Pages

KAPIPI TV

Wednesday, May 20, 2015

SERIKALI YAIAGIZA HALMASAHAURI YA WILAYA YA KALIUA KUWALIPIA KADI ZA CHF WALEMAVU NA WAZEE WASIOJIWEZA

Mkuu wa wilaya ya Kaliua Bw.Venas Mwamoto akizungumza na wadau wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya wilayani humo ambapo alitoa agizo la Serikali kwa Halmashauri kuanza utaratibu wa kuwalipia Kadi ya Mfuko wa Afya ya Jamii Walemavu na Wazee wasiojiweza fedha ambazo ameamuru zitoke kwenye mfuko wa maendeleo kuanzia ngazi za vijiji.
Meneja wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya kanda ya Magharibi Bw.Emmanuel Adina akisoma taarifa fupi ya uanzishwaji wa Mfuko wa Afya ya Jamii wilayani Kaliua ambapo alihimiza Viongozi wa Serikali na Vyama vya Siasa kuifanya ajenda ya CHF ni muhimu kila wanapopata fursa ya kuzungumza na Wananchi katika mikutano mbalimbali hatua ambayo itasaidia kuihamasisha jamii kujiunga na CHF.
Dr.Gunini Kamba mganga mkuu mkoa wa Tabora akizungumzia umuhimu wa wananchi kujiunga na Mfuko wa Afya ya Jamii CHF,na kueleza mkakati mzima namna ambavyo mwananchi anaweza kunufaika atakapochangia Mfuko huo wa Afya ya Jamii.
Wadau wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya wilayani Kaliua  wakipata elimu kuhusu faida za Mfuko wa Afya ya Jamii CHF.







MO AKUTANA NA RAIS FILIPE NYUSI WA MOZAMBIQUE JIJINI DAR

IMG-20150518-WA0054
CEO wa Makampuni ya MeTL Group na Mbunge wa Jimbo la Singida mjini, Mh. Mohammed Dewji (kulia) katika picha ya pamoja na Rais wa Mozambique, Mh. Filipe Nyusi walipokutana jijini Dar es Salaam. Rais huyo anayefanya ziara yake ya kwanza nje ya nchi kama Rais wa Msumbiji yuko katika ziara rasmi ya siku tatu nchini Tanzania.

UNESCO WATOA MAFUNZO YA TEHAMA KWA WALIMU WA VYUO VYA UALIMU HAPA NCHINI

 
Head of India Tanzania Center of Excellence in ICT (DIT), Dr. Amos Nungu akiwakaribisha wafanyakazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), wakufunzi pamoja na walimu waliofika kwenye mafunzo ya elimu kwa njia ya mtandao.(Picha zote na Geofrey Adroph wa pamoja blog).
Afisa mipango kutoka UNESCO, Bi Faith Shayo akimkaribisha Ofisa anayeshughulikia na masuala ya Elimu Kitaifa wa UNESCO, Tumsifu Mmari (wa kwanza kutoka kushoto) wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya elimu kwa njia ya mtandao kwa walimu wa vyuo vya elimu
Ofisa anayeshughulikia masuala ya Elimu Kitaifa wa UNESCO, Tumsifu Mmari akifungua mafunzo kupitia njia ya mtandao iliyoandaliwa na UNESCO yaliyofanyika jijini Dar.
Bi. Eunice Gachoka kutoka Kenya Institute of Curriculum Development akijitambulisha kwa walimu (hawapo pichani) waliofika kwenye mafunzo ya kupitia mtandao.
Daudi Mbona mkufunzi kutoka chuo cha DIT akiendelea kutoa mafunzo kwa baadhi ya walimu walioudhuria mafunzo ya kupitia njia ya mtandao yaliyofanyika kwenye chuo cha Dar es Salaam Institute of Technology (DIT) hapa jijini Dar.
Godfrey Haongo mkufunzi kutoka Open University nchini Tanzania akitoa elimu ya njia ya mtandao.
Baadhi ya walimu wanaoshiriki mafunzo hayo. 
  

Na Geofrey Adroph, Pamoja blog  

 UNESCO imeaandaa mafunzo ya uboreshaji wa elimu kwa walimu hususani katika somo la Tehama kwa vyuo mbalimbali vya hapa nchini vinavyotoa elimu ya ualimu. Mafunzo hayo yaliyoandaliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania yamefanyika katika chuo cha Dar es Salaam Institute of Technology (DIT) ili kuweza kuwapa fursa hiyo waalimu wa vyuo mbalimbali katika ufundishaji na uelimishaji namna ya matumizi ya Tehama. 

  Hii inatokana na baada ya mkutano wa viongozi wa vyuo mbalimbali pamoja na wadau wa elimu wa hapa nchini Tanzania hivyo kuona kama kuna mapungufu katika masuala la uelewa na matumizi ya Tehama hasa katika vyuo hivyo.  

Baada ya kuona kuna mapungufu hayo UNESCO waliamua kuanzisha mradi uitwao UNESCO-China Funds in Trust Project (CFIT) wakishirikiana na vyuo vya elimu hapa nchini Tanzania waliamua kuanzisha mradi huo kwa malengo makuu matatu ambayo ni kuboresha elimu kwa walimu wa vyuo vya ualimu, kuweka mafunzo ya walimu wanapofundisha katika Tehama ili kuendana na mabadiliko ya teknolojia pamoja na kuwanunulia vifaa vya Tehama ambavyo vitasaidia katika kufundishia na kujifunzia, 

Afisa mipango kutoka UNESCO, Bi Faith Shayo alivitaja vifaa hivyo kwa kuviorodhesha kuwa ni pamoja na kompyuta, Projecta, na Sola ili kuhakikisha hakuna tatizo la umeme katika ufundishaji wa masomo hayo .  

Kupitia mradi huo wa (CFIT), UNESCO imeandaa mafunzo ya siku tano kwa walimu wa vyuo vya ualimu kutoka vyuo mbalimbali vya Elimu hapa nchini Tanzania ili kuongeza ujuzi na ufanisi katika ukuzaji wa Tehama hasa kupitia kwenye njia ya mtandao na pia kuendana na wakati kutokana na mabadiliko pamoja na ukuaji wa matumizi ya Teknolojia Mafunzo haya yaliyoandaliwa na UNESCO yanafanyika katika chuo cha Dar es Salaam Institute of Technology (DIT) kwa ajili ya kuwapa elimu kwa baadhi ya walimu wa vyuo ili kupata uelewa zaidi juu ya Tehama.  

Wakufunzi wa mafunzo hayo ni Daudi Mboma ambaye ni Mkuu wa idara ya maendeleo ya biashara kutoka (DIT) na Godfrey Haongo kutoka Open University of Tanzania ambao wanajukumu la kuwafundisha walimu mbalimbali kutoka vyuo tofauti hapa . Waalimu tisa kutoka chuo cha ualimuTabora, waalimu tisa kutoka chuo cha ualimu Monduli , walimu wanne kutoka chuo cha ualimu Morogoro, mmoja kutoka Shule direct, wawili kutoka Chuo kikuu cha Nelson Mandela, mmoja kutoka Ngorongoro Waso District, pia kuna baadhi ya watakao pata mafunzo hayo wanatokea Wizara ya elimu ambao wanafanya kazi kwa ushirikiano na UNESCO ili kuweza kufikia malengo ya mradi huo kwa vyuo vya elimu hapa nchini.  

Kutokana na kuwa na uelewa mdogo wa masuala ya Tehama UNESCO wamejipanga kuweza kupambana na kutoa mafunzo ya kiteknolojia ili kuweza kuboresha matumizi na upatikanaji wa huduma za kitehama katika taifa la Tanzania kwa kuanzisha mradi huo wa kutoa mafunzo kwa walimu nao walimu waweze kwenda kuutumia ujuzi huo katika ufundishaji kwenye vyuo wanavyofundisha ilikuweza kuwapa upeo mkubwa wanafunzi wa ualimu ambao ndio watakao kuwa kipaumbele katika kufanya nchi iwe katika mfumo mzuri wa Tehama.

NHC YAFUNGUA RASMI KITUO CHA HUDUMA KWA WATEJA.

Mkurugenzi wa Shirika la Nyumba la Taifa, Nehemia Kyando Mchechu akizungumza kuashiria uzinduzi rasmi wa kituo cha huduma kwa wateja cha Shirika hilo uliofanyika kwenye ukumbi wa Kituo hicho kilichopo Makao makuu ya Shirika barabara ya Ufukoni na Ali Hassan Mwinyi, jijini Dar es salaam, Kulia kwake ni Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Huduma kwa Jamii, Susan Omari.
Pichani ni baadhi ya waandishi wa habari wanaoshuhudia tukio hilo .
Maofisa wa Shirika la Nyumba wanaokiendesha kituo hicho kipya cha huduma kwa Wateja wakiwa kazini mara baada ya kuzinduliwa, timu ya kituo hicho inaongozwa na mwanahabari Mzoefu Domina Rwemanyila.
Mkurugenzi waShirika la Nyumba la Taifa, Nehemia Kyando Mchechu akizungumza kuashiria uzinduzi rasmi wa kituo cha huduma kwa wateja cha Shirika hilo uliofanyika kwenye ukumbi wa Kituo hicho kilichopo Makao makuu ya Shirika barabara ya Ufukoni na Ali Hassan Mwinyi, jijini Dar es salaam, Kulia kwake ni Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Huduma kwa Jamii, Susan Omari.
Mkurugenzi waShirika la Nyumba la Taifa, Nehemia Kyando Mchechu akizungumza kuashiria uzinduzi rasmi wa kituo cha huduma kwa wateja cha Shirika hilo uliofanyika kwenye ukumbi wa Kituo hicho kilichopo Makao makuu ya Shirika barabara ya Ufukoni na Ali Hassan Mwinyi, jijini Dar es salaam, Kulia kwake ni Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano kwa Umma na Huduma kwa Jamii, Susan Omari.
Maofisa wa Shirika la Nyumba wanaokiendesha kituo hicho kipya cha huduma kwa Wateja wakiwa kazini mara baada ya kuzinduliwa, timu ya kituo hicho inaongozwa na mwanahabari Mzoefu Domina Rwemanyila.
Maofisa wa Shirika la Nyumba wanaokiendesha kituo hicho kipya cha huduma kwa Wateja wakiwa kazini mara baada ya kuzinduliwa, timu ya kituo hicho inaongozwa na mwanahabari Mzoefu Domina Rwemanyila.
Wakurugenzi wa Shirika hilo wakishuhudia tukio la kuzinduliwa kwa tukio hilo
Pichani ni baadhi ya waandishi wa habari wanaoshuhudia tukio hilo .
Picha zaidi za tukio la uzinduzi huu tutawaleteeni baadaye.
&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&

SHIRIKA LA NYUMBA LA TAIFA

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI KUHUSU UZINDUZI WA KITUO CHA HUDUMA KWA WATEJA KWA NJIA YA SIMU NA MALIPO YA KODI KWA MFUMO WA SIMU ZA KIGANJANI – MEI 19, 2015
.................................................................................................
Katika jitihada za Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) kuboresha huduma kwa wateja kama ilivyoainishwa kwenye Mkataba wa Huduma kwa Mteja, leo Shirika la Nyumba la Taifa linazindua huduma mbili, ambazo ni kituo cha huduma kwa wateja na pili ni mfumo wa kulipa kodi za nyumba kwa kutumia simu ya kiganjani.

Kituo cha huduma kwa wateja kwa njia ya simu kitatumika kuhudumia wateja wetu wote kwa kupiga simu pale wanapohitaji kufahamu juu ya huduma zetu na bidhaa mbalimbali pamoja na kutoa taarifa mbalimbali za shirika zinazohusu huduma kwenye makazi yao. 

Wateja wataweza kupata huduma hii kupitia nambari +255 784 105 200 na + 255 222 162 800. Kupitia kituo hiki Shirika linawaahidi kwamba maulizo na taarifa zozote zitakazoripotiwa zitapewa kipaumbele kwa kupatiwa ufumbuzi haraka iwezekanavyo.

Katika kuendelea kuboresha mfumo wa ukusanyaji kodi kutoka kwa wapangaji wetu, Shirika limeanzisha mfumo wa kulipa kodi kupitia simu za kiganjani ili wapangaji waweze kufanya malipo ya kodi zao bila ya usumbufu wowote kupitia tigopesa, mpesa na airtel money. 

Kupitia mfumo huu, wapangaji wataweza kufanya malipo kwa kutumia simu zao na wataweza kuhamisha fedha kutoka kwenye benki akaunti zao na kwenda Shirika la Nyumba mahali popote walipo na kwa muda wowote ambao ni muafaka kwao bila ya kufika katika vituo vyetu vya makusanyo ya kodi.

Monday, May 18, 2015

TAKWIMU ZAKWAMISHA UPATIKANAJI WA MAENDELEO


Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango Zanzibar, Bi Amina Shabani akifungua semina ya siku moja ya kujadili mpango utekelezaji wa Maendeleo ya Malengo ya Millenia MDG’s, iliyofanyika katika Hoteli ya Zanzibar Beach Resort Mazizini Zanzibar na kuwashirikisha Maofisa Mipango wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na Viongozi wa Taasisi zisizo za Kiserekali, ulioandaliwa na Tume ya Mipango Zanzibar na Wizara ya Mambo ya Nje Tanzania na kufadhiliwa na UNDP. Na Mwandishi wetu, Zanzibar UKOSEFU wa takwimu sahihi katika masuala mbalimbali umeelezwa kuchangia kutopiga hatua kwenye mipango ya kimaendeleo inayopangwa na serikali juu ya wananchi. Aidha upotoshaji wa takwimu hizo unaofanywa na baadhi ya watendaji kwa kutaka kujinufaisha wao wenyewe pia umekuwa ukichangia kuchelewa hatua za kimaendeleo. Hayo yameelezwa na Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango ya Zanzibar, Amina Shaaban wakati akifungua semina ya siku moja ya kujadili Malengo ya Millenia baada ya 2015 iliyofanyika mjini hapa. Amina alisema, kuwa takwimu ndiyo zinaonesha hali halisi na pia zinawezesha fedha kutoka kulingana na mahitaji, hivyo ni muhimu kuzingatiwa kwa jambo hilo ili mipango ya maendelo iweze kufanyika kwa wakati. "Kulikuwa na kamati ile ya ufundi na ya muda, siku hizi hazipo kama zimekufa ni vyema zikarudishwe tena maana zilikuwa na jukumu la ufuatiliaji na kutukumbusha mara kwa mara," alisema Amina. Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Masuala ya Kiuchumi (ESRF), Dk. Oswald Mashindano alisema, semina hiyo inalenga kujadaili utekelezaji wa malengo ya millenia kabla ya kumalizika Septemba, mwaka huu na ajenda mpya ya maendeleo baada ya Septemba, mwaka huu. Aidha alisema, nchi nyingi hazijakuwa na uwezo wa kutekeleza malengo ya millenia ikiwemo Tanzania, hivyo kutokana na hali hiyo ilikubalika kuwepo kwa ajenda mpya ya maendeleo baada ya Septemba, mwaka huu. "Kwa sisi Tanzania kidogo tuna bahati ya kuiga hatua kidogo, lakini pamoja na kutimiza baadhi ya malengo, bado kuna maeneo ambayo hatujafanikiwa sana na moja kati ya sababu iliyofanya tukwame ni pamoja na ukuaji wetu wa uchumi," alisema. Akizungumzia kuhusu kamati za ufundi na ya muda, Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kiamatifa wa Wizara ya mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Celestine Mushy alisema, kuwa suala hilo atalirudisha kwenye tume ya mipango ya Tanzania Bara ili liweze kushughulikiwa kwa wakati. Hata hivyo alisema, ili nchi iweze kupiga hatua katika mikakati ya maendeleo ni muhimu kwa sekta binafsi kushiriki kwa mstari wa mbele kutokana na kuwa nafasi kubwa katika kuendeleza maendeleo na uchumi wa taifa. "Sekta binafsi wao ndiyo wenye pesa nyingi sana kuliko serikali, ukiangalia hata katika nchi zilizoendelea sekta binafsi kwa kiasi kikubwa zimechangia sehemu kubwa ya maendeleo yao," alisema Balozi Mushy. Balozi Mushy alisisitiza umuhimu wa takwimu sahihi kwa kuwa ndiyo silaha pekee katika kufanikisha mipango ya kimaendeleo kukamilika kwa wakati. Semina hiyo iliwashirikisha wataalamu wa tume ya mipango ya Zanzibar na tasisi zingine za serikali ilikuwa inalenga kuwajengea uwezo na kujadili ajenda 17 ya Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDGs) na mipango ya maendeleo baada ya kukamilika kwa Malengo ya Maendeleo ya Millenia (MDGs) Septemba, mwaka huu.
Washiriki wa mkutano huo wakifuatilia hutuba ya Katibu Mtendaji Bi Amina Shabani akifungua mkutano huo.
Mwakilishi wa UN Zanzibar Bi. Anna Senga akitoa salamu za Umoja wa Mataifa (UN) wakati wa mkutano wa kupitia mafanikio ya Maendeleo ya Malengo ya Millenia MDG's.
Washiriki wakiwa katika ukumbi wa Mkutano hoteli ya Zanzibar Beach Resort Mazizini Zanzibar. wakifuatilia mada zinazotolewa wakati wa mkutano huo.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Masuala ya Kiuchumi (ESRF), Dk Oswald Mashindano akifafanua jambo wakati wa mkutano wa kupitia mafanikio ya Maendeleo ya Malengo ya Millenia MDG's Tanzania uliofanyika katika hoteli ya Zanzibar Beach Resort Mazizini Zanzibar.
Washiriki wakiwa katika ukumbi wa mkutano wakifuatilia kwa utulivu michango na mada zilizoku zikiwasilishwa.
Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa Wizara ya Mambo ya Nchi za Nje na Ushirikiano Wa Kimataifa Balozi Celestine Mushy akiwasilisha mada jinsi mataifa yalivyofikia SDGs, michakato inayoendelea na namna ambavyo Tanzania inaweza kunufaika na mkakati mzima wa maendeleo.
Balozi Celestine Mushy akisisitiza jambo wakati wa mkutano huo .
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Masuala ya Kiuchumi (ESRF), Dk Oswald Mashindano akiwasilisha mada ya "Elucidating SDG 17 on means of implementation and Global Partnership for Development and Financing of Post MDG's Development Agenda".
Washiriki wakiwa katika ukumbi wa mkutano wakifuatilia mada zinazowasilishwa na wahusika.
Dk. Kenneth Mdadila, Mhadhiri kutoka Chuo Kikuu cha Dar-es-Salaam Idara ya Uchumi akiwasilisha mada ya "Tanzania's preparedness in Monitoring Sustainable Development Goals- Analysis Based on Global Indicator Framework" katika semina hiyo..
Pichani juu na chini ni washiriki wa semina ya siku moja ya kujadili Malengo ya Millenia baada ya 2015 iliyofanyika mwishoni mwa wiki visiwani Zanzibar.
Pichani juu na chini ni Maofisa mipango wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na viongozi wa taasisi zisizo za Kiserikali wakishiriki kuchangia mada katika semina hiyo ya siku moja iliyofadhiliwa na UNDP.
Mdau Yasser Manu kutoka ESRF.
Washiriki wakichangia mada zilizowakilishwa wakati wa semina ya siku moja iliofanyika katika ukumbi wa hoteli ya Zanzibar Beach Resort Mazizini Zanzibar.

