomba uongozi wa hospitali hiyo kuboresha mfumo wa ukusanyaji mapato kwa kutumia njia ya ki-elekroniki kwa sababu umeonyesha matokeo chanya katika hospitali nyinigine.
Akizungumzia kuhusu suala la upungufu wa bajeti, Dkt. Kigwangalla alisema ni vema viongozi hao wadini, asasi za kijamii na taasisi zisizo za kiserikali zinazotoa huduma za afya kutafuta vyanzo mbadala vya kuongeza fedha za kuboresha huduma hizo, kwa kuwa si sekta hiyo pekee yenye changamoto hiyo.
Pia vipaumbele vya shughuli mbalimbali za kuwaletea maendeleo wananchi viko vingi, wakati rasimali fedha haitoshelezi.
Aliwataka uongozi wa hospitali hiyo na nyinginezo za mashirika ya hiari kuwasilisha taarifa za (data cleaning) UTUMISHI ikiwa ni pamoja na kuorodhesha watumishi wanaotakiwa kuondolewa kwenye malipo ya mshahara ili waweze kupatiwa kibali cha kuajiri kwani bila kufanya hivyo kibali hakitaweza kutolewa.
Dkt. Kigwangalla aliongeza kwamba hivi sasa wizara yake iko katika mchakato wa kuhakikisha Watanzania wote wanapata huduma za matibabu za kwa kutumia mifuko ya bima ya afya.
Maadhimisho hayo ni ya kila mwaka ya siku 11 Februari, Wakristo wote wanafanya sala maalum ya kuwaombea wagonjwa wanaosumbuka na maradhi na kuwaombea wapone haraka huku wakiyapokea mateso hayo na kuyaunganisha na mateso ya kristo na kanisa lake hii ni pamoja na kuwaombea ndugu wa wagonjwa katika kuwasaidia wagonjwa wao wakati wa kuwauguza.
Maadhimisho hayo yanaenda sambamba pamoja na kuwahudumia na kutoa misasada mbalimbali.
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Ludocivk Mwananzila aliwataka Watanzania kuwa na tabia ya kuwatembelea wagonjwa na wafungwa ili waweze kupata faraja.
Kihistoria, Hospitali hiyo ya Ndala, ilianza miaka ya 1930 kama Zahanati ndogo chini ya Masista Wamissionary wa Afrika (Missionary of Our Lady of Afrika-White Sisters) katika jimbo kuu hilo la Tabora
Mwaka 1963 ilikuja kuwa Hospitali kamili huku ikianza na vitanda 115 na wauguzi 15 na daktari mmoja, hata hivyo hadi sasa ina jumla ya vitanda 152, wafanyakaz 125 huku wakiweza kutoa huduma kwa wagonjwa wa nje wapatao 38,917 na wagonjwa wa kulazwa 8,428.
Hospitali hiyo baadae ikapandishwa ngazi ya Hospitali huku ikiwa na vitanda 152 huku ikiwa na madaktari mbalimbali.
Wakitoa shukrani zao ni pamoja na serikali ya Tanzania kupitia Wizara ya Afya kwa kuweza kushirikiana bega kwa bega ikiwemo kutoa ruzuku kwa baadhi ya watumishi, posho za watumishi, vitanda vulivyohainishwa, madawa, mafunzo ya watumishi, na mambo mbalimbali.

kigwa3333Dk. Kigwangalla akitoa zawadi kwa mmoja wa akina mama waliokuwa kwenye wodi ya wazazi katika Hospitali ya Ndala, iliyopo Kata ya Ndala, Wilaya ya Nzega, mkoani Tabora.

KIGWA1Baadhi ya wananchi wakiwa katika tukio hilo. (Picha zote na Andrew Chale,modewjiblog-Nzega.)

Monday, February 8, 2016

DUNIA YAAGIZWA KUMALIZA UKEKETAJI 2030

FGM
WATENDAJI wakuu wa mashirika mawili makubwa ya Umoja wa Mataifa ya Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Idadi ya Watu Duniani (UNFPA) na Shirika la Kimataifa la Kuhudumia watoto (UNICEF) wametoa wito kwa dunia kujipanga vyema kumaliza kabisa tatizo la ukeketaji (FGM) ifikapo mwaka 2030.

