Pages

KAPIPI TV

Wednesday, October 22, 2014

RAIS KIKWETE AKUTANA NA MABALOZI WA AFRIKA NCHINI CHINA


unnamedRais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza na mabalozi wa Afrika wanaoziwakilkisha nchi zao nchini China wakati alipokutana nao jijini Beijing China leo asubuhi.Rais Kikwete yupo nchini China kwa ziara ya kiserikali(picha na Freddy Maro)unnamed3

SHIRIKA LA NDEGE LA FLY DUBAI LAZINDUA NJIA MBILI MPYA ZA NDEGE


Makamu wa Rais mwandamizi katika shughuli za kibiashara wa shirika la ndege la FlyDubai ,Bwa.Sudhir Sreedharan akizungumza mbele ya wageni waalikwa mbalimbali wakiwemo wana habari kutoka vyombo mbalimbali (hawapo pichani) katika hafla fupi ya uzinduzi wa njia mbili mpya za shirika la ndege hiyo kutoka Dubai kuja jijini Dar es salaam na Zanzibara (nchini Tanzania). Bwa.Sudhir amesema kuwa shirika hilo la Flydubai liliingia katika soko la kibiashara kuanzia mnamo mwaka 12009,ambapo mpaka sasa wamefanikiwa kuongeza njia mpya sita (six new routes ) .
Mgeni rasmi,Waziri wa nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano,Mh Samia Suluhu akizungumza mapema leo katika uzinduzi wa njia mbili mpya za ndege ya FlyDubai aina ya Boieng 737-800,uliofanyika katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere,jijini Dar.

Wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya uzinduzi huo wa njia mpya ya shirika la ndege la Flydubai lenye makao yake makuu Dubai..

 Wageni waalikwa wakishangilia jambo.
Sehemu ya wageni waalikwa wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri kwenye tukio hilo .

MAHAKAMA YA TANZANIA IMEDHAMIRIA KUTEKELEZA DIRA YAKE YA HAKI SAWA KWA WOTE


Kaimu Mkurugenzi, Kurugenzi ya Usimamizi na Uendeshaji wa Mashauri kutoka Mahakama ya Tanzania Bw. John Kahyoza akiwaeleza waandishi wa (hawapo pichani) mikakati iliyoweka iliyowekwa na Mahakama ya Tanzania ili kutekeleza dira yake ya haki sawa kwa wote na kwa wakati kwa vitendo, kwa kuhakikisha inapunguza muda wa mashauri kukaa mahakamani, wakati wa mkutano uliofanyika leo Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Afisa Habari wa Mahakama ya Tanzania Bi. Mary Gwera. Picha na Hassan silayo-maelezo
………………………………………………………………………………..

Na Georgina Misama-MAELEZO.
Mahakama ya Tanzania imedhamiria kutekeleza dira yake ya haki sawa kwa wote ili kuhakikisha inapunguza muda wa mashauri na rufaa kukaa Mahakamani kwa muda mrefu. Hayo yamesemwa na Afisa Habari wa Mahakama ya Tanzania Bi Mary Gwera wakati wa mkutano uliofanyika leo Jijini Dar es Salaam.
 
Akizitaja hatua zilizochukuliwa na Mahakama Bi Mary alisema, kuboresha bajeti ya kushughulikia mashauri kupitia mfuko wa mahakama toka bilioni 57 kwa mwaka 2012/13 mpaka bilioni 88 mwaka 2014/15, Idadi ya vikao vya Mahakama ya Rufani vimeongezeka kutoka 26 mwaka 2012 hadi 34 mwaka 2013/14.
 
Aidha, Bi Mary alisema kuwa hatua nyingine ni pamoja na kuanzisha kitengo cha Mahakama Kuu Dar es Salaam kitakachoshughulikia masuala ya utatuzi wa mashauri kwa njia ya suluhu muafaka, pia uundwaji wa kamati ya kanuni za Mahakama itakayosaidia kutunga au kurekebisha kanuni ili kuhakikisha kuwa kanuni zinazotumika Mahakamani si chanzo cha kuchelewa mashauri Mahakamami
 
Naye, Kaimu Mkurugenzi, Kurugenzi ya Usimamizi na Uendeshaji wa Mashauri kutoka Mahakama ya Tanzania Bw. John Kahyoza alisema kuwa Mahakama imeanza kuchukua hatua za kuimarisha ukaguzi wa shughuli za Mahakama na maadili ya watumishi kwa kuanzisha kurugenzi ya ukaguzi na maadili.
 
Aidha, Bw Kahyoza alivitaja viwango ambavyo kila hakimu au Jaji anatakiwa kuvitimiza kwa mwaka na muda ambao mashauri yanatakiwa kuwa Mahakamani kuwa ni Mh. Jaji wa Mahakama Kuu analenga kumaliza kesi 220, Mahakimu wa Mahakama za Wilaya na Hakimu Mkazi kesi 250 na Mahakimu wa Mahakama za mwanzo kesi 260
 
Mahakama Kuu inatoa rai kwa Watanzania kufika Mahakamani kwa Tarehe zinazopangwa ili kuisaidia Mahakama kuhakikisha inapunguza muda wa mashauri kukaa Mahakamani.

"MADIWANI SIMAMIENI VIZURI MAPATO NA MIRADI YA MAENDELEO"; KAMOGA

Na Allan Ntana, Sikonge

MADIWANI wa halmashauri ya wilaya ya Sikonge mkoani Tabora wametakiwa
kusimamia kwa nguvu zote ukusanyaji wa mapato ya ndani na kufuatilia
kwa karibu zaidi utekelezaji wa miradi ya maendeleo ili kufanikisha
shughuli zote za uendeshaji wa halmashauri hiyo kwa kiwango
kinachotakiwa.

Rai hiyo imetolewa na Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya hiyo Robert
Kamoga katika hotuba yake ya ufunguzi wa kikao cha baraza la madiwani
wa halmashauri hiyo kilichofanyika jana katika ukumbi wa Chuo cha
Maendeleo ya Jamii (FDC) mjini Sikonge.

Alisema ili halmashauri hiyo iweze kufanikisha utekelezaji wa mipango
yake ya kimaendeleo kwa mwaka wa fedha 2014/2015 kama ilivyopangwa
wanapaswa kuongeza juhudi katika suala zima la ukusanyaji mapato
kutoka katika vyanzo vyake vya ndani sambamba na kuwa na usimamaizi
mzuri wa mapato hayo.

Akielezea jitihada zilizowezesha halmashauri hiyo kuvuka lengo la
makusanyo katika kipindi cha msimu wa 2013/2014, alisema watendaji
wote walishikamana na kuwa kitu kimoja huku kila mmoja akitekeleza
wajibu wake ipasavyo, hivyo akawataka madiwani hao kusimamia kwa nguvu
zote ukusanyaji mapato na utekelezaji miradi ili kufanikisha malengo
ya halmashauri hiyo.

‘Waheshimiwa madiwani ili kufikia lengo la kukusanya kile
tulichojipangia hatuna budi kusimamia kwa nguvu zetu zote ili tuweze
kufanikisha utekelezaji wa miradi mbalimbali ikiwemo ujenzi wa maabara
kwa kila shule na shughuli zote za uendeshaji wa halmashauri yetu’,
aliongeza.

Akizungumzia mafanikio ya miradi mbalimbali ya maendeleo, Kamoga
alisema huduma katika zahanati na vituo vya afya Kitunda na Mazinge
zimeendelea kuboreshwa kwa kuongeza majengo ya upasuaji na vifaa tiba
kupitia mapato ya halmashauri na michango ya wahisani.

Huduma nyingine ambazo zimeendelea kuboreshwa ni usambazaji wa maji
safi na salama sambamba na ukamilishaji ujenzi wa miradi ya maji
Majojoro na Mibono ikiwemo mradi wa usambazaji maji Sikonge mjini,
japokuwa changamoto kadhaa zimekuwa zikijitokeza ikiwemo uharibifu wa
miundo mbinu, ukosefu wa nishati ya kuendeshea mitambo na maji
kutowafikia wananchi wote.

Aidha Kamoga alisema sekta ya elimu pia imeendelea kuboreshwa kwa
kiwango kikubwa kwa kuongeza madawati mashuleni, ujenzi wa nyumba za
waalimu na vyumba vya madarasa sambamba na uboreshaji miundo mbinu ya
barabara kwa kufanya matengenezo ya mara kwa mara ya barabara zote za
vijijini na mjini.

Akitoa salaamu kwa niaba ya Mkuu wa wilaya hiyo Hanifa Selengu,
KatibuTawala wa halmashauri hiyo Geofrey Mtalemwa aliwataka watendaji
wote wa vijiji na kata kwa kushirikiana na madiwani kuhamasisha
kuhamasisha wananchi kushiriki kikamilifu katika suala zima la kilimo
kwani msimu wa mvua ndio umeanza.

Pia aliwataka watendaji wote wa halmashauri, tarafa, kata na vijiji
kuhamasisha na kusimamia ipasavyo suala la elimu kwa kulipa uzito
unaostahili hasa ikizingatiwa kuwa taifa zima liko katika mchakato wa
ujenzi wa maabara katika kila shule, kwani maabara zinaendana na uwepo
wa wanafunzi, vinginevyo hatuwezi kufanikiwa.

WATU WATATU WAUAWA MKOANI MBEYA


WATATU WAUAWA MBEYA 

WATU WATATU WASIOFAHAMIKA MAJINA WALA MAKAZI YAO, JINSI ZA KIUME, UMRI KATI YA MIAKA 25 -29, WALIUAWA KWA KUPIGWA NA KUNDI LA WANANCHI WALIOAMUA KUJICHUKULIA SHERIA MKONONI WAKITUMIA SILAHA ZA JADI, FIMBO, MAWE KUTOKANA NA TUHUMA ZA UVUNJAJI.

TUKIO HILO USIKU WA KUAMKIA LEO MAJIRA YA SAA 00:51 HUKO KATIKA HOSPITALI YA RUFAA MKOA WA MBEYA, KATA NA TARAFA YA SISIMBA, JIJI NA MKOA WA MBEYA.

INADAIWA KUWA, WANANCHI HAO WAISHIO KATIKA ENEO LA FOREST MPYA NYUMA YA HOSPITALI YA MKOA WA MBEYA WALIWAKAMATA WATU HAO WAKIWA NA VIFAA VINAVYOTUMIKA KUVUNJIA VIKIWEMO NONDO, PLAIZI PAMOJA NA MISUMARI NA NDIPO WALIAMUA KUWASHAMBULIA KWA KUWAPIGA SEHEMU MBALIMBALI ZA MIILI.

WATU HAO WALIFARIKI DUNIA WAKIWA NJIANI KUPELEKWA HOSPITALI YA RUFAA MBEYA NA ASKARI WA KIKOSI CHA KUZUIA NA KUPAMBANA NA UJAMBAZI CHA WILAYA YA MBEYA, JUHUDI ZA KUWATAFUTA WALIOHUSIKA KATIKA TUKIO HILI ZINAENDELEA. 

MIILI YA MAREHEMU IMEHIFADHIWA KATIKA HOSPITALI YA RUFAA MBEYA KWA UCHUNGUZI WA KITABIBU NA UTAMBUZI.

KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI BARAKAEL N. MASAKI ANATOA WITO KWA WANANCHI KUACHA TABIA YA KUJICHUKULIA SHERIA MKONONI KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA BADALA YAKE WAWAFIKISHE WATUHUMIWA WANAOWAKAMATA KWA TUHUMA MBALIMBALI KATIKA MAMLAKA HUSIKA KWA HATUA ZAIDI ZA KISHERIA.

KATIKA TUKIO LA PILI:
 MTU MMOJA MKAZI WA KIJIJI CHA KANGAGA WILAYANI MBARALI AITWAYE FUNGO KIFANGA (50) ALIUAWA KWA KUPIGWA NA KITU KIZITO SEHEMU ZA KICHWANI NA MTU/WATU WASIOFAHAMIKA.

TUKIO HILO LIMETOKEA MNAMO TAREHE 21.10.2014 MAJIRA YA SAA 19:00 JIONI HUKO KATIKA KIJIJI CHA KANGAGA, KATA YA MAWINDI, TARAFA YA RUJEWA, WILAYA YA MBARALI, MKOA WA MBEYA.

INADAIWA KUWA, CHANZO CHA MAUAJI HAYO NI UGOMVI WA ARDHI KATI YA MAREHEMU NA WATU HAO AMBAO BADO KUFAHAMIKA. AIDHA, WATU WATATU WANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA MAHOJIANO ZAIDI KUHUSIANA NA TUKIO HILO AMBAO NI 1. CLEMENCE KIBIKI, (28) MKAZI WA KANGAGA 2. IMANI KIBIKI (23) MKAZI WA KANGAGA NA 3. FIDELIS KIBIKI (34) MKAZI WA KANGAGA. 

MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA KATIKA HOSPITALI YA WILAYA YA MBARALI KWA UCHUNGUZI WA KITABIBU.
KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI BARAKAEL N. MASAKI ANATOA WITO KWA WANANCHI KUTATUA MIGOGORO YAO KWA NJIA YA AMANI NA UTULIVU ILI KUEPUKA MADHARA YANAYOWEZA KUEPUKIKA.

KATIKA TUKIO LA TATU:
MTU MMOJA MKAZI WA KIJIJI CHA MBIGILI WILAYA YA RUNGWE AITWAYE AMANI LIKENEME MWAKYOMA (50) ALIUAWA KWA KUKATWA NA KITU CHENYE NCHA KALI SEHEMU ZA KICHWANI NA MTU/WATU WASIOFAHAMIKA.

TUKIO HILO LIMETOKEA MNAMO TAREHE 20.10.2014 MAJIRA YA SAA 23:00 USIKU HUKO KATIKA KIJIJI CHA MBIGILI, KATA YA RWANGWA, TARAFA YA BUSOKELO, WILAYA YA RUNGWE, MKOA WA MBEYA.

CHANZO CHA MAUAJI HAYO BADO HAKIJAFAHAMIKA, JUHUDI ZA KUWATAFUTA WALIOHUSIKA KATIKA TUKIO HILI ZINAENDELEA. MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA KATIKA HOSPITALI YA WILAYA YA RUNGWE.

KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI BARAKAEL N. MASAKI ANATOA WITO KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA ZA MAHALI ALIPO/WALIPO WATU WALIOHUSIKA KATIKA TUKIO HILI AZITOE KATIKA MAMLAKA HUSIKA KWA HATUA ZAIDI ZA KISHERIA. Imesainiwa na: [BARAKAEL N. MASAKI – ACP] KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.

MAAMBUKIZI VVU KUTOKA KWA MAMA KWENDA KWA MTOTO YAPUNGUA-EGPAF

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr.Jakaya Mrisho  Kikwete akipata maelezo kwa Meneja wa Shirika la EGPAF Dr.Alphaxard Lwitakubi, wakati wa maonesho ya wiki ya vijana iliyofanyika kitaifa mkoani Tabora.
MAAMBUKIZI ya virusi vya Ukimwi (VVU), kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto yamepungua kwa asilimia 90. Imeelezwa.
Hayo yalisemwa na Meneja wa shirika la EGPAF Mkoa wa Tabora, Dk. Alphaxard Lwitakubi, mara baada ya Rais Jakaya Kikwete kukagua banda la shirika hilo katika maonyesho ya wiki ya vijana iliyoambatana na kilele cha kuzimwa kwa Mwenge wa Uhuru.
Lwitakubi, alisema lengo la EGPAF ni kufikia asilimia 98 ifikapo mwishoni mwa mwaka 2015.
Alisema hatua hiyo itafikiwa endapo wanaume wataambatana na wake zao kwenda kwenye vituo vya afya kama inavyotakiwa, kwani hadi sasa zimefikiwa asilimia 48 kwa mwaka 2014 kutoka asilimia 5 mwaka 2010.
Dk. Lwitakubi, alisema Shirika la EGPAF limekuwa likijihusisha na kazi za kuzuia na kutokomeza maambukizi ya virusi vya Ukimwi (VVU), kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto.
Alisema EGPAF inafanya kazi zake katika mikoa ya Tabora, KilimanjaroArusha, Lindi, Shinyanga, Geita na Simiyu.
Aliongeza kuwa EGPAF pia imekuwa ikijihusisha na wagonjwa wa majumbani katika mikoa ya Pwani, Zanzibar na Mwanza huku likitoa huduma za uchunguzi wa
saratani ya shingo ya kizazi mikoa ya Tabora, Kilimanjaro,
Shinyanga, Arusha, Simiyu, Lindi na Geita.


Kwa upande wake, Mratibu wa Mawasiliano na Utetezi wa EGPAF, Mercy Nyanda, alisema katika huduma zao kumekuwa na mafanikio, kwani kwa sasa wajawazito wengi wanajifungulia vituoni tofauti hapo mwanzo.
Nyanda, alisema uelewa kwa jamii umeongezeka zaidi kuhusu hali halisi ya maamukizi ya VVU na jamii hiyo kuendelea kubadilika.

BREAKING NEWS:KITU KINACHOSADIKIWA KUWA NI BOMU KIMELIPUKA KARIBU NA KITUO CHA POLISI LINDI

Picha kutoka Maktaba

Kitu kinachosadikiwa kuwa ni bomu kimelipuka Mkoani Lindi karibu na kituo cha Polisi wakati Askari Polisi hao wakifanya usafi kwa kuchoma taka karibu na kituo hicho cha polisi

eatv.tv
Read more

LUNDENGA AOMBA VITHIBITISHO VYA MISS TANZANIA 2014

Tuesday, October 21, 2014

GAIDI MKUU WA ULIPUAJI WA MABOMU AUAWA NA POLISI ARUSHA


1
Kamanda wa Polisi mkoa wa Arusha, Liberatus Sabas.
Kiongozi wa  matukio ya ulipuaji wa mabomu na umwagiaji tindikali viongozi wa dini aliyejulikana kwa jina la Yahaya Hassani Omary ameuwawa na jeshi la polisi wakati alivyokuwa akijaribu kukimbia.

Akithitisha kutokea kwa tukio hilo kamanda wa polisi mkoani Arusha, Liberatus Sabas, alisema kuwa tukio hilo limetokea  October 19 majira ya saa tano na nusu  katika barabara ya Babati mkoani Arusha wakati alipokuwa akijaribu kuwakimbia polisi.

Alisema kuwa mtuhumiwa huyo wa ugaidi alishikiliwa wiki mbili zilizopita  huko mkoani Morogoro  mara baada ya kutafutwa kwa muda mrefu na hapo jana alikuwa akipelekwa wilayani Kondoa mkoani Dodoma  kwa ajili ya kwenda kuonyesha sehemu ambazo alikuwa ameficha mabomu mengine.

“mtuhumiwa huyu alikuwa anasakwa kwa muda mrefu bila mafanikio kwani alikuwa hakai sehemu moja ila jeshi la polisi huko mkoani Morogoro lilimkamata wiki mbili zilizopita na baada ya kufanyia mahojiano alisema ameficha mabomu mengine huko Kondoa na juzi alikuwa akipelekwa kuonyesha ndipo alipotumia triki zake ambazo amefundishwa za ugaidi kwa kupiga judo na kutaka kuwakimbia askari ndio akapigwa risasi mbili”,  alisema Sabas.

Kamanda Sabas, alitoa wito kwa wananchi kuendelea kuwafichua waovu  ili kuwaza kuteketeza matukio ya uhalifu. Habari kwa hisani ya woindeshizza blog

MSANII MAARUFU NCHINI Y-P WA TMK AFARIKI DUNIA

Wasanii wa Wanaume Family, kutoka kushoto, Dogo Aslay, Stiko na Yesaya Ambilikile YP (kulia) wakiwa katika pozi.

Msanii wa kundi la TMK Wanaume Family,Yesaya Ambilikile ‘ Y- P’ amefariki dunia usiku wa leo katika Hospitali ya Temeke baada ya kusumbuliwa kwa muda mrefu na ugonjwa wa kifua.
Akizungumza na mtandao huu Kiongozi wa kundi hilo, Said Fela, amethibitisha msiba huo na kusema ratiba kamili itatoka leo mchana.

“Mpaka sasa hivi bado hatujaandaa ratiba, tunasubirika kaka yake kwa sababu huyo mtu kafariki usiku hospitali. Kwahiyo ndugu zake wakishakuja ndo watasema tunazikaje, kwa sababu alikuwa mkristo. Kwahiyo kwenye saa 7 mchana ratiba itakuwa tayari,” amesema Fela.

“Tatizo alikuwa anaumwa kifua muda tu, lakini alishaanza kunywa dozi lakini majuzi akazidiwa na tukampeleka hospitali. Jana ndo mwenyezi Mungu kampenda zaidi akamchukua. Wazazi wa marehemu wapo Keko pale, lakini wazazi wake baba na mama walifariki ila ndugu zake wapo, na kuna kibanda waliachiwa na wazazi wake, kwahiyo msiba utakuwa Keko.”
 http://www.globalpublishers.info/)

AIRTEL YAZINDUA WIKI YA RASILIMALI WATU KWA WAFANYAKAZI WAKE


DSC_6938
Mkurugenzi Mkuu wa Airtel  Tanzania Bwn Sunil Colaso akiongea na wafanyazi wakati wa uzinduzi wa wiki ya Rasimali watu uliofanyika katika Ofisi za makao makuu ya  Airtel ambapo wafanyakazi watapata fulsa ya kupata elimu juu ya sera kuhusu mafao mbalimbali na haki yaoza kimsingi  na huduma nyinginezo zinazotolewa na kusimamiwa na kitengo cha Rasilimali  watu, hafla ya uzinduzi huo imefanyika katika ofisi za Airtel Moroko leo HR group photo 2Baadhi ya wafanyakazi wa kitengo cha rasilimali watu cha Airtel Tanzania wakiwa katika picha ya pamoja  wakati wa uzinduzi wa wiki ya Rasilimali watu iliyozinduliwa  rasmi jana katika ofisi za makao makuu ya Airtel jijini Dar es saalam, IMG_6107wafanyakazi wa Airtel wakifatilia uzinduzi wa  uzinduzi wa wiki ya Rasilimali watu iliyozinduliwa  rasmi jana katika ofisi za makao makuu ya Airtel jijini Dar es saalam
PIC 2Mkurugenzi wa Kitengo cha Rasilimali watu Airtel  Tanzania Patric Foya akiongea wakati wa uzinduzi wa wiki ya Rasimali watu uliofanyika katika Ofisi za makao makuu ya  Airtel ambapo wafanyakazi watapata fulsa ya kupata elimu juu ya sera kuhusu mafao mbalimbali na haki yao
za kimsingi  na huduma nyinginezo zinazotolewa na kusimamiwa na kitengo cha Rasilimali  watu, hafla ya uzinduzi huo imefanyika katika ofisi za Airtel Moroko leo Pic 4Mchekeshaji na mshereheshaji  maarufu kama MC Pilipili  akitoa burdani kwa wafanyakazi wa Airtel wakati wa uzinduzi wa wiki ya Rasimali watu iliyozinduliwa mahususi kwa wafanyakazi wa Airtel kupata elimu juu ya sera na huduma mbalimbali zinazotolewa na kusimamiwa na Kitengo cha Rasilimali watu, hafla ya uzinduzi huo imefanyika katika ofisi za
Airtel Moroko leo
pIC 5Wafanyakazi wa Airtel wakifurahia burdani toka kwa Mchekeshaji na mshereheshaji  maarufu kama MC Pilipili  wakati wa uzinduzi wa wiki ya Rasimali watu iliyozinduliwa mahususi kwa wafanyakazi wa Airtel kupata elimu juu ya sera na huduma mbalimbali zinazotolewa na kusimamiwa na Kitengo cha Rasilimali watu, hafla ya uzinduzi huo imefanyika katika
ofisi za Airtel Moroko leo
…………………………………………………….
Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel leo imezindua rasmi wiki ya Rasilimali watu itakayowawezesha wafanyakazi wake kupata elimu kuhusu Sera  na  huduma mbalimbali zinazotolewa kwa wafanyakazi na kusimamiwa na kitengo cha Rasillimali watu kwa lengo la kuwaongezea wafanyakazi ufanisi zaidi wa kuhudumia wateja

Airtel imeandaa wiki hiyo ya rasilimali watu katika nchini zote Afrika ambapo Airtel inafanya biashara zake na kuzinduliwa rasmi leo nchi Tanzania, airtel imefanya hivyo leo  ikiwa ni muda mfupi tu tangu ilipoadhimisha  wiki ya huduma kwa wateja inayoadhimishwa duniani kote ambapo airtel ilishiriki katika maadhimisho hayo .

Akiongea wakati wa uzinduzi huo Mkurugenzi  wa kitengo cha Rasilimali watu Bwana Patrick Foya alisema”  Tunategemea kuwa na wiki yenye mafanikio ambayo itawawezesha wafanyakazi wetu kupata ufafanuzi juu ya maswala mbalimbali yanayohusu sera na  haki zao za msingi kama wafanyakazi wa Airtel. 

Sambamba na hilo tutakuwa na watoa huduma kutoka kwenye makampuni mengine wakiwemo strategies inayotoa huduma za bima ya afya, NSSF  inayotoa mikopo ya nyumba na mafao kwa wafanyakazi
 na makapuni mengine mengi  ambayo yatatoa fulsa ya wafanyakazi wetu
kupata elimu zaidi kuhusu huduma hizi muhimu na jinsi yakufaidika nazo hii ni fulsa kwa wafanyakazi wetu nasi tuko tayari kuwafikishia wote ili kuongeza ufanisi kazini”.

Natoa wito kwa wafanyakazi kujitokeza katika sehemu maalumu zilizoandaliwa kutoa huduma na kupata mambo mazuri tuliyowaandalia wiki nzima alingoza Foya

Naye Mkurugenzi Mkuu wa Airtel Bwana Sunil Colaso aliwashukuru wafanyakazi wa kitengo cha rasilimali watu kwa kujipanga vyema kwa wiki hii na kusisitiza kuwa elimu na mafunzo haya ni mwendelezo wa mpango mkakati wa kuhakikisha kuwa wafanya kazi wote wanajua mambo muhimu yanayotokana na ajira zao, sera mbalimbali kama vile za afya na zile zinazogusa maslahi yao’.
Colaso alisema “ natoa wito kwa wafanyakazi kutumia wiki vyema na kuuliza mswali mengi yatakayo toa ufafanuzi wa maswala wanayohitaji elimu  na uelewa zaidi.

WAFUGAJI KAKONKO WAUA WATU WAWILI FAMILIA MOJA KISA KISASI...KIGOMA

Na Magreth Magosso,Kigoma

WAFUGAJI   wanaoishi kijiji cha Minyinya Kata ya Nyamtukuza wilaya ya Kakonko Mkoa wa Kigoma,wamewashambulia  Baba  na mtoto  kisha kuwachoma moto hadi kufa kwa madai ya kuwaamuru  waoneshe walipo majambazi walioua  Mfugaji wa ng'ombe katika tukio la Octoba ,15,2014.

Akielezea  tukio hilo Mwenyekiti wa kijiji cha Minyinya Justini Kilegea   alisema tukio hilo ni  la kulipiza kisasi kwa wakulima ambapo wafugaji walihisi waliovamia na kuua mwenzao wiki iliyopita alitoka katika jamii ya wakulima hivyo walitaka waoneshe waliofanya tukio hilo jambo ambalo lilizua tafrani na kuanza kushambuliwa hatimaye kuwaua.

“sasa usiku wa Octoba ,19 kuamkia 20,mwaka huu ndipo wafugaji  walivamia nyumba za wakulima zipo hukohuko mashambani na kuzichoma moto na hatimae  kumuua mtu na mwanae Kachila Kahegele (48) na Lameck Kahegele (26) .

Baadhi ya wakazi wa kijiji hicho Daniel Paulo ,Jonas Matwa na Silace Kahebela walidai mwenyekiti wa kijiji hicho ndio chanzo cha mauaji baina ya wafugaji wageni na wakulima ,ambapo hugawa ardhi kinyemela ,bila kushirikisha wananchi ,hatua ambayo imekuwa ni chanzo  na  chokochoko za mapigano baina ya pande hizo  mbili.
 
Kwa upande wa Mkuu wa wilaya ya Kibondo Venance Mwamoto alisema wafugaji hao walifika hapo wakisaka madini na walipokosa walianzisha kilimo na ufugaji  wa ngombe ukashamiri na hatimaye wakanzisha kijiji hali iliyowavutia wakazi wa Minyinya kuhamia huko mashambani  na 15,Octoba,2014  miongoni mwa wakulima waliua mfugaji  mmoja.

 
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kigoma  Jafari Mohamed alipoulizwa juu ya mauwaji hayo ,alisema yupo nje ya mkoa ,hivyo hajapewa taarifa ya tukio hilo na kusisitiza kuwa kila raia anawajibu wa kutii sheria bila shuruti hata kama alionewa akithibitika anawajibika katika vyombo vya dola.

OFISI YA WAZIRI MKUU YAFANYA TATHMINI YA HALI YA CHAKULA NA LISHE MKOANI SIMIYU

PICHA NO. 4Baadhi ya wanakijiji wa kijiji cha Kabita wilayani Busega, Simiyu wakifuatilia mkutano wa kijiji uliokuwa ukijadili hali ya Chakula na Lishe kijijini hapo wakati Ofisi ya Waziri Mkuu ilipofika kijijini hapo kufanya tathmini ya masuala hayo Oktoba, 2014.
PICHA NO. 1Bw. Clement Ngosha wa kijijini Kabita Wilayani Busega, Simiyu, akitumia mbegu za mahindi kueleza hali ya chakula kijijini hapo kwa wataalam wa Tathmini ya Hali ya Chakula na Lishe inayofanywa na Ofisi ya Waziri Mkuu, Oktoba, 2014.
PICHA NO. 2Mtaalam wa Usalama wa chakula kutoka Wizara ya kilimo, chakula na Ushirika, Bi. Tatu Kayumbu akiihoji moja ya kaya kijijini Mwamanyili,Wilayani Busega, Simiyu wakati wa Tathmini ya Hali ya Chakula na Lishe inayofanywa na Ofisi ya Waziri Mkuu kijijini hapo, Oktoba, 2014.
……………………………………………………………….
Na. Ibrahim Hamidu Ofisi ya Waziri Mkuu kupitia Idara ya Uratibu wa maafa inafanya Tathmini ya Hali ya Chakula na Lishe Mkoani Simiyu katika Wilaya zake zote ambazo ni; Halmashauri za Wilaya za Bariadi, Itilima, Maswa ,Bariadi Meatu na Busega.
 
Akiongea mkoani Simiyu kiongozi wa Wataalam wa tathmini ambaye pia ni mratibu wa shughuli za maafa Ofisi ya Waziri Mkuu Bw. Edgar Senga alibainisha kuwa Ofisi ya Waziri Mkuu imefikia maamuzi hayo ya kufanya tathmini mkoani Simiyu baada ya mkoa huo kutuma maombi katika Ofisi hiyo kuwa wana upungufu wa chakula.
 
“ Ofisi ya mkoa ya Simiyu ilileta maombi kwa ofisi ya Waziri Mkuu kuwa wanaoupungufu wa chakula takribani tani 48,975, kwa kuwa Ofisi yetu ndio yenye dhamana ya kuratibu misaada ya chakula hivyo haikuwanabudi kufanya tathmini ya haraka ili kubaini hali ya chakula ya mkoa huu ili kuweza kuamua namna ya kushughulikia maombi yao ya msaada wa chakula” alisema Senga
 
Senga alibainisha kuwa Wataalam wa tathimini hiyo wanatoka Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika katika Idara ya Usalama wa Chakula ambao kwa kushirikiana na Ofisi ya Waziri Mkuu wametawanyika katika Wilaya zote za Mkoa wa Simiyu ambapo katika kila Wilaya vitachaguliwa vijiji vitatu vya kufanyiwa tathmini.
 
“Katika kila kijiji wataalamu hawa watakuwa wanamadodoso ya Wilaya na kijiji ambayo yatasaidia kutoa taarifa mahsusi za hali ya chakula na Lishe katika ngazi ya Wilaya na Kijiji, lakini pia wataalamu wanayo madodoso ya kaya ambayo yanalenga kupata taarifa za hali ya chakula na Lishe kwa kaya husika kwa vijiji vitakavyoteuliwa na Serikali za vijiji hivyo. Kwa kuzingatia kuwa wataalam wa masual ya chakula katika ngazi ya Wilaya watakuwa wanahusishwa ninaamini tutapata taarifa bora ya hali ya chakula ya mkoa wa Simiyu ” alisisitiza Senga.
 
Akiongea Ofisini kwake alipotembelewa na ujumbe wa Wataalamu hao Katibu Tawala Msaidizi (Uchumi na Uzalishaji) mkoani Simiyu, Bw. Joseph Nandira alibainisha kuwa Katika kipindi cha msimu wa 2013/2014, Mkoa ulijiwekea malengo ya kuzalisha jumla ya tani 1,003,578 za mazao ya chakula aina ya nafaka/wanga na tani 150,257 aina ya mikunde. Mavuno halisi yaliyopatikana ni tani 476,024 za chakula aina ya nafaka/wanga na tani 74,944 za chakula aina ya mikunde.
 
Nandira alibainisha kuwa kutokana na tabia ya wananchi kuuza sehemu kubwa ya chakula ili kukidhi mahitaji ya familia zao, tathmini ya hali ya chakula tuliyoifanya mwezi Julai 2014, tulibaini kuwa Mkoa Unaupungufu wa chakula wa tani 48,975 za nafaka ambao umeanza kuanzia mwezi Oktoba na upungufu huo wa chakula unatarjiwa kuwepo mwezi Novemba/Desemba hadi Februari, 2015 kama wilaya hazitapata msaada wa chakula.
 
“Tathmini hiyo ilibaini Halmashauri za Wilaya za Busega na Meatu zina upungufu wa chakula kuanzia mwezi Agosti, 2014 hadi Februari, 2015. Halmashauri za Wilaya za Bariadi, Itilima, Maswa na Bariadi Mji zina upungufu wa chakula kuanzia mwezi Oktoba, 2014 hadi mwezi Februari, 2015. Ili kukidhi haja ya upungufu wa chakula ndio maana tuliomba jumla ya tani 48,975 kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu.” Alisema Nandira
 
Nandira alifafanua kuwa ili kuhakikisha tatizo la upungufu wa chakula linakwisha tayari mkoa unayomikakati ambayo inajikita katika Kuwahimiza wananchi kutumia vizuri chakula kilichopatikana na kuepuka matumizi yasiyo ya lazima. Kutoa elimu kwa wananchi kuhusu makadirio ya mahitaji ya chakula ngazi ya kaya kwa mwakapamoja na Kuwashauri wananchi kuuza sehemu ya mifugo yao na kujinunulia chakula wakati huu ambapo chakula bado kina bei ndogo na kinapatikana ndani ya Wilaya na Mkoa.

Aliongeza kuwa mkoa unaendelea kuwashauri wananchi kujinunulia chakula kutokana na fedha za mauzo ya pamba. Kutoa elimu kwa wananchi kuhusu hifadhi bora ya chakula, ikiwa ni pamoja na matumizi ya vihenge bora/vya kisasa na madawa ili chakula kisibunguliwe na wadudu. Kuwashauri wananchi kuuza ziada ya chakula walichovuna na si vinginevyo.

Kwa mujibu wa sensa ya watu ya mwaka 2012 mkoa wa Simiyu una jumla ya watu 1,584,157 ambao wanahitaji jumla ya tani 404,752 za chakula aina ya nafaka/wanga na tani 144,553 za chakula aina ya mikunde kwa kipindi cha msimu wa mwaka 2013/2014.

GARI AINA YA TOYOTA KLUGER INAUZWA BEI SAFI KABISAAA!

 MODEL NI YA MWAKA 2002 TOYOTA KLUGER
UWEZO WA ENGINE NI 2360 CC
IMETEMBEA KILOMITA 170000
BEI NI MILIONI 17 MAELEWANO YAPO 
MAWASILIANO NI 0713242888

CHADEMA YAMPA SIKU 14 DC MANENO ZA UWAJIBIKAJI--KIGOMA

 
Na Magreth Magosso,Kigoma

MWENYEKITI wa chama cha (CHADEMA)  Mkoa wa kigoma Ally Kisala ametoa  siku 14  za uwajibikaji kwa  Mkuu wa wilaya ya Kigoma Ramadhan Maneno  endapo hatawadhibiti wanachama wa chama cha Alliance Transparency For Change(ACT)  kwa kitendo cha  utovu wa nidhamu ,madili,kwa mujibu wa  katiba ya Nchi.

Kauli hiyo ilitolewa jana katika mkutano wa hadhara uliofanyika eneo la Mwanga urusi uliokuwa ukiwataka wananchama wake waache kulumbana hoja na wanachama wa ACT  na kudai chama hicho kuwa ni SACCOS ya mtu mmoja ambaye analengo la kudhofisha vyama vya upinzani .

Chanzo cha kupewa siku 14 ni kutokana na sintofahamu  dhidi ya mgogoro wa  eneo la urusi ambapo awali kulikuwa na Bango la Chadema lililokuwa na wanachama wapatao 20,hatimaye wote wamejiunga   na ACT  na hivyo bango linatumika na ACT .

Hali iliyochangia Mkuu wa wilaya  hiyo  Ramadhan Maneno kuwapa amri wanachama  wa ACT na Chadema wasitishe huduma zao kutpitia bango hilo la Urusi  hadi suala litakapopatiwa ufumbuzi na vyombo vya dola.

“nitatumia nguvu ya watu ili kutimiza uwajibikaji kwa mkuu wa wilaya  itakuwaje walitumie wao na ndio maana Jeshi la Polisi wametoa bendera ya ACT lakini maneno anawabeba nitatumia nguvu ya umma ,damu itamwagika na wataokota maiti” alidai Kisala.

Katibu wa Chadema wilaya ya Kigoma  Frank Lucas alisema kwa miezi mitatu siasa ya kigoma imegubikwa na lugha chafu ambazo hazina  mashiko katika jamii,ilihali wanakabiliwa na adha mbalimbali na kuwaonya wasilumbane hoja na wananchama wa ACT kuanzia jana na kuendelea.

Akijibia hilo Mwenyekiti wa ACT Kigoma  Ibrahim Sendwe alisema siasa za kumwaga damu ni kawaida ya chadema na kudai suala hilo lipo mahakamani na Octoba ,27,2014 kesi itaanza kusikilizwa ,huku akionya Jeshi la Polisi waache kuingilia hoja za wanasiasa na kudai kitendo cha kuondoa bendera ya ACT ni kuidharau Mahakama.

Mbali na hilo uongozi wa chadema wametumia zaidi y ash.200,000 kwa kununua  katoni za juisi,matunda na sabuni za Gwanji na kuzigawa kwa wagonjwa waliolazwa katika Hospitali ya Rufaa ya maweni ,Huku Kaimu Mganga Mkuu wa hospitali hiyo Fadhili Kibaya akiwaongoza katika wodi ya kina mama,watoto na kina baba ili kufanikisha ugawaji huo.

Mjumbe wa Uongozi wa Chadema  kanda ya Kati Taifa Alphonce Mbasa alisema wamejipanga kubadili mwelekeo wa siasa kwa kutoa  huduma  zitakazowafikia wananchi moja kwa  moja hasa kusaidia makundi tete likiwemo wagonjwa na yatima.

JK ACHANGIA KITUO CHA VIJANA SIKONGE MIL. 10


Na Mwandishi wetu, Tabora

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr Jakaya Mrisho Kikwete ameahidi kuchangia kiasi cha sh milioni 10 na trekta moja kwa Kituo chaVijana cha Pathfinder Green City kilichoko  wilaya ya Sikonge mkoani Tabora.

Aliitoa ahadi hiyo alipotembelea kituo hicho chenye vijana wapatao 100 ambao wanajifundishwa utaalamu wa aina mbalimbali ikiwemo ufundi, ujenzi, ufyatuaji matofali ya kisasa (aina ya interlock), kilimo, ufugaji nyuki, ufugaji wa kuku na ng’ombe na ujasiriamali.

Rais alionyeshwa dhahiri kufurahishwa na shughuli za uzalishaji mali zinazofanywa na vijana hao sambamba na kujishughulisha na kilimo cha mazao mbalimbali kama vile tumbaku, mahindi, mpunga na mbogamboga ambapo tayari wameshaanza kujipatia kiasi kikubwa cha fedha kutokana na mauzo ya mazao hayo.

‘Kazi niliyokuta kwenye kijiji cha mfano pale Sikonge imenifurahisha sana, wanafanya mambo makubwa, wanalima tumbaku, mahindi, wanafuga nyuki, kuku, ng’ombe, wanashona viatu, nguo, wanafyatua tofali na kujenga nyumba za kisasa wao wenyewe, hawa vijana ni mfano wa kuigwa, wanastahili pongezi’, alisema.

Nimeahidi kuwasaidia shilingi milioni 10 na trekta ili wafanye kilimo kilicho bora zaidi kitakachowafanikisha kiuchumi wao wenyewe, familia zao, jamii inayowazunguka, wananchi wa wilaya ya Sikonge, mkoa mzima wa Tabora na taifa kwa ujumla, aliongeza.

JK alibainisha kuwa vijana walioko katika kituo hicho kilichoko katikati ya vijiji vya Lufwisi na Tumbili wilayani humo watakuwa mfano wa kuigwa na waalimu wazuri kwa wenzao na jamii nzima kwani mafunzo wanayopata yanawapa ujuzi mkubwa sana katika kilimo na fani nyinginezo.

Aidha JK alipongeza uongozi wa halmashauri ya wilaya hiyo chini ya Mkuu wa wilaya Hanifa Selengu na Mkurugenzi Mtendaji Shadrack Mhagama na serikali ya mkoa huo kwa kufanikisha uanzishwaji kituo hicho cha mfano katika mkoa huo huku akiwataka waendelee kukisimamia vizuri zaidi.

Aidha akiwa katika ziara hiyo aliziagiza halmashauri zote hapa nchini kujiwekea utaratibu wa kutoa taarifa za maendeleo mara kwa mara angalau kila baada ya miezi nne ili kubaini mafanikio yako wapi na changamoto ni zipi ili waweze kuweka utaratibu wa namna ya kukabiliana nazo, kwa kuanzia aliwataka kutoa taarifa za maendeleo mwezi desemba na nyingine baada ya miezi 4.

BI REHEMA AMEPOTEA KWA YEYOTE ATAKAYEMUONA ANAOMBWA KURIPOTI KITUO CHA POLISI AU KILICHOPO KARIBU NAWE

Bi Rehema Salum Msambya pichani juu amepotea tokea tarehe 16/10/2014 maeneo ya Kigamboni - Kisota karibu na Shule ya Sekondari ya Abdu jumbe. 
Siku hiyo alikuwa amevaa Dela Na Skintirt ya Rangi ya Blue. Bi Rehema ana Matatizo ya Akili. Yeyote atakayemuona anaombwa kutoa taarifa katika kituo cha Polisi Kigamboni au kilicho karibu  au Apige simu namba
0712 22 77 22
0753 63 49 67
0712 70 77 87
0713 23 52 94