Pages

KAPIPI TV

Monday, November 24, 2014

UHARAMIA ZIWA TANGANYIKA KIGOMA HAUKWEPEKI

Na Mageth Magosso,Kigoma

“MAPATO  ya halmashauri ya kigoma hutegemea shughuli za uvuvi na kila mwezi kupitia mwalo wa kibirizi ambayo  inakusanya kiasi cha shilingi milioni 12 ,uporaji wa zana za wavuvi ziwa Tanganyika limebaki kwa wahanga wenyewe,serikali haisikii ,kilio cha wavuvi kinaishia majini  thamani yetu ipo katika  kodi tu, alisema ” Mwenyekiti wa Wavuvi  mkoani kigoma Sendwe Ibrahim.

“kipindi cha miezi 11  zaidi ya injini 25 zimeporwa, shida  ipo katika uwajibikaji,kila tunapopata  tarifa ya tukio  kutoka kwa wavuvi ziwani tunafikisha kwa uongozi wa juu ,jiografia ya ukanda wa ziwa ni fursa kwa wahalifu” alisema  Ibrahim.

Hayo yalisemwa jana asubuhi mbele ya wananchi waliokwenda kulangua dagaa na samaki katika mwalo wa Kibirizi uliopo manispaa ya kigoma ujiji,aliwambia zao hilo lipo mashakani kutoa ajira kutokana na wimbi la uporwaji wa zana husika.

Katibu wa Umoja wa wavuvi kigoma (UWAKI)Mohamed Kasambwe alisema usiku wa saa 4.00 ,23,Novemba mwaka huu km 5 kutoka bandari ya kigoma mjini eneo la Nondwa kata ya kibirizi majambazi watatu wakiwa na silaha ya moto  aina ya SMG walipora injini 2 na 16,Novemba injini 9 ,mafuta ya petrol lita 3000 na mipira ya kunyonya mafuta.

Thamani ya injini moja ni sh.milioni 7,mpira wa kunyonya mafuta sh.100,000 na lita moja ya mafuta inauzwa  sh.2,500 hali inayochangia  kupanda kwa bei ya dagaa na samaki,ambapo boksi moja  la dagaa huuzwa sh.250,000 na samaki  sh.350,000.

Kwa upande wa Mkuu wa wilaya ya kigoma Ramadhan Maneno akiri janga hilo katika ziwa tanganyika halina ujanja,kutokana na ukosefu wa mawasiliano ya simu za mkononi kwa ukanda wa ziwa hilo, wahalifu hujinufaisha na uporaji wa zana za wavuvi.

Pia wananchi huficha tarifa za raia wageni na likitokea tukio ovu ndio hutoa tarifa na kuwasihi watoe ushirikiano wa wazi  kwa vyombo vya dola na wasimwamini kila mtu wafichue wahamiaji wasio rasmi.

Mkuu wa idara ya uhamiaji kigoma Ebrosy Mwanguku alisema changamoto ya uharamia ziwani na utekaji mabasi ya abiria yatakoma kupitia mfumo mpya wa uandikishwaji wa wahamiaji wasio rasmi kupitia "Data system".

Lengo ni kubaini wanaoingia na kutoka ambapo wananchi wa vijiji vilivyopo mipakani  , watendaji na madiwani wahakikshe kila  raia mgeni andikishe tarifa zake eneo husika na muovu atabainika kupitia vifaa maalum.

Akithibitisha hilo Kamanda wa Polisi wa hapa Jafari Mohamed alisema wamemtuma Ofisa wa majini na anafuatilia ili kubaini tukio hilo.

TASAF LAWAMANI - KIGOMA


Na Magreth Magosso, Kigoma.
 
ZAIDI ya wakazi 200 wanaoishi katika kata ya Buhanda mtaa wa Mgeo Manispaa ya Kigoma Ujiji mkoani hapo, wamekosa malipo ya fedha zao kupitia mfuko wa maendeleo ya jamii (TASAF) ilihali wanavocha ya kupata fedha hizo na kudai viongozi husika wanahusika na uchakachuaji wa stahiki za malipo yao .

Lengo la serikali ni kuzinusuru kaya zilizogubikwa na hali duni ya kipato,lakini uchakachuaji wa majina kwenye zoezi la utojai wa fedha umekuwa na utata kwa walengwa hasa wazee.

Hayo yalisema mkoani humo na wakazi zaidi ya 200 , walisema kitendo cha kuondolewa kwa baadhi ya majina ambayo yalipitishwa awali kwa kufuata vigezo vilivyotolewa imewatia mashaka na kudai ni dhuluma inayofanywa na viongozi husika.

 Kassim Kagoma (73), Mwajuma Juma (62) na Mariamu Bakari (75) wote wakazi wa kata ya Buhanda na wahanga wa tukio hilo  kwa nyakati tofauti walisema majina yao yamekatwa katika mchakato wa ulipaji wa fedha za mpango wa TASAF ambapo awali majina hayo yalikuwemo katika orodha ya wanaolipwa.

“Hatuelewi sababu ya sisi wazee kukatwa majina ,tupo 50  ajabu vijana wamelipwa  wengi wao wana miaka 19 tu,wakiwa ni vijana wana  uwezo wa kumudu maisha  ya kila siku, wamedai  fedha zilizobaki zitarudishwa benki” walisema wakazi hao.

Serikali ina nia ya kuwakomboa raia wake lakini shida ipo kwa viongozi husika ,ambao si waminifu na hawana imani ya walengwa ili waondokane na adha zinazowakabili ,ambapo hutumia nafasi hiyo kujinufaisha wenyewe.


Aidha mwenyekiti wa kamati ya usimamizi wa mpango wa kulipa fedha katika kaya maskini Azizi Rusiga alisema jumla ya kaya zilizopo kwenye orodha ya malipo ni takribani kaya 533 kati ya hizo kaya 288 ndio zimelipwa na kaya 244  hazijalipwa fedha  hizo.

 Mchakato wa ulipaji ulianza rasmi Novemba 20 mwaka huu ambapo zaidi ya sh. milioni 13.9 kilitengwa kwa ajili ya kulipa kaya 533 na v kiasi kiongozi walilipa sh.milioni 7.6 na zaidi ya milioni 6.4 zikiwa zimebaki na kudaiwa zitarudishwa benki.

Alisema aligundua uongozi wa TASAF ulitumia orodha mpya ambayo hatukushirikishwa kama ile orodha ya awali haijakidhi kigezo,mbaya zaidi uongozi wa kata hawajui ilihali walengwa wana vocha za kupewa sh.17 kila baada ya miezi miwili na walipoomba orodha mpya walinyimwa.


Mratibu wa TASAF mkoa wa Kigoma Staphod Lilakoma alipohojiwa shutuma hizo alisema malipo yaliyolipwa yamelenga kuanzia mwezi Septemba hadi Octoba na majina yanayotumika kulipa ni majina yaliyofanyiwa marekebisho kwa mara ya pili katika kipindi cha Novemba hadi Desemba ambayo yalikuwa hayana mashaka.

Alisema chanzo cha kukatwa majina  ni kutokana na udanganyifu uliotokea awali na kwamba majina yaliyoorodheshwa awali yalikuwa na mashaka baada ya kugundua kuwepo kwa kaya ndani ya kaya  na lengo la mpango ni kusaidia kaya moja .


Alisema fedha zilizobaki zitarudi benki na taratibu za madai zipo wazi ikiwa ni pamoja na kujaza fomu husika  ili   makao makuu wa yafanyie kazi.

"MUDA WA KULINDANA KWENYE WIZI WA FEDHA ZA UMMA HAUPO TENA"-KINANA

DATIUS JOVIT ALAMBA NONDOZ YA ELIMU YA CHUO KIKUU KISHIRIKI CHA DUCE


 Kijana Datius akiwa katika Picha ya Pamoja na Baba yake Mzazi (nyuma ya babu yake aliyevaa miwani) Babu zake na dada zake wakati alipotunukiwa nondo yake ya elimu kutoka Chuo Kikuu Kishiriki cha DUCE hapo jana
 Datius Akiwa katika picha ya pamoja na Baba yake Mzazi (Kushoto) pamoja na Babu yake mdogo (kulia)
 Akivishwa taji na Dada yake aitwaye Neema
Akiwa na Dada mara baada ya kulamba nondoz.Picha Zote na Josephat Lukaza wa http://www.josephatlukaza.com

Saturday, November 22, 2014

KINANA AUNGURUMA RUANGWA

 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwasili kwenye uwanja wa Ruangwa Likangara tayari kuhutubia wakazi wa wilaya ya Ruangwa mkoani Lindi.
 Wananchi wa Ruangwa wakionyesha furaha yao wakati wa kumkaribisha Katibu Mkuu wa CCM kwenye uwanja wa mkutano Ruangwa Likangara.
 Wananchi wa Ruangwa wakiwa na mabango yaliyobeba ujumbe wakati wa mkutano wa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana ambaye amekuwa mstari wa mbele katika kujenga na kukiimarisha chama,Katibu Mkuu wa CCM ameongozana na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye .
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi CCM Taifa Nape Nnauye akiwahutubia wakazi wa wilaya ya Ruangwa.
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi CCM Taifa Nape Nnauye akihutubia wakazi wa Ruangwa ambapo aliwaambia CCM inaimarika kutokana na kuwa na sera zenye kuleta maendeleo kwa Watanzania pamoja na kuthamini amani iliyopo nchini.(Picha na Adam Mzee)

Umati wa wakazi wa wilaya ya Ruangwa wakifuatilia kwa makini hotuba za viongozi wao wa CCM Taifa.

 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwasalimu wakazi wa wilaya ya Ruangwa waliojitokeza kwa wingi kumsikiliza,Kinana amekuwa Katibu Mkuu wa kwanza wa CCM kuzunguka nchi nzima ,kushiriki kwenye miradi mbali mbali ya maendeleo,kukagua ilani ya uchaguzi ya CCM 2010 pamoja na kutoa elimu kwa wananchi hasa ya kujiunga na mfuko wa afya ya jamii.
 Mbunge wa Jimbo la Ruangwa Majaliwa Kassim Majaliwa akihutubia wakazi wa Ruangwa ambapo alielezea katika kipindi chake tangu alipochaguliwa kuwa Mbunge ameshiriki shughuli mbali mbali za maendeleo jimboni kwake.
 Mbunge wa Jimbo la Ruangwa Majaliwa Kassim Majaliwa akihutubia wananchi wa Ruangwa ambapo alichukua muda wa kutosha kufafanua kwa wananchi namna alivyotekeleza wakatoi wa kipindi chake kama Mbunge wa Jimbo wakati wa mkutano wa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana ambaye anafanya ziara katika mikoa ya Lindi na Mtwara
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwahutubia wananchi wa Ruangwa ambapo alisema uongozi mbovu kwenye vyama vya ushirika ni chanzo cha kusababisha matatizo kwenye zao la korosho,aliwaambia wananchi hao hakuna sababu ya msingi ya kuwa na utitiri wa vyama vya ushirika.
 Wananchi wa kijiji cha Mibure wakiwa na furaha wakati wa kumkaribisha Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana  kwenye kijiji chao kilichopo wilaya ya Ruangwa.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wananchi wa kijiji cha Mibure ambapo aliwapongeza uamuzi wao wa kujenga Zahanati ya kijiji kwa kushirikiana na Mbunge wao pamoja na Halmashauri.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa kijiji cha Mibure ambapo aliwashauri vijana kujiunga vikundi na kufanya shughuli za ujenzi kwani kuna miradi mingi ambayo vijana wanaweza kupatiwa fursa ya kuifanya kwa gharama nafuu.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akikagua jengo la zahanati ya kijiji cha Mibure ambacho kinajengwa na mafundi wa kawaida wa kijijini hapo.
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akiwasalimu wananchi wa kata ya Chienjele wilayani Ruangwa.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwahutubia wakazi wa kata ya Chienjele wilaya ya Ruangwa ambapo aliwaambia vijana kuwa bado kuna fursa nzuri nchini katika kuleta maendeleo.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki ujenzi wa ofisi ya CCMkata ya Nandagala wilayani Ruangwa.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiangalia chanzo cha maji kwenye mto Ole kijiji cha Ng’au kata ya Mnachu wilaya ya Ruangwa.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki kupanda miti kwa ajili ya kutunza mazingira pamoja na vyanzo vya maji.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wananchi wa kijiji cha Ng’au Ole wilaya ya Ruangwa ambapo aliwahimiza kutunza mazingira kwa kutokata miti badala yake wapande miti kutunza vyanzo vya maji.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa kata ya Nandagala ,Katibu Mkuu yupo kwenye ziara ya kuimarisha chama mkoa wa Lindi.

TRA YATOA MSAADA KITUO CHA WATOTO YATIMA KIGOMA

Na Magreth Magosso,Kigoma


MAMLAKA ya mapato Tawi la kigoma (TRA) imetumia zaidi ya  sh. Milioni  1.6 kwa kutoa msaada kwa mahitaji ya wajawazito katika vituo vya afya vlivyopo Mkoani ya kigoma ili kuhamasisha jamii juu ya ulipaji kodi.


Mamlaka hiyo imetembelea vituo vya afya vya Kikunku iliyopo manispaa ya Kigoma Ujiji pamoja na Kituo Cha  kulea watoto (vichanga ) yatima  ambacho kinapatikana Halmshauri ya Wilya ya Kigoma vijijini kata ya manyovu ikiwa ni moja kati ya makundi yenye uhitaji zaidi kwaajili ya ukuaji wao.


Misaada iliyotolewa ni pamoja na  maziwa,sabuni ,sukari na mafuta ya kupaka kwa watoto huku wodi ya wajawazito wakinufaika na neti, sabuni na gloves ili kuwawezesha akina mama hawa kujifungua katika mazingira mazuri.


  Akitoa misaada hiyo, kaimu meneja wa TRA Patrice Mushi alisema hakujua kama kituo hicho kina mahitaji makubwa  zinzoendana na changamoto za  kulea watoto hao na kuhakikisha mahitaji yao yote ya muhimu yanapatikana.


“ ofisa ustawi  wilaya ya kigoma alinishauri nilete msaada ,nahisi nilicholeta hakitakidhi hitaji,watoto wana umri wa mika 0-1 wanahitaji madawa na uangalizi mzuri ,motisha kwa walezi  na hawa wenye mambukizi ya virusi vya ukimwi na huyu ana maji kichwani 


Akipokea msaada Mlezi wa kituo cha Matiazo Mary Leonard alisema changamoto iliyopo ni uhaba wa maziwa ,mafuta ya kupakaa,nepi za kisasa,madawa na usafiri na ghrama za kuwapeleka kliniki watoto walio na shida kubwa ya afya,hasa mwenye maji kichwani na wenye shida ya kutoboka kwa moyo.


“ nina miaka 19 tangu nianze kulea watoto vichanga,ambao wengi walitupwa na kufiwa na mama ,ambapo tunalea na ikifika mwaka 1 familia inawajibu wa kumchukua ,shida familia huwatelekeza hawaji kuwachukua na maofisa ustawi hutuachia jukumu la kumsomesha ,mfadhili kajitoa “ alibainisha Leonard.


Kwa upande wa mchungaji wa kanisa la Aglikana Fredy  Stephano alisema chamgamoto ya ugumu wa maisha inachangia familia kutelekeza watoto waliovuka umri wa mika miwili washindwe kuwachukua ,hasa waliofiwa na wazazi wa kike.


Naye ofisa ustawi wa jamii halmashauri ya wilaya ya kigoma  Penina Mbwete alisema awali kituo cha matyazo kilifadhiliwa na WFP kwa kushirikiana na kanisa la anglikana ,hivi sasa WFP  anafadhili wakimbizi na wanatarajia katika bajeti ya 2015/16 kituo kitawekewa bajeti ili kuendelea kutoa huduma husika.


Alisema wanawake waliowengi hivi sasa wanatupa watoto baada ya kujifungua,ambapo mwanzoni mwa mwaka huu kuna mwanamke mmoja alitundika mtoto na kondo lake juu ya mti na kuondoka ambapo wananchi wakishirikiana na ofisa ustawi walimwahisha hospitali ya rufaa na leo ana mwaka 1 na anaitwa Pamela.


Hali ya kutupa watoto vichakani inachangiwa na wanaume kuwakana wanawake wanaowapa ujauzito na wanaume wenye ndoa zaidi ya moja sanjari na michepuko ni chachu ya mimba zenye kutelekeza watoto hatimaye taifa linakabiliana na watoto waishio katika mazingira hatarishi.

Thursday, November 20, 2014

"ILI KUONDOKANA NA HALI HII SULUHISHO NI KUJIUNGA NA MFUKO WA BIMA YA AFYA"

"Ni vema kwa kila Mtanzania bila kujali rangi,dini,kabila au itikadi za kisiasa akawa na mtazamo wa kujali afya yake na familia kwa ujumla.....Kuna kila sababu ya kutambua kuwa msingi mkuu wa maisha ya binadamu ni kutambua umuhimu wa utatuzi wa changamoto mbalimbali zinazokabili maisha ya kila siku ya mwanadamu ikiwa ni pamoja na upatikanaji wa uhakika wa chakula cha kila siku huku ukitoa kipaumbele chenye umuhimu wa pekee katika suala zima la AFYA YA MSINGI....Ili kufikia hatua za kukabiliana ipasavyo na  uboreshaji wa huduma za AFYA,hakuna jambo kubwa zaidi ya kuwepo kwa mikakati makini na inayoweza kutekelezeka huku ikiwekewa misingi imara kwa kufuata taratibu,kanuni na sheria ili kuweza kufikia Malengo....Kwa mwananchi masikini njia pekee itakayomsaidia kufikia malengo ya kujiwekea ulinzi kwenye AFYA yake ni kujiunga na MFUKO WA AFYA YA JAMII unaosimamiwa na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya NHIF...Kwa kufanya hivyo mwananchi huyu masikini atakuwa amejihakikishia upatikanaji wa huduma muhimu za afya mahali popote alipo". 

TIMU YA UKAGUZI WA MIRADI YA MAENDELEO YAKAGUA MADARAJA LUHEKEI MKOANI RUVUMA

SONY DSCMeneja wa wakala wa barabara (TANROADS) mkoani Ruvuma, Mhandisi Abraham Kissimbo akizungumza na timu ya ukaguzi wa miradi ya maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango ilipofika ofisini kwake. SONY DSCKiongozi wa Timu ya ukaguzi wa miradi ya maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Bibi Florence Mwanri (mwenye koti jekundu) pamoja na timu yake wakijinea Daraja la Luhekei C lenye urefu wa mita 60. SONY DSCKiongozi wa Timu ya ukaguzi wa miradi ya maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Bibi Florence Mwanri (mwenye koti jekundu) pamoja na timu yake wakijinea Daraja la Luhekei C lenye urefu wa mita 60. SONY DSCTimu ya ukaguzi wa miradi ya maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango ikiwa katika picha ya pamoja na  mwenyeji wao Mhandisi Lusage Mulenzi katika kibao cha ufunguzi rasmi wa Darala la Luhekei C. Daraja hili lina urefu wa mita 60, lilifunguliwa rasmi tarehe 18 Julai, 2014 na Mheshimiwa Rais, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete.
PICHA ZOTE NA SAIDI MKABAKULI