Katika kauli zao walizotoa katika taarifa ya pamoja iliyotolewa na ofisi ya Mratibu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa mjini Dar es salaam watendaji hao Mkurugenzi Mtendaji wa UNFPA Dk. BabatundeOsotimehin, na Mkurugenzi Mtendaji wa UNCEF, Anthony Lake, wamesema ipo haja ya dunia kuadhimisha siku hiyo kwa kulenga kuwa na kiwango sifuri katika vitendo vya ukeketaji.

Mashirika hayo ya Umoja wa Mataifa yamesema kwamba ukeketaji ni vitendo vya kikatili vinavyowanyima wanawake haki yao ya msingi na kuwazuia kuchanua inavyostahili kama wanawake.

Viongozi hao wamesema kwamba vitendo vya ukeketaji vimesambaa duniani kote kuanzia Afrika, Mashariki ya Kati ambako imekuwa kama vitu vya kawaida vikiathiri pia familia katika nchi za Asia Australia, Ulaya, Amerika ya Kaskazini na Kusini.
Wamesema kwamba kama hatua zisipochukuliwa kutokomeza ukeketaji idadi ya mabinti na wanawake wanaoweza kuingizwa katika mkumbo huo itakuwa inaongezeka ikiwapeleka katika mzunguko ule ule wa kushamirisha ukeketaji na kurejesha nyuma maendeleo ya wanawake na binadamu kwa ujumla kama familia.

“ Ili kuhami utu wa mwanamke, tunahitaji kuchukua hatua sasa na kuwajibika kama dunia kutokomeza ukeketaji. “ ilisema sehemu ya taarifa ya viongozi hao kwa vyombo vya habari.

Septemba mwaka jana katika mkutano wa kutengeneza mpango wa kimataifa wa maendeleo endelevu, nchi 193 zilikubaliana kuhakikisha kwamba ukeketaji unakuw aumetokomezwa ifikapo mwaka 2030.

Taarifa hiyo imesema kwamba ili kufanikiwa wananchi wanatakiwa kushawishi familia nyingi duniani hapa kuachana na tabia ya ukeketaji.

“Tunahitaji kufanyakazi na idadi kubwa ya wataalamu wa tiba katika jamii zetu – wakiwemo waganga wa jadi na wataalamu wa kisasa wa matibabu, tukiwashawishi wakatae kutoa huduma ya ukeketaji.” Ilisema taarifa hiyo.

Aidha taarifa hiyo hiyo imetaka wanawake waliofanyiwa ukeketaji kusaidiwa huduma mbalimbali zikiwamo za kisaikolojia na nyingine zinazostahili ili kuwapunguzia maumivu waliyoyapata na wanayoendelea kuyapata kutokana na kukeketwa.

MRADI WA NG'OMBE KUWANUFAISHA WANAWAKE WA VIJIJINI WILAYANI NGORONGORO

  Mkuu wa Wilaya ya Ngorongoro Mhe. Hashim Mgandilwa akiongea na wakazi wa Ngorongoro wakati wa kukabidhi Ng'ombe hao
 Robert Kamakia kutoka shirika la PALISEP akimkabidhi Mkuu wa Wilaya Mhe. Hashim Mgandilwa risala kuhusu makabidhiano hayo. Theresia Irafay, Afisa Maendeleo ya Jamii wilaya ya Ngorongoro akizungumza wakati wa ugawaji wa Ng'ombe hao.
 Laurent Wambura kutoka shirika la Oxfam akizungumza wakati wa ugawaji wa Ng'ombe hao.
Mh. Hashim Mgandilwa, Mkuu wa wa Wilaya ya Ngorongoro akikabidhi Ng'ombe kwa wanawake wa wilaya ya Ngorongoro.
 Wakazi wa vijiji vya Enguserosambu, Naan, Ng’arwa na Orkiu Juu wakihudhuria ugawaji wa Ng'ombe uliofanyika katika kijiji cha Enguserosambu.
 Picha ya pamoja 

Wanawake wenye kipato cha chini kutoka vijiji vinne vya wilaya ya Ngorongoro wamekabidhiwa Ng’ombe ili kuwasaidia kuondokana na umasikini.

