Pages

KAPIPI TV

Wednesday, July 23, 2014

BENKI YA EXIM TANZANIA YAANDAA FUTARI KWA WATEJA WAKE WA MKOANI TANGA


PIX 1
Baadhi ya wateja wa Benki ya Exim Tanzania na wafanyakazi wakifuatilia yaliyokuwa yakizungumzwa wakati wa futari iliyoandaliwa na benki hiyo mkoani Tanga kwa ajili ya wateja wake. Picha na mpiga picha wetu.
PIX 2
Meya wa Jiji la Tanga, Mhe. Omary Uledi, ambaye pia ni mgeni rasmi (wapili kulia)  akizungumza wakati wa futari iliyoandaliwa na Benki ya Exim Tanzania kwa wateja wake wa mkoani Tanga hivi karibuni. Wa pili kushoto ni Meneja wa Benki ya Exim Tawi la Tanga, Deogratius Makwaia, Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Suleiman Lighuchu (watatu kushoto)na Katibu wa Bakwata wa Mkoa, Bw. Mohamed Riami (wa kwanza kulia). Picha na mpiga picha wetu.
PIX 3
Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Suleiman Lighuchu akizungumza wakati wa futari iliyoandaliwa na Benki ya Exim Tanzania kwa wateja wake wa mkoani Tanga hivi karibuni. Wa pili kushoto ni Meneja wa Benki ya Exim Tawi la Tanga, Deogratius Makwaia, Mgeni Rasmi Meya wa Jiji la Tanga, Mhe. Omary Uledi (Wa pili kulia)na Katibu wa Bakwata wa Mkoa, Bw. Mohamed Riami (wa kwanza kulia). Picha na mpiga picha wetu.
PIX 4
Baadhi ya wateja wa Benki ya Exim Tanzania na wafanyakazi wakichukua vyakula mbali mbali vilivyoandaliwa malum kwa ajili ya futari iliyoandaliwa na benki hiyo mkoani Tanga kwa ajili ya wateja wake. Picha na mpiga picha wetu.

MEYA WA ILALA JERRY SILAA AKAGUA MAENDELEO YA UJENZI WA BARABARA YA UKONGA KUELEKEA MAZIZINI MPAKA MOSHI BAR


Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya
Ilala Jerry Silaa Jana amefanya ziara fundi ya ukaguzi wa ujenzi wa barabara ya ukonga Moshibar
kilometa 3 kiwango cha changalawe awamu yakwanza. Ikiwa ni utekelezaji wa miradi ya
dharura kulingana na uharibifu wa miundo mbinuulitokea baada ya Mvua kubwa. Mradi huo
ambao unaghalimu kiasi cha shilingi millioni 90.Pesa za Ujenzi huohizo zinatoka Halmashauri ya Manispaa ya Ilala.Pia Barabara hiyo itawekwa Lami kwa awamu ya pili ndani ya mwaka huu kwa kilomita tatu.Picha Zote Na Dj Sek Blog

Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala Jerry Silaa wa Kwanza kushoto akiwa na Mhandisi wa Barabara(mwenye shati Jeusi) pamoja na Diwani wa ukonga Elizabeth Mbano(katikati) na wa kwanza Kulia ni Mhandisi wa Manispaa Bwana Muhinda Kassimu wakitazama maendeleo ya ujenzi wa kipande cha barabara kutoka ukonga-mazizini mpaka moshi bar.
Mhandisi wa Manispaa Bwana Muhinda Kassimu Akielezea namna ambavyo awamu ya kwanza ya ukarabati wa barabara hiyo utakavyo kuwa  kwa kiwango cha changarawe na itafuata awamu ya pili ambayo ni Lami.
Diwani wa ukonga Elizabeth Mbano akiongea na vyombo vya habari kushukuru Manispaa kwa kuikumbuka barabara hiyo kwani imekuwa ikileta sana shida ya usafiri kwa wakazi wa eneo hilo hasa kipindi cha mvua.
Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala Jerry Silaa Akielezea namna Barabara hiyo itakavyotengenezwa na pia akasisitiza kwamba Pesa za Ujenzi wa Barabara Hiyo zimetoka ndani ya manispaa na si Vinginevyo.
Greda likirekebisha Barabara ya Ukonga-mazizini kulekea moshi bar
Mwonekano wa Bara barabara hiyo
Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala Jerry Silaa akimwelezea mkazi wa mazizini namna mradi wa barabara hiyo ulivyo.
Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala Jerry Silaa akimuelezea kwa kumuonyesha mkazi wa mazizini gharama za mradi huo na pia pesa za mradi huo kutoka ndani ya Halmashauri na si vinginevyo.
Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala Jerry Silaa akiwa amempa nafasi mkazi wa Mazizini kupitia majalada yenye maelezo na mikataba ya ujenzi wa barabara hiyo
Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala Jerry Silaa akiongea na wakazi wa mazizini waliotaka kujua mradi utachukua mda gani na utaisha lini.

Tuesday, July 22, 2014

POLISI KANDA MAALUM YA DAR INAWASHIKILIA WATU WANANE KWA KUTUPA VIUNGO VYA BINADAMU HUKO BUNJU.

3
Halima Mdee's photo. 
Na Rose Masaka-MAELEZO_DAR ESALAAM
JESHI la Polisi Kanda ya Dar es Salaam linawashikilia  na kuwahoji watu wanane kwa kutupa  viungo vya binadamu katika bonde la Mbweni Mpiji eneo la Bunju wilayani Kinondoni .
Kamishna wa Polisi  Kanda Maalum ya Dar es Salaan  Suleiman Kova amesema hayo leo Ofisi kwake wakati wa mkutano na waandishi wa habari .
Amesema kuwa watu hao wakimemo madaktari wa International Medical and Technological University (IMTU) wanashikiliwa na Jeshi la Polisi baada ya kukiri kuhusika na tukio la utupaji wa  viungo  vya binadamu katika eneo hilo.
 Kamishna Kova amesema kuwa Jeshi la Polisi linaendelea kuwahoji na kufanya uchunguzi kuona kama wahusika wamefanya kosa  linalohitaji kuchukuliwa hatua za kisheria au hawana kosa.
Ameongeza kuwa kufuatia tukio hilo tayari Jeshi la Polisi Kanda Maalum limeshafungua jarada la uchunguzi kubaini ikiwa wahusika wametenda kosa linalohitaji kufikishwa kwenye vyombo vya sharia kwa hatua zaidi.
Kamishna huyo amesema kuwa katika kutekeleza jambo hilo tayari jopo la wachunguzi likiongozwa na Mkuu wa Upelelezi Kanda Maalum ya Dar es Salaam  Jaffar Mohamed linaendelea na uchunguzi ili kubaini chanzo cha watu hao kutupa viungo hivyo katika eneo hilo na idadi ya watu kulingana na viungo vilivyotupwa
.
Aidha Kamishna Kova amewasihi wananchi wasiwe na wasiwasi kwani viungo vilivyookotwa  havina uhusiano na mauaji ya watu wengi na wala havihusiki na masuala ya ushirikina.
Amewaahidi wananchi kutoa taarifa kamili mara tu upepelezi utakapokamilika.
Viungo vya binadamu vikiwemo mikono, miguu, vichwa , mapafu na mioyo viligundulika jana (21.7.2014) jioni vikiwa vimehifadhiwa katika mifuko ya plastiki 85 na kutupa katika bonde la Mbweni Mpiji eneo la Bunju wilayani Kinondoni.
Mara baada ya kugunduliwa Jeshi la Polisi Mkoa wa Kipolisi wa Kinondoni walivichukua na kuvipeleka katika Hospitali ya Taifa kwa uchunguzi zaidi.

WAZIRI WA BIASHARA VIWANDA, NA MASOKO ZANZIBAR NASSOR AHMED MAZROUR AZUNGUMZA NA WANAHABARIMPYA YA BIASHARA NAMBA 14 YA MWAKA 2013.

02
05
Baadhi ya wandishi wa Habari waliofika katka sherehe ya uzinduzi wa mpango wa elimu kwa wananchi kuhusu kuanzishwa kwa sheria ya Biashara Zanzibar No. 14 ya mwaka 2013 wakifuatilia maelezo ya Waziri Mazrui (hayupo pichani) Sherehe hiyo iliofanyika Hoteli ya Grand Palace Malindi Mjini Zanzibar .
04
Waziri wa Biashara, Viwanda na Masoko Mhe. Nassor Ahmed Mazrui akijibu maswali ya wandishi wa Habari (hawapo pichani), kulia Naibu Waziri wake  Thuwaiba Edington Kisasi na (kushoto) Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Julian Raphael.
03
Mwandishi wa Habari Abdallah Pandu wa Star tv akiuliza swali juu ya uanzishwaji wa sheria hiyo.
01
Katibu Mkuu Wizara ya Biashara, Viwanda na Masoko Zanzibar Julian Raphael akimkaribisha Waziri Mazrui (hayupo pichani) azungumze na wandishi wa Habari katika sherehe ya uzinduzi wa mpango wa elimu kwa wananchi kuhusu kuanzishwa kwa Sheria ya Biashara Zanzibar No. 14 ya mwaka 2013 katika Hoteli ya Grand Palace Malindi Mjini Zanzibar.

JESHI LA POLISI LAWASHIKILIA 25 KWA UCHUNGUZI TUKIO LA MLIPUKO WA MABOMU


mngulujuly152014
Kufuatia tukio la mlipuko wa bomu siku ya tarehe 7/7/2014 majira ya saa 22.15 usiku katika mgahawa wa VAMA, eneo la Uzunguni Jijini Arusha, ambapo watu wanane walijeruhiwa, Jeshi la Polisi limewakamata watuhumiwa 25 kwa uchunguzi. Kufuatia uchunguzi huo kati yao watu sita watafikishwa mahakamani mapema iwezakanavyo.
Watuhumiwa watakaofikishwa Mahakamani kwa tukio hilo ni:
 
1. SHAABAN MUSSA MMASA @ JAMAL, Umri miaka 26 Kabila, Msambaa. Mlinzi aliyekuwa zamu siku hiyo kwenye mgahawa huo.
 
2. ATHUMAN HUSSEIN MMASA, Umri miaka 38 kabila Msambaa, Mlinzi katika Mgahawa wa Chinese uliopo eneo la GYMKHANA jirani na eneo la tukio.
 
3. MOHAMED NURU @ MUHAKA, Umri miaka 30 Kabila Msambaa, Mlinzi katika mgahawa wa Chinese jirani na eneo la tukio.
 
4. JAFFAR HASHIM LEMA, Umri miaka 38 Mchaga Mwalimu wa Shule ya Msingi Olturmet Wilaya ya Arumeru. Pia alikuwa Imam wa Msikiti wa QUBA mjini Arusha. Huyu ametambuliwa kama mmoja wa viongozi walioratibu matukio ya milipuko ya mabomu maeneo mbalimbali nchini.
 
5. ABDUL MOHAMED HUMUD SALIM,@Wagoba; umri wa miaka 31, Mmanyema wa Ujiji Kigoma, wakala wa Mabasi Stendi Arusha.
 
6. SAIDI MICHAEL TEMBA; umri wa miaka 42, Mchaga, mfanyabiashara wa Arusha.
Aidha tarehe 21/07/2014 majira ya saa 20.00 usiku maeneo ya Sombetini walikamatwa YUSUFU HUSSEIN ALLY @ HUTA, kabila Mrangi, umri wa miaka 30 na mkewe SUMAIYA JUMA , kabila mwasi umri wa miaka 19 wakiwa nyumbani kwao baada ya kupekuliwa walikutwa na mabomu ya kutupwa kwa mkono saba, risasi sita za shortgun, mapanga mawili, unga wa baruti unaokadiriwa kufika nusu kilo na bisibisi moja. 

Mtuhumiwa YUSUFU HUSSEIN ni miongini mwa watuhumiwa waliokuwa wanatafutwa kwa ulipuaji wa mabomu maeneo yote jijini Arusha. Mahojiano yanaendelea dhidi yake.
 
Uchunguzi wa shauri hili pamoja na matukio mengine ya milipuko unaendelea, ikiwa ni pamoja na kuwahoji watuhumiwa walioko mikononi mwa Polisi na kuwakamata watakao bainika kuhusika na matukio hayo, mtajulishwa matokeo ya uchunguzi huo mara utakapokamilika.
 
Hata hivyo Jeshi la Polisi linatangaza kumtafuta YAHAYA HASSAN HELLA, kabila mrangi, umri wa miaka 33, mkazi wa Mianzini Arusha, mwenye asili ya eneo la Chemchemu Kondoa Dodoma kwa tuhuma za kuhusika na matukio ya ulipuaji mabomu nchini. Zawadi nono itatolewa kwa yeyote atakaye toa taarifa zitakazowezesha ukamatwaji wa mhalifu huyu. Jeshi la Polisi linawashukuru wananchi kwa ushirikiano mkubwa wanaoutoa. Asanteni.
…………………………….. ISAYA MNGULU-CP MKURUGENZI WA UPELELEZI WA MAKOSA YA JINAI TANZANIA

PINDA AZINDUA CHUO CHA VETA NA KUKABIDHIWA NYUMBA YA WALIMU SAME

PG4A5283
PG4A5427
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiweka jiwe la Msingi la  Chuo cha Ufundi ( VTC)   cha Maore wilayani Same Julai 21, 2014. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
PG4A5458
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akikata utepe katika uzinduzi wa   Chuo cha Ufundi ( VTC)   cha Maore wilayani Same Julai 21, 2014. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
PG4A5682
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda  akizungumza na Jaji  Mstaafu, Amir Manento baada ya kukabidhiwa  nyumba iliyojengwa  na Jaji huyo kama mchango wake kwa Wananchi wa kijiji alichozaliwa cha Mtii.  Nyumba hiyo ilitolewa kwa  Halmashauri ya Wilaya ya Same ili ilitumike kama makazi ya Walimu. Julai 20, 2014. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
PG4A5714
 Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akisalimiana na watoto wa kijiji cha Mtii wilayani Same baada  ya kukabidhiwa nyimba ya walimu iliyojengwa katika kijiji hicho na Jaji Mstaafu Amir Manento, Julai 20, 2014. (Picha na Ofisi ya  Waziri Mkuu)
PG4A5782
Mke wa Waziri Mkuu, Mama Tunu Pinda  (kushoto) akipokea zawadi ya miwa kutoka kwa mkazi wa kijiji cha Mtii wilayani Same (jina Halikupatikana)
PG4A5395 1
Mke wa Waziri uu Mama Tunu Pinda akipanda mti chuoni hapo.

NHIF KIGOMA YAWAFUNDA WANDISHI WA HABARI

Na Magreth Magosso,Kigoma


CHAMA cha wandishi wa habari Mkoa wa Kigoma,wametakiwa watumie chama chao  kujiunga na mfuko wa Afya (Nhif)  kwa  lengo  la  kupunguza  changamoto ya kipato inayochangiwa na kutokuwa na mikataba ya ajira husika.


Hayo yalisema  na Meneja wa mfuko huo mkoani hapa Elias Odhiambo alipokuwa akizungumza na wanachama hao  kigoma Ujiji ,katika ofisi za  KGPC kwa tija ya kutaka watumie fursa ya huduma ya vikundi ili kunufaika na mafao ya matibabu yatolewayo na mfuko huo.


“ changamoto kubwa ni uhakika wa kipato,ambapo kupitia huduma mpya ya vikundi rasmi vya uzalishaji mali ni nafuu kwenu, kujiunga na bima ya afya na kila mwanachama atachangia sh.76,800 tu kwa mwaka” alibainisha Odhiambo.


Alianisha huduma ya vikundi ni chachu kwa kila mtanzania kuwa na uwezo wa kuchangia kiasi hicho kwa mwaka na endapo atahitaji kuongeza hitaji la mtegemezi anapaswa amchangie kiasi hichohicho,kwa dhati ya kuondoka na adha ya kulipa  matibabu ya papo kwa papo.

Alisema wananchi wote waliopo katika vikundi vidogo na vikubwa ambavyo vipo kihalali ni wakati wao kutumia fursa hiyo. ambayo inakidhi hali halisi ya maisha ya mtanzania na kusisitiza wananchi wathubutu hilo kwa faida ya leo na siku za usoni.


Mwenyekiti wa Kgpc Deogratius Nsokolo aliunga mkono huduma hiyo ,ambayo ni fursa kwa wanachama wake,ambao asilimia 99 hawana mikataba ya ajira ,hali inayochangia washindwe kwenda kupima afya zao kwa wakati .


Alisema  wataweka  utaratibu,kanuni na sheria  kwa kuhakiki  kila mchango wa  mwandishi kuingia katika mfuko huo kwa  wakati, ili kuwajengea uwezo wa kulipia huduma hiyo ambayo ni tija katika uwajibikaji wao.

MIILI INAYODAIWA NI YA BINADAMU ILIYOKUTWA JANA JIJINI DAR IKIWA NDANI YA MIFUKO IMETUPWA

63a4c18aba35870d3d4177324b654bae
Gari likiwa limebeba mifuko yenye viuongo hivyo, ambapo Jeshi la Polisi wilaya ya Kinondoni limesema kuwa limeanza uchunguzi wa kina baada ya kukakamata viungo mbalimbali vinavyodhaniwa kuwa ni vya binadamu katika mifuko ya plastiki katika machimbo ya kokoto sehemu za Mbweni Mpiji, Magohe, nje kidogo ya jiji la Dar es salaam .http://daresalaam-yetu.blogspot.com
ad41c51ed504857ec7b80c1988a66e05
Sehemu ya mifuko ya plastiki iliyokutwa na viungo hivyo ambavyo inasemekana ni pamoja na mikono, miguu, ngozi na sehemu nyingine za miili

PPF YAFUTURISHA WAFANYAKAZI WAKE

Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, William Erio, akipakua chakula wakati  futari iliyoandaliwa na ofisi yake katika hoteli ya serena leo
Baadhi ya wafanyakazi wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, wakichukua chakula wakati wa futari iliyoandaliwa na Mfuko huo wa Pensheni wa PPF leo.
Afisa Mahusiano wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Bi Janeth Ezekiel akimuonyesha baadhi ya vyakula mjumbe wa bodi ya PPF, Mh Mbaruku Igangula wakati wa futari iliyoandaliwa na mfuko wa Pensheni wa PPF.
 Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, William Erio, akitoa hotuba kwa wafanyakazi wa Mfuko huo baada ya futari iliyoandaliwa na Ofisi yake kwa wafanyakazi wake kwenye hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam, Pembeni ni Msimamizi wa Masoko wa mfuko huo wa Pensheni wa PPF, Bw Alfred Elia
 Baadhi ya wafanyakazi wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, wakishiriki futari iliyoandaliwa na Mfuko huo kwenye hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.Picha Zote na Josephat Lukaza - Lukaza Blog

MAUAJI YA VIKONGWE YASHIKA KASI MLELE- KATAVI

???????????????????????????????
(Picha zote na Kibada Kibada –Mlele Katavi)

Na Kibada Kibada –Mlele Katavi.
Wimbi la mauaji kwa watu wenye umri kuanzia  miaka 60 na kuendelea  Wilayani Mlele Mkoani Katavi linaonekana kushika kasi na kutishia hali ya ulinzi na usalama kama hatua za makusudi hazitachukuliwa.

Hii ni kwa Mujibu wa Taarifa ya Hali ya ulinzi na Usalama Wilayani humo  iliyotolewa na Mkuu wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai wa wilaya hiyo , Zabron Ibeganisa kwenye Mkutano Mkuu wa Baraza la Madiwani uliokuwa ukipokea taarifa ya utekelezaji wa shughuli mbalimbali zilizotekelezwa kwa kipindi cha mwaka  wa 2013/2014.

Mkuu huyo wa upelelezi wa makosa ya jinai alieleza kuwa changamoto zitokanazo na matukio ya mauaji ni kubwa katika wilaya hiyo  na watu wanaolengwa na mauaji hayo ni wale wenye umri kuanzia miaka 60 na kuendelea ambapo kwa sehemu kubwa mauaji hufanyika nyakati za usiku kwa kuwavamia walengwa kwenye makazi yao.

Alisema katika matukio 24 yaliyotokea, watu 24 kwa kipindi cha januari hadi juni mwaka 2014   wameuwawa na waliolengwa hasa ni watu wa umri huo.

Alisema kuwa wauaji hao hutumia silaha zenye makali kama panga,shoka, na sime kuwakata waliowalenga na kisha kutoweka bila kuchukua kitu chochote.

Mauaji haya yanafanana sana na jinsi yanavyotokea katika mikoa ya Shinyanga kwa kuwaua vikongwe kwa imani kwamba ni wachawi.

Aidha akifafanua zaidi alieleza kuwa katika kipindi cha miezi sita iliyopita kuanzia mwezi januari hadi juni 2014 ,  yametokea mauaji 24 na watu 24 wameuwawa  ambapo kati ya mauaji hayo watuhumiwa sita walikamatwa.

Akibainisha hali ya uhalifu katika wilaya hiyo alieleza kuwa matukio mbalimbali ya makosa madogo ya kuwania mali yalikuwa 107 makosa makubwa dhidi ya binadamu kwa mauaji yalikuwa 24, kubaka 23,kulawiti mawili ,makosa madogo dhidi ya Binadamu yalikuwa 194, makosa madogo dhidi ya uvunjwaji wa maadili yalikuwa 108,  ajali zilizosababisha vifo ni mbili,ajali zilizosababisha majeruhi zilikuwa 39, ajali za kawada 17, makosa mengine 844.

Makosa makubwa dhidi ya maadili ya jamii kama kupatikana na bangi yalikuwa manane, kupatikana na pombe ya moshi 8, makosa ya kupatikana na nyara za serikali yalikuwa matatu na kupatikana na silaha moja
Ipo changamoto kutokana na ugumu uliopo wa kuwatambua wauaji ,hata hivyo jeshi la polisi linatoa wito kwa jamii kutoa ushirikiano kwa jeshi hilo na kuwaasa  wana jamii  kuendeleza  ule utaratibu wa  daftari la wakazi kwa kuwaorodhesha wakazi kwenye maeneo kwa kuwa ni muhimu na litasaidia kuwatambau wageni wanaoingia kwenye maeneo na iwapo watakuwa na nia mbaya watabainika.

Monday, July 21, 2014

WANAWAKE WATWANGANA SOKONI HUKU WAKIWA NA SWAUMU-TABORA







Baadhi ya wanawake watatu katika soko la mkulima Tabora mjini wamejikuta wakipeana kipigo kikali mchana kweupe wakati walipokuwa wakifanya biashara za mbogamboga hatua ambao ilisababisha kuharibu sehemu ya bidhaa wanazouza ambapo muda mfupi baadae waliamuliwa ugomvi huo na askari polisi Fakih Abdul aliyekuwa akipita sokoni hapo,hata hivyo chanzo cha ugomvi huo kimetokana na mmoja wa wanawake hao kuwa mbabe kwa wenzake na hivyo kushindwa kumvumilia kutokana na vituko vyake. 

MWIGAMBA ATAKA ACT WATUMIE FURSA CHAGUZI SERIKALI ZA MITAA-KIGOMA

Na Magreth Magosso, Kigoma.

KATIBU mkuu wa chama cha Alliance for change and Transparency(ACT)  taifa  Samson Mwigamba amewataka viongozi wa chama hicho  kuanzia ngazi ya kata na majimbo kuhakiki viongozi  watakaogombea katika uchaguzi ujao 2014 wa serikali za mitaa kwa kuwasimika viongozi wenye upeo wa  mambo na wanaokubalika katika jamii.

Akitoa kauli hiyo  kigoma Ujiji jana katika kikao cha viongozi na wanachama wa chama hicho kutoka jimbo la Kigoma Kaskazini, Kusini na kigoma mjini alisema watumie fursa ya hiyo kuwapa nafasi viongozi wenye sifa na vigezo  kwa lengo la kuboresha mfumo wa utawala.

Alisema ili chama kiweze kupata nyadhifa mbalimbali za uongozi ni lazima kila kiongozi katika jimbo alilopo ahakikishe kunakuwa na uongozi kamili katika vijiji ,ili kunyakua majimbo katika nafasi za udiwani, ubunge na urais.

Hata hivyo aliwataka viongozi na wanachama kuacha siasa za matusi katika majukwaa na badala yake watumie lugha za hekima,busara na kizalendo kwa hoja zenye mashiko ya kuelimisha umma na kufanya kazi kwa uwazi na uwajibikaji.

Mwigamba alisema lengo la chama hicho kurekebisha siasa ya nchi kupitia vyama pinzani kwa kuondoa tofauti zilizopo pamoja na kuondoa utashi wa mwasisi wa chama katika vyama vilivyopo, kuwa na demokrasia ya kweli ambapo vyama vingine havizingatii hilo.

Naye katibu wa mawasiliano na habari Muhamedi Masaga alisema kuanzishwa kwa chama sio kwa lengo la kudhohofisha vyama vingine ni kuwa na chama chenye mshikamano, umoja na kulinda uzalendo wa   n chi ili kushika dola ya nchi katika chaguzi zijazo.

Alisema katika ziara walizozifanya katika mikoa mitatu, mkoa wa kigoma umekuwa kinara  wa wanachama waanzilishi ambao wamefikia 570 ikifuatiwa na Katavi 400 pamoja na Tabora 150 ambapo ni mwanzo unaoleta matumaini katika kukiendeleza chama.

TANZANIA MOVIE TALENTS (TMT) : NANI KUCHOMWA NA JUA LA UTOSI WIKI HII?

ILI KUWANUSURU AU KUMNUSURU MSHIRIKI UMPENDAE AENDELEE KUWEPO NDANI YA NYUMBA YA TMT UNACHOTAKIWA KUFANYA NI KUMPIGIA KURA KWA WINGI SANA.
JINSI YA KUPIGA KURA NI ANDIKA NENO "TMT" ikifuatiwa na namba yake ya ushiriki halafu tuma kwenda 15678. Mfano TMT00 tuma kwenda 15678.