Pages

KAPIPI TV

Wednesday, July 29, 2015

PAISHA YAZINDULIWA RASMI JIJINI DAR-ES-SALAAM.

Mgeni rasmi ambae pia ni rais wa Makampuni ya Convivium Africa Investment, Ndg Alfonso ippolito akizungumza machache wakati wa uzinduzi wa platform mpya ya matangazo iliyozinduliwa hapo jana katika hoteli ya serena.Paisha ni platform ya matangazo ambayo inapatikana kupitia simu za mkononi yaani smartphone na kupitia tovuti ambapo watumiaji wa simu za smartphone wanaweza kuipakua kupitia google play and playstore bure kabisa.
Meneja bidhaa wa Paisha, Godfrey Fataki akizungumzia jinsi paisha inavyofanya kazi na faida zake wakati wa uzinduzi wa platform hiyo uliofanyika jana katika hoteli ya serena
 Mgeni rasmi akifungua pazia kuashiria kuwa Paisha imezinduliwa rasmi 
Mtangazaji wa Redio Clouds Ephraim Kibonde akiwa katika picha ya Pamoja na Balozi wa Paisha wakati wa uzinduzi wa platform mpya ya matangazo iliyozinduliwa jana katika ukumbi wa Marquee Serena Hotel.
 Mdau akiwa pembeni ya mfano wa simu ya Iphone ambayo inaonyesha application ya Paisha.Paisha inapatikana kupitia playstore na google store bure na endapo utakuwa na application hiyo utaweza kufahamu na kupata huduma zote zitolewazo nchini huku wateja takribani Milioni 1 wameshajiunga huku watumiaji wakipata urahisi wa huduma hizo
tukipata selfie
 Black ryhino akipata selfie na mabest zake wakati wa uzinduzi huo
 Ni mwendo wa selfie tu
 Wadau wakifuatilia uzinduzi wa application ya Paisha
Picha zote na Josephat Lukaza wa Lukaza Blog
Paisha ni platform ambayo inapatika katika simu za smartphone pamoja na tovuti platform hii ni kwaajili ya watoa huduma na wauzaji wa bidhaa ambao wanapenda kuwafikia wateja wao kirahisi,Paisha inapatikana kupitia google play na playstore huku watumiaji wa paisha wananufaika kufahamu sehemu ambapo wanaweza kupata huduma mbalimbali kama vile maduka na hata huduma nyingine sehemu ambapo watuamiaji hao sio wenyeji au wenyeji lakini hawafahamu baadhi ya bidhaa zinapatikana wapi.
Ukiwa na application ya paisha katika simu inakusaidi kufahamu kuanzia ramani alipo mtoa huduma huyo pamoja na mawasiliano yake mfano umeenda tegeta na umepata pancha na haufahamu sehemu ilipo gereji ukiwa na paisha kwenye simu yako itakusaidia kufahamu ilipo gereji ambapo itakuonyesha jina la gereji iliyopo karibu na wewe hapo huku ikikuonyesha na ramani pamoja na mawasiliano ya gereji hiyo vilevile kwa bidhaa na huduma nyingine.
Ni application ambayo inawalete urahisi watumiaji na watangazaji wa bidhaa hizo kupitia paisha.kufahamu zaidi kuhusu paisha unachotakiwa kufanya ni tembelea tovuti yao ya www.paisha.co.tz na vilevile unaweza kupakua application hiyo kupitia playstore na google play sasa
Kuweza kupata faida zaidi

MAHOJIANO NA BALOZI AMINA SALUM ALI KWENYE KIPINDI CHA JUKWAA LANGU.

