Pages

KAPIPI TV

Tuesday, August 12, 2014

"CCM WAMKATAA KATIBU WA WILAYA YA TABORA MJINI,WAMEDAI ANAKIPELEKA CHAMA PABAYA"

Katibu wa CCM mkoa wa Tabora Bw.Idd Ame akitoka nje baada ya kuahirishwa kwa mkutano wa kupokea taarifa ya utekelezaji wa Ilani ya CCM ambapo wajumbe walianza kwa kumkataa Katibu wa CCM wilaya ya Tabora mjini  Bw.Bakari Mfaume na kushinikiza uongozi wa ngazi ya juu ya chama hicho kumhamisha katibu huyo ambaye walidai kuwa amekuwa chanzo cha migogoro ndani ya Chama. 
Pamoja na kuahirishwa kwa mkutano huo lakini wajumbe hao bado wameendelea kusisitiza kuwa hawatakuwa tayari kufanyakazi na Katibu wa CCM wilaya ya Tabora mjini ambaye tayari malalamiko ya wajumbe hao walishayafikisha kwa Katibu mkuu wa CCM Taifa Bw.Abdulrahman Kinana licha ya kuwa hadi sasa wajumbe hao  hawajaona mafanikio.Hata hivyo Chama cha mapinduzi wilaya ya Tabora mjini kimekuwa katika sekeseke la mvurugano wa wanachama na viongozi hali ambayo imeelezwa na baadhi ya wanaCCM imetokana na Katibu huyo kudaiwa kuwa anatumiwa na baadhi ya vigogo hasa kwenye maandalizi ya Uchaguzi mkuu wa mwaka 2015.
 Na Mwandishi wetu 
Sakata la Wajumbe wa halmashauri kuu ya CCM wilaya ya Tabora mjini kuendelea kumkataa Katibu wa CCM wilaya ya Tabora mjini bado linaendelea kuchukua kasi na hivyo kuanza kusikika hadharani baada ya wajumbe hao kutoka nje ya kikao cha kupokea utekelezaji wa ilani ya Chama hicho,mkutano uliowakutanisha wajumbe hao na timu ya wataalamu kutoka halmashauri ya manispaa ya Tabora.

Katika mkutano ulioanza majira ya saa nne na nusu ulifanyika uwanja wa Ali Hassan Mwinyi,ambapo mgeni rasmi alikuwa ni Katibu wa CCM mkoa wa Tabora Bw.Idd Ame,mara baada ya hotuba ya ufunguzi wa mkutano huo wajumbe walinyoosha mikono na kudai kuwa hawamtaki Katibu wa CCM wilaya ya Tabora Bw.Bakari Mfaume kutokana na kukosa imani naye na hivyo kuhitaji aondolewe katika mkutano huo muhimu kwa maendeleo ya wilaya ya Tabora.

Hata hivyo pamoja na Katibu wa CCM mkoa wa Tabora  Bw.Ame kuingilia kati na kujaribu kuwatuliza wajumbe kwa kuwafahamisha kuhusu lalamiko lao dhidi ya Katibu wa wilaya lakini jitihada hizo hazikuzaa matunda kutokana na baadhi ya wajumbe kuanza kutoka nje ya kikao hicho.

"Tafadharini wanaCCM wenzangu suala la Katibu inaeleweka wazi kuwa linashughulikiwa na makao makuu kwahiyo sisi tuvute subira,tusubiri maamuzi ya Katibu mkuu Kinana,nawaombeni tuliache kwa muda ili tuendelee na kikao chetu hili lisituharibie mipango yetu jamani"alisisitiza Bw.Ame

Pamoja na rai hiyo ya Katibu wa mkoa Bw.Ame Wajumbe waliendelea kutoka nje ya kikao hicho mmoja baada ya mwingine licha ya kuwa baadaye kililazimika kuahirishwa kutokana na kutokuwepo kwa Meya wa halmashauri ya manispaa ya Tabora Bw.Ghulam Dewij ambaye alikuwa kwenye ziara ya kichama jumuiya ya Wazazi mkoa wa Tabora.

Kufuatia kuendelea kuwepo kwa sakata hilo la wajumbe wa halmashauri kuu ya CCM wilaya ya Tabora mjini na baadhi ya wanachama wa chama hicho kumkataa Katibu wa wilaya ni wazi kwamba Chama cha Mapinduzi kimekwishaingia kwenye mgogoro ambao suluhisho la  msingi wake ni kuondolewa kwa Katibu huyo wa CCM wilaya ya Tabora Bw.Bakari Mfaume kama madai ya baadhi ya wanachama wa chama hicho wanavyoeleza.

''Sisi tunachojua Katibu huyu anatumiwa na viongozi wachache wenye pesa kwa maandalizi ya uchaguzi mkuu,mpaka viongozi hao wamefikia kuwa wanachangishana wanamlipa mshahara mwingine nje ya mshahara anaolipwa na CCM,sasa tunasema hatumtaki,atuachie chama chetu,kwanza amekwishafanya madudu kwenye Wilaya karibu zote za Tabora,anakiharibu chama jamani"    

Aidha kwa upande mwingine baadhi ya Wazee wa Tabora mjini ambao hawakutaka kutajwa majina yao wameeleza kuwa endapo viongozi hawatakuwa makini kuhusu madai ya wajumbe na wanaccm kwa ujumla,kuna wasiwasi mkubwa wa kupoteza viti vingi vya serikali ya mtaa na pengine hata nafasi za udiwani na ubunge pia.

Hata hivyo kabla ya kuanza kwa mkutano huo Katibu huyo wa CCM wilaya ya Tabora mjini Bw.Mfaume aliwafukuza waandishi wa habari nje ya ukumbi wa mkutano huo kwa madai kwamba yeye ndiye mwenye mamlaka ya kuwaita waandishi endapo kama watahitajika na kuwatishia kuwa anaweza akawalalamikia kwa kuharibu mkutano huo jambo lililoleta tafsiri mbaya kwa waandishi wa habari na watu walioshuhudia kitendo hicho.

"Sasa huyu Katibu anataka kuficha nini wakati hiyo taarifa itakayosomwa kwa wajumbe wa halmas 
hauri kuu inatakiwa wananchi wajue nini Serikali yao imefanya,au ana ajenda za siri?baadhi ya watu waliokuwa nje ya ukumbi huo walisikika wakihoji uhalali wa Katibu huyo Bw.Mfaume kuwafukuza waandishi wa habari eneo la mkutano huo.

VODACOM YAMKABIDHI WAZIRI CHIKAWE MAMILIONI YA WIKI YA NENDA KWA USALAMA BARABARANI

PIX 1.Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe (wapili kulia) akimshukuru Ofisa wa Mawasiliano na Uhusiano wa Kampuni ya Vodacom Tanzania, Georgia Mutagahywa (kushoto) baada ya kupokea hundi yenye thamani ya Sh. Milioni 40 msaada uliotolewa kwa ajili ya Wiki ya Nenda kwa Usalama Barabarani inayotarajiwa kufanyika mwishoni mwa mwezi Septemba mwaka huu, jijini Arusha. Wapili kushoto ni Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Ernest Mangu, na kulia ni Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani nchini, Naibu Kamishna, Mohamed Mpinga. Makabidhiano hayo yalifanyika katika Ukumbi wa Wizara hiyo, jijini Dar es Salaam leo.
PIX 2.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe (wapili kulia) akimshukuru Ofisa wa Mawasiliano na Uhusiano wa Kampuni ya Vodacom Tanzania, Georgia Mutagahywa (kushoto) baada ya kupokea hundi yenye thamani ya Sh. Milioni 40 msaada uliotolewa kwa ajili ya Wiki ya Nenda kwa Usalama Barabarani inayotarajiwa kufanyika mwishoni mwa mwezi Septemba mwaka huu, jijini Arusha. Wapili kushoto ni Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Ernest Mangu, na kulia ni Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani nchini, Naibu Kamishna, Mohamed Mpinga. Makabidhiano hayo yalifanyika katika Ukumbi wa Wizara hiyo, jijini Dar es Salaam leo.
PIX 3.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe (wapili kulia) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) baada ya kupokea hundi ya Sh. Milioni kwa ajili ya maandalizi ya Wiki ya Nenda kwa Usalama Barabarani, kutoka kwa Ofisa wa Mawasiliano na Uhusiano wa Kampuni ya Vodacom Tanzania, Georgia Mutagahywa (watatu kulia). 

Wiki ya Nenda kwa Usalama Barabarani inatarajiwa kufanyika mwishoni mwa mwezi Septemba mwaka huu, jijini Arusha. Kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Mbarak Abdulwakil. Wapili kushoto ni Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Ernest Mangu, na kushoto ni Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani nchini, Naibu Kamishna, Mohamed Mpinga. Makabidhiano hayo yalifanyika katika Ukumbi wa Wizara hiyo, jijini Dar es Salaam leo. Picha zote na Felix Mwagara wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
PICHA ZOTE NA KITENGO CHA MAWASILIANO YA SERIKALI WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI

BENKI YA CRDB YAZINDUA HUDUMA YA INDIA DESK

Balozi wa India, Shri Debnath Shaw (wa tatu kulia), Mkurugenzi
Mtendaji wa Benki ya CRD, Dk. Charles Kimei (wa pili kushoto), wakizindua kwa
pamoja huduma
mpya ya
India Desk
inayowaunganisha wawekezaji na wafanyabiashara nchini India kufanya
huduma za kibenki bila ya kuwa na akaunti nchini. Wa pili kulia ni Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo anayeshughulika na Uendeshaji na Huduma kwa Wateja, Saugata Bandyadhiyay, mjumbe wa bodi ya Wakurugenzi, Ally Laay (kushoto), Celina Mkonyi (kulia). Uzinduzi huo ulifanyika
jijini Dar es Salaam.

Balozi wa India, Shri Debnath Shaw (wa tatu kulia), Mkurugenzi
Mtendaji wa Benki ya CRD, Dk. Charles Kimei (wa pili kushoto), Wa pili kulia ni Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo anayeshughulika na Uendeshaji na Huduma kwa Wateja, Saugata Bandyadhiyay, mjumbe wa bodi ya Wakurugenzi, Ally Laay (kushoto), Celina Mkonyi (kulia).

Balozi wa India, Shri Debnath Shaw (wa tatu kulia), Mkurugenzi
Mtendaji wa Benki ya CRD, Dk. Charles Kimei (wa pili kushoto), Wa pili kulia ni Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo anayeshughulika na Uendeshaji na Huduma kwa Wateja, Saugata Bandyadhiyay wakiwa na furaha baada ya kuzindua huduma hiyo.

Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo anayeshughulika na Uendeshaji na Huduma kwa Wateja, Saugata Bandyadhiyay akizungumza wakati wa uzinduzi wa huduma India Desk inayotolewa na Benki ya CRDB.
Wadau wa Benki ya CRDB.
Wadau mbalimbali wa Benki ya CRDB.
 Mkurugenzi wa Masoko Utafiti na Huduma kwa Wateja wa Benki ya CRDB, Tully Mwambapa (katikati) akiwa na maofisa wa Benki hiyo wakati wa hafla ya uzinduzi wa huduma ya India Deski.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB Dk. Charles Kimei akizungumza wakati wa uzinduzi wa huduma ya India Deski uliofanyika jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wageni waalikwa wakiwa katika uzinduzi mpya ya India Desk inayotolewa na Benki ya CRDB.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei (kulia) na  Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo anayeshughulika na Uendeshaji na Huduma kwa Wateja, Saugata Bandyadhiyay (kushoto) wakisakata rhumba wakati wa hafla hiyo.
Burudani ya muziki kwa kwenda mbele

Friday, August 8, 2014

UNAAMBIWA HIVIII:::UKITAKA RAHA NA BURUDANI YA MUZIKI MZURI BASI IPO SKYLIGHT BAND PEKEE NDANI YA THAI VILLAGE

 Divas wa Skylight Band Aneth Kushaba (wa kwanza kushoto) na Digna Mpera(wa pili toka kushoto) wakilianzisha Burudani kwa nguvu zoteee ndani ya Thai Village masaki.Kila ijumaa Bendi yako mahiri na isiyoshikika Skylight Banda wanakuwa Thai Village wakikupa burudani ya nguvuuuu na suprizeee kibaooooo,Usikose Ijumaa Hii.
 Divas wa Skylight Band Aneth Kushaba (wa kwanza kushoto) na Digna Mpera(wa pili toka kushoto) wakiimba kwa umakini kabisa ili kuwapa ile kitu roho inapenda mashabiki wao
 Digna Mpers akipiga Vocal Kaliii kabisa na kwa madaha ili kuwapa burudani mashabiki na wapenzi wa Skylight Band ndani ya Thai Village Ijumaa iliyopita
 Anaitwa Mkali wa Sauti Mary Lukos akiimba Vizuri kabisa ili kuwapa burudani mashabiki wake ndani ya Thai Village
 Tamu ya warembo Sam Mapenzi akizitiririsha Sauti kaliiii na zenye utamu kwa wapenzi na mashabiki wa Skylight Band
 Le Meneja Her Self Aneth Kushaba akiwa na furahaa sana kuona mashabiki wao wanapata kile wanachokiitaji kutoka kwao na si kingine ni burudani iliyokwenda shule.
 Babaa ya Kongo Sony Masamba Akizipiga zile za kikongo kwa umakini kabisaaaaa ndani ya Thai Village ili kuwapa raha mashabiki wa Skylight Band
 Uniongozeeeee bila neema zako siwezi kwendaaaaaa,kwa mkono wako kweliiiiiiii umenibarikiiiiii Le Meneja Her Self Aneth Kushaba akiimba kwa Hisiaaaa kali
 Baraka zakooo ziweee na Mimiiiiii kwa mkono wakooo kweliii umenibarikiiiiiiiii Le Meneja Her Self Aneth Kushaba(katikati)akiimba kwa upoleeee kabisaaa kumshukuru Mungu kwa kila jambo
 Hashimu Donode Akizipigaaa Sauti kali na zenye mpangilio ndani ya Thai Village 
 Aneth Kushaba(wa kwanza kushoto)akiwa na Digna Mpera(wa pili toka kushoto) wakiimba kwa kupokezana kwa rahaaaa zaooo,yote ikiwa ni kuwapa burudani mashabiki wao
 Le Meneja Akiwa na Furahaaa ya kutoshaaaaa kupona mashabiki wanapata burudani nzuriii,kwa mbaliiiii Mpiga solo Allen Kisoo akichungulia
 Ukafika wakati ambao Ulikukwa unasubiliwa ni Kumpongeza Mrembo Digna Mpera kwa kutimiza miaka kadhaa ya kuzaliwa kwake,Aneth Kushaba akimwelezea kidogo Kijana wake

 Wowww wowwww Ilove you allllllll ni Digna Mpera akifurahia kuona shangwe za kumtakia heri ya siku yake ya kuzaliwa 
 Ohhhhhh My God!!!!!!! Ni mshangao kwa Digna Mpera baada ya kuona zawadi za keki zikimiminika kwake
 Digna Mpera(katikati) akifurahia zawadi ya keki alizopewaa
 Operation Manager wa MoBlog Zainul Mzige Akilishwa keki na Digna Mperaa
                                   Digna Mpera akimlisha keki Mpiga Bass wa Skylight Band.......
                                                 Digna Akimlisha keki Hashimu Donodeee
 Hahahaha Donode na Imma Wakipongezana kwa raha zaoo baaada ya kushiba keki Vijana hatari hawaaaa acha kabisaaa
 Donode wa kwanza kushoto akimuonesha Meneja wake Aneth kushaba ni kwa jinsi gani alivyo mzuri kwa kuyarudi mastep huku meneja akicopy kwa mbaliiiii...
 Aneth kushaba akamwambia weweeee dogo sana Donode subili nikuonyeshe wewe utakaaa mwenyewe kimyaaaaa
 Umeonaa Donodeee umeonaaa ubishi unakuponza sasa,mama yangu Ona viuono vya Aneth Kushaba hatariiii
 Mpaka chiniiii chini kabisaaaa,Donode kimyaaaa Akishangaaa tui,usimchezeee Meneja wewe kwa kuyarudi
 Wapenzi na mashabiki wa Skylight band wakicheza muziki mzuri kwa rahaaa zao
                               Nyomiiii la kutoshaaaaa Usikose Leo upate raha na Skylight Band
 Hapo sasa ukafika wakati wa mduara hapo ni mwanaume kazi na mwanamke nyongaaaaa
 Si umeona viuno Hivyooooo Usikose leo Thai Village upate burudani ya kufa mtu
 Kweli Skylight Kuna Mengi Oparation Manager wa MoBlog Zainul Mzige akapata na Bahati ya kukutana na Classmate wake wa kitambooooooo,
                              Divasss wa kutoshaaa wanakuwepo kupata burudani na Rahaaaa
                               Zainul Mzige Akipata Ukodak na Mkali wa Vocal Mary Lukos
Mpiga solo mahiri wa Skylight band Allen Kiso akipata Ukodak wa nguvu na kukuambia,Usikoseeeeee Leo ndani ya Thai Village nitazikata nyuzi za gitaaaa kwa uppigaji wa hali ya Juuu