Pages

KAPIPI TV

Friday, November 27, 2015

BINAGI RADIO: KILICHOJIRI MAHAKAMA KUU KANDA YA MWANZA KUHUSU MWILI WA MAWAZO


Jana Novemba 26,2015 Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza ilitengua zuio la Jeshi la Polisi Mkoani hapa la kuzuia ibada ya mazishi ya kuuaga mwili wa aliekuwa Mwenyekiti wa Chadema Mkoani Geita Alphonce Mawazo alieuawa kwa kukatwa mapanga na watu wasiojulikana Novemba 14 mwaka huu Mkoani humo.
BONYEZA PLAY KUSIKILIZA BINAGI RADIO-HABARI JUU YA HABARI HIYO.

MAKUNDI YA JAMII ASILIA YA WAHADZABE, WABARABAIG, WAMASAI WAIOMBA SERIKALI YA TANZANIA KUWATAMBUA KAMA JAMII NYINGINE

DSC_0928
Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu, Mh. Idd Ramadhan Mapuri (katikati) akizindua taarifa ya Tume ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu kuhusu utafiti wa Hali ya Haki za watu wenye kuishi maisha asilia Tanzania. kushoto kwake ni Katibu Mtendaji wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora Bi. Mary Massay na (kulia) ni mmoja wa wajumbe walioshiriki kuandaa ripoti hiyo, kutoka nchini Kenya katika taasisi ya ACHPR, Dk. Naomi Kipuri.(Picha zote na Andrew Chale, Modewjiblog).
Na Andrew Chale, Modewjiblog
[DAR ES SALAAM-TANZANIA] Jamii ya watu wa asili na makundi yao wameiomba Serikali ya Tanzania kutambua uwepo wao hapa nchini ikiwemo kuwatangaza kwa mema na kuwasaidia kwa misingi ya haki, hutu na kimaendeleo kama watu wengine wanaotambulika ndani na nje ya mipaka yao.
Hayo yameelezwa mapema leo jijini hapa wakati wa uzinduzi wa taarifa ya Tume ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu kuhusu utafiti wa Hali ya Haki za watu wenye kuishi maisha asilia Tanzania wakiwemo makabila ya Wa-Akiye,Wa- Hadzabe,Wa- IIparakuyio Masai na wengine wengi.
Akielezea katika uzinduzi huo mmoja wa wajumbe walioandaa taarifa ya Tume hiyo, ambaye anatoka nchini Kenya, katika taasisi ya African Commission on Human and Peoples Rights (ACHPR), Dk. Naomi Kipuri amebainisha kuwa jamii ya watu asilia wamekuwa na kilio cha muda mrefu cha kutaka kupata haki zao zao msingi na kutambulika zaidi.
“Utafiti tuliofanya jamii ya watu asilia wamekuwa katika malalamiko ya muda mrefu ikiwemo kutaka haki zao za msingi. Ikiwemo masuala ya elimu, makazi na haki zingine. Pia wameomba Serikali kuwatangaza watu hawa wa asilia ili wasionekane wageni kwani jamii nyingi bado hazijawatambua na hata kupelekea kuwavunjia hutu wao” alieleza Dk. Naomi.
Aidha, Dk. Naomi katika uwakilishi wake wa mada kwenye mkutano huo amelezea namna ya jamii inavyoendelea kuwaona watu hao ni tofauti kiasi cha kupelekea watu hao kudumaa na maisha yale yale ya asilia.
DSC_0961
Mtangazaji wa radio Deutsche Welle (DW) ya Ujerumani, George Njogopa akifanya mahojiano na Katibu Mtendaji wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora Bi. Mary Massay. Kushoto ni Mratibu wa NGONET Ngorongoro, Samweli Nangiria “Jamii zingine zinawatenga watu wa jamii ya Wamasai, tumeshuhudia lugha na matamshi kwenye mizunguko ya watu ikiwemo kwenye madaladala, mitaani huku wakimuona Mmasai kama mtu tofauti, sasa katika ripoti hii imeweza kuelezea mambo mengi sana. Ikiwemo suala la Haki ya kuishi, kufanya kazi na mambo yote kama watu wengine” alimalizia Dk. Naomi. Kwa upande wake Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu, Mh. Idd Ramadhan Mapuri ameeleza kuwa kupitia