Mhe. Balozi Amina Salum Ali akifafanua jambo ndani ya Kilimanjaro Studio
Kipindi hiki ambacho kinakujia kila JUMATATU, kinajadili mambo mbalimbali na zaidi kuhusu UCHAGUZI MKUU WA TANZANIA 2015
Katika kipindi hiki utasikia mahojiano yetu na watu mbalimbali kuhusu DEMOKRASIA kuelekea uchaguzi nchini Tanzania
Katika kipindi cha wiki hii tumebahatika kuungana na Balozi wa Kudumu wa Umoja wa Afrika nchini Marekani Mhe. Amina Salum Ali
Karibu

MAZUNGUMZO NA MTANGAZAJI ROSE CHITALLAH KWENYE KIPINDI CHA JUKWAA LANGU

Mubelwa Bandio na Rose Chitallah studioni
Kipindi hiki ambacho kinakujia kila JUMATATU, kinajadili mambo mbalimbali na zaidi kuhusu UCHAGUZI MKUU WA TANZANIA 2015
Katika kipindi hiki utasikia mahojiano yetu na watu mbalimbali kuhusu DEMOKRASIA kuelekea uchaguzi nchini Tanzania
Katika kipindi cha wiki hii tumebahatika kuungana na mtangazaji Rose Chitallah
Karibu

Tuesday, July 28, 2015

LOWASSA AKABIDHIWA RASMI KADI YA CHADEMA


MMGL0885
Mwenyekiti wa Taifa wa Chadema,Freeman Mbowe akimkabidhi kadi ya uanachama wa chama hicho, Mh.Waziri Mkuu Mstaafu, Edward Lowassa leo katika hoteli ya Bahari Beach jijini Dar es Salaam.
MMGL0688
 Waziri Mkuu Mstaafu,Edward Lowassa akizungumza na mamia wakati wa kutangaza adhima yake ya kujiunga na Chadema katika Hoteli ya Bahari Beach jijini Dar es Salaam.
MMGL0816
 Waziri Mkuu Mstaafu,Edward Lowassa akijibu maswali ya waandishi wa habari juu ya kujunga kwake katika Hoteli ya Bahari Beach leo jijini Dar es Salaam.
Picha zaidi ingia Michuziblog

WAGOMBEA UBUNGE NDANI YA CCM WAENDELEA KUJINADI KWENYE KATA,WANANCHI WACHAMBUA MBIVU NA MBICHI

Emmanuel Mwakasaka akijinadi mbele ya wakazi wa kata ya Kiloleni ambapo aliwataka wamchague ili aweze kushirikiana nao katika kuleta maendeleo,katika mazungumzo yake wakati wa kujinadi aliepuka ahadi za uongo katika kutekeleza majukumu yake ya Ubunge endapo atapata ridhaa ya kuwa Mbunge wa Jimbo la Tabora mjini.Amesema kutokana na kutambua vema matatizo yanayowakabili wakazi wa Jimbo la Tabora mjini atahakikisha anayaunganisha makundi ya Wanawake,Vijana na Wazee na kutumia fursa zilizopo katika mfuko wa Jimbo kuwainua kiuchumi pamoja na kuwatafutia fursa nyinginezo zitakazokuwa chachu ya maendeleo kwa kushirikiana nao.Amesema atakuwa Mbunge wa kuwatumikia wananchi na kamwe hatowakimbia kama wanavyofanya Wabunge wengine ambao wanakabiliwa na Uchoyo wa kupindukia.  
Mkangala akijinadi kwa baadhi ya wakazi wa kata ya Kiloleni ambapo alihimiza umuhimu wa kuchagua viongozi wenye nia ya kuwatumikia wananchi huku akieleza kuguswa kwake na namna ambavyo viongozi waliopita walivyoshindwa kuleta maendeleo katika jimbo la Tabora mjini na hata kusababisha huduma za kijamii zikiwemo za Afya na nyinginezo kuwa kero kubwa kwa wananchi hususani akinamama wajawazito wanapokwenda kujifungua hospitali ya mkoa wa Tabora Kitete ambapo hukosa huduma zinazostahili kwa wakati muafaka.