Wanawake hao wapatao 28 kutoka vijiji vya Enguserosambu, Naan, Ng’arwa na Orkiu Juu walichaguliwa kulingana na hali yao ngumu ya maisha inayowapelekea wakati mwingine kunyanyaswa kijinsia kupitia mfumo dume. Wanawake wengine 15 watakabidhiwa Ng’ombe wao mnamo mwezi Machi mwaka huu kufanya idadi ya wanufaika kufikia 43.

Makabidhiano hayo yaliyofanyika katika kijiji cha Enguserosambu yalihudhuriwa na  Mkuu wa Wilaya ya Ngorongoro, viongozi mbalimbali wa vijiji, pamoja na wakazi wa eneo hilo.

Akikabidhi Ng’ombe hao Mkuu wa Wilaya ya Ngorongoro Mhe. Hashim Mgandilwa aliwataka wanawake hao kuhifadhi vizuri mifugo hiyo ili iwasaidie kujikwamua kiuchumi kwa kuuza bidhaa zitokanazo na Ng’ombe ikiwemo maziwa. Aidha Mkuu huyo wa wilaya alitoa rai kwa viongozi wa vijiji hivyo kuhakikisha kwamba inapotokea misaada kama hii iwanufaishe walengwa ambao mara nyingi ni watu maskini ili kuwaepusha na balaa la njaa.

Ng’ombe hao wametolewa kama msaada na shirika la Oxfam kupitia wadau wake shirika la PALISEP.

Akizungumza katika hafla hiyo Meneja wa programu ya wafugaji wa Shirika la Oxfam ndugu Laurent Wambura alisema shirika lake limefanya hivi ili kuwainua kiuchumi wanawake wenye kipato cha chini na kubadilisha mtazamo wa jamii ione kwamba hata wanawake wanaweza kumiliki mali ikiwemo mifugo na kubadilisha kabisa maisha yao.

Naye Mkurugenzi wa shirika la PALISEP Robert Kamakia alisema lengo la mradi huo ni kuwezesha upatikanaji wa lishe bora na maziwa kwa familia zisizo na uwezo pamoja na kupunguza makali ya magonjwa kwa watoto kama vile utapiamlo.

Hii sio mara ya kwanza kwa shirika la Oxfam kugawa Ng’ombe katika wilaya ya Ngorongoro, mnamo mwaka 2014 wanawake wapatao 66 walinufaika na mradi huu kwa kugawiwa ngo’mbe mmoja jike kila mmoja huku viongozi wa vijiji vinne vya Enguserosambu, Naan, Ng’arwa na Orkiu Juu wakikabidhiwa madume 6 wa mbegu kama sehemu ya kuboresha mifugo ili kukidhi mahitaji ya soko. Ndama wote wanaozaliwa kama uzao wa kwanza wa Ng’ombe hawa hugawiwa kwa wanawake wengine wenye kipato cha chini hivyo kunufaisha jamii kubwa.

WAIMBAJI WA NYIMBO ZA INJILI WATUNUKIWA TUZO ZA HESHIMA KUTOKA CHUO KIKUU AFRICAN GRADUATE UNIVERSITY CHA JIJINI DAR ES SALAAM

Makamu Mkuu wa Chuo hicho, Askofu Profesa Stephano Nzowa akimvika kofia Mwimbaji wa nyimbo za injili, Stella Joel wakati akimtunuku Tuzo ya Heshima ya Shahada ya Uzamili ya Mahusiano katika mahafali hayo. Kushoto ni Mkuu wa Chuo hicho kutoka nchini Zambia, Profesa Timothy Kazembe.