ofisi yake itahakikisha inashughulikia suala hilo la kuwa karibu na watu asilia na kutambua misingi ya haki zao ambapo amebainisha watu hao wa asilia kwa Tanzania wanafikia makundi zaidi ya sita. Kwa upande wao baadhi ya wawakilishi wa watu hao wa watu asilia wakielezea katika mkutano huo, waliomba na wao na wapate wawakilishi maalum ikiwemo Bungeni ama sehemu za maamuzi ikiwemo Halmashauri na maeneo mengine ya Serikali ilikutambua michakato ya Kimaendeleo kwa kina. “Jambo la ardhi, ndilo linalotuumiza kwa sasa. Sie tunaporwa ardhi yetu kila siku na kesi nyingi ni za kuporwa ardhi na migogoro ya wakulima na wafugaji, ndani ya migogoro hii ina siri kubwa bila kujua kiini chake ni wakati wa kufika kule na kupata ukweli zaidi” alielezea Adam Ole Mwarabu Kwa upande wake, Mratibu wa NGONET Ngorongoro, Samweli Nangiria ambaye anawakilisha watu hao asilia anaeleza kuwa, wao wamekuwa wakitambuana kwa desturi ikiwemo suala la ufugaji na maisha mengine, Jamii nyingine imekuwa wakiwaona wao ni watu wa tofauti kiasi cha kupora mali zao ikiwemo ardhi, mifugo na mambo mengine ya msingi.
DSC_0953
Baadhi ya wawakilishi wa Jamii za watu asilia wakiwemo Wahadzabe, Masai, Wabarabaig na wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora na wadau wengineo wakiwa kwenye picha ya pamoja wakati wa uzinduzi wa ripoti hiyo juu ya usawa na kutambulika kama jamii asilia yenye tamaduni na desturi zake.
“Sie watu asilia tuna mahusiano mbalimbali na jamii zetu za kifugaji licha ya jamii zingine kutuingilia kwenye maeneo yetu na kupora ardhi yetu. Watu asilia tunahitajika kutambulika zaidi na hata kupatiwa huduma muhimu ikiwemo kujengewa shule, vyuo na mahitaji mengine ikiwemo haki na hutu kama watu wengine.” Alieleza Samweli Nangiria.
Kwa upande wake, .. ameweza kuipongeza tume ya Haki za Binadamu kwa kuweza kushughulikia suala hilo na hata kuandaa tukio hilo kwa kushirikisha wadau wengine wakiemo wao wa asilia.
“Tanzania ndio nchi ya kwanza kuaandaa kikao cha Afrika kwa watu hawa wa makundi maalum wa asilia, kilichofanyika mwaka uliopita. Hili ni jambo bora sana kwani watu asilia tunaendelea kutambulika zaidi.
Ripoti hiyo iliyozinduliwa ya taarifa ya Tume ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu kuhusu utafiti wa Hali ya Haki za watu wenye kuishi maisha asilia Tanzania, imeweza kuangalia mambo mbalimbali ikiwemo suala la haki ya kuishi, Utawala bora na namna ya jamii hizo zinapotokea katika maeneo yao hapa nchini.
DSC_0944
Wadau wa haki za binadamu wakiwa katika picha ya pamoja katika mkutano huo baada ya uzinduzi wa ripoti hiyo ya kuwatambua watu wa makundi asilia. Mkutano unaofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Blue Pearl Ubungo jijini Dar es Salaam.
DSC_2541
Mmoja wa washiriki wa mkutano huo Mhifadhi Mkuu, kutoka ofisi ya Makamu wa Rais, Bw. Seleman Kisimbo akichangia mada juu ya hali iliyopo sasa ikiwemo jamii hiyo ya watu asilia na changamoto za Mabadiliko ya tabia nchi ikiwemo suala la ukame inayowakabili katika maisha yao ya vijijini.
DSC_0946
Dk. Naomi Kipuri wa taasisi ya ACHPR, ya nchini Kenya akijadiliana jambo na Mhadhiri wa Sheria Chuo Kikuu cha Tumaini-Makumira, Bw. Elifuraha Laltaika.
DSC_0955
Baadhi ya wawakilishi wa Jamii za watu asilia wakiwemo Wahadzabe, Masai, Wabarabaig na wengineo wakiwa kwenye picha ya pamoja kwenye mkutano huo.

