Pages

KAPIPI TV

Saturday, July 26, 2014

JANUARY MAKAMBA AONGOZA MKUTANO WA WANAMUZIKI WA MUZIKI WA INJILI NA WASAMBAZAJI ULIOFANYIKA LEO HOTELI YA WANYAMA SINZA JIJINI DAR ES SALAAM

Rais wa Shirikisho la Muziki wa Injili Tanzania (TAF), Ado Novemba
Naibu Waziri wa Mawasiliano Sayansi na Teknolojia, Mhe. January Makamba (kulia), akizungumza na wadau wa Muziki wa Injili Tanaznia Hoteli ya Wanyama Sinza Dar es Salaam leo.
Rais wa Shirikisho la Muziki wa Injili Tanzania (TAF), Ado Novemba (kushoto), akizungumza na wadau wa Muziki wa Injili Tanaznia Hoteli ya Wanyama Sinza Dar es Salaam leo kabla ya kumakribisha mgeni rasmi wa mkutanmo huo, Mhe. January Makamba.
Naibu Waziri wa Mawasiliano Sayansi na Teknolojia, Mhe. January Makamba, akisalimiana na Mzee Makassy.
Mwimbaji, Adelita Mshumba akitoa burudani katika mkutano huo.
Wanamuziki wa nyimbo za Injili wakiwa kwenye mkutano huo. Kutoka kulia ni Enock Jonas, Dyna Sakatebela na Joyce Ombeni.
Viongozi mbalimbali na wadau wa muziki wa Injili wakiwa wamejipanga foleni wakati wakisubiri kumpokea mgeni rasmi wa mkutano huo, Mhe.January Makamba.
Mwanahabari wa Kituo cha TV 1, Gervas Mwaitebela naye alikuwepo kupata taarifa za mkutano huo.
Naibu Waziri wa Mawasiliano Sayansi na Teknolojia, Mhe. January Makamba, akisalimiana na Ofisa Mtendaji Mkuu wa COSOTA, Doreen Sinare.
Naibu Waziri wa Mawasiliano Sayansi na Teknolojia, Mhe. January Makamba, akisalimiana na Mwenyekiti wa Mtandao wa Wanamuziki Tanzania (TAMUNET), John Kitime.
Rais wa Shirikisho la Muziki wa Injili Tanzania (TAF), Ado Novemba (kushoto), akimuongoza mgeni rasmi Mhe. January Makamba kuingia ukumbini.
Viongozi mbalimbali wakiwa kwenye mkutano huo.
Wadau wa muziki wa Injili wakiwa kwenye mkutano huo.
Katibu wa Shirikisho la Muziki wa Injili John Shaban akiendesha mkutano.
Wadau wa eneo la usambazaji wa kazi za wanamuziki wakiwa kwenye mkutano huo.
Wadau wa muziki wa Injili wakiwa kwenye mkutano huo.
Mwenyekiti wa Mtandao wa Wanamuziki Tanzania (TAMUNET), John Kitime, akizungumza na wadau hao katika mkutano huo
Ofisa Mtendaji Mkuu wa COSOTA, Doreen Sinare (kulia), akitoa ufafanuzi wa masuala mbalimba kwa wadau wa muziki wa Injili. Wa pli kulia ni Muimbaji wa nyimbo za Injili, Christina Shusho.
Balozi mstaafu, Profesa Coster Mahalu akizungumza na wadau wa muziki wa nyimbo za Injili. Kushoto kwake ni Mkurugenzi wa Kinondoni Revival Choir, Dk. Jotham Mackenzie
Wadau wa muziki wakiwa kwenye mkutano huo wakifuatiliamambo mbalimbali.
Wadau wa muziki wakiwa kwenye mkutano huo. Imeandaliwa na www.habari za jamii.com-simu namba 0712-727062)

KUTAYBA SACCOSS YATOA MSAADA WA CHAKULA KWA WATOTO YATIMA KWA AJILI YA SIKUKUU YA EID-FITR-TABORA

Mratibu wa asasi ya Kutayba Saccoss Bw.Ramadhani Mdula akikabidhi msaada wa chakula kwa mmoja kinamama ambao ni waangalizi wa Kituo cha Kulea Watoto Yatima cha Igambiro kilichopo nje kidogo ya manispaa ya Tabora.
Baadhi ya watoto wakiangalia zawadi ya Chakula walichopatiwa
Wapo baadhi ya watoto yatima ambao ni wakubwa wamekuwa wakiishi kwenye Kituo hicho na kusaidia kuwabeba wenzao ambao ni wadogo zaidi hii inaonesha wazi watoto hawa wamekuwa wakipendana.







KAMPUNI YA TTCL YATOA ZAWADI YA EID EL FITR KWA WATOTO YATIMA DAR


Wawakilishi wa Kituo cha Watoto Yatima cha Mama Theresa kilichopo Mburahati, wakipokea msaada wao toka kwa Meneja wa TTCL, Dar es Salaam Kati, Jane Mwakalebela kwa niaba ya Ofisa Mtendaji Mkuu wa TTCL.
Wawakilishi wa Kituo cha Watoto Yatima cha Mama Theresa kilichopo Mburahati, wakipokea msaada wao toka kwa Meneja wa TTCL, Dar es Salaam Kati, Jane Mwakalebela kwa niaba ya Ofisa Mtendaji Mkuu wa TTCL.
Vikundi vya Watoto Yatima vya Mama Theresa kilichopo Mburahati, Kituo cha Mwandaliwa cha Mbweni na Kituo cha Chakuwama cha Sinza katika picha ya pamoja mara baada ya kupokea zawadi zao jijini Dar es Salaam.
Vikundi vya Watoto Yatima vya Mama Theresa kilichopo Mburahati, Kituo cha Mwandaliwa cha Mbweni na Kituo cha Chakuwama cha Sinza katika picha ya pamoja mara baada ya kupokea zawadi zao jijini Dar es Salaam.
Wawakilishi wa Kituo cha Watoto Yatima cha Mwandaliwa cha Mbweni wakipokea msaada wao toka kwa Meneja wa TTCL, Dar es Salaam Kati, Jane Mwakalebela kwa niaba ya Ofisa Mtendaji Mkuu wa TTCL.
Wawakilishi wa Kituo cha Watoto Yatima cha Mwandaliwa cha Mbweni wakipokea msaada wao toka kwa Meneja wa TTCL, Dar es Salaam Kati, Jane Mwakalebela kwa niaba ya Ofisa Mtendaji Mkuu wa TTCL.


KAMPUNI ya Simu Tanzania (TTCL) imetoa msaa wa vyakula kwa vituo vitatu vya kulelea watoto yatima na wanaoishi katika mazingira magumu vya jijini Dar es Salaam ikiwa ni kuvisaidia viweze kusherehekea vizuri siku kuu ya Eid El Fitr.

Msaada huo wenye jumla ya thamani ya shilingi milioni 3 umekabidhiwa na Meneja wa TTCL, Dar es Salaam Kati, Jane Mwakalebela kwa niaba ya Ofisa Mtendaji Mkuu wa TTCL, ambaye alisema utaratibu huo ni wakawaida kwa kampuni yao kusaidia makundi na taasisi na idara anuai kwa masuala ya kijamii.

Bi. Mwakalebela alivitaja vituo ambavyo vimekabidhiwa msaada huo ni pamoja na Kituo cha Watoto Yatima cha Mama Theresa kilichopo Mburahati, Kituo cha Mwandaliwa cha Mbweni na Kituo cha Chakuwama cha Sinza vyote vya jijini Dar es Salaam.

“…Msaada huu ni maalum kwa ajili ya kusherehekea siku kuu ya Eid El Fitr, jambo hili la leo ni utaratibu wa kampuni ya TTCL kusaidia makundi, taasisi na idara mbalimbali kuhusu mambo yanayohusu maendeleo na ustawi wa jamii,” alisema Bi. Mwakalebela kwa niaba ya Ofisa Mtendaji Mkuu wa TTCL, Dk. Kamugisha Kazaura.

Msaada uliotolewa kwa vituo hivyo ni pamoja na mchele, mafuta ya kupikia, sukari, unga, unga wa sembe, maharage pamoja na katoni za juisi za maboksi.

Kwa upande wao wawakilishi wa vituo hivyo waliishukuru Kampuni ya TTCL kwa uamuzi wake wa kuwakumbuka watoto yatima ili nao waweze kusherehekea vizuri siku kuu ya Eid El Fitr kama ilivyo kwa familia nyingine majumbani.
*Imeandaliwa na www.thehabari.com

MBUNGE WA CHALINZE AWEKA JIWE LA MSINGI LA NYUMBA ZA WALIMU,AKAGUA UJENZI WA ZAHANATI LUGOBA


h1
 Mbunge wa Chalinze Mheshimiwa Ridhiwani Kikwete akielekea kuweka jiwe la msingi katika nyumba ya walimu iliyojengwa kutokana na michango ya wadau mbalimbali ikiwamo ofisi ya Mbunge wa Chalinze
h3
 Jengo jipya la Zahanati linaloendelea kujengwa katika kijiji cha Kinzagu, kata ya Lugoba Jimbo la Chalinze linaloongozwa na Mheshimiwa Ridhiwani Kikwete.
h6
 Mbunge wa Chalinze Mheshimiwa Ridhiwani Kikwete akisalimiana na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Bagamoyo ndugu Samuel Saliyanga wakati wa ukaguzi wa ujenzi wa Zahanati ya Kijiji cha Kinzagu, kata ya Lugoba 
h4
Mbunge wa Chalinze Mheshimiwa Ridhiwani Kikwete akiweka jiwe la msingi katika nyumba ya walimu iliyojengwa kwa na michango ya wadau mbalimbali ikiwamo ofisi ya Mbunge wa Chalinze

KIPINDI CHA “MIMI NA TANZANIA” CHAVUKA MIPAKA YA TANZANIA, SAFARI NI NDANI YA JIJI LA WASHINGTON DC

IMG-20140725-WA0004
IMG-20140725-WA0006
Mtangazaji wa Kipindi cha Mimi na Tanzania Hoyce Temu akitia saini kitabu cha wageni kwenye Ubalozi wetu wa Tanzania nchini Marekani.
IMG-20140725-WA0005
Hapa akiwa mapokezi ya Ubalozi wetu wa Tanzania nchini Marekani huku akisema …Naipenda Tanzania yangu!
IMG-20140725-WA0003
Hoyce Temu akiangalia baadhi ya picha za Mabalozi 15 ambao tayari wameshaongoza Ubalozi wetu wa Tanzania nchini Marekani. wakiwemo Rais Mstaafu Benjamin William Mkapa, Mustafa Nyang’anyi na Balozi Ombeni Sefue pamoja Wanawake wawili ambao ni Mama Balozi Mwanaidi Maajar na Balozi wa sasa Mh. Liberata MulaMula.
IMG-20140725-WA0007
Mheshimiwa Balozi Liberata MulaMula ndani ya mahojiano na mtangazaji wa kipindi cha Mimi Na Tanzania Hoyce Temu ofisini kwake jijini Washington DC, Marekani!
Mahojiano hayo ya moja kwa moja katika Balozi ya Tanzania nchini Marekani na Mheshimiwa Balozi Liberata Mulamula ambapo wameangazia masuala mbalimbali yakiwemo Utalii, kujitangaza katika miradi ya kimaendeleo na uwekezaji ,malalamiko ya watanzania waishio Marekani kuhusu uraia, kwa mengineyo mengi usikose kuangalia Channel Ten wiki ijayo Jumapili saa moja na nusu usiku kilicho bora kabisa.
IMG-20140725-WA0009
Na wale waliokuja kuomba Visa wakapiga picha na aliyewahi kuwa mrembo wa Tanzania na muongozaji wa kipindi cha Mimi na Tanzania Hoyce Temu.
IMG-20140725-WA0008
Hoyce Temu akipata picha ya ukumbusho na mpiga picha Iska JoJo aliyerekodi kipindi hicho.
Hoyce Temu anatoa shukrani za pekee kwa Blogger Mzee wa VIJIMAMBO DJ Luke Joe kufanikisha mahojiano ya Hoyce Temu na Balozi Liberata Mulamula.

Friday, July 25, 2014

MKUTANO KATI YA WAJUMBE WA BUNGE MAALUM NA WANAMTANDAO WA WANAWAKE NA KATIBA NA TAMWA

 Doreen E. Maro kutoka TAMPRODA ambaye pia ni Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba akiwakilisha Wafugaji Akileta Mrejesho wa walichokuwa wakikijadili katika Kundi lao juu ya mapendekezo ya kuimarisha Masuala muhimu ya Rasimu ya Pili ya Katiba Mpya
 Dkt. Macca A. Mbalwa  Mkurugenzi wa Giyedo Tanzania akiwa anatoa Mrejesho wa kile ambacho walikuwa wamekijadili na kutoa mapendekezo yao ya Kuboresha masuala muhimu katika Rasimu ya pili ya Katiba Mpya.
 Salama Aboud Talib Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba  na Naibu Katibu Mkuu wa UWT akizungumzia makosa mbalimbali ambayo yapo katika Rasimu ya Pili ya Katiba mpya na kutoa mapendekezo kuwa Iboreshwe ili kuweka usawa.
 Executive Director wa  Women Fund Tanzania Mary Rusimbi akizungumza juu ya Majumuisho ya pomoja na Kupanga mikakati ambayo yatasaidia Kuimarisha Masuala Muhimu ya Rasimu ya Pili ya Katiba Mpya
 Mgeni Hassan Juma Mwenyekiti wa Wawakilishi  Wanawake Zanzibar akitoa neno la Shukurani kwa wote waliohudhuria kwa muda wa siku mbili katika mkutano wa Wajumbe wa Bunge Maalum la  Katiba, Mtandao wa wanawake na TAMWA
 Profesa Ruth Meena  Akitoa Majumuisho pia kutoa Shukurani kwa wale wote waliohudhuria katika Mkutano huo uliochukua siku mbili.
 Valerie Msoka akifunga Rasmi Mkutano huo.
 Fredrick Msigala Mjumbe Bunge Maalum la Katiba ambaye ni Mlemavu wa Miguu akielezea masikitiko yake ya Jinsi watu wenye ulemavu wakiwemo wanawake na wanaume ambavyo wametengwa na kukosa haki zao, amesisitiza Serikali katika Rasimu Mpya ya Pili ya Katiba wawaangalie walemavu kwa umakini na ukaribu maana wanahaki sawa na watu wengine. Pia amesisitiza walemavu wajaliwe katika huduma za Afya mana ni Muhimu kwao. Mwisho amesisitiza kuwa wanawake wenye ulemavu wanahaki ya Kuolewa na kuto nyanyaswa pindi wanapokuwa katika ndoa zao.
 Modesta Mpereme ambaye ni Kiziwi hasikii lakini anaongea vizuri pia ni Mwenyekiti kutoka  Sauti ya Wanawake  wenye Ulemavu Tanzania, Ameiomba serikali iwe na vitendea kazi vya kutosha ambavyo vitawasaidia walemavu katika secta mbalimbali Mfano katika Mabenki kuwe na vifaa maalum vya kuwasaidia walemavu, Katika Upande wa Afya amesisitiza kuwe na hata watu wanaoweza kutoa msaada wa kutafsiri mambo mbalimbali mfano kwa Viziwi, wasio ona na ambao Hawawezi kuongea.
 Siti Ally Mwanasheria na Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba kutoka Zanzibar akisisitiza umuhimu wa usawa kati ya haki za wanawake na wanaume katika jamii , Pia alisisitiza juu ya mabinti wanaopata Mimba za utotoni wakiwa mashuleni na kusisitiza kuwa wanaruhusiwa kusimama masomo mpaka kipindi mtoto atakapokuwa mkubwa anaruhusiwa kuendelea na masomo,  Mwanaume aliyesababisha Mimba anaweza akashtakiwa .
 Baadhi ya Wajumbe wa Bunge Maalum la katiba pamoja na Wadau mbalimbali waliofika katika Mkutano huo.