Hapa Stella Joel akipongezwa na ndugu yake.
Mkuu wa Chuo hicho kutoka nchini Zambia, Profesa Timothy Kazembe akimvika kofia Rais wa Shirikisho la Muziki Tanzania, Ado Novemba wakati akimtunuku tuzo ya heshima ya udaktari. Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Ushindani Tanzania (FCC), Dk.Fredrick Ringo akimkabidhi tuzo hiyo.
Waimbaji wa nyimbo za injili, Stella Joel (kulia) ambaye ametunukiwa Tuzo ya Heshima ya Shahada ya Uzamili ya Mahusiano na mwenzake Upendo Mbila (kushoto), aliyetunukiwa Tuzo ya Heshima ya Shahada ya Uzamili ya Uongozi wa Umma wakiteta jambo kwenye mahafali hayo ya pili ya Chuo cha African Graduate University yaliyofanyika Dar es Salaam juzi.
Wahitimu wakiwa katika picha ya pamoja.
Paul Mbila (kulia), akimvika taji mama yake Upendo Mbila ambaye ni mwimbaji wa nyimbo za injili baada ya kutunukiwa tuzo Heshima ya Shahada ya Uzamili ya Uongozi wa Umma.

Na Dotto Mwaibale

Chuo Kikuu cha African Graduate University kimewatunuku tuzo za heshima za stashahada ya uzamili katika ngazi mbalimbali waimbaji wa nyimbo za injili nchini kutokana na mchango wao katika jamii.

Akizungumza wakati wa kukabidhi tuzo hizo kwa waimbaji hao katika mahafali ya pili ya chuo hicho yaliyofanyika Dar es Salaam juzi Makamu Mkuu wa Chuo hicho, Askofu Profesa Stephano Nzowa alisema ni jambo jema kuwakumbuka watu mbalimbali waliolifanyia taifa mambo mazuri.

"Chuo chetu kimeona ni vema kikawapa tuzo za heshima watu mbalimbali wakiwemo wanamuziki wa nyimbo za injili kwani kupitia uimbaji wao wameweza kutoa mafunzo kwa watu na wengine kuacha kutenda dhambi na kuamua kuokoka" alisema Profesa Nzowa.

Baadhi ya waimbaji wa nyimbo za injili waliotunukiwa tuzo hizo ni Rais wa Shirikisho la Muziki  Tanzania, Ado Novemba ambaye alitunukiwa tuzo ya heshima ya udaktari, Stella Joel ambaye ametunukiwa Tuzo ya Heshima ya Shahada ya Uzamili ya Mahusiano na Upendo Mbila aliyetunukiwa Tuzo ya Heshima ya Shahada ya Uzamili ya Uongozi wa Umma.

Akizungumza baada ya kupata tuzo hiyo Stella Joel alisema anamshukuru mungu kwa kumuwezesha kupata tuzo hiyo na kuwa imemtia nguvu kuendelea kufanya kazi ya mungu kupitia uimbaji.

Kwa upande wake Upendo Mbila alitoa shukurani zake kwa chuo hicho kwa kutambua mchango wa waimbaji wa nyimbo za injili kwa kuwapa tuzo hizo ambazo ni muhimu kwao.

CHUO KIKUU CHA AFRICAN GRADUATE UNIVERSITY CHAFANYA MAHAFALI YAKE YA PILI NCHINI JIJINI DAR ES SALAAM

 Makamu Mkuu wa Chuo cha African Graduate University, Askofu Profesa Stephano Nzowa (kulia), akizungumza katika mahafali ya pili ya chuo hicho yaliyofanyika Dar es Salaam juzi.Kushoto ni Mkuu wa chuo hicho, Profesa Timothy Kazembe kutoka nchini Zambia na mgeni rasmi wa mahafali hayo, Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Ushindani Tanzania (FCC), Dk. Fredrick Ringo.
  Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Ushindani Tanzania (FCC), Dk. Fredrick Ringo, ambaye alikuwa mgeni rasmi akihutubia katika mahafali hayo.
 Wahitimu wa chuo hicho wakiwa wamejipanga tayari kwa kuingia ndani kuanza kwa shughuli mbalimbali za mahafali hayo.
 Ndugu na jamaa na wageni waalikwa  kwenye mahafali hayo.

