Pages

KAPIPI TV

Saturday, April 25, 2015

WADAU WA KISWAHILI SIKU YA CHAUKIDU CHUO KIKUU CHA HOWARD


 Asha Nyang.anyi akiwa kwenye meza akikagua majina ya wadau wa Kiswahili kwenye sherehe ya  Chama Cha Ukuzaji Wa Kiswahili Duniani (CHAUKIDU) inayoendelea sasa hizi chuo kikuu cha Howard kilichopo Washington, DC na Rais msataafu Ali Hassan Mwinyi atakua mgeni rasmi.
Wadau wa Kiswahili wakiendelea kuingia ukumbini.
 Wadau kutoka Zanzibar wakipata picha
 Walimu wa kiswahili wa vyuo mbalimbali wakipata picha ya pamoja.
 wadau wa Kiswahili wakihudhuria sherehe ya CHAUKIDU
 Walimu na maporofesa wa vyuo wakiwa ndani ukumbi wa Blackburn Center siku ya Alhamisi April 23, 2015 chuo kikuu cha Howard kilichopo Washington, DC.
 Wadau wa Kiswahili wakibadilishana mawili matatu.
Wadau wa Kiswahili wakilonga Picha zaidi Baadae

Thursday, April 23, 2015

WANAFUNZI WA SHULE YA MSINGI YA BAJAVERO DAR WAPATA MAFUNZO JUU YA HEDHI SALAMA

 Mratibu wa Mradi wa Afya wa Help Kids Edith Peter Mziray akiwasihi wanafunzi kuwa wasikivu wakati wa semina ya Hedhi salama

Mkurugenzi mtendaji wa Kasole Secrets Hyasintha Ntuyeko ambao pia ni waandaaji wa siku ya Hedhi Duniani kwa Tanzania akiwauliza wanafunzi wa Darasa la tano hadi la saba changamoto wazipatazo wakati wanapoingia katika siku zao na pia kuwaelimisha juu ya Hedhi salama. 
 Mwanafunzi wa Darasa la Tano Anitha Norbart (12) akiuliza swali kama ni sahihi kutumia Mdalasini wakati akiwa katika siku zake?
 Daktari Edna Kiogwe akitoa elimu juu ya umuhimu wa kujitambua wakati wakiwa katika Hedhi na njia mbadala za kujiweka sawa pindi wanapokuwa katika kipindi hicho
 Wanafunzi wakiwa wanafundishwa moja ya mazoezi wanayotakiwa kuyafanya na Daktari Edna Kiogwe.
 Baadhi ya wanafunzi wa Darasa la Tano sita na saba wakiwa wanafurahia Jambo wakati wa mafunzo
 Baadhi ya wanafunzi wakifuatilia kwa Makini Semina Hiyo
 Mmoja wa wanafunzi wa shule ya Msingi ya Bajavero akipewa zawadi ya Glory Pads ikiwa ni sehemu ya kusherekea siku ya Hedhi Duniani.
 Baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Msingi ya Bajavero zamani Wamato  wakifurahia Pads za Glory walizopewa ikiwa ni ishara ya kusherehekea sikukuu ya Hedhi Duniani.

****
Kuelekea Kilele cha siku ya Hedhi Duniani ambayo itakuwa tarehe 28.05.2015 Mtandao wa Hedhi salama www.hedhisalama.com  umeendelea kutoa mafunzo juu ya Hedhi salama ikiwa ni pamoja na changamoto,Magonjwa na mambo mbalimbali ambayo yanamtokea mwanamke anapokuwa katika Hedhi pamoja na ushiriki wa wanaume katika kujua maswala ya hedhi katika shule ya msingi ya yatima ya Bajavero,

Akitoa mafunzo ya Semina hiyo Daktari Edna Kiogwe alieleza kuwa kuna haja ya vijana tangu wakiwa wadogo wakapata Elimu juu ya Hedhi ili wanapokuwa wasijeshtuka pindi hali hiyo inapo wajia.