NHC YAZINDUA MAUZO YA NYUMBA KATIKA MRADI WA KAWE JIJINI DAR ES SALAAM

NH9Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) Bw. Nehemia Kyando Mchechu (kushoto), akizungumza na waandishi wa habari Novemba 26, 2015 Jijini Dar es Salaam (hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa mauzo ya nyumba katika mradi mpya wa Seven Eleven (711) ulioko Kawe Jijini Dar es Salaam (kulia) Mkurugenzi wa Usimamizi wa Miliki wa Shirika la Nyumba la Taifa, Hamad Abdallah.
NH2Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) Bw. Nehemia Kyando Mchechu akiwaonesha waandishi wa habari michoro ya ramani ya mradi wa nyumba ulioko Kawe Jijini Dar es Salaam.
NH3Wafanyakazi wa NHC wakimsikiliza kwa umakini, Bw. Nehemia Kyando Mchechu.
NH4
NH1Mkutano ukiendelea.
NH5Waandishi wa habari wakitembelea katika eneo la ujenzi huo.
NH6Ujenzi ukiendelea
NH7Ujenzi ukiendelea
NH8Waandshi wa habari pamoja na wafanyakazi wa Shirika la Nyumba la Taifa wakimsikiliza Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) Bw. Nehemia Kyando Mchechu wakati wa uzinduzi huo.
Picha zote na Philemon Solomon-Fullshangweblog.
..................................................................................................
Na Philemon Solomon Fullshangweblog
SHIRIKA la Nyumba la Taifa (NHC) lazindua mauzo ya nyumba katika mradi wake mpya wa Seven Eleven (711) ulioko Kawe ,ambapo ujenzi huo ulianza Januari 2015.

Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi huo Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) Bw. Nehemia Kyando Mchechu alisema ujenzi wa mradi huo unatarajiwa kukamilika ifikapo Desemba 2018 ,ikiwa ni takribani miezi 48 baada ya kuanza ujenzi. Mradi huo una ukubwa wa mita za mraba 111,842.90 ambao unatarajiwa kugarimu kiasi cha zaidi ya Sh 187, 927, 105,500 mpaka utakapomalizika .

Pia ikumbukwe kuwa mradi huu ni seemu ya mji mpya wa kisasa (Satellite City) unajengwa hapa ,mradi huu upo katika eneo tulivu la Kawe Jijini Dar es Salaam ambalo liko mita chache kutoka fuko za bahari ya Hindi pia karibu na maeneo muhimu kama Mbezi Beach, Masaki, Oysterbay, Morocco na Mikocheni mradi huu una jumla ya nyumba 422 za kuuzwa zilizopo kwenye majengo nane tofauti ya ghorofa 18 kila moja, ukiwa na huduma zote muhimu za kijamii.pia kutakuwepo na seemu ya maduka makubwa kwa ajili ya wakazi na maeneo ya jirani”Alisema Mchechu.

MBUNGE WA UBUNGO SAID KUBENEA AWATEMBELEA WANANCHI WAKE KUWASHUKURU KUMCHAGUA NA KUJUA CHANGAMOTO ZAO

 Mbunge wa Jimbo la Ubungo, Said Kubenea akiongea na wananchi Stendi ya Mabasi ya Ubungo Dar es Salaam leo, kuwashukuru kwa kumchagua na kujua changamoto zao mbalimbali. Mbunge huyo jana alitembelea Soko la Ndizi la Mabibo, Soko la Mabibo, Kituo cha Mabasi cha Mawasiliano  na kumpa pole ya sh. milioni 1.1 Diwani wa Kata ya Manzese, Ramadhani Kwangaya ambaye ni Mkuu wa Chuo cha Mus'ab kilicho chomwa moto na kuunguza magodoro 30.
 Kubenea akizungumza na waandishi wa habari na wananchi katika Soko la Ndizi la Mabibo.
 Hapa akiwaunga mkono wananchi kununua mananasi katika soko la ndizi la mabibo
 Mbunge Kubenea akisalimiana na wananchi katika soko hilo.
 Wafanyabiashara katika soko la ndizi la mabibo wakimsikiliza mbunge wao Said Kubenea.
 Vijana wakiserebuka baada ya kuzungumza na mbunge wao Said Kubenea katika Soko la Mabibo.
 Mbunge Kubenea akizungumza na viongozi wa soko la Mabibo.
Hapa akiwahutubia wananchi katika soko la Mabibo.
(Imeandaliwa na mtandao wa www. habari za jamii.com-simu namba 0712-727062)