 Wahitimu hao wakishiriki kuimba wimbo wa taifa.
 Mahafali yakiendelea.
 Taswira katika ukumbi wa mahafali.
 Waliotoa huduma katika mahafali hayo wakiwa katika pozi.
 Waimbaji wa nyimbo za injili wakitoa burudani.
 Makamu Mkuu wa Chuo hicho, Askofu Profesa Stephano Nzowa akimvika kofia Mwimbaji wa nyimbo za injili, Stella Joel wakati akimtunuku Tuzo ya Heshima ya Shahada ya Uzamili ya Mahusiano katika mahafali hayo. Kushoto ni Mkuu wa Chuo hicho kutoka nchini Zambia, Profesa Timothy Kazembe.
Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Ushindani Tanzania (FCC), Dk. Fredrick Ringo akimpongeza mwimbaji Stella Joel kwa kupata tuzo hiyo.



Na Dotto Mwaibale

WAHITIMU wa Chuo Kikuu cha African Graduate University katika ngazi mbalimbali wametakiwa kutumia elimu waliyopata kwa ajili ya wananchi na taifa kwa ujumla.

Mwito huo ulitolewa na Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Ushindani Tanzania (FCC), Dk. Fredrick Ringomgeni aliye kuwa mgeni rasmi katika mahafali ya pili ya chuo hicho yaliyofanyika Dar es Salaam juzi.

"Nawaombeni sana elimu mliyopata itumieni kwa ajili ya kuinua maisha ya familia zetu, wananchi na taifa kwa ujumla na si vinginevyo" alisema Dk.Ringo.

Makamu Mkuu wa chuo hicho Askofu Profesa Stephano Nzowa aliwata wahitimu hao kuendelea kujiendeleza kielimu hadi kufikia ngazi mbalimbali za juu.

Nzowa alisema watu wengi wamekuwa wakijiendeleza kielimu wakiwa na matumaini ya kuja kupata kazi nzuri jambo ambalo alisema ni bahati.

"Msisome kwa ajili ya kuja kupata kazi nzuri bali someni ili kujiongezea uelewa wa mambo mengi ambayo yatawasaidieni kuanzisha miradi mbalimbali ya kuwaingizia fedha" alisema Nzowa.

Profesa Nzowa alisema chuo hicho chenye makao makuu yake nchini Sieralaoni kipo katika nchi kadhaa barani Afrika na kwa Tanzania kinajengwa Wanging'ombe mkoani Njombe na kuwa mahafali hayo ni ya 25 na kwa hapa nchini ni ya pili.


Mkuu wa chuo hicho Profesa Timothy Kazembe kutoka nchini Zambia alisema lengo lao ni kufungua chuo hicho katika nchi mbalimbali duniani ili wanafunzi kujua mambo mbalimbali yakiwemo ya kijamii na ya mungu.