Alieleza juu ya umakini na ufaulu mashuleni kuwa Wasichana wengi  huahirisha shughuli za kimasomo  kama kuhudhuria vipindi mbalimbali vya masomo yao

Aliongeza ili Binti apate kuendana na hali hii anatakiwa ajivunie na kufurahia kipindi chote anachokua hedhi, atambue kwamba kila mwanamke hupitia kipindi hicho na hata wenzake darasani huvipitia vipindi hivyo vya hedhi, si yeye
peke yake anaeingia hedhi. 


Pia Dkt. Edna alisisitiza kuwa  Wanaume na wavulana wanahitajika kuelimishwa juu ya hedhi, wengi wao hawajui chochote juu ya hedhi na hua wanadhani mwanamke peke yake ndo anapaswa kufahamu juu ya hedhi. "Tukiwaelimisha wanaume juu ya hedhi, watakua msaada mkubwa kwa wake zao, watoto wao, dada zao,mama zao na ndugu zao wa kike. Kulingana na tamaduni zetu za kiafrika baba ndo mtafutaji na mwenyekauli ya mwisho katika familia" Alisema Dkt. Edna

Nao wanafunzi wa shule ya msingi ya  Bajavero  walipata nafasi ya kuuliza maswali mbalimbali na kupata majibu pia kufurahishwa na elimu bora  na kujitambua zaidi, pia walishukuru kupata zawadi za Pads aina ya Glory  ikiwa ni kuelekea katika siku ya Hedhi duniani.

KITABU CHA 'THE 7 HABITS OF HIGHLY EFFECTIVE PEOPLE' CHAZINDULIWA UPYA KWA LUGHA YA KISWAHILI

DSC_0006
Ofisa Mtendaji Mkuu wa NFT Consult/Franklin Covey, Badru Ntege (kulia) akimwonyesha kitabu cha "The 7 Habits of highly effective People" kilichotafsiriwa kwa lugha ya Kiswahili kwa mara ya kwanza nchini Tanzania mgeni rasmi Mkurugenzi wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Nehemia Mchechu mara baada ya kuwasili kwenye uzinduzi huo uliofanyika jana jijini Dar es Salaam katika hoteli ya Serena.(Picha zote na Zainul Mzige wa Modewjiblog).
DSC_0007
Mkurugenzi wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Nehemia Mchechu (kushoto) akipitia kurasa mbalimbali za kitabu hicho kabla ya uzinduzi rasmi. Kulia ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa NFT Consult/Franklin Covey, Badru Ntege.
DSC_0053
Mwezeshaji wa Franklin Covey, Alice Levora akichambua kwa ufupi tabia 7 zilizomo kwenye kitabu hicho kwa wageni waalikuwa (hawapo pichani) kabla ya uzinduzi rasmi.

Na Mwandishi wetu
UWEKEZAJI mkubwa unatakiwa kufanywa katika eneo la raslimali watu, kama taifa hili linahitaji kuondokana na malalamiko kuhusu maendeleo na ajira.

Kauli hiyo imetolewa na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) Nehemia Mchechu wakati akizindua tafsiri ya kiswahili ya kitabu cha “The 7 Habits of Highly effective people” kilichoandikwa na Mmarekani, Stephen Covey.

Hii inakuwa tafsiri ya kwanza ya kitabu hiki kwa lugha za asili zinazotumika bara la Afrika .
Alisema malalamiko mengi kuhusiana na taifa kuwa na raslimali nyingi na umaskini kuendelea kuwepo yanatokana na kutoendelezwa kwa raslimali watu kwa lengo la watu kujitambua, kutambua wanachotaka na kusababisha kiwepo.