Kamaliza Kayaga mgombea aliyejinadi kwa kuwataka wanaCCM  wamchague ili aweze kuwania nafasi ya Ubunge Jimbo la Tabora mjini ambalo wananchi wake wamekuwa na migogoro ya ardhi isiyokwisha kwakuwa yeye kitaaluma ni Mwanasheria hivyo amesema atatumia uwezo wake na elimu aliyonayo kusaidia kuondosha adha hiyo ambayo ni kero kubwa kwa wananchi,atafanya hivyo endapo atachaguliwa kuwa Mbunge na kuahidi kuwa akiwa Bungeni  atatetea baadhi ya Sheria kandamizi ziondolewe ili kumpa fursa wananchi kuishi katika mazingira yenye kuzingatia haki na usawa.  
William Masubi akijinadi mbele ya wananchi wa kata ya Kiloleni ambapo alizungumzia suala la elimu bora kwa wanafunzi pamoja na changamoto nyingine zinazokwamisha maendeleo ya Jimbo la Tabora mjini,aliahidi kuwa karibu na wananchi na kusikiliza kero zao kwakuwa yeye ni mkazi wa Tabora na hata kama endapo atachaguliwa kuwa Mbunge kamwe hatokuwa kama walivyo wabunge waliotangulia ambao baada ya kuchaguliwa wanakimbilia kuishi jijini Dar-es-salaam huku wananchi wakiendelea kukosa mtu wa kupokea na kufanyia kazi changamoto zinazowakabili.


Aden Rage ambaye ni mbunge aliyemaliza muda wake wakati akijinadi amewataka wanaCCM wampe ridhaa ya kuwania nafasi ya Ubunge kwa mara nyingine tena huku akidai kuwa yeye tayari ni mzoefu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  na kwamba  atawatumikia vyema kwa kuwaletea maendeleo,akipigia mfano wa Ujenzi wa barabara za lami,huduma za maji Tabora mjini,maboresho ya huduma za afya katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Tabora Kitete ingawa jambo hilo wananchi waliowengi walionesha kutokubaliana nalo kwakuwa huduma za afya hospitali bado haziridhishi na waathirika wakubwa ni akinamama wajawazito ambao wanalazimika kulala wawili wawili hadi watatu katika kitanda kimoja.

Bandora Mirambo amesema endapo atapata ridhaa ya wanaCCM na kufanikiwa kushinda katika uchaguzi mkuu atashirikiana na wananchi katika masuala mbalimbali ya maendeleo kwakuwa ofisi yake kama mbunge itafungua milango ya dawati la kusikiliza kero za wananchi huku akiwaasa kuwapima wagombea wote kwakumuangalia ambaye ana hofu ya MwenyeziMungu kwani ndiye atakuwa mgombea bora atakayewatumikia wananchi.Amesema tatizo la linalokwamisha maendeleo ya Jimbo la Tabora mjini ni kukosa Mbunge anayeyatambua matatizo yanayowakabili wananchi kwani kila anayechaguliwa kushika nafasi ya Ubunge wa Jimbo la Tabora mjini anasahau na kutowajali waliomuweka madarakani.



Amon Mkoga amejinadi kwa kuwataka wananchi wamchague kwani yeye ndiye mtu sahihi anayefaa kuwatumikia kwakuwa amekuwa akifanya mambo mengi ya Maendeleo hususani ya elimu kwa kuyahamasisha baadhi ya makampuni na mashirika kusaidia Shule za msingi na Sekondari,amesema endapo atapata ridhaa ya kuwania Ubunge na kufanikiwa atasaidia vikundi mbalimbali vya wajasiliamali kwa kuwapa elimu itakayowawezesha kuondokana na umasikini.

Monday, July 27, 2015

BASI LAGONGA TRENI YA MIZIGO NA KUUA WANNE - TABORA MJINI



Askari Polisi wakifanya ukaguzi kwa maiti zilizokutwa eneo la ajali hiyo

Kaimu kamanda wa Polisi mkoa wa Tabora ACP Juma Bwire akizungumza na waandishi wa habari katika eneo la tukio la ajali mbaya iliyotokea eneo la kata ya Malolo manispaa ya Tabora ambapo watu wanne walikuwa wamepanda basi hilo la kampuni ya Dont Worry ambapo lilisababisha ajali hiyo baada ya kugonga treni ya mizigo,watu kadhaa wamejeruhiwa vibaya na kulazwa hospitali ya mkoa wa Tabora Kitete.
Eneo la chini la basi hilo la kampuni ya Dont Worry ambalo lilisababisha ajali hiyo ambapo mbali na uzembe wa dereva lakini basi hilo lililokuwa likifanya safari zake kutoka Tabora mjini kwenda Ufuluma wilaya ya Uyui limeonekana sehemu hiyo ya chini imefungwa kamba za mipira kuzuia vyuma vinavyunganishwa na usukani visichomoke kitu ambacho ni hatari kwa usalama wa maisha ya wasafiri.