PROFESA KILLIAN WA CHUO CHA MKWAWA ASHINDA SAFARI KUTAZAMA BUNDESLIGA UJERUMANI NA STARTIMES

 Mtangazaji wa luninga na redio wa Clouds Media, Bw. Shaffih Dauda (katikati), ambaye pia ni balozi wa kampuni ya StarTimes Tanzania kwa upande wa chaneli na vipindi vya michezo, akichezesha droo ya kwanza ya bahati nasibu ya kumpata mshindi wa safari ya kujishindia tiketi kutazama Ligi ya Bundesliga ‘Live’ Ujerumani iliyochezeshwa mwishoni mwa wiki katika ofisi za kampuni hiyo jijini Dar es Salaam. Wakishuhudia tukio hilo pamoja naye ni Makamu wa Rais wa StarTimes Tanzania, Bi. Zuhura Hanif (kushoto) na Mkaguzi kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Bw. Abdalla Hemedy (Kulia).
 Mkaguzi kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Bw. Abdalla Hemedy (Kulia) akiandika namba ya mshindi wa droo ya kwanza ya bahati nasibu ya kumpata mshindi wa safari ya kujishindia tiketi kutazama Ligi ya Bundesliga ‘Live’ Ujerumani iliyochezeshwa mwishoni mwa wiki katika ofisi za kampuni hiyo jijini Dar es Salaam. Wakishuhudia tukio hilo pamoja naye ni Makamu wa Rais wa StarTimes Tanzania, Bi. Zuhura Hanif (kushoto) na Mtangazaji wa luninga na redio wa Clouds Media, Bw. Shaffih Dauda (katikati), ambaye pia ni balozi wa kampuni ya StarTimes Tanzania kwa upande wa chaneli na vipindi vya michezo.
 Makamu wa Rais wa StarTimes Tanzania, Bi. Zuhura Hanif (kushoto) akipiga namba ya simu ya mshindi aliyepatikana katika droo ya kwanza ya bahati nasibu ya kumpata mshindi wa safari ya kujishindia tiketi kutazama Ligi ya Bundesliga ‘Live’ Ujerumani iliyochezeshwa mwishoni mwa wiki katika ofisi za kampuni hiyo jijini Dar es Salaam. Wakishuhudia tukio hilo pamoja naye ni Mtangazaji wa luninga na redio wa Clouds Media, Bw. Shaffih Dauda (katikati), ambaye pia ni balozi wa kampuni ya StarTimes Tanzania kwa upande wa chaneli na vipindi vya michezo na Mkaguzi kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Bw. Abdalla Hemedy (Kulia). 

 Mtangazaji wa luninga na redio wa Clouds Media, Bw. Shaffih Dauda (katikati), ambaye pia ni balozi wa kampuni ya StarTimes Tanzania kwa upande wa chaneli na vipindi vya michezo akizungumza na mshindi kwa njia ya simu aliyepatikana wakati wa uchezeshwaji wa droo ya kwanza ya bahati nasibu ya kumpata mshindi wa safari ya kujishindia tiketi kutazama Ligi ya Bundesliga ‘Live’ Ujerumani iliyochezeshwa mwishoni mwa wiki katika ofisi za kampuni hiyo jijini Dar es Salaam. Wakishuhudia tukio hilo pamoja naye ni Makamu wa Rais wa StarTimes Tanzania, Bi. Zuhura Hanif (kushoto) na Mkaguzi kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Bw. Abdalla Hemedy (Kulia).
Wanahabari wakichukua taarifa hiyo.

Na Dotto Mwaibale

MKUU wa Chuo cha Ualimu cha Mkwawa cha mkoani Iringa ambacho ni chuo kishiriki cha Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Profesa Bernadeta Killian (50) amefanikiwa kuibuka mteja wa kwanza mwenye bahati kwa kujinyakulia tiketi ya kwenda Ujerumani kutazama mechi ya Bundesliga kutoka kwa kampuni ya StarTimes katika droo iliyochezeshwa mwishoni mwa wiki iliyopita.

Akizungumza kwa njia ya simu Profesa Killian baada ya kutangazwa kuwa ni mshindi amesema kuwa anayo furaha isiyoelezeka kupata taarifa hiyo ya ushindi ambao hakufikiria kama kuna ofa hiyo nzuri kwa wateja.

“Ninajisikia furaha kwa kutangazwa kuwa mshindi kwani sikutarajia kama wateja wa StarTimes tunaweza kupewa kubwa kiasi hiki ya kwenda Ujerumani kutazama mechi ‘Live’. Naweza kusema mwaka umeanza vizuri kwa kuonyesha dalili ya neema kama hii, ni fursa kubwa kwangu mimi kama mteja kwani kuna maelefu ya wateja ambao wangependa kupata fursa hii. 

Nawashukuru kwa hili kwani wameliendesha zoezi bila ya upendeleo na sisi wateja wao tunafurahi na kuwapongeza sana na tutandelea kuwaunga mkono.” Alieleza Profesa Killian

Mshindi huyo wa kwanza wa droo iliyopewa jina la ‘Pasua Anga na StarTimes’ alipatikana baada ya kujiunga na kifurushi cha Super ambacho ni shilingi 36,000/- katika dishi. Lakini pia mteja yoyote wa StarTimes anaweza kuibuka mshindi kwa kujiunga na kifurushi chochote kuanzia cha shilingi 5,000/- na kuendelea kwa upande wa ving’amuzi vya dishi na antenna. Na kwa wateja wapya pindi wajiungapo na huduma za kampuni hiyo wamekuwa wameunganishwa moja kwa moja na droo ya bahati nasibu.