Alisema inasikitisha kuona kwamba watanzania wengi wanalalamika kuhusu hali ngumu kumbe ilhali wao huenda ndio wakawa sababu za matatizo hayo ya ukosefu wa maendeleo.
Alisema ni vyema watanzania wakajenga utamaduni wa kujisomea vitabu mbalimbali vinavyotoa mwanga wa kujituma na kuwajibika kwa kuwa vitabu hivyo vina tafiti nyingi za miaka mingi ambazo watanzania wakitumia kwa muda mfupi watafanya mabadiliko katika maisha yao.
Alisema uwapo kwa tafsiri ya Kiswahili kwa moja ya vitabu vyenye sifa kubwa duniani katika masuala ya menejimenti na ambacho kimekuwa katika 20 bora za vitabu duniani kwa miaka 20, kutasaidia watanzania wengi kujiangalia na kujifunza kuwa na dira na nidhamu ya kutekeleza yale ambayo wanayafikiria.

Alisema kwamba ari ya kusoma kazi mbalimbali kutasaidia watanzania kuwa na upeo mpana wa kujituma na kuwa na nidhamu ya malengo wanayostahili ya kufikia kwa muda mfupi na kwa ufanisi mkubwa.

Tafsiri hiyo ya kitabu ambayo imewezeshwa na Baraza la Kiswahili nchini Tanzania (BAKITA) na imeandaliwa taasisi ya ushauri wa masuala ya maendeleo ya raslimali watu (NFT).

NFT ambayo makao makuu yake yapo mjini Kampala, Uganda ina matawi Kenya, Tanzania, Rwanda, Burundi na Sudan Kusini.

Wajibu wake mkubwa taasisi hiyo ni kukabilina na changamoto mbalimbali za wafanyakazi kwa kutoa mafunzo yenye kutengeneza manufaa kwao na kwa menejimenti ya uhuru na kutegemeana katika kufanikisha maono ya taasisi husika.

Kutumika kwa kitabu hicho chenye kurasa 380 kwa kuangalia tabia zenye manufaa kunatokana na haja ya kubadilisha mfumo wa uongozi na ushirikishaji wenye lengo la kuchochea kutegemeana katika kuleta ufanisi.
DSC_0115
Mgeni rasmi Mkurugenzi wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Nehemia Mchechu (kulia) na Mtafsiri mkuu kutoka Baraza la Kiswahili Tanzania (BAKITA) ambao wameshiriki kuandaa tafsiri ya kitabu hicho kwa lugha fasaha ya Kiswahili, Vida Mutasa (wa pili kushoto) pamoja na wadau wengine wakifuatilia uchambuzi wa kitabu hicho.
DSC_0081
Ofisa Mtendaji Mkuu wa NFT Consult/Franklin Covey, Badru Ntege akizungumza machache kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi kuzungumza na wageni waalikwa.
DSC_0248
Mgeni rasmi Mkurugenzi wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Nehemia Mchechu akizungumza kwenye hafla ya uzinduzi wa kitabu cha "The 7 Habits of highly effective People" kilichotafsiriwa kwa lugha ya Kiswahili kwa mara ya kwanza nchini Tanzania ambapo alitoa rai kwa Watanzania kujenga utamaduni wa kujisomea vitabu mbalimbali vinavyotoa mwanga wa kujituma na kuwajibika.
DSC_0149
Mtafsiri mkuu kutoka Baraza la Kiswahili Tanzania (BAKITA) ambao wameshiriki kuandaa tafsiri ya kitabu hicho kwa lugha fasaha ya Kiswahili, Vida Mutasa akielezea changamoto alizokutana nazo wakati wa kutafsiri kitabu hicho.
DSC_0278
Pichani ni kikundi cha burudani kutoka Tanzania House of Talent (THT) wakitumia sanaa "Choreograph" kuzindua rasmi kitabu cha "The 7 Habits of highly effective People" kilichotafsiriwa kwa lugha ya Kiswahili kwa mara ya kwanza nchini Tanzania.
DSC_0291
DSC_0303
Sasa kimezinduliwa rasmi.
DSC_0308
Mgeni rasmi Mkurugenzi wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Nehemia Mchechu akipokea kitabu cha "The 7 Habits of highly effective People" kilichotafsiriwa kwa lugha ya Kiswahili kwa mara ya kwanza nchini Tanzania kwa ajili ya mafunzo ya kuongeza manufaa binafsi na maeneo ya kazi kutoka kwa Ofisa Mtendaji Mkuu wa NFT Consult/Franklin Covey, Badru Ntege (kulia). Katikati anayeshuhudia tukio hilo ni Mtafsiri mkuu kutoka Baraza la Kiswahili Tanzania (BAKITA) ambao wameshiriki kuandaa tafsiri ya kitabu hicho kwa lugha fasaha ya Kiswahili, Vida Mutasa
DSC_0313
Mgeni rasmi Mkurugenzi wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Nehemia Mchechu akionyesha kitabu cha "The 7 Habits of highly effective People" kilichotafsiriwa kwa lugha ya Kiswahili kwa mara ya kwanza nchini Tanzania kwa ajili ya mafunzo ya kuongeza manufaa binafsi na maeneo ya kazi kwa waandishi wa habari na wageni waalikwa (hawapo pichani).
DSC_0316
Kutoka kushoto ni Mgeni rasmi Mkurugenzi wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Nehemia Mchechu, Mtafsiri mkuu kutoka Baraza la Kiswahili Tanzania (BAKITA), Vida Mutasa, Ofisa Mtendaji Mkuu wa NFT Consult/Franklin Covey, Badru Ntege, Mkurugenzi wa NFT Consult, Nambie Kiwanuka pamoja na Meneja biashara mkazi wa NFT Consult/Franklin Covey Tanzania, Joan Ajilong.
DSC_0339
Mgeni rasmi Mkurugenzi wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Nehemia Mchechu katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa NFT Consult/Franklin Covey Tanzania.
DSC_0252
Mratibu wa shughuli ya uzinduzi wa kitabu cha "The 7 Habits of highly effective People"kilichotafsiriwa kwa lugha ya Kiswahili kwa mara ya kwanza nchini Tanzania kutoka JB's PR & Events, Babbie Kabae akifafanua jambo kwa wageni waalikwa (hawapo pichani).
DSC_0061
Pichani juu na chini ni baadhi ya wageni waalikwa ambao ni maafisa rasilimali watu na wadau kutoka makampuni mbalimbali waliohudhuria uzinduzi huo.
DSC_0055
DSC_0100
DSC_0103
DSC_0106
DSC_0379

SHIRIKA LA TMT 2015 LAZINDULIWA RASMI LEO, MWANZA KUFUNGUA PAZIA TAREHE 24 APRIL,2015



Afisa Masoko na Mahusiano wa Proin Promotions Ltd, Josephat Lukaza akizungumzia Uzinduzi wa msimu wa pili wa Shindano la TMT 2015 lililopo chini ya Kampuni ya Proin Promotions Ltd ambao pia ni wasambazaji, wauzaji na watengenezaji wa filamu za Kitanzania. Anayeshuhudia pembeni ni Mratibu wa Masoko wa ITV/Radio One ambao ni mmoja wa wadhamini wa Shindano la TMT 2015.
 Mratibu wa masoko kutoka ITV/Radio One (wa pili kulia) akizungumzia juu ya umuhimu wa wao ITV/Radio one kuwa washirika wa TMT 2015 na kuhaidi makubwa zaidi kwa mwaka 2015.P
 Mmoja wa majaji wa shindano la TMT 2015 Yvonne Cherry au Monalisa akizungumza mbele ya waandishi wa habari(hawapo pichani) kuhusiana na shindano la TMT 2015 lililozinduliwa rasmi leo jijini Dar Es Salaam
Shindano la Tanzania Movie Talents (TMT) 2015 limezinduliwa rasmi leo huku baadhi ya vigezo vikiwa vimeboreshwa, akizungumzia hayo Meneja wa Mradi wa TMT 2015, Saul Mpock amesema kuwa "Mwaka Huu Kigezo kimojawapo ni mshiriki kuwa na umri kuanzia miaka 16 na kuendelea huku fomu za kushiriki shindano hilo zikipatika siku ya usaili katika mkoa husika na bila gharama yoyote"
Shindano la Tanzania Movie Talents 2015 linaanza rasmi Kesho huku Kanda ya Ziwa ndio itakayofungua pazia la shindano hili kwa Mwaka 2015, Shindano hili linafanyika kikanda ambapo kanda sita za Tanzania zitafikiwa na shindano hili.

Kwa kanda ya Ziwa usaili utaanza tarehe 24 Aprili 2015 huku zoezi zima likifanyika mkoani Mwanza na hatimaye zoezi kuendelea kanda ya Kaskazini, Arusha, Kanda ya Kati, Dodoma, Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, Mbeya, Kanda ya Kusini, Mtwara na Kumalizika Kanda ya Pwani, Dar Es Salaam.

Katika kanda zote tano ikiwa Kanda ya Ziwa, Kaskazini, Kati, nyanda za juu kusini na Kusini Washindi watakuwa ni watatu kutoka kila kanda ambapo kila mshindi ataibuka na kitita cha shilingi laki tano kila mmoja huku kanda ya Pwani itatoa washindi watano na kila mmoja kuondoka na shilingi laki tano pia na kupelekea Washindi kuwa 20 na kuingia kwenye nyumba ya TMT kwaajili ya Hatua ya Mchujo.

TMT 2015 itarushwa na kituo cha ITV siku ya Jumapili saa tatu usiku huku kipindi cha kwanza kabisa cha TMT kikitarajiwa kuonekana tarehe 10 May 2015.

Shindano hili la TMT 2015 limedhaminiwa na Kampuni ya Usafirishaji ya Precision Air, I-View Studio, Global Publishers na Kituo cha ITV/Radio One ambao ndio watakaokuwa wakirusha matangazo ya TMT 2015. TMT ikiendelea kupata sapoti kutoka katika vituo mbalimbali za redio mikoani. Vilevile tunatoa nafasi kwa makampuni mengine ambao wangependa kushirikiana na TMT kwa mwaka 2015
Kauli Mbiu ya TMT 2015 ni Mpaka Kieleweke.

UVCCM WILAYA YA KIGOMA MJINI WAFANYA ZIARA NA KUBAINI CHANGAMOTO ZA HUDUMA ZA AFYA

Na Magreth  Magosso, Kigoma.

KAMATI  ya utekelezaji ya baraza kuu la umoja wa vijana UVCCM wilaya,  mkoani Kigoma imefanya ziara katika vijiji vya mwambao wa ziwa Tanganyika na kubaini changamoto mbalimbali zinazo wakabili wananchi wa maeneo hayo.

Katibu wa vijana wilaya Pantaleon Rumanyika akizungumza na wandishi wa habari mkoa wa Kigoma alisema  baada ya ziara na  kubaini changamoto kadhaa ikiwemo ya ukosefu wa mganga pamoja na nesi katika zahanati ya Kijiji cha Kagunga.

Amesema zahanati hiyo ina mtumishi mmoja ambaye analalamikiwa na wananchi kutokuwa na vigezo vya kitaalamu sanjari na akinamama wajawazito kutokubali kujifungulia katika zahanati hiyo kwa kuhofia aibu.
 
Rumanyika alisema mtumishi aliyepo ni mwanaume na hivyo kuwa ngumu kwa akinamama wajawazito kufika katika zahanati hiyo na kulazimika kwenda katika vituo vingine na wengina kujifungulia majumbani.

Alisema sambamba na hilo wakazi hao waliiomba serikali iweze kuwatatulia tatizo la ukosefu wa miundombinu ya barabara ya Chankere, Mwamgongo hadi Kagunga ambayo imekuwa ni kero ya muda mrefu licha ya diwani wa kata hiyo Kassimu Nyamkunga kupiga kelele ujenzi wa barabara hiyo katita vijao vya baraza la madiwani.

Alisema kukamilika kwa barabara hiyo itasaidia kuponguza ajali na vifo vinavyojitokeza kwa wasafiri pamoja na akinamama wajawazito ambapo kwa usafiri wa boti hutumia masaa kumi na moja kufika Kigoma mjini kufuata huduma ya kujifungua.

Rumanyika alisema lengo hasa la ziara hiyo katika vijiji vya Kagongo, Mwamgongo, Kagunga, Mahembe pamoja Nyarubanda  ni kuwaandaa vijana kuwa tayari kujiandikisha katika daftari la kudumu la wapiga kura, kusoma vizuri  rasimu ya katiba mpya pamoja na kuwahamasisha kujiunga katika vikundi vya ujasiliamali.

Mganga mkuu wa wilaya Dkt. Jems Jumanne alikiri kuwepo kwa tatizo hilo na kueleza kuwa taratibu za kuagiza mtumishi katika Zahanati zinaendelea na kwamba taratibu za kupata nesi  kwa lengo la kuwahudumia wajawazito zitafanyika.

Alisema tatizo kubwa ni upungufu wa watumishi katika wilaya hiyo ambapo ina jumla ya watumishi 130 na hivyo kuwa na upungufu wa watumishi 294 ambapo kila kijiji kina Zahanati katika wilaya hiyo.

MMOJA AFARIKI DUNIA KWA KUGONGWA NA GARI-KIGOMA

Na MagrethMagosso, Kigoma.

MKAZI mmoja amekufa papo hapo na mweingine kujeruhiwa mara baada ya kugongwa na gari aina ya Toyota  maarufu kwa jina la Mchomoko lililokuwa likitokea Manyovu kuelekea Mjini katika barabara ya Kigoma- Kasulu eneo la Sido lililopo Manispaa ya Kigoma Ujiji mkoani Kigoma.

Akitoa taarifa ya tukio hilo Kamanda wa polisi Mkoa wa Kigoma SACP Fredinandi Mtui alisema tukio hilo lilitokea majira ya saa tatu usiku katika eneo Mlole - Sido  ambapo gari aina ya Toyota lenye namba za usajiri T616 DXR lililokuwa likiendesha na Pitolus Silasi (33), lilisababisha ajali hiyo.

Kamanda alimtaja marehemu kuwa ni Pantoleo Philipo (30) ambaye alikufa popa hapo haku abiria aliyekuwa amembeba katika pikipiki yake akiwa amejeruhiwa vibaya maeneo ya kichwani na kuvunjika mkono na mguu.

Alisema chanzo cha ajali hiyo ni mwendo kasi wa gari ambapo mara baada ya ajali dereva wa gari alitokomea kusiko julikana na kwamba jitihadi za kumsaka zilifanyika na kumkamata ambapo atafikishwa mahakamani mara baada ya kukamilika kwa upelelezi.

Akithibitisha kupokea maiti na majeruhi katika Hospitali ya rufaa Maweni mganga mfawidhi wa hospitali Fadhili Kibaya amesema majira ya usiku alipokea mwili wa marehemu pamoja na majeruhi mmoja aliyetambuliwa kwa jina la Michael Madyane ambaye amelazwa katika hospitali ya Rufaa maweni kwa matibabu.

Kibaya alisema hali ya majeruhi ni mbaya na kwamba anatakiwa kufanyiwa upasuaji wa mifupa na hivyo kulazimika kumpatia rufaa katika hospitali ya Bugando ambapo kuna  madaktari bingwa wa upasuaji huo.

Alisema licha ya hospitali hiyo kuwa ya rufaa lakini bado inakabiliwa na changamoto ya madaktari bingwa wa magonjwa mbalimbali pamoja na vifaa tiba ambapo jitihada za maksudi zinaendelea ili kukabiliana na changamoto hiyo.

CCM YAONYA UVUVI HARAMU ZIWA TANGANYIKA

Na Mwajabu Kigaza, Kigoma.

WAVUVI katika ziwa Tanganyika mkoa wa Kigoma  wametakiwa kuacha tabia ya kufanya uvuvi haramu unaosababisha uharibifu wa mazalia ya samaki yaliyopo katika ziwa hilo na kusababisha samaki kutoweka siku za badae.

Kauli hiyo imetolewa na katibu wa umoja wa Vijana UVCCM wilaya Pantaleon Rumanyika wakati wa ziara ya kamati ya utekelezaji  baraza kuu la umoja wa vijana wilaya iliyofanywa katika vijiji mbalimbali vilivyopo mwambao wa ziwa Tanganyika Mkoa wa Kigoma.

Alisema tabia ya uvuvi haramu kwa kutumia nyavu zisizo kubalika kisheria zinaadhiri uharibifu wa mazingira katika ziwa hilo kwa kuuwa mazalia na kusababisha siku za usoni kutoweka kwa samaki katika ziwa Tanganyika.

“Samaki hao wanapo vuliwa huwa wanaoza kwa muda mfupi kutokana na nyavu zinazotumika kusababisha majeraha kwa samaki na hivyo wadudu kushambulia na kuleta madhara kwa binadamu”alisema Rumanyika.

Rumanyika alisema lengo hasa la ziara hiyo katika vijiji vya Kagongo, Mwamgongo, Kagunga, Mahembe pamoja Nyarubanda  ni kuwaandaa vijana kuwa tayari kujiandikisha katika daftari la kudumu la wapiga kura, kusoma vizuri  rasimu ya katiba mpya pamoja na kuwahamasisha kujiunga katika vikundi vya ujasiliamali.

Akizungumzia hilo  ofisa uvuvi wilaya Josephat Gowele alisema tatizo la uvuvi haramu ni changamoto hasa ipo katika maeneo ya Kaskazini ambapo  chanzo kikubwa cha uvuvi haramu ni wavuvi wanaotoka nchi jirani ya Burundi.
Amesema licha ya kuharibu mazalia ya samaki wakati wa uvuvi lakini pia nyavu hizo huwa haziozi mara baada zinapotupwa ziwani na hivyo kusababisha kila samaki anayepita karibu na nyavu hizo kunaswa.

 Amesema uvuvi wa aina hiyo unatoka nchi jirani ya Burundi wakishirikiana na wenyeji wa maeneo hayo hivyo inakuwa vigumu kutokomeza uvuvi huo ambapo watu saba kutoka Burundi walifikishwa mahakamani mara baada ya kufanya doria.

Gowele amesema ili kutokomeza tabia hiyo hakuna budi kufanya doria za mara kwa mara, ulinzi shirikishi baina ya maafisa uvuvi na jamii ambapo vikundi vya BMU  vimeanzishwa katika maeneo yote ya uvuvi lengo likiwa ni kulinda rasilimali zilizopo ziwani.

BALOZI MPYA WA ANGOLA ATEMBELEA UBALOZI WA TANZANIA WASHINGTON DC.


 Mhe, balozi wa Angola Agostinho Tavares akipokelewa na afisa wa ubalozi  Swahiba Mndeme alipotembelea ubalozi .
 Mhe, balozi Liberata Mulamula akiwa na furaha baada ya mgeni wake kufika ofisini .
 Mhe balozi Liberata Mulamula kwenye picha ya pamoja na mgeni wake balozi wa Angola Agostinho Tavares.
 Mhe Balozi wa Angola nchini Marekani Agostinho Tavares akiweka sahihi  kitabu cha wageni.
 Mhe balozi wa Angola chini Marekani Agostinho Tavares akimsikiliza kwa makini mwenyeji wake balozi Liberata Mulamula alipokua akijitambulisha .
Mhe balozi Libarata Mulamula na balozi wa Angola nchini marekani Agostinho Tavares pamoja na afisa wa ubalozi Swahiba Mndeme walipokua wakibadilishana mawazo.
               PICHA ZOTE KWA HISANI YA CAMERA YA UBALOZI