Kiwanja kipya cha maraha Uefa Goo Night Club kinatarajiwa kuzinduliwa mkesha wa sikukuu ya Krismas jijini Dar es salaam Kiwanja hiki ni cha Kisasa kiko maeneo ya Ukonga Mombasa Barabara ya kuelekea Moshi Baa Karibu na njia panda ya Mahitamita 200 kutoka barabara kuu iendayo Pugu, siku ya mkesha wa Krismas burudani kibao zimeandaliwa na na kiko katika hatua za mwisho mwisho kukamilisha kila kitu ili kuwapa burudani wateja wake ikiwa ni pamoja na Ligi mbalimbali za ulaya, muziki wa kisasa kama vile Bongofleva na muziki wa zamani na vyakula mbalimbali vitapatikana
Sunday, December 21, 2014
UEFA GOO NIGHT CLUB KUZINDULIWA MKESHA WA KRISMAS
WAIMBAJI WA TAMASHA LA KRISMAS MKOANI MBEYA WAELEZEA MAANDALIZI YAO
Mwimbaji wa muziki wa injili Tumaini Njole akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi za kampuni ya Msama Promotion ambayo inaandaa Tamasha la Pasaka litakalofanyika sikukuu ya Krismas tarehe 25/12/2014 mkoani Mbeya wakati alipozungumzia maadalizi ya tamasha hilo na jinsi alivyojipanga kukonga mioyo ya mashabiki wa nyimbo za injili mkoani Mbeya , Tamasha hilo linatarajiwa kuanza muda wa Saa nane mchana viingilio vikiwa ni shilingi 5000 kwa watu wazima na watoto shilingi 2000, Katika tamasha hilo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Waziri Mkuu Mstaafu Mh. Fredrick Sumaye na waimbaji wengine watakaotumbuiza ni Faraja Ntaboba, Upendo Nkone, Upendo Kirahilo, Rose Muhando, Bony Mwaiteje Edson Mwasabwite, Ambwene Mwasongwe na wengine wengi, Pia matamasha mengine yanatarajiwa kufanyika mkoani Iringa tarehe 26/12/2014 na Songea tarehe 28/12/2014, Katika Picha kushoto ni Mwimbaji Joshua Mlelwa.(PICHA NA KIKOSIKAZI CHA FULLSHANGWE-DAR ES SALAAM) Mwimbaji wa muziki wa Injili Edson Mwasabwite akifafanua jambo wakati wa mkutano huo uliofanyika leo jijini Dar es salaam , Kushoto ni mwimbaji Joshua Mlelwa na katikati ni Mwimbaji Tumaini Njole Mwimbaji Joshua Mlelwa akielezea maandalizi yake wakati wa Tamasha la Pasaka litakalofanyika mkoani Mbeya wakati wa Sikukuu ya Krismas kulia ni Mwimbaji Tumaini Njole.
Saturday, December 20, 2014
AJALI YAUA WATU WAWILI,YAJERUHI 25-BARABARA YA KIGWA, TABORA
Friday, December 19, 2014
FEDHA ZAPORWA ENEO LA MSIKITINI ZANZIBAR,NI EURO 1000 NA SHILINGI MILIONI TANO ZA KITANZANIA
Umati mkubwa wa wananchi wakistaajabu tukio hilo la wizi wa fedha eneo la msikitini. |
Watu wasiofahamika wamevunja kioo cha gari na kuiba pesa Euro 1000 na shilingi milioni tano za kitanzania.
Kwa mujibu wa vyanzo vya habari kutoka eneo la tukio mwenye gari hilo aina ya Landcruiser lenye nambari za usajili Z 977 BM alifika na kuliegesha na kisha kuingia Msikitini kusali sala ya Ijumaa katika Msikiti wa eneo la Mlandege mjini Zanzibar.
Aidha baada ya kuegeshwa gari hilo lilitokea gari jingine nyuma yake ambalo mtu mmoja alishuka akiwa na Panga mkononi na kuanza kugonga kioo cha gari hiyo na kufanikiwa kufungua mlango na kutoa mkoba uliokuwa umehifadhiwa kiasi hicho kikubwa cha fedha na kutoweka nacho kusikojulikana.
Hata hivyo imeelezwa kuwa askari wa Jeshi la polisi walifika eneo la tukio kwa lengo la kufuatilia sakata hilo la uporaji.
SERIKALI YAZINDUA RASMI USAMBAZAJI TAKWIMU ZA PATO LA TAIFA, PATO LA MWANACHI LAONGEZEKA
Waziri wa Fedha Mh. Saada Mkuya Salum (katikati) akizindua rasmi Takwimu za Pato la Taifa zilizorekebishwa kwa mwaka wa kizio wa 2007 leo jijini Dar es salaam. Waziri wa Fedha Mh. Saada Mkuya Salum (kulia) akimkabidhi Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Dkt. Servicius Likwelile chapisho la lenye Takwimu za Pato la Taifa zilizorekebishwa kwa mwaka wa kizio wa 2007 wakati wa uzinduzi wa usambazaji wa takwimu hizo leo jijini Dar es salaam. Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Dkt. Albina Chuwa(Kushoto) akitoa ufafanuzi wa kazi ya kurekebisha takwimu za Pato la Taifa iliyofanywa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu iliyotumia tafiti za taifa zilizofanyika kwa kipindi cha mwaka 2001 hadi 2007.Kulia ni Waziri wa Fedha Mh. Saada Salum Mkuya. Baadhi ya viongozi na wageni waliohudhuria uzinduzi wa usambazaji wa Takwimu za Pato la Taifa zilizorekebishwa kwa mwaka wa kizio wa 2007 wakimsikiliza Meneja wa Takwimu za Pato la Taifa, Bw. Daniel Masolwa wakati akiwasilisha mada kuhusu Pato la Taifa leo jijini Dar es salaam.
....................................................................................................
Na. Aron Msigwa – MAELEZO.
. Dar es salaam.
Serikali imesema kuwa Pato la Taifa kwa mwaka 2007 limeongezeka hadi kufikia shilingi trilioni 26.8 ikilinganishwa na trilioni 20.9 za mwaka 2001, ambapo wastani wa pato la mwananchi mmoja mmoja limeongezeka kutoka shilingi milioni1,186,200/= mwaka 2001 hadi shilingi milioni 1, 561,050/= mwaka 2013.
Akizindua usambazaji wa takwimu hizo leo jijini Dar es salaam, Waziri wa Fedha Mh. Saada Mkuya Salum ameeleza kuwa matokeo hayo ni sawa na ongezeko la ukubwa wa Pato la Taifa kwa asilimia 27.8.
Amesema ongezeko hilo ni matokeo ya juhudi za Serikali kuweka mazingira mazuri na kutengeneza fursa za kuwawezesha wananchi kufanya kazi za kujiajiri na hatimaye kupata kipato halali kwa kazi wanazofanya.
Mh. Mkuya amesema kuwa kukua kwa uchumi wa Tanzania kumechangiwa na kujumuishwa kwa shughuli mbalimbali zikiwemo Sayansi na Teknolojia ambako kumetoa fursa kwa wananchi kujiongezea kipato hususan matumizi ya simu za kiganjani ambazo zimerahisisha mawasiliano na utafutaji wa masoko ya bidhaa ndani na nje ya nchi.
Amezitaja shughuli nyingine kuwa ni ukamilishaji wa miamala mbalimbali ya kibenki na mikopo ambazo zimekuzwa na sekta ya mawasiliano , kuongeza ajira na kupunguza muda wa kusubiri huduma za malipo katika maeneo mbalimbali nchini.
Aidha, amefafanua kuwa kuongezeka kwa thamani ya Pato la Taifa kunaiongezea Serikali uwezo kimapato kupitia kodi na kuiwezesha kugharamia ujenzi wa miundombinu na utoaji wa huduma mbalimbali kwa wananchi.
“Serikali imeendelea kuimarisha upatikanaji wa huduma ya maji safi na salama, utafiti wa mapato na matumizi ya Kaya Binafsi ya mwaka 2012 unaonyesha asilimia 60 ya kaya zote nchini zinapata maji safi na salama hasa hususan maeneo ya mijini,zaidi ya asilimia 20 ya kaya zote nchini zinatumia nishati umeme haya ni mafanikio makubwa ya matokeo ya ukuaji wa uchumi nchini” Amesisitiza Mh. Mkuya.
Akizungumzia mchango wa Sekta Binafsi katika kukua kwa pato la taifa nchini amesema kuwa ajira zipatazo laki nne kati ya laki sita katika sekta iliyo rasmi zimepatikana.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Dkt. Albina Chuwa akizungumza wakati wa uzinduzi huo amesema kuwa kazi ya kurekebisha takwimu za Pato la Taifa imetumia Tafiti za Taifa zilizofanyika kwa kipindi cha mwaka 2001 hadi 2007.
Amezitaja tafiti hizo kuwa ni pamoja na utafiti wa mapato na matumizi ya Kaya wa mwaka 2007, Sensa ya Kilimo iliyofanyika mwaka 2008 na Takwimu nyingine za utawala kutoka katika Wizara na Idara za Serikali.
Aidha, amefafanua kuwa ukokotoaji wa takwimu hizo umefuata mfumo wa Umoja wa Mataifa wa kutayarisha takwimu za Pato la Taifa wa mwaka 1993 na 2008 kwa lengo la kuhakikisha kuwa takwimu hizo zinalinganishwa na takwimu nyingine duniani.
KAJALA AKUNWA NA KUMWAGA MAHELA KWA WAIMBAJI WA SKYLIGHT BAND WANAOTOA BURUDANI KILA IJUMAA THAI VILLAGE,MASAKI
Meneja wa Skylight Band Aneth Kushaba AK47 akitoa burudani kwa mashabiki wa bendi hiyo Ijumaa iliyopita ndani ya kiota cha Thai Village huku akipewa sapoti na Digna Mbepera.
Digna Mbepera na Bela Kombo wakimpa back up Aneth Kushaba AK47 kwenye show zao za kila Ijumaa ndani ya viunga vya Thai Village Masaki jijini Dar.
Majembe ya Skylight Band yakionyesha manjonjo yao jukwaani Ijumaa iliyopita ndani ya kiota cha Thai Village Masaki.
Aneth Kushaba na Sam Mapenzi wakiwapa raha mashabiki wao huku Digna Mbepera na Bella Kombo.
Sam Mapenzi na Aneth Kushaba AK47 wakifanya yao jukwaani.
Pichani juu na chini ni mashabiki wa Skylight Band wakiserebuka mdogo mdogo.
Birthday girl nae hakubaki nyuma aliunga tela na kuburudika na Skylight Band.
Msanii wa bongo movie Kajala akitembeza manoti ya wekundu wa msimbazi kwa waimbaji wa Skylight Band Ijumaa iliyopita alipokunwa na uimbaji wao.
Kajala akizichomoa tu kwenye pochi lake.
Joniko Flower akisubiria zamu yake.
Joniko Flower akipokea manoti yake kutoka kwa Msanii wa bongo movie Kajala.
Na kwa wale wasanii waliokuwa back stage pia walibahatika kujizolea manoti kutoka kwa Kajala.
Wapenzi wa Skylight Band wakishuhudia tukio hilo.
Twende kazi... na burudani iendeleeee..!
Mashabiki nao wakajibu mapigo.
Sam Mapenzi akitunzwa na shabiki wake.
Sam Mapenzi akiwapa raha mashabiki wa Skylight Band, Ijumaa iliyopita huku Joniko Flower na Sony Masamba wakimpa sapoti.
Mashabiki wakiendelea kula raha..!
Birthday girl na mabeste zake wakicheza mdogo mdogo.
Mguu wa kushoto mbele wa kulia nyuma...... mashabiki wakiondoka ma-style ya Skylight Band.
Hashim Donode na Bela Kombo wakiburudisha mashabiki wa Skylight Band huku wakipewa back up na Aneth Kushaba pamoja na Digna Mbepera.
nakupenda pia pia aha...Nakupenda pia...You make me wanna say....Nakupenda pia pia ahaa.....Vijana wakiwa kwenye hisia kali jukwaani.
Majembe ya Skylight Band yakisebeneka jukwaani huku yakijaribu kuwafundisha mashabiki wao.
Mkongwe wa muziki wa dansi nchini, Joniko Flower akiwachezesha ligwaride la sebene majembe ya Skylight Band Ijumaa iliyopita ndani ya Thai Village .
Mtaalamu wa kupiga kinanda Danny akifanya yake huku akipata Ukodak.
Mmoja wa mashabiki wa Skylight Band alikuwa akisheherekea siku yake ya kuzaliwa ndani ya kiota cha Thai Village Masaki huku bendi hiyo ikimpa zawadi ya kumwimbia wimbo maalum wa sherehe hizo kumpongeza.
Birthday girl akiendelea na zozezi la kulisha vipande vya cake shosti zake.
Birthday girl akiteta jambo na mchumba wake Lota Mollel.
Mahaba niuweeeeeeee! Birthday girl akipata kiss kutoka kwa mchumba wake Lota Mollel.
Birthday girl akiendelea kukata cake kwa ajili ya kuwalisha ndugu, jamaa na marafiki waliojumuika naye.
Birthday gilr na mchumba wake wakilishana cake kimahaba zaidi....!
Emma Beyz na Danny Kinanda.
Wadau wakipata Ukodak.
Mdau Iddi Baka na Blogger King Kif wakishow love mbele ya camera yetu.
Warembo wa ukweli na wenye viwango na ubora wanapatikana Skylight Band pekee hakunaga kwingine.
Nyomi la mashabiki wa Skylight Band likiwa limeshona Ijumaa iliyopita ndani ya Thai Village.