TAMASHA KUBWA LA BURUDANI LA INSTAGRAM PARTY KUFANYIKA JUMAMOSI VIWANJA VYA ESCAPE ONE MIKOCHENI JIJINI DAR ES SALAAM

  Mkurugenzi wa Freconic ideaz, Fred Ngimba.
 Mkurugenzi wa Freconic ideaz, Fred Ngimba (kushoto), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo asubuhi, kuhusu tamasha kubwa la burudani la Instagram party litakalofanyika Jumamosi katika viwanja vya Escape One Mikocheni likiwa na kauli mbiu Bongo Throw Back. Kulia ni Meneja Mawasiliano, Krantz Mwantepele.
 Wanahabari wakichukua taarifa hiyo.
wanahabari wakiwa kwenye mkutano huo.

Na Dotto Mwaibale

KAMPUNI ya Freconic Ideaz, imeandaa tamasha la burudani la 'Instagram party' litakalofanyika kesho kutwa kwenye Ukumbi wa Escape One Mikocheni jijini  Dar es Salaam likiwa na lengo la kuwakumbusha wapenzi wa muziki, mavazi na misemo ya kizamani.

Akizungumza Dar es Salaam leo asubuhi, Mkurugenzi wa  Freconic Ideaz, Fred Ngimba alisema pia tamasha hilo litahusisha watu wenye ushawishi mkubwa katika mitandao ya kijamii na wasanii mbalimbali wa muziki na filamu.

Alisema wadau na marafiki mbalimbali wanaotumia mitandao ya kijamii watakutana siku hiyo kuweza kufahamiana na kubadilishana mawazo huku wakipata burudani mbalimbali.

"Kiingilio katika tamasha hili kitakuwa ni sh. 50,000 kwa viti maalumu na vile vya kawaida ni sh. 10,000, ambapo halitaishia hapa ila litaendelea katika Mikoa ya Mwanza, Morogoro, Tanga, Dodoma na Iringa," alisema Ngimba.

Alitoa mwito kwa wadau wa muziki wa mikoa ya jirani kujitokeza kwa wingi kushuhudia burudani itakayotolewa siku hiyo.



UULIZE MO!: TUANDIKIE MASWALI YAKO KUMUULIZA MOHAMMED DEWJI (CEO WA METL GROUP) MO BLOG ITAKUWA NA MAHOJIANO NAYE HIVI KARIBUNI

mo
Msomaji na mdau wa mtandao wako wa habari www.modewjiblog.com unakupa nafasi wewe kumuuliza maswali/swali lolote lile Afisa Mtendaji Mkuu wa MeTL Group, Mohammed Dewji. Maswali yote yatajibiwa na kutolewa ufafanuzi wa kina. Tutakuwa na mahojiano naye karibuni. Asanteni sana.
Utaratibu wa kumuuliza maswali ni kwa kukomenti kwenye post hii kisanduku cha maoni, Zingatia Kanuni na sheria ikiwemo kutotumia lugha zisizo rasmi.
Pia waweza kutoa maoni yako kupitia kurasa za mitandao ya kijamii ukiwemo ukurasa wa Mohammed Dewji : https://www.facebook.com/mohammeddewjitz/
au Ukurasa wa Mohammed Enterprises Tanzania Limited (METL):https://www.facebook.com/MeTLGroup/photos

WENGI WAJITOKEZA KATIKA UZINDUZI WA MAADHIMISHO YA SIKU 16 ZA KUPINGA UKATILI DHIDI YA WANAWAKE JIJINI DAR ES SALAAM

Maelfu wajitokeza katika maandamano ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia, hapa wakiendelea na matembezi ya kupinga ukatili wa Kijinsia
  Maandamano yakipokelewa na Mkurugenzi wa shirika la misaada la Marekani USAID  Daniel Moore, Mwakilishi wa Balozi wa Ireland nchini Maire Matthews, Mwakilishi kutoka shirika la Umoja wa Mataifa Wanawake Lucy Melele, Mkurugenzi wa shirika la Wanawake katika Sheria na Maendeleo barani Afrika - WiLDAF, Dr. Judith Odunga, pamoja na wawakilishi wa mashirika wahisani na viongozi mbalimbali.
 Dr. Judith Odunga kutoka WiLDAF akiwakaribisha wageni.
 Mwanaharakati mama Siwale, Mwenyekiti wa ACT Wazalendo Anna Mghwira(wa kwanza kulia) ni miongoni mwa waliohudhuria maadhimisho hayo.
 Wageni mbalimbali
 Maigizo kuhusu uchapaji wa viboko kwa wanafunzi
 Mwakilishi wa Balozi wa Ireland Maire Matthews akizungumza
  Lucy Melele kutoka shirika la UN Women akizungumza
 Mwalimu akitoa ushuhuda
  Paulina Mkonongo(wa kwanza kulia), Mkurugenzi wa Elimu ya Sekondari kutoka Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi. Akisikiliza jambo
 Mgeni rasmi Bi. Paulina Mkonongo Mkurugenzi wa Elimu ya Sekondari kutoka Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi akitembelea sehemu za maonyesho kutoka kwa mashirika mbalimbali.
 Baadhi ya wadau wakitembelea mabanda
 Wadau mbalimbali waliohudhuria maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili dhidi ya wanawake.

Maadhimisho ya Siku 16 za kupinga ukatili dhidi ya wanawake leo yamefunguliwa rasmi kwa kuanza na maandamano ya amani yaliyoanzia uwanja wa Tipi Sinza darajani hadi ukumbi wa hoteli ya Blue Pearl iliyopo jengo la Ubungo Plaza jijini Dar es salaam.

Maandamano hayo yalihudhuriwa na maelfu ya watu yaliongozwa na bendi ya jeshi la polisi kupitia njia za Shekilango kisha barabara ya Morogoro hadi katika jengo la Ubungo Plaza ambapo yalipokelewa na Mkurugenzi wa shirika la misaada la Marekani USAID  Daniel Moore, Mwakilishi wa Balozi wa Ireland nchini Maire Matthews, Mwakilishi kutoka shirika la Umoja wa Mataifa Wanawake Lucy Melele, Mkurugenzi wa shirika la Wanawake katika Sheria na Maendeleo barani Afrika - WiLDAF, Dr. Judith Odunga, pamoja na wawakilishi wa mashirika wahisani na viongozi mbalimbali.

Akitoa neno la ukaribisho, Dr. Judith Odunga alisema kampeni ya siku 16 kwa mwaka huu imelenga zaidi kuzungumzia suala zima la usalama mashuleni. Lengo kuu ikiwa kuhamasisha umma kuhusu ukubwa wa ukatili wa kijinsia kwa vijana na watoto wetu mashuleni.

“Ni kutokana na unyeti wa tatizo la ukatili wa kijinsia mashuleni, WILDAF na wadau mbalimbali tumeona kuna umuhimu wa kushirikisha Wizara ya elimu na ufundi stadi ili kuzungumzia ukatili wa kijinsia mashuleni na kujenga mikakati ya kuzuia ukatili huo” Aliongezea.

Dr. Odunga aliitaja kauli mbiu ya mwaka huu kuwa ni FUNGUKA! CHUKUA HATUA, MLINDE MTOTO APATE ELIMU. “Kauli hii inalenga kumshawishi mtu binafsi, kuwashawishi walimu, wanafunzi, wazazi na jamii kwa ujumla, kuwalinda watoto dhidi ya ukatili wa kijinsia na kuhakikisha kwamba shule ni mahala salama. Ni vyema kutafakari kwa kina jinsi vitendo vya ukatili wa kijinsia mashuleni vinavyoathiri maendeleo ya watoto wetu kielimu.” Alisema Dr. Odunga.

Dr. Odunga alitumia nafasi hiyo kuiomba serikali kufanya yafuatayo:

1.      Kufutwa kabisa kwa adhabu ya viboko mashuleni na waalimu kufundishwa au kutafuta mbinu za kutoa adhabu mbadala.
2.      Kutengeneza mwongozo wa utekelezaji wa sera ya elimu ya mwaka 2014 utakaoelekeza upatikanaji wa elimu ya msingi iliyo bora na salama.
3.      Kuboresha miundombinu rafiki ya elimu ikiwa ni pamoja na kuwa na madarasa ya kutosha, madawati, vyoo na sehemu za kujisitiri watoto wa kike, mabweni, uzio pamoja na kuwa na usafiri wa uhakika kwa wanafunzi.
4.      Serikali kuweza kuunda na kusimamia mabaraza yatakayo kuwa yanasikiliza malalamiko ya wanafunzi mashuleni.
5.      Tunaomba Wizara ya elimu na ufundi stadi kushirikiana na wizara ya Katiba na Sheria na Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto kutunga Sheria ya Ukatili wa Majumbani sambamba na kubadilisha Sheria ya Ndoa ya mwaka 1971 inayoruhusu ndoa kwa mtoto chini ya miaka 18.


Akifungua rasmi kampeni hizi, mgeni rasmi Paulina Mkonongo ambaye ni Mkurugenzi wa Elimu ya sekondari kutoka Wizara ya Elimu na mafunzo ya ufundi aliyemuwakilisha Katibu mkuu wa wizara hiyo alisema, “ukatili wa kijinsia huleta athari hasi katika utoaji na upatikana wa fursa mbalimbali za kijamii ikiwemo fursa ya elimu kwa watoto wetu, hivyo kuwa ni kikwazo katika kujenga usawa wa kijinsia nchini.

Aidha Mkonongo alisema serikali imefanya juhudi za makusudi kuzuia ukatili na kuleta usawa katika kupambana na ukatili wa kijinsia kwa kuweka sera na mipango inayozingatia usawa na kupinga ukatili kwa makundi mbalimbali, katika jamii ukiwemo ukatili wa kijinsia.

Mkonongo alitoa wito kwa wananchi wote kuwalinda watoto dhidi ya vitendo vya ukatili na kwamba kila mtoto ana haki ya kulindwa popote anapokuwepo iwe nyumbani, shuleni, kwenye vyombo vya usafiri, michezoni na njiani wanapokwenda na kurudi shuleni pia kuwapa mbinu za kujilinda wenyewe.

Naye mwakilishi wa Balozi wa Ireland nchini Bi. Maire Matthews alisema kuwa takwimu za hivi karibuni zinaonyesha kuwa wastani wa asilimia 45 ya wanawake Tanzania wenye umri kati ya miaka 15 – 49 waliripoti kuwahi kufanyiwa ukatili wa kimwili au kingono katika maisha yao. Alisema takwimu nyingine zinakadiria kiwango hicho kuwa kati ya 41 – 56%.

Kwa upande wake Lucy Melele kutoka shirika la UN Women aliyemwakilisha Mwakilishi wa shirika hilo hapa nchini Anna Collins alisema wanawake na wasichana ulimwenguni kote wanapitia aina mbalimbali za ukatili ambayo inawanyima haki zao za msingi, ni tishio la demokrasia na ni kizuizi cha amani ya kudumu. Hata hivyo alisema shirika la umoja wa mataifa litaendelea kufanya kazi kwa ukaribu na wadau wa maendeleo, serikali, mashirika mbalimbali, na jamii katika kampeni ya kupinga ukatili dhidi ya wanawake na watoto.

Kampeni ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia pia inafanyika kikanda katika kanda ya ziwa (Mwanza, Mara na Shinyanga, kanda ya Kaskazini (Manyara, Arusha, Kilimanjaro na Tanga), kanda ya kati (Dodoma, Morogoro na Singida), kanda ya Kusini (Mtwara, Songea, Mbeya, Iringa na Lindi, Kanda ya Pwani (Dar es salaam na Pwani) zikisimamiwa na wadau mbalimbali wakiwemo mashirika ya Kivulini, CWCA, NAFGEM, Morogoro Paralegal,  Mtwara paralegal, WiLDAF, TWCWC pamoja na jeshi la Polisi.




SERIKALI YAAHIDI KUSHIRIKIANA NA MASHIRIKA NA WADAU WA HABARI KUTOKOMEZA VITENDO VYA UKATILI KWA WAANDISHI WA HABARI.

IMG_2832
Mkuu wa ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linalohudumia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) nchini, Zulmira Rodrigues (katikati) akisalimiana na Mjumbe wa bodi udhamini ya Mtandao wa Radio Jamii Tanzania (COMNETA), Balozi Mstaafu, Christopher Liundi alipowasili katika mkutano wa kitaifa wa mashauriano kuhusu hali ya usalama wa waandishi wa habari, uzinduzi wa kikosi kazi cha usalama wa waandishi wa habari na uandishi unaozingatia maadili ulioandaliwa na UNESCO. Kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Prof. Ole Sante Gabriel.
Na Rabi Hume, Modewjiblog
Serikali mpya ya awamu ya tano iliyochini ya rais Dr. John Magufuli, imeahidi kushirikiana na mashirika na wadau mbalimbali ambao wamekuwa wakipambana kuhakikisha waandishi wa habari wanakuwa salama na kufanya kazi zao kwa uhuru bili kuingiliwa ufanyaji wa kazi zao na mtu yoyote.
Ahadi hiyo imetolewa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Prof. Ole Sante Gabriel katika mkutano wa kitaifa wa mashauriano kuhusu hali ya usalama wa waandishi wa habari, uzinduzi wa kikosi kazi cha usalama wa waandishi wa habari na uandishi unaozingatia maadili ulioandaliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia na Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) nchini, Prof. Gabriel amesema serikali ya awamu ya tano ipo tayari kushirikiana na mashirika na wadau mbalimbali ambao wapo kuwasaidia waandishi wa habari ili haki zao ziweze kutekelezwa kutokana na kuwepo kwa uvunjaji wa haki za wanahabari.
Amesema wanatambua kuwepo kwa changamoto hizo kwa waandishi wa habari na kwa serikali ya awamu ya tano itahakikisha kushirikiana na mashirika na wadau ili kutetea haki za wanahabari kwa kuwa na uhuru katika utendaji wa kazi zao bila kuingiliwa na mtu.
“Naahidi kuanzia sasa serikali itakuwa ikishirikiana nanyi kusaidia kuhakikisha kunakuwa na uhuru wa vyombo vya habari, nchi yetu kwa sasa haina sababu ya kuacha kuungana na ninyi kutokomeza vitendo hivyo kwa wanahabari, serikali ni mpya na tutalitekeleza jambo hilo kila tumaposhirikishwa kuhusu vitendo vibaya kwa wanahabari,” amesema Prof. Gabriel.
IMG_2843
Mkuu wa ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linalohudumia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) nchini, Zulmira Rodrigues akitoa neno la ufunguzi katika mkutano huo kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi kufungua.
Aidha Katibu Mkuu huyo amewata waandishi wa habari kuwa pamoja na usaidizi ambao wizara imeamua kujitoa kuwasaidia pia wanapaswa kuandika habari zenye weledi na zilizo sahihi kwani kumekuwepo na kundi kubwa la waandishi wa habari ambao wamekuwa wakiandika habari ambazo hazina uhakika wala weledi na hivyo kuupotosha umma kwa habari wanazoandika ila kuanzia sasa wanabidi kubadilika kwa kuandika habari ambazo zitakuwa na fadia kwa jamii inayowazunguka.
Kwa upande wa UNESCO, kupitia kwa Mkuu wa ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) nchini, Zulmira Rodrigues, amesema kumekuwepo na vitendo vingi ambavyo sio vya kibinadamu ambavyo wamekuwa wakifanyiwa waandishi wa habari na wao wameamua kujitoa kuhakikisha wanatokomeza vitendo hivyo.
Amesema kama jamii ikiungana kwa pamoja kutokomeza vitendo hivyo inawezekana kwani kutokuwepo uhuru wa waandishi wa habari katika utendaji wao wa kazi kunapelekea jamii kukosa baadhi ya taarifa muhimu ambazo kama kukipatikana uhuru wa habari kutawapa fursa wanahabari wa kuzitoa taarifa hizo.
IMG_2914
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Prof. Ole Sante Gabriel akisisitiza jambo wakati akifungua rasmi mkutano wa kitaifa wa mashauriano kuhusu hali ya usalama wa waandishi wa habari, uzinduzi wa kikosi kazi cha usalama wa waandishi wa habari na uandishi unaozingatia maadili ambao umeandaliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na Elimu, Sayansi (UNESCO).
“UNESCO tunapenda kuona vitendo hivyo havifanyiki kwa waandishi wa habari kama kuweka sheria ambazo zinawabana na kusababisha wanashindwa kufanya kazi zao kwa uhuru na tunaweza kuona kama serikali na kila mtu akiwa tayari tunaweza kumaliza tatizo hilo,” amesema Rodrigues.
Nae Makamu wa Rais wa Chama cha Kijamii cha Wanasheria wa Tanganyika (TLS), Flaviana Charles amesema imekuwa ngumu kesi zinazokuwa zikiwahusu waandishi wa habari juu ya vitendo vya kikatili wanavyotendewa kutokana na ucheleweshwaji wa upelelezi unaofanywa na Jeshi la Polisi Tanzania akitolea mfano kesi ya mwandishi wa zamani wa Chaneli 10 mkoani Iringa, Daudi Mwangosi ambapo mpaka sasa ina miaka 4 na bado upelelezi haujakamilika.
IMG_3149
Makamu wa Rais wa Chama cha Kijamii cha Wanasheria wa Tanganyika, Bi. Flaviana Charles akifafanua jambo wakati wa mkutano huo.
IMG_2873
Pichani juu na chini ni wahariri wa vyombo vya habari, waandishi wa habari, wadau wa tasnia ya habari pamoja na maafisa wa UNESCO na taasisi mbalimbali walioshiriki mkutano huo.
IMG_2925
IMG_3178
Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) katika tasnia ya Habari na Mawasiliano, Ayub Rioba akiwasilisha mada ya wajibu wa vyombo vya habari huku akitolea mfano wa moja ya habari iliyobeba kichwa cha habari "Uhuru wa habari watikiswa Zimbabwe" katika moja ya magazeti ya Serikali wakati wa mkutano wa kitaifa wa mashauriano kuhusu hali ya usalama wa waandishi wa habari, uzinduzi wa kikosi kazi cha usalama wa waandishi wa habari na uandishi unaozingatia maadili ulioandaliwa na UNESCO.
IMG_3115
Ofisa Miradi katika kitengo cha Mawasiliano na Tehama UNESCO, Nancy Kaizilege akiwasilisha mada ya Uhuru wa vyombo vya Habari katika mkutano huo.
IMG_3191
Mratibu wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC), Mwanasheria Onesmo Olengurumwa akielezea jinsi mtandao wake unavyotoa msaada kwa wanahabari wanaokumbwa matukio mbalimbali katika utendaji wao hususan msaada wa kisheria.
IMG_3206
Mhariri Mtendaji wa Gazeti la Tanzania Daima, Neville Meena akiuliza swali kwa Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO), Assah Mwambene (hayupo pichani) katika mkutano wa kitaifa wa mashauriano kuhusu hali ya usalama wa waandishi wa habari, uzinduzi wa kikosi kazi cha usalama wa waandishi wa habari na uandishi unaozingatia maadili sambamba na kuadhimisha "International Day to #EndImpunity" ulioandaliwa na UNESCO.
IMG_3212
Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO), Assah Mwambene akitolea ufafanuzi wa swali la Mhariri Mtendaji wa Gazeti la Tanzania Daima, Neville Meena (hayupo pichani).
IMG_3227
Mkuu wa ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linalohudumia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) nchini, Zulmira Rodrigues akitoa maoni katika katika mkutano wa kitaifa wa mashauriano kuhusu hali ya usalama wa waandishi wa habari, uzinduzi wa kikosi kazi cha usalama wa waandishi wa habari na uandishi unaozingatia maadili sambamba na kuadhimisha "International Day to #EndImpunity" ulioandaliwa na UNESCO.
IMG_3234
Mjumbe wa bodi udhamini ya Mtandao wa Radio Jamii Tanzania (COMNETA), Balozi Mstaafu, Christopher Liundi akitoa pongezi kwa Shirika la UNESCO katika kuhamasisha Amani kupitia, Redio za Jamii, makongamano mbalimbali pamoja na kuwashirikisha viongozi wa dini kuhubiri Amani nchini katika mkutano huo.
IMG_3237
Mwandishi wa habari mkongwe, Halima Sharrif akitoa maoni katika mkutano huo.
IMG_3047
IMG_3069
Kutoka kushoto ni Ofisa miradi katika kitengo cha Mawasiliano na Tehama UNESCO, Nancy Kaizilege, Mratibu wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC), Mwanasheria Onesmo Olengurumwa, Mkuu wa ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linalohudumia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) nchini, Zulmira Rodrigues pamoja na Makamu wa Rais wa Chama cha Kijamii cha Wanasheria wa Tanganyika, Bi. Flaviana Charles katika picha ya ukumbusho.
IMG_3107
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Prof. Ole Sante Gabriel (kushoto) akifurahi jambo na Mhariri Mtendaji wa Gazeti la Tanzania Daima, Neville Meena mara baada ya zoezi la picha ya pamoja.