Pages

KAPIPI TV

Monday, April 29, 2013

MKUTANO WA CHADEMA WAIBOMOA CCM TABORA

Na Mwandishi wetu maalum,Tabora

CHAMA cha demokrasia na maendeleo kimedhihirisha kuwa bado ni chaguo la Watanzania walio wengi kwa kuendelea kukubalika kila kona ya nchi licha ya upinzani mkali wanaopata kutoka kwa chama tawala, ambapo kimebainisha kuwa propaganda za CCM dhidi yake hazitafanikiwa na badala yake kitaendelea kusimama na kuwatetea wananchi kwa nguu zake zote.
Hayo yalibainishwa na mwenyekiti wa CHADEMA taifa, Freeman Mbowe wakati
akihutubia mkutano wa hadhara uliohudhuriwa na maelfu ya watu kwenye viwanja vya shule ya msingi Town School katika manispaa ya Tabora.

Mbowe alisema kuwa CCM baada ya kuona hali ni mbaya kwao wameamua kuanzisha propaganda za kukichafua CHADEMA kwa kudai kuwa ni chama cha wakristo, magaidi na ni chama cha wachaga hivyo hakifai kuongoza nchi.

Mbowe alisema hivi sasa CCM wamegundua kuwa mwaka 2015
hawatatoka na hivyo wamekuwa wakiibuka na program kadhaa dhidi ya CHADEMA ili kukidhoofisha lakini kamwe hawatafanikiwa kwani chama hicho kiko imara zaidi.

Aidha, Mbowe alitolea mfano wa vyama vya NCCR-Mageuzi na CUF jinsi vilivyopakaziwa udini na ukabila ili kuvidhoofisha na hatimaye visambaratike na sasa wamehamia
CHADEMA, lakini hawataweza, badala yake wanazidi kutuimarisha zaidi, watashangaa matokeo ya mwaka 2015 kwenye uchaguzi.

Aidha aliongeza kuwa propaganda zao zimekufikia mahali wanatumia
vyombo kadhaa vya ulinzi na uslama na zaidi wao kama CHADEMA wameendelea kujipanga vyema na na kwa kuwahakikishia kuwa watafanikiwa vita hii kwa sababu Mungu yupo pamoja nao.

“Ndugu zangu Watanzania tunahitaji kuungana……sisi pekee hatuwezi, naomba wasomi wote, wakulima, waalimu, wafanyabiashara, wakiwemo usalama wa taifa, polisi , JWTZ na wananchi wote, ili tuweze kuikomboa Tanzania , kwani kama ni kupigika kimaisha tumepigika wote.

Akishangiliwa na umati mkubwa wa watu Mbowe alisema kuwa nchi yetu i hoi kiuchumi
kiasi kwamba inashindwa hata na nchi zilizokuwa nyuma yetu kiuchumi ambapo sasa nchi hizo ziko vizuri wakati Tanzania tukiendelea kusuasua na umasikini wetu japo tunazo raslimali tele.

Mbowe alisema yako mambo ambayo Watanzania wakiyasikia wanaweza wakatokwa

na machozi akitolea mfano wa viongozi waastaafu tisa ambao wametengewa sh.bilioni 12, huku kila mmoja wao akilipwa mshahara mnono kwa mwezi ambapo

ukizigawanya kwa mwaka unapata kiasi cha sh milioni 920 kwa kila mmoja
anazopata.
Alisema haya mambo yanafahamika ndani ya wabunge na ndiyo maana
wanasema iko siku mle bungeni zitapigwa kavukavu, huku akiwapongeza

wabunge wa upinzani na wachache wa CCM waliosimama kidete kuondoa hoja
ya maji.

Alisema endapo wananchi wataendelea kuikumbatia CCM hakuna mabadiliko
yoyote yatakayokuja hata tukiweka manabii wa ukweli kama mfumo ndiyo huu huu, haitasaidia na ana imani siku CCM itakapoondoka madarakani
watasambaratika.

Naye mbunge Zitto Kabwe alisema serikali ya CCM imefikia mahali
imekalia taarifa za utendaji wa CAG ambapo amesema fedha za walipa kodi zinatafunwa
na watumishi wa umma na serikali imegoma taarifa hiyo isijadiliwe
Kabwe aliongeza kuwa hivi sasa kutokana na serikali ya CCM kushindwa
kuongoza dola imekuwa kama Tanzania tumerudi nyuma miaka 20 kule tulikotoka kiuwajibikaji , hali ambayo ni hatari sana.