“Ningependa kutoa wito kwa wateja wenzangu waendelee kujiunga kwani bado nafasi zimebaki kushindaniwa na zote zipo kwa ajili yao, hivyo wasilaze damu. Ninaahidi kuitumia fursa hii ipasavyo kwa kuenda kutazama wenzetu wa ulaya wanafanya nini kwa upande wa soka kwani kwa muda mrefu tumekuwa tukitazama kupitia kwenye luninga, pongezi tena kwa StarTimes kwa kuifanya ligi ya Bundesliga ionekane kupitia ving’amuzi vyake kwa gharama nafuu kabisa ambayo kila mtu anaweza kuimudu. Wamefanikiwa kwa kiasi kikubwa kuipa ligi hiyo umaarufu nchini kwani sasa kwa kiasi kikubwa michezo yote inaonekana ‘Live’ na kufuatiliwa na watu wengi.” alihitimisha Mkuu huyo wa Chuo cha Ualimu Mkwawa

Naye kwa upande wake Makamu wa Rais wa kampuni ya StarTimes Tanzania, Bi. Zuhura Hanif amebainisha kuwa, “Hii si mara ya kwanza sisi kuchezesha droo ya bahati nasibu kwa kuwazawadia wateja wetu ni zawadi mbalimbali, hivyo basi huu ni muendelezo tu wa ofa nyingi zinazoendelea kumiminwa kwa wateja wetu waaminifu. Safari hii wateja wetu tumeamua kuwazawadia safari itakayolipiwa gharama zote na kampuni kwenda Ujerumani kutazama ligi ya Bundesliga ambayo kwa Afrika ndio kampuni pekee yenye hakimiliki ya kuionyesha ‘Live’.”

“Makubaliano baina ya wamiliki wa ligi hiyo ya Ujerumani na kampuni ya StarTimes yaliingiwa kwa dhumuni kubwa la kuifanya ligi hiyo maarufu barani Afrika kama ligi zingine. Na ni kwa kupitia StarTimes pekee hilo linaweza kufanikiwa kutokana na wingi wa wateja wetu, ubora wa huduma na gharama nafuu ambazo mwananchi yoyote wa kipato cha chini anaweza kuzimudu,” alisema Bi. Hanif na kumalizia, “Hivyo basi nampongeza mshindi wa leo na nawasihi wateja wetu waendelee kujiunga nasi au walipie vifurushi vyao ili waingie kwenye droo ya bahati nasibu na kujishindia safari hii kubwa kwenda Ulaya kutazama mechi moja kwa moja pamoja na mashabiki wengine ulimwenguni.”

Akielezea machache kutokana na ushuhuda wake baada ya kupata fursa ya kutembelea ofisi za Bundesliga na kushuhudia mechi kadhaa nchini Ujerumani, Mtangazaji wa luninga na redio wa Clouds Media, Bw. Shaffih Dauda, ambaye pia ni balozi wa kampuni ya StarTimes Tanzania kwa upande wa chaneli za michezo, amesema kuwa, “Bahati ya kupata safari ya kwenda Ujerumani ni fursa kubwa sana kwa wateja na ningependa waitumie vema. Kuna mengi tu ya kujifunza licha ya kufurahia safari hiyo. Wenzetu wamepiga hatua kubwa na tunayo mengi ya kujifunza kutoka kwao, hivyo nawasihi waitumie vemam ili waje kutuhadithia na sie huku.”

Zoezi zima la uchezeshwaji wa droo ya bahati nasibu ya kumpata mshindi ilichezeshwa kwa uwazi na haki mbele ya waandishi wa habari ikishuhudiwa na mkaguzi kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania.