Pages

KAPIPI TV

Sunday, August 30, 2015

KESI YA TALAKA YA MMILIKI WA ST. MATHEW YAAHIRISHWA TENA

court_gavel
Na Mwandishi wetu
MAHAKAMA ya Mwanzo Kizuiani Mbagala, Dar es Salaam, imepanga Septemba Mosi mwaka huu kutoa hukumu katika kesi ya madai ya talaka na mgawanyo wa mali zenye thamani ya Sh Milioni 800 inayomkabili Mmiliki wa Shule ya Sekondari ya St. Mathew na St. Marks, Thadei Mtembei.

Hukumu hiyo ilipangwa kusomwa juzi lakini iliahirishwa kutokana na upande wa mlalamikaji kutofika mahakamani.

Akiahirisha kesi hiyo, Hakimu Rajab Tamambele alisema kuwa kesi hiyo ilikuja kwa ajili ya hukumu na kwamba itaendelea Septemba Mosi mwaka huu.

Mlalamikaji Magreth Mwangu anaiomba mahakama imuamuru mdaiwa kutoa Sh. Milioni 800 na makazi ya kukaa yeye na watoto wake.

Katika kesi hiyo, upande wa mlalamikaji ulikuwa na mashahidi wanne wakiwamo watoto watatu aliozaa na Mtembei ambao wanasoma katika shule za St Mary’s International na Hijra Seminari ya Dodoma.

Watoto hao walidai kuwa wanasumbuliwa ada shuleni na kwamba wanahitaji malezi yote kutoka kwa baba yao.

Pia waliieleza mahakama kuwa mara ya mwisho kumuona baba yao ni mwaka 2011.

Mtoto wa kwanza wa Mwangu alidai kuwa mwaka 2012 walifika katika Hoteli ya baba yao ya Sleep inn ndipo aliwafukuza na kuwaambia kuwa hawezi kuwalipia ada na badala yake aliwapa Sh 40,000 kila mmoja, fedha ambazo aliziacha mezani.

Pia walidai kuwa Mtembei aliwatolea maneno ya kashfa kwamba hata mama yao aende wapi, anao uwezo na kwamba anajeshi ambalo popote linafika.

 Aidha, kwa upande wa mdaiwa, ulikuwa na mashahidi watatu akiwemo Mtembei ambaye alikiri kuzaa na Mwangu na kwamba alitoa ng’ombe watano kama faini ya kuzaa naye.

Mutembei alidai alifahamiana na Mwangu wakati akiwa mfanya usafi katika duka lake la dawa na kwamba hakuwahi kuishi naye.

Hata hivyo, Agosti Mosi mwaka huu, mahakama hiyo ilihamia Singida kwa ajili ya kuthibitisha kama kweli mdai ameuza nyumba ambazo alizijenga pamoja na mdaiwa.

Kiongozi wa msafara huo ni pamoja na Hakimu Tamambele, karani wa mahakama, na ofisa ustawi wa jamii wa mahakama pamoja na mdaiwa, lakini ilidaiwa kuwa hakukuwa na mzee wa baraza ili kuthibitisha.

Aidha mlamikaji huyo alidai kuwa hatendewi haki kutokana na mahakama kusikiliza upande mmoja wa mdaiwa.

Saturday, August 29, 2015

UZINDUZI WA TAMASHA LA KUOMBEA AMANI TAIFA KUELEKEA UCHAGUZI MKUU KUFANYIKA OKTOBA 4, 2015 UWANJA WA TAIFA JIJINI DAR ES SALAAM

 Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion, waandaaji wa matamasha mbalimbali kama lile la Krismas na Pasaka, Alex Msama (kulia), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari ofisini kwake Dar es Salaam leo asubuhi kuhusu uzinduzi wa Tamasha la kuliombea Taifa kuelekea ucahguzi Mkuu utakaofanyika Oktoba 25 mwaka huu  utakaofanyika Oktoba 4, 2015 Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
 Mjumbe wa Kamati ya maandalizi ya tamasha hilo, Benno Chilele (kushoto), akizungumza katika tamasha hilo. Kulia ni  Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion, waandaaji wa Tamasha la Krismas na Pasaka, Alex Msama. 
 Mkutano na waandishi wa habari ukiendelea.
Waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali wakichukua taarifa hiyo.
(Imeandaliwa na mtandao wa www. habari za jamii.com-simu namba 0712-727062)

MSD YAZINDUA RASMI TAARIFA YAKE YA MWAKA 2013/2014 (ANNUAL REPORT)


 Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini wa MSD, Profesa Idris Ali Mtulia (kushoto), akikata utepe kuashiria uzinduzi wa taarifa ya MSD ya mwaka 2013/2014 uliofanyika Ofisi za MSD Keko jijini Dar es Salaam jana. Kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa MSD, Cosmas Mwaifwani.


 Kaimu Mkurugenzi wa Rasilimali Watu na Utawala wa MSD, Johnson Mwakalitolo, akizungumza katika uzinduzi huo.
 Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya MSD, Profesa Idris Ali Mtulia, akizungumza katika uzinduzi huo.
 Mkurugenzi wa Tehama  wa MSD, Issaya Mzolo, akizungumza katika hafla ya uzinduzi huo.
Ofisa Uhusiano Mkuu wa MSD, Etty Kusiluka (kushoto), akizingumza kwenye uzinduzi huo. Kulia ni Meneja wa Uhasibu wa MSD, Sako Mwakalobo.
Keki ya Birthday ya Kaimu Mkurugenzi wa MSD, Cosmas Mwaifwani katika muonekano.
Kaimu Mkurugenzi wa MSD, Cosmas Mwaifwani (kushoto), akikata keki hiyo aliyoandaliwa na wafanyakazi wenzake wakati wakimpongeza kutimiza miaka 55 ya kuzaliwa kwake. Kulia ni Katibu Muhtasi wa Mkurugenzi wa MSD, Doreen Josia. Wafanyakazi hao waliamua kumpongeza Mwaifwani baada ya kumalizika kwa uzinduzi wa ripoti hiyo.
Mwaifwani akimlisha keki, Mkurugenzi wa Shughuli za Kanda na Huduma kwa Wateja wa MSD, Edward Terry.
Hapa ni zamu ya Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya MSD, Profesa Idris Ali Mtulia akilishwa keki.
Mkurugenzi wa Shughuli za Kanda na Huduma kwa Wateja wa MSD, Edward Terry, akimlisha keki, Kaimu Mkurugenzi wa MSD, Cosmas Mwaifwani.
Hapa Katibu Muhtasi wa Mkurugenzi MSD, Dinah Dileya (kushoto), akilshwa keki.


Ofisa Uhusiano wa MSD, Benjamin Massangya (kulia), akigawa ripoti hiyo kwa wafanyakazi wa MSD.
Ofisa Uhusiano Mkuu wa MSD, Etty Kusiluka (kushoto), akizingumza kwenye uzinduzi huo.
Wafanyakazi wa MSD, wakifuatilia uzinduzi huo.
Wafanyakazi wa MSD, wakiwa kwenye uzinduzi huo.
Ni furaha tupu katika uzinduzi huo na hafla ya wafanyakazi hao kumpongeza Kaimu Mkurugenzi wa MSD, Cosmas Mwaifwani kutimiza miaka 55 tangu azaliwe.
Viongozi wa MSD wakiwa kwenye uzinduzi huo.
Hii ni timu ya wajumbe walioandaa ripoti hiyo ya mwaka 2013/2014. 'Big Up wajumbe kwa kazi nzuri'

Na Dotto Mwaibale

BOHARI ya Dawa (MSD) imezindua rasmi taarifa yake ya mwaka 2013/2014 (Annual Report), ambayo ilizinduliwa Dar es Salaam jana na Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini wa MSD, Profesa Idris Ali Mtulia.

Akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa taarifa hiyo, Profesa Mtulia alisema kupanda kwa huduma za usambazaji dawa, upatikanaji wa dawa kutoka asilimia 55 hadi 85 ni jambo la kujivunia.

Kaimu Mkurugenzi wa MSD, Cosmas Mwaifwani alisema mpango wa MSD kwa sasa ni kuanzisha maduka ya dawa ambayo yataendeshwa na MSD ambapo kwa kuanzia hivi karibuni litazinduliwa mkoani Mbeya na baadae itafuatia mikoa Kanda za  Dar es Salaam, Mwanza na Moshi. 

WHO YATOA DAWA ZA MILIONI 42.2 KUPAMBANA NA KIPINDUPINDU NCHINI

 Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Dk.Donan Mmbando (kushoto), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo asubuhi wakati akipokea msaada huo kutoka WHO. Kulia ni Mwakilishi wa Shirika la Afya Duniani (WHO), Nchini Dk. Rufaro Chatora.
 Taarifa ikitolewa kabla ya kupokea msaada huo.
 Hapa wakitiliana saini mkataba wa kupokea msaada huo.
Mwakilishi wa Shirika la Afya Duniani (WHO), Nchini Dk. Rufaro Chatora (katikati), akimkabidhi Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Dk.Donan Mmbando (kushoto), dawa ya maji zenye thamani ya sh.milioni 42.2 zilizotolewa na WHO kwa ajili ya kusaidia kukabiliana na magonjwa ya mlipuko nchini,  Dar es Salaam leo asubuhi. Anayeshuhudia tukio hilo kulia ni Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Uhakiki na Ubora wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Dk.Mohamed Ali Mohamed.

Na Dotto Mwaibale

SERIKALI imepokea msaada wa dawa ya  kutakasa maji ya Waterguard kutoka Shirika la Afya Duniani (WHO),kwa lengo la kukabiliana na magonjwa ya mlipuko zenye thamani ya sh. milioni 42.

Akizungumza Dar es Salaam leo asubuhi mara baada ya kupokea dawa hiyo, Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Donan Mmbando, alisema dawa hizo ni waterguard cotton (1000) na Cresol Saponated Liquid (100) litres  ambayo itasaidia kutakasa maji ili kuepusha magonjwa ya mlipuko kama kipindupindu. 

Alisema dawa hiyo itasaidia kudhibiti ugonjwa huo kwani kila siku zinavyozidi kwenda wagonjwa wanazidi kuongezeka hivyo dawa hiyo itatumika kupunguza maambukizi mapya.

"Hali ya mazingira bado hairidhishi idadi ya wagonjwa inazidi kuongezeka hadi sasa, tangu ugonjwa uanze kuripotiwa wagonjwa walioripotiwa kwa Dar es salaam ni 385 na vifo vya watu 8," alisema.

Alitaja mgawanyiko wa wagonjwa katika kila manispaa Kinondoni  292 , Ilala  60 na Temeke 33, aliongeza idadi ya wagonjwa waliopo kwenye kambi za matibabu hadi Agosti 27, jumla ni 74 ambapo kituo cha Mburahati 53 , Buguruni ikiwa na wagonjwa 14 huku Temeke 7.

"Kwa Mkoa wa Morogoro idadi ya wagonjwa hadi Agosti 28, wagonjwa 60 na walioko kambini ni 9 na kifo 1...moja ya sababu ambazo zinachangia kuendelea kua na ugonjwa huu hapa nchini ni kunywa maji yasiyo safi na salama,"alisema.

Mmbando alitoa tahadhali kwa wananchi kujizuia kunywa maji yasiyo safi na salama,kuepuka kula chakula kilichopoa au kuandaliwa katika mazingira yasiyo safi hali hiyo itasaidia kutokomeza ugonjwa huo na kuwataka kuchemsha  maji ya kunywa na kuweka dawa. 

Akikabidhi msaada huo  Mwakilishi Shirika la afya duniani (WHO), Dr. Rufaro Chatora alisema anamini dawa hizo zitasaidia kukabiliana na mlipuko wa ugonjwa wa  kipindupindu.

"Msaada huu tuliyotoa utasaidia wananchi kwa kiasi kikubwa katika kupunguza maambukizo mapya ya ugonjwa huu ambao huwa unaua kwa kiasi kikubwa,"alisema.

MBUNGE WA LUDEWA DEO FILIKUNJOMBE APINGWA KUPITA BILA KUPINGWA MCHAKATO WA UCHAGUZI MKUU

 Mgombea Ubunge Jimbo la Ludewa kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Msambichaka Mkinga (kushoto), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo asubuhi, wakati akipinga kupitishwa bila kupingwa mgombea mwenzake wa jimbo hilo kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Deo Filikunjombe na kudai kulikuwa na hujuma. Kulia ni Wakili wake, Paulo Kalomo.
  Mgombea Ubunge Jimbo la Ludewa kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Msambichaka Mkinga, akionesha fomu namba 10 ambazo alikabidhi kwa Msimamizi wa Uchaguzi. 
 Wakili wake, Paulo Kalomo, akizungumza katika mkutano huo kuhusu sheria inavyoelekeza.
Wanahabari wakichukua taarifa hiyo.



Na Dotto Mwaibale

MGOMBEA Ubunge wa Jimbo la Ludewa kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Msambichaka Mkinga amepinga vikali kupitishwa bila kupingwa mgombea mwenzake wa jimbo hilo kwa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Deo Filikunjombe na kudai kulikuwa na hujuma.

Mkinga alitoa malalamiko hayo mbele ya waandishi wa habari Dar es Salaam leo asubuhi na kueleleza kuwa sababu zilizotolewa na msimamizi wa uchaguzi wa jimbo hilo kuwa hakupeleka fomu namba 10 hazikuwa na ukweli wowote.

"Nilipofika ofisi ya msimamizi wa uchaguzi Jimbo la Ludewa nilisaini na kukabidhi tamko la kuheshimu na kutekeleza maadili ya uchaguzi ya mwaka 2015 (fomu namba 10) na baada ya kusaini nilimkabidhi msimamizi wa uchaguzi pamoja na fomu namba 8B,picha, stakabadhi ya malipo ya dhamana ambapo vilihakikiwa na Msimamizi Msaidizi wa Uchaguzi, Gervas Lupembe" alisema Mkinga.

Mkinga alisema katika jambo lisilo la kawaida msimamizi wa uchaguzi wa jimbo hilo hilo hakubandika kwenye ubao wa matangazo tamko hilo na alipomfuata msimamizi huyo kumuulizia msaidizi wake Lupembe alikiri kupokea na kuziwasilisha kwa kiongozi wake ili kutia saini ambaye naye alikiri kuzipokea lakini wakati ana bandika tamko hilo la Mgombea wa CCM fomu hiyo hakuiona.

Alisema katika pingamizi alilowekewa dai mojawapo ni kutokuwepo  tamko hilo kwenye fomu zake hali inayoonesha wazi kuwa kulikuwa na mchezo mchafu uliofanyika ili kumpitisha Filikunjombe bila kupingwa.

Mkinga alisema kuwa kuwaondoa wagombea kwa sababu zisizo za msingi ni kuiminya demokrasia na kuirudisha nchi nyuma kwani kunaweza kusababisha kukosa viongozi wazuri na kubakia na viongozi wasiofaa na wasiotaka kushindanishwa kwa kuwapa nafasi wananchi ya kumchagua kiongozi wanayemtaka.

Mgombea huyo alisema kutokana na sintofahamu hiyo alimuomba msimami wa uchaguzi wa jimbo hilo kutupiliambali pingamizi lililotolewa dhidi yake na mgombea mwenzake ambapo anasubiri majibu baada ya kuandika barua ya malalamiko.

ABBAS MAZIKU: MFANYABIASHARA ANAYETAMANI KUFUATA NYAYO ZA BILIONEA MO DEWJI

04.jpgk
Mfanyabiashara wa Kimataifa Abbas Maziku akiwa katika picha ya pamoja na Mfanyabiashara ambaye pia ni Bilionea kijana Barani Afrika, Mtendaji Mkuu wa kampuni ya MeTL Group, Mohammed Dewji, 'MO' amabaye anafuata nyayo zake katika kufikia malengo yake kibiashara.

Na Mwandishi Wetu
BIASHARA ya kusafirisha mazao ni miongoni mwa biashara zenye ushindani mkubwa kutokana na kutawaliwa na matajiri wenye asili ya Kiasia.

Kutokana na sababu hiyo imewafanya waafrika wengi kuwa na uthubutu katika biashara kwa kuhofia huenda wasifanikiwe na kujitanua kibiashara.

Mbali na ugumu huo lakini pia waafrika wengi hasa watanzania wamejikuta wakiishia kuwa wafanyabiashara ya kawaida na kupoteza fursa za kimataifa .

Kupoteza fursa muhimu za kimataifa kumefanya wakose fursa ambazo zingeweza kuwafanya wawe na mawazo mengine ya kuchangamkia fursa za kibiashara na kufikiri nje ya boksi.

Makala haya ndani ya mtandao huu yanaangazia mahojiano na mfanyabiashara wa kwanza wa kitanzania kufanya biashara ya kusafirisha Korosho kwenda nchini Vietnam aitwaye Abbas Maziku ambapo alielezea alipoanzia, vikwazo, mafanikio na matarajio yake kibiashara.

Alipoanzia

Maziku anasema alianza biashara ya kusafirisha mazao mnamo mwaka 2013 baada ya kuvutiwa na mjomba yake ambaye alikuwa na mashamba yaliyokuwa na mazao mbalimbali.
Miongoni mwa mazao ambayo Maziku alianza nayo na anaendelea nayo ni pamoja na Korosho, Ufuta, Mbaazi, Choroko, Mtama, Alizeti, Mashudu yapamba na pamoja na Pilipili Manga.

Anayapata wapi mazao?

Anasema mazao huyakusanya kutoka kwa wafanyabaishara wadogo wadogo ambao hukusanya mazao kwa wakulima pamoja na minada inayofanywa na vyama vya ushirika katika mikoa ya Lindi, Mtwara, Dodoma, Singida, Shinyanga na Tanga ambayo hufanyika mara moja kwa kila wiki.

Anayasafirisha kwa njia gani?

Akizungumzia jinsi anavyosafirisha mazao hayo, Maziku anasema hutumia usafiri wa barabara kuyatoa mikoani hadi kuyafikisha kwenye maghala ambayo hutumia kuyahifadhi kabla ya kufungasha.
"Wakati wa kuyafungasha unapofika huwa nayafungasha kwa kutumia vibarua na katika vifungashio vyangu huwa na nembo inayoonyesha jina la kampuni yangu na baada ya hapo sampuli hupelekwa katika maabara za kupima kupima ubora wa mazao kimataifa iitwayo SGS na ndipo hufuatiwa na hatua ya mwisho ya usafirishaji ambayo huwa natumia Meli za mashirika mbalimbali ikiwemo IPTL, MAERSK na nyinginezo kwa ajili ya kwenda nchini Vietnam", anasema Maziku.
Anabainisha baada ya hatua zote hizo hufuata taratibu zinazotakiwa ikiwemo watu wa Mamlaka ya mapato T.R.A, wataalamu kutoka Wizara ya Kilimo na Ufugaji, Wanasheria pamoja na maofisa wa usalama wa Taifa ambao uhakikisha hatua zote halali zimefutwa.
Maziku anaweka bayana kwamba kwa biashara za kimataifa taasisi kama Shirika la viwango TBS na mamlaka ya Chakula na Dawa huwa hawahusiki bali wahusika wakuu ni SGS.

Anajiendeshaje Kibiashara?

Maziku anajinasibu kuwa biashara ya mazao kupeleka nje ya nchi ni biashara yenye ushindani mkubwa hivyo anakumbuka alianza na mtaji wa sh 2,000,000 na sasa anazungumzia mtaji wa sh mil 200.
“Si rahisi kufika nilipofikia kwa sababu biashara hii ina ushindani mkubwa, ninashindana na matajiri wakubwa wenye uwezo wa kujipangia bei za mazao hivyo ingawa nimepiga hatua lakini bado ninahitaji kupanua biashara yangu zaidi na zaidi”, anasisitiza kwa hisia kali.
Anaeleza kuwa mwaka 2013 alipata hasara ya mamilioni ya pesa baada ya ubora wa mazao kupimwa na kuonekana upo kwenye kiwango cha 48 badala ya 51 inayotakiwa hivyo ilimpa wakati mgumu ambao aliyumba kibiashara kutokana na mtaji wake kukata hivyo ili mlazimu kuingia benki na kukopa pesa ambazo hadi sasa bado analipa deni hilo.
“Nilipata hasara kubwa sana ambayo hadi leo hii bado ninalipa hilo deni nililokopa benki ingawa pia fedha kutoka kwenye vyanzo mbalimbali vya mapato ya biashara zingine ninazozifanya zinaendelea kuifanya biashara hii ya mazao kwenda nje ya nchi iendelee kuwepo” anasema Mfanyabiashara huyo wa kimataifa.
 

Thursday, August 27, 2015

NEC YAKABIDHI POLISI MAJINA YA WATU 52,078 WALIOJIANDIKISHA ZAIDI YA MARA MBILI KATIKA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA

 Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Kailima Ramadhan (kushoto), akimkabidhi Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP), Benedict Wakulyamba orodha ya majina 52,078 ya watu waliojiandika katika daftari la kudumu la wapiga kura kwa mfumo wa BVR zaidi ya mara mbili Dar es Salaam leo, kwa ajili ya uchunguzi na baadae hatua za kisheria zichukuliwe kwa wahusika.
 Masanduku ya BVR yakiwa yamehifadhiwa Bohari ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi.
 Mkurugenzi wa Idara ya Daftari la mpiga kura, Dk. Sisti Cariah (kushoto), akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam leo kuhusu hatua waliyoifikia kuhusu daftari hilo na shughuli mbalimbali zinazoendelea kufanywa na NEC kuelekea uchaguzi mkuu.
 Mtaalami wa Tehama wa NEC, Fatuma Mkanguzi akiwaelezea wanahabari jinsi mfumo wa Tehama unavyofanyakazi.
 Fundi, Francis Skale akiwa kazini.
 Mafundi wa NEC wakiendelea na kazi.
 Mtaalamu wa mfumo wa ulinzi wa NEC, Adolf Kinyelo akitoa maelekezo ya jinsi ya mfumo huo unavyofanya kazi.
 Wanahabari wakichukua taarifa mbalimbali kuhusu NEC inavyofanyakazi zake na hatua waliyofikia kuelekea uchaguzi mkuu. 
Picha hii ni baadhi ya watu waliojiandikisha zaidi ya mara mbili katika daftari hilo.

Na Dotto Mwaibale


TUME ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imelikabidhi jeshi la polisi orodha ya majina ya watu zaidi ya 52,000 ambao wamebainika kujiandikisha zaidi ya mara moja kwenye daftari la kupigia kura kwa mfumo wa Biometric Voters Registration (BVR), akiwemo Diwani wa Kata ya Kimara, Pascal Manota (Chadema).

Idadi hiyo ilibainishwa Dar es Salaam leo na Mkurugenzi wa NEC, Ramadhan Kailima wakati wa ziara na waandishi wa habari katika bohari ya utayarishaji wa vitambulisho vya kupigia kura kwa mfumo wa BVR.

Akizungumza mara baada ya kukabidhi orodha ya majina hayo kwa Jeshi la Polisi, Kailima alisema watu hao watachukuliwa hatua kisheria kwani kujiandikisha zaidi ya mara moja ni kosa kisheria huku akiwatoa hofu wananchi waliojiandikisha na kutoonekana majina yao.

"Mchakato wa kutoa majina ni suala ya kisheria kwa sababu ukiangalia kifungu namba cha sheria ya uchaguzi namba 11 (a) kinasema baada ya kuboresha daftari tume itaweka wazi majina hayo ili watu waweze kupitia, lakini kifungu namba 23 cha sheria hiyo hiyo kinasema, iwapo mtu hataliona jina lake kwenye daftari anapaswa atoe taarifa kwa mkurugenzi wa uchaguzi au ngazi ya halmashauri ili taarifa zake ziweze kufanyiwa marekebisho,"alisema

Akizungumzia namna ya kupiga kura kwa walemavu wasioona, Kailima alisema hadi sasa wapo kwenye mchakato wa kuleta vifaa vya kupigia kura kwa kundi hilo ili kuwe na usiri wakati wa upigaji kura na kuepusha watu kupiga kura zaidi ya mara moja.

"Ijumaa (leo) mtashuhudia tukifanya maridhiano ya mwisho na kundi hilo, tumewashirikisha kwenye kikao chetu cha ndani na tukawapa wenyewe kazi ya kwenda kubuni aina ya karatasi za kupigia kura na tumewapa uhuru ambapo tutakubaliana nao na tuone mahitaji yao wenyewe kwa wale wanaojua kusoma maneno yao na wasioweza wapige kura,"alisema.

Kwa upande wa Msimamizi wa Kitengo cha Kufanya Marekebisho ya 'BVR Kit' na Kuchakata data, Aguta Obala alisema tuhuma za vitambulisho feki vilivyokamatwa hivi karibuni si ya tume ya uchaguzi.

"Hizo taarifa sina uhakika kwa sababu sijaona kama taarifa zinafanana na za hapa tume, lazima wahakikishe wametoa taarifa za vitambulisho hivyo kwenye BVR Kit ipi,"alisema.

Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP), Benedict Wakuryamba baada ya kupokea orodha hiyo alisema baada watu hao na taarifa zao zitafanyiwa upelelezi na kufikishwa mahakamani endapo atakutwa na hatia.

Naibu Katibu Mkuu wa Teknlojia ya Habari na Mawasiliano (Tehama) wa NEC, Dk. Sisti Cariah alisema kwa kutumia mfumo wa BVR ni vigumu mtu kujiandikisha zaidi ya mara moja kwani mfumo huo ni rahisi kumgundua huku akibainisha kurekebisha kasoro ndogo ndogo. 

Manota ajibu tuhuma

Akizungumza na mwandishi wa gazeti hili kuhusu kutuhumiwa kujiandikisha zaidi ya mara moja, Manota alisema tuhuma hizo si za kweli na kwamba alijiandikisha mara moja ambapo jina lake katika kitambulisho hicho halikuonekana vizuri.

Alisema kutokana na hali hiyo ilimpasa arudie kujiandikisha upya katika kituo hicho hicho huku ikiwa muda ni tofauti kutokana na msongamano wa watu katika mchakato wa uandikishaji.

"Nilipojiandikisha mara ya kwanza jina langu lilififia kwenye kitambulisho na hapo ndipo nilipoomba nijiandikishe tena ambapo nilivua koti na kupiga picha," alisema na kuongeza kuwa muandikishaji huyo alishindwa kurekebisha data 'edit'.

Manota alisema baada ya kujiandikisha upya kitambulisho cha awali alikiacha na kwamba kitambulisho hicho kipo halmashauri ya manispaa hiyo huku akiamini hiyo ni siasa na kumpigia kampeni.

Rufaa za ubunge 

Katika hatua nyingine, NEC imesema hadi kufikia jana rufaa za wagombea ubunge na udiwani katika maeneo mbalimbali nchini zilikuwa zimefikia 60.

Pia, imesema hadi kufikia Agosti 30 ya wiki ijayo rufaa 31 zitakuwa zimetolewa uamuzi, hivyo tume itakuwa katika nafasi nzuri ya kuzungumzia hilo.

Akizungumza na gazeti hili, Mkurugenzi wa NEC, Ramadhan Kailima alisema rufaa za ubunge zilikuwa 31 na udiwani 29 lakini zinaweza kuongezeka .

Hata hivyo, alitoa mwito kwa vyama ambavyo vitaona havikuridhika na matokeo kwa njia moja ama nyingine katika maeneo waliyogombea kuwasilisha rufaa zao tume hiyo kutokana na kutoridhishwa na wakurugenzi wa uchaguzi katika maeneo yao.

Alisema miongoni mwa chama kilichowasilisha rufaa zake tume ni ACT -Wazalendo ambacho kinalalamikia wagombea wake kutotendewa haki.

RUVU JKT ILIVYOWAKILISHA WIZARA YA ULINZI NA JESHI LA KUJENGA TAIFA KUONYESHA MAFANIKIO YA SHUGHULI MBALIMBALI ZA MAJESHI NCHINI

Wanahabari kutoka vyombo mbalimbali wakiwasili Kambi ya Jeshi la Kujenga Taifa Kikosi namba 832 Ruvu JKT mkoani Pwani jana kwa ajili ya kujionea shughuli mbalimbali za uzalishaji mali. Kikosi hicho kilichaguliwa kuiwakilisha Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), kuonyesha mafanikio ya majeshi nchini katika shughuli mbalimbali zikiwemo za uzalishaji mali ili kuinua uchumi wa taifa.
Mkuu wa Utawala na Mafunzo wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Brigedia Jenelari, Jacob Gedion Kingu, alikuwa mgeni rasmi katika ziara hiyo ya siku moja ya waandishi wa habari kutembelea kikosi hicho. Kingu alimwakilisha Mkuu wa JKT nchini.
Mkuu wa Utawala na Mafunzo wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Brigedia Jenelari, Jacob Gedion Kingu (kulia), akizungumza na wanahabari kabla ya kutembelea miradi mbalimbali inayofanywa na kikosi hicho.
Mkuu wa Kikosi  832 Ruvu JKT, Luteni Kanali Charles Mbuge, akizungumza na waandishi wa habari wakati akimkaribisha Mkuu wa Utawala na Mafunzo wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Brigedia Jenelari, Jacob Gedion Kingu kuzungumza na wanahabari katika ziara hiyo.
Mkuu wa Kikosi  832 Ruvu JKT, Luteni Kanali Charles Mbuge (kushoto), akiwaelekeza wanahabari wakati walipofika uwanja wa gwaride kuona vijana wa kidato cha sita wanaopitia JKT kwa mujibu wa sheria wanavyofanya mazoezi ya gwaride la kuhitimu mafunzo yao ya miezi sita mapema mwezi ujao.
Vijana wa kidato cha sita wanaopitia JKT kwa mujibu wa sheria wakionesha jinsi ya kukabiliana na adui kwa kutumia singe.
Mary Raphael kutoka mkoani Singida  mmoja wa vijana hao waliopo katika kambi hiyo kwa mujibu wa sheria akizungumza na waandishi wa habari baada ya kuonyesha jinsi ya kukabiliana na adui kwa kutumia singe.
January Sungura (kulia), akizungumza na wanahabari baada ya kuonesha jinsi ya kukabiliana na adui kwa kutumia singe.
Gelemaya Kibuga akizungumza na wanahabari.
Dk. Meja Agustino Maile akiwaeleza wanahabari mambo yanafuatwa kabla ya kumnyoa mteja katika saluni ya kisasa iliyopo katika kikosi hicho kwa kuzingatia afya na kuepuka maambukizi ya magonjwa mbalimbali.
Vijana wa mujibu wa sheria wakisubiri kunyolewa katika saluni hiyo.
Unyoaji katika saluni hiyo ukiendelea.
Rehama Hashim muuza wa duka katika kikosi hicho akiwaeleza wanahabari bidhaa zinazopatikana katika  duka hilo.
Hapa ni eneo la kiwanda cha kushona nguo ambapo vijana wanaopitia jeshi hilo kwa mujibu wa sheria wanapata mafunzo.
Wanahabari wakiangalia bweni lililojengwa kwa nguvu ya kikosi hicho kwa ajili ya kukabilana na uhaba wa vyumba vya kulala vijana hao.
Wanahabari wakiwa katika picha ya pamoja na mgeni rasmi Mkuu wa Utawala na Mafunzo wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Brigedia Jenelari, Jacob Gedion (katikati waliokaa mbele), pamoja na maofisa wa jeshi kutoka Makao Makuu ya JKT na Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa na Maofisa Habari kutoka Idara ya Habari Maelezo.
Vijana hao wakipiga kwata mbele ya wanahabari na mgeni rasmi.
Vijana hao wakionesha onyesho la kuruka vikwazo.
Onyesho la kuruka vikwazo likiendelea.
Hapa wakiendelea kuruka vikwazo.
Ni Gwaride bila ya kutumia bunduki.
Wanahabari wakiangalia Intaneti iliyojengwa kwa nguvu ya kikosini hicho kwa ajili ya kusaidia wanafunzi kuona matokea yao pamoja na mambo mengine ya masomo yao.
Vijana wakiwa katika intaneti hiyo.
Wanahabari wakiangalia mradi wa kuku wa nyama uliopo katika kikosi hicho.
Daktari wa Mifugo, Luteni  Ezekiel Mtani (kushoto), akiwaelezea waandishi wa habari kuhusu mradi wa kuku uliopo kikosini hapo.
Kuku wanaofugwa kikosini hapo wakiwa katika banda maalumu.
Wanahabari wakiangalia mabwawa ya samaki.
Msimamizi wa mradi wa samaki katika kambi hiyo, Luteni Kelvin Ngodo (katikati), akitoa maelezo ya mradi huo kwa waandishi wa habari.
Moja ya bwawa la samaki 
Bwana shamba wa kikosi hicho, Ndabemeye Ludovick Rwikima (kulia), akizungumza na wanahabari kuhusu mradi wa shamba la matunda kikosini hapo.
Bata maji wanaofugwa kikosini hapo wakiwa kwenye banda lao.
Msimamizi wa mradi wa bata maji Rachel Muuta (kushoto), akitoa maelezo kwa wanahabari.
Kilimo cha Vitunguu si Ilula pekee hata Ruvu JKT kinafanyika. Vijana wa JKT wakipalilia vitunguu. 
Msimamizi wa shamba la vitunguu, Koplo Robert Eliezer (kushoto), akizungumza na waandishi wa habari kuhusu kilimo cha vitunguu.
Utunzaji Mazingira. Wanahabari wakiangalia shamba la miti iliyipandwa na viongozi mbalimbali katika kikosi hicho.
Wanahabari wakiingia ulipo mradi wa usagishaji nafaka uliopo katika kikosi hicho.
Shughuli za usagishaji nafaka ukiendelea. usagishaji huo unafanywa na vijana wa JKT kwa mujibu wa sheria.
Wanahabari wakinagalia mradi wa usagishaji wa vyakula vya mifugo.
Burudani mbalimbali zikiendelea kutolewa na vijana hao.
Wanenguaji wa bendi ya JKT katika kikosi wakishambulia jukwaa.
Msemaji wa Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Luteni Kanali, Juma Sipe, akizungumza na wanahabari baada ya kumalizika kwa ziara hiyo ambapo aliwaomba wanahabari kuwa na ushirikiano na jeshi.
Mwakilishi wa wanahabari hao, Mwanahabari Kibwana Dachi, akitoa neno la shukurani baada ya kumalizika kwa ziara hilo.(Imeandaliwa na mtandao wa www.habari za jamii.com-simu namba 0712-727062)