"NITALETA MABADILIKO MAKUBWA YA MAENDELEO KATA YA CHEYO"-YUSUPH KITUMBO

Mkurugenzi wa Kitumbo Security Guard Bw.Yusuph Kitumbo akisalimiana na baadhi ya akina mama wa Kata ya Cheyo wakati wa mkutano wa kujinadi kwa wajumbe wa halmashauri ya Kata wa Chama cha Mapinduzi ikiwa ni hatua ya kuomba ridhaa ya kuteuliwa kupata nafasi ya kuwa mgombea nafasi ya Udiwani kupitia CCM kata ya Cheyo manispaa ya Tabora......''Endapo nitapata ridhaa yenu na kushinda kwenye uchaguzi mkuu,nitahakikisha ninashirikiana na ninyi wananchi wenzangu kuleta heshima ya kata yetu ya Cheyo kwa kushughulikia kero mbalimbali zinazokwamisha maendeleo katani kwetu"alisema Kitumbo ambaye amekuwa akishiriki kikamilifu shughuli mbalimbali za kijamii na kusaidia vikundi vya akina mama,Waathirika wanaoishi na virusi vya Ukimwi ikiwa ni pamoja na kuwachimbia visima virefu.
Wagombea wa nafasi ya Udiwani wakiwa katika mkutano wa wajumbe kuomba ridhaa ya Chama ili wachaguliwe kuwania nafasi hiyo wakati wa Uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba mwaka huu.
Yusuph Kitumbo akiteta jambo  muhimu   na Diwani wa kata ya Cheyo aliyemaliza muda wake.
Baadhi ya akinamama wakiwa na shauku kubwa ya kuzungumza na mgombea udiwani kata ya Cheyo
"Wewe kama kijana wetu Kuna mambo muhimu ambayo utalazimika kuyashugulikia endapo utafanikiwa kupata nafasi hiyo ya udiwani na ninapenda kukuasa usitutupe kabisa sisi Wazee wako ambao kero zetu kubwa ni huduma za matibabu bure,wastaafu tumetelekezwa kabisa na Serikali,tunaomba pia tupatiwe mikopo  yenye masharti nafuu ili tufanye hata biashara ndogo ndogo"-Ndivyo mmoja kati ya Wazee wa kata ya Cheyo alisikika akimnong'oneza jambo hilo Bw.Kitumbo. 





MAHOJIANO NA CHARLES MAGALI NDANI YA WASHINGTON DMV

Charles Magali akiwa ndani ya Kilimanjaro Studio zinazomilikiwa na Vijimambo Radio, Kwanza Production na NesiWangu Media
Ijumaa ya Julai 24, 2015, mwigizaji na mwimbaji wa muziki nchini Tanzania Charles Magali alipata fursa ya kutembelea studio zetu zilizopo Beltsville Maryland. Hapo akazungumza nasi kwa ufupi
Karibu umsikilize akihojiwa na Mbunifu na Mtayarishaji wa kipindi hiki Dj Luke Joe na Mubelwa Bandio

MBUNGE CHIKU ABWAO WA CHADEMA AMFUATA ZITTO KABWE ACT-WAZALENDO


 Katibu wa Mipango na Mikakati wa Chama cha ACT-Wazalendo, Habibu Mchange (kushoto), akimkabidhi kadi ya chama hicho, aliyekuwa mbunge wa Viti maalumu kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Iringa mjini, Chiku Abwao baada ya kuhamia rasmi ACT-Wazalendo Dar es Salaam leo mchana.
 Mbunge Chiku Abwao (kulia), akionesha kadi ya chama cha ACT-Wazalendo baada ya kukabidhiwa.
  Mbunge Chiku Abwao (kulia), akizungumza na wanahabari baada ya kukabidhiwa kadi ya chama cha ACT-Wazalendo.

Friday, July 24, 2015

UZINDUZI WA KAMPENI YA WAZAZI NIPENDENI AWAMU YA PILI WAFANYIKA VIWANJA VYA MWEMBE YANGA TEMEKE JIJINI DAR ES SALAAM LEO

 Mkurugenzi wa Huduma za Kinga Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Dk.Neema Rusibamayila kwa niaba ya Waziri wa wizara hiyo Dk. Seif Rashid  (wa pili kushoto), akikata utepe kuashiria uzinduzi wa  kampeni ya Wazazi Nipendeni awamu ya pili  katika viwanja vya Mwembe Yanga Temeke Dar es Salaam leo mchana. Wa kwanza kushoto ni Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo ya Kimataifa la Marekani (USAID), Anna Bodipo Memba na wa pili kulia ni Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Grace Magema. 
 Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo ya Kimataifa la Marekani (USAID), Anna Bodipo Memba (kulia), akitoa hutuba yake kwenye uzinduzi huo.
 Mshauri wa masuala ya Afya ya Jamii kutoka Taasisi ya HBC, Mdadike Thabit (kulia), akimuelekeza jambo mgeni rasmi katika uzinduzi huo Mkurugenzi wa Huduma za Kinga Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Dk.Neema Rusibamayila wakati alipokuwa akitembelea mabanda ya watoa huduma kabla ya kufanyika uzinduzi huo.
 Wananchi wakiwa wamejipanga foleni kwa ajili ya kupata huduma za afya ya jamii kwenye uzinduzi huo.
 Wanamuzi wa bendi ya muziki wa dansi ya FM Academia 
wakitoa burudani.
 Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Grace Magema akizungumzia mikakati ya Afya ya Jamii katika mkoa huo.



 Mkurugenzi wa Huduma za Kinga Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Dk.Neema Rusibamayila, akitoa hutuba yake ya uzinduzi.
 Watoto nao walikuwepo kwenye uzinduzi huo.
 Mwanamuziki Juma Nature akitoa burudani kwenye uzinduzi huo.
 Wananchi walioshiriki uzinduzi huo.
Kiongozi wa kundi la muziki la Wanaume Family, Chege (kulia), akishambulia jukwaa katika uzinduzi huo.
Msanii wa kundi la utamaduni la HD Entertainment la Mbezi Beach, Michael Kamugisha, akiwa ameruka juu wakati wa kundi hilo lilipokuewa likitoa burudani katika uzinduzi huo.


Na Dotto Mwaibale

TANZANIA imeweza kufikia lengo la milenia namba 4 la kupunguza vifo vya watoto kwa theluthi mbili kutoka vifo 152 hadi 54 kwa kila watoto 1,000 wanaozaliwa hai.

Hayo yalibainishwa na Mkurugenzi wa Huduma za Kinga Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Dk.Neema Rusibamayila kwa niaba ya Waziri wa wizara hiyo Dk. Seif Rashid wakati akizindua kampeni ya awamu ya pili ya Wazazi Nipendeni katika viwanja vya Mwembe Yanga Temeke Dar es Salaam leo mchana.

Alisema pamoja na kutofikia lengo la melenia namba 5 la kupunguza vifo vitokanavyo na uzazi kwa robo tatu kufikia vifo 193 kwa kila vizazi hai laki moja, taarifa za umoja wa mataifa za mwaka 2014 zinaonyesha kuwa Tanzania imeweza kupunguza vifo hivyo toka 770 kwa kila vizazi hai 100,000 mwaka 1990 hadi kufikia 410 kwa kila vizazi hai 100,000 mwaka 2014.

"Sababu zinazosababisha watoto waliochini ya miaka mitano kupoteza maisha ni kuharisha, nimonia na malaria na kuwa zinachangia takribani asilimia 50 ya vifo vya watoto hao waliochini ya miaka mitano" alisema Dk.Rusibamayila.

Alisema utapiamlo nao ni tatizo linalochangia vifo vya watoto hao kwani takwimu za mwaka 2010 zinaonyesha kuwa kiwango cha udumavu ni asilimia 42 kwa watoto waliochini ya umri wa miaka mitano.


Dk.Rusibamayila aliongeza kuwa vifo vya watoto wachanga havijapungua kwa kasi inayoridhisha na vinachangiwa na wale watoto wanaozaliwa njiti, kushindwa kupumua vizuri mara baada ya kuzaliwa na maambukizi ya bakteria.