Katika ziara hiyo mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe alizindua
uhai wa chama hicho kwa kuweka utaratibu wa kufungua matawi kila mtaa
na Zitto kupewa ulezi wa program hiyo ambapo itatengwa ratiba kila
mwishoni mwa wiki kufanya kazi hiyo hadi kieleleweke.
Katika mkutano huo makada wawili wa CCM walitangaza kukihama chama hicho na kujiunga na CHADEMA akiwemo katibu wa UVCCM wilayani Uyui na mjumbe wa mkutano mkuu wa UVCCM mkoani Tabora, Lumola Steven Kahumbi, na kada mwingine ni  Moses Singu, aliyekuwa diwani wa CCM kata ya Itonjanda katika Manispaa ya Tabora mwaka 2000-2005 na mwenyekiti wa UVCCM Tabora mjini  2003-2008 .

Saturday, April 27, 2013

UZINDUZI WA MISS TABORA 2O13 - 2014 WAFANYIKA FRANKMANN HOTEL LEO

 Baadhi ya warimbwende ambao wamepanda jukwaani jioni hii katika ukumbi wa Frankmann Hotel kwa ajili ya ufunguzi wa kuanza kwa mchakato wa mashindano ya Miss Tabora 2013-2014

"HATUPOKEI VIONGOZI WANAOFUKUZWA NA CCM KUINGIA NDANI YA CHAMA CHETU"-CHADEMA

 Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema Bw.Freeman Mbowe akizungumza katika mkutano wa ndani wa chama hicho wakati wa uzinduzi wa kanda ya Magharibi uliofanyika mjini Tabora katika ukumbi wa Chuo cha ualimu TTC.
 Naibu katibu mkuu Chadema Bw.Zitto Kabwe ambaye pia alipata fursa ya kuzungumza katika mkutano huo wa ndani uliowakutanisha wajumbe kutoka mikoa ya Kigoma,Katavi na Tabora.
 Mwenyekiti wa Chadema Bw.Freeman Mbowe akipokelewa na baadhi ya viongozi wa wanachama wa Chadema mikoa ya kanda ya Magharibi.

Na Juma Kapipi-Tabora
Mwenyekiti wa Taifa  wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema,Bw.Freeman Mbowe amesema kamwe Chadema haitakuwa tayari kupokea na kuwapa nafasi  za uongozi viongozi watakaofukuzwa na CCM na kuja kutaka kujiunga na Chadema.

Bw.Mbowe ametoa kauli hiyo leo  hapa mjini Tabora kwenye ukumbi wa  Chuo cha ualimu katika mkutano wa  ndani wakati akizungumza na baadhi ya makamanda wa Chama hicho kanda ya magharibi inayojumuisha mikoa ya  Kigoma,Katavi na Tabora.

Alisema dhamira ya Chadema kwasasa ni kukiimarisha chama hicho na kupata viongozi walioandaliwa badala ya viongozi wanaozuka kama wanavyopatikana kwa vyama vingine vya kisiasa nchini huku akikitolea mfano Chama cha Mapinduzi ambacho idadi kubwa ya viongozi wake wanapatikana kutokana na uwezo wao wa kifedha akimaanisha wamekuwa watoaji wa rushwa hasa unapofikia wakati wa uchaguzi.

Mbowe akifafanua hilo mbele ya wajumbe hao alisema Chadema itahakikisha kiongozi kuanzia ngazi  ya  chini atakuwa na wajibu wa kuwatumikia wananchi na endapo atabainika kutowajibika katika kutekeleza majukumu yake hakitasita kuchukua hatua kwa mujibu wa katiba wa katiba ya chama hicho ikiwa ni pamoja na kumvua madaraka.

Aidha akizungumzia lengo la kuanzishwa kwa kanda hapa nchini,Mbowe alisema sababu kubwa na ya msingi ni kutaka kuwa na uwezo wa kuimarisha utoaji wa huduma bora kwa wananchi jambo ambalo limekuwa ni gumu kwa Serikali inayoongozwa na chama cha mapinduzi.   

Hata hivyo Mwenyekiti huyo ambaye pia  ni kiongozi wa kambi ya upinzani Bungeni alisema lazima kwasasa wabunge wa Chadema watapimwa uwezo wao wa uongozi kutokana na utaratibu huu wa kanda na namna wanavyoweza kutekeleza majukumu yao kwa kusaidiana kati ya mbunge na mbunge ambao watakuwa katika kanda moja licha ya kuwa watakuwa wakitofautiana majimbo.

Kwaupande wake naibu katibu mkuu wa Chadema ngazi Taifa Bw.Zitto Kabwe aliwataka viongozi hao Chadema kanda ya magharibi kuwa tayari kujitolea kwa ajili ya Chama chao wakati huu wa kipindi kigumu alichodai kuwa ni wakati wa kuimarisha chama hicho kwa ngazi ya kanda mpango ambao ni mpya tangu kuanzishwa kwa Chadema miaka 22 iliyopita.

Monday, April 22, 2013

VIONGOZI WA TANZANIA IGENI MFANO HUU!!

Photo: VIONGOZI WA TANZANIA NA AFRIKA KWA UJUMLA..
MAGARI HATUKUZALIWA NAYO..
ANGALIA NA MJIFUNZE TOKA KWA WAZIRI MKUU WA UHOLANZI BWANA MARK MUTE, AKIREJEA NYUMBANI TOKA OFISINI KWA USAFIRI WA BAISKELI, TENA AKIENDESHA MWENYEWE HUKU WALINZI WAKE WAKIMPIGIA SALUTI..
JE VIONGOZI WATANZANIA MNAWEZA KUIGA WALAU KUTEMBELEA BAJAJI??

       {Picha kwa hisani ya BBC}

ANGALIA NA MJIFUNZE TOKA KWA WAZIRI MKUU WA UHOLANZI BW. MARK MUTE, AKIREJEA NYUMBANI TOKA OFISINI KWA USAFIRI WA BAISKELI, TENA AKIENDESHA MWENYEWE HUKU WALINZI WAKE WAKIMPIGIA SALUTI..
JE VIONGOZI WATANZANIA MNAWEZA KUIGA WALAU KUTEMBELEA BAJAJI??



Friday, April 19, 2013

SHULE INAYOJITOSHELEZA KWA MADAWATI MENGI HII HAPA!!!

Baadhi ya wanafunzi wakiwa darasani kwa ajili ya kujipatia elimu ya msingi,Shule katika mtazamo wa kawaida haina kabisa upungufu wa madawati,kwa hatua hii Serikali imekabiliana vema na tatizo la upungufu wa madawati

Tuesday, April 16, 2013

POLISI DUBAI WANAVYOFAIDI MAISHA KWASASA!!!!

Name:  url.jpg
Views: 0
Size:  1.07 MB




Na Mwandishi wetu.

Wakati bado wakazi wa dubai hawajasahau kufunguliwa kwa jengo refu kuliko yote duniani..kiongozi wao ametoa kali nyingine,Al maktoum aligawa new mode lamborghini aventador katika vituo vya polisi ili zitumiwe katika patrol..kabda ya hapo polisi walikuwa wakitumia prado suv na bmw 5 series,

Nchi ya Qatar ndio ilikuwa ya kwanza kwa polisi wake kutumia lamborghini kama magari ya patrol,katika hotuba yake al maktoum alisema ameamua kutoa lamborghini na ferrari kutokana na spidi nzuri ya magari hayo..lamborghini ina spidi ya 217mph.

Polisi wa hapa dubai wanaishi maisha mazuri kuliko fani nyingine nyingi na ndoto ya vijana wengi walio vyuoni na shuleni ukiwauliza wanasema wanataka kuwa polisi,katika pitapita zangu niliwahi kuulizia mshahara wa polisi nikaambiwa kwa kuanzia ni almost 35,000/ dhs ambazo ni sawa na tsh 15ml..pia wana huduma zote..ukienda kwenye vituo vyao utakuta magari na pikipiki nyingi kuliko ata namba ya polisi wenyewe..
 
Wakati mwingine mimi siwalaumu polisi wetu wa bongo maana maisha yao tunayajua....usiongelee vifaa vya kazi bali ata uniform tu ni tatizo,tazama viatu!!nyumba zao!!wakiomba chai huwa sishangai ata kidogo..maana mtu hajui kesho atakula nini!!!!

Sunday, April 14, 2013

UKATILI:-BABA AWANYONGA WATOTO WAKE WATATU MBELE YA MAMA YAO



UKATILI wa kusikitisha! Watoto watatu wa famila moja, wameuawa kikatili kwa kunyongwa huku mama yao akishuhudia. Miili yao pamoja na mama yao akiwa hai, wakatumbukizwa katika kisima cha maji. Baba wa watoto hao, Justine Albert (24) anatuhumiwa kufanya unyama huo.


Kabla ya mauaji hayo, inadaiwa baba huyo alimfunga kamba mkewe na kumziba mdomo kwa kitambaa ili asipige kelele, kisha akaanza kuwanyonga watoto wake wote watatu kwa zamu.


Kamanda wa Polisi Mkoa wa Katavi, Dhahiri Kidavashari, alisema mauaji hayo ya kikatili yalifanyika juzi saa 11:30 alfajiri katika Kijiji cha Majimoto, Bonde la Ziwa Rukwa wilayani Mlele mkoani humo.


Kwa mujibu wa Kamanda Kidavashari, kisa cha kufanya mauaji hayo ni mzozo wa mtuhumiwa na mkewe, Jacqueline Luvika (21), kwamba baadhi ya watoto hao mama huyo kazaa na jirani yao.

Watoto hao ni Frank Justine (6), Elizabeth Justine (4) na kitinda mimba Maria Justine, mwenye umri wa miezi minne.

Baada ya kuwanyonga watoto hao,

inadaiwa baba huyo alibeba miili ya watoto Frank na Eliza, na kwenda kuwatumbukiza kwenye kisima cha jirani yao, Kawaida Jonas.


Kwa mujibu wa madai ya Kamanda Kidavashari, mtuhumiwa baada ya kuwatumbukiza watoto hao kisimani, alimfungua

kamba mkewe na kumtoa kitamba alichomziba mdomoni, kisha akamburuta hadi kwenye kisima hicho na kumtumbukiza.


Kugundulika Baada ya matukio hayo yanayodaiwa kufanyika alfajiri, kulipopambazuka baadhi ya wakazi wa kijiji hicho, waliodamka kwenda katika shughuli zao, waliuona mwili wa mtoto ukiwa umetelekeza kando ya njia na kutambua kuwa ni Maria, ambaye ni kitindamimba katika familia hiyo.


Inadaiwa wakazi hao walisitisha safari yao na kwenda nyumbani kwa mtuhumiwa, kumpatia taarifa hiyo ya kuhuzunisha, huku wakiuliza mama wa mtoto aliko.

Kamanda Kidavashari alidai mtuhumiwa aliwaeleza wakazi hao kuwa mama wa mtoto huyo, alikuwa ametoroka kwenda kusikofahamika na watoto wote.


Majibu hayo ‘rahisi’ kwa mujibu Kamanda Kidavashari, yalisababisha wakazi hao wamtilie shaka mtuhumiwa, wakaamua kutoa taarifa kituo cha Polisi kijijini hapo, ambao walifika ulipo mwili wa mtoto Maria.

Wakati wakiwa katika eneo la tukio, Kamanda Kidavashari alidai walibaini alama za mburuzo ardhini, wakaanza kuifuatilia na zikawafikisha kisimani. Walipofungua mfuniko wa kisima hicho, walishtuka kuona miili wa watu watatu, ikielea kwenye maji kisimani humo.


Askari Polisi kwa kushirikiana na wakazi wa kijiji hicho, waliopoa miili yote, lakini watoto hao wawili tayari walikuwa wamefariki, huku mama yao akiwa amekunywa maji mengi na kupoteza fahamu.


Kutokana na hali hiyo, wakazi hao walipandwa na hasira na kwenda kuvamia nyumba ya mtuhumiwa na kumkamata ili wamchome moto. Hata hivyo, Kidavashari alisema polisi walifanikiwa kufika kwa wakati katika eneo hilo na kumwokoa mtuhumiwa, ambaye kwa sasa bado ameshikiliwa Polisi kwa mahojiano.


Mama wa watoto hao kwa mujibu wa Kamanda Kidavashari, alikimbizwa katika Kituo cha Afya cha Kijijini cha Mamba wilayani humo, ambako amelazwa kwa matibabu, lakini hadi jana bado alikuwa amezirai. Mtuhumiwa anatarajiwa kufikishwa mahakamani mara tu baada ya uchunguzi wa awali wa shauri lake kukamilika.


Chanzo:-JF

NDEGE YA MAREHEMU NYAGA MAWALA YAANGUKA

Click image for larger version. 

Name: DSC00017.JPG 
Views: 0 
Size: 163.3 KB 
ID: 90009Click image for larger version. 

Name: DSC00006.JPG 
Views: 0 
Size: 164.3 KB 
ID: 90003Habari zilizonifikia hivi punde ni kwamba ndege iliyokuwa inamilikiwa na Wakili maarufu Marehemu Nyaga Mawala aliyefariki wiki 3 zilizopita na kuzikwa huko Nairobi imeanguka ikiwa katika hatua za mwisho za kutua (final approach) katika kiwanja cha ndege cha arusha.

Taarifa zinasema kuwa ndege hiyo ilikuwa na rubani pekee anayejulikana kwa jina Babu Sambeke, au maarufu kama Bob Sambeke aliyekuwa anatokea West Kilimanjaro.


Taarifa zaidi zinasema kuwa hali ya rubani huyo si nzuri sana, na amekimbizwa kwenye hospitali ya Mount Meru kwa matibabu.


Maelezo zaidi kuhusu ajali hiyo ni kwamba ndege hiyo ilijaribu kutua baada ya masaa ya kawaida ya kufunga kiwanja(saa 12.30jioni) kupita.











BINTI ANYWESHWA MKOJO WA MAMA YAKE MDOGO - IRINGA



Vituko mjini Iringa haviwezi kuisha kama jamii haitakubali kwa moyo mmoja kupambana na ukatili wa kijinsia. Huyu ni Binti ZAWAD KARIM miaka 16 mkazi wa mshindo nyuma ya banki ya NBC manispaa ya Iringa amepigwa na hatimaye kunyweshwa mkojo na mama yake mdogo aitwaye Ever ubamba.
Tukio lilikuwa hivi:


Zawadi kimsingi anaishi na mama yake mzazi ambaye kwa kipindi hicho dada mtu huyo alikuwa anaumwa. Ever alikuwa nje na marafiki zake ndipo mama yake mdogo huyo akamwiita ndani ya nyumba yao hiyo wanayoishi mtaa wa mshindo.

Baada ya kumwita na kisha mtoto huyo kushindwa kusikia baadaye aliitika na kuingia ndani na ndipo alipo ambiwa avue nguo zote na huyo mama yake mdogo Ever .Baada ya muda mfupi Zawadi alianza kupokea kipigo kikali kutoka kwa mama yake mdogo.

Katika kipigo hicho Zawadi alipigwa pamoja na kunyweshwa mkojo kutoka kwa mama yake mdogo huyo.Zawadi ambaye ni mtoto wa kuzaliwa na Dada yake Ever inadaiwa kipigo hicho kimesababishwa na tuhuma kwamba eti familia hiyo haina mtoto kama yeye zawadi.

Zawadi inadaiwa aliwahi kwenda zanzibar kwa nia ya kufanya kazi na baada ya muda mama yake mzazi ambaye jina lake bado halijafahamika alimpigia simu arudi nyumbani na mara baada ya kurudi ndipo kutokuelewana huko kukajitokeza.

Aidha taarifa za ndani kuhusu tukio hilo zinasema kuwa Mama yake Msichana Zawadi alitupwa akiwa mchanga na kuokotwa na wasamalia wema na hatimaye kulelewa na Bibi yake ambaye hata hivyo amefariki dunia.

Kisa cha yote hayo ni madai ya mtoto zawadi kuomba aoneshwe Baba yake mzazi ili walau aweze kupata pumziko la adha anazo zipata kutoka kwa ushirika wa ndugu zake hao.Zawadi pamoja na majirani wameuambia mtandao huu kuwa vitu vilivyo tumika kumwadhibu vilikuwa ni pamoja na nyaya za simu,mkandaa,na vipande vya chupa katika kumchoma navyo.

Hata hivyo hadi mtandao huu unachapisha taarifa hii watuhumiwa wa tukio hili yaani Mama mzazi pamoja na Mama mdogo wa Zawadi