WAZIRI BERNALD MEMBE KWA MGENI RASMI TAMASHA LA QASWIDA MEI 25

Q1
Jumanne Ali Ligopora Mkurugenzi wa Taasisi ya Ulamaa Qaswida Promotion Centre akizungumza na waandishi wa habari kwenye hoteli ya Traveltine Magomeni jijini Dar es salaam wakati akizungumzia mashindano ya kuimba Qaswida yatakayofanyika kwenye viwanja vya shule ya Sekondari ya Benjamin Mkapa mgeni rasmi akiwa Waziri wa mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mh. Bernald Membe.Tamasha hilo litafanyikaMei 25 kuanzia saa saba mchana, Kulia ni Sheikh Muharami Pembe na kushoto ni Ustaadhi Jumanne Gereza.
Q2
Jumanne Ali Ligopora Mkurugenzi wa Taasisi ya Ulamaa Qaswida Promotion Centre akiwa ameongozana na viongozi mbalimbali wa taasisi hiyo wakizungumza na waandishi wa habari kwenye hoteli ya Traveltine Magomeni jijini Dar es salaam kuhusu Tamasha la Qaswida litakalofanyika Mei 25 kwenye viwanja vya Sekondari ya Benjamin Wiliam Mkapa Kariakoo.
Q3
Jumanne Ali Ligopora Mkurugenzi wa Taasisi ya Ulamaa Qaswida Promotion Centre akisisitiza jambo katika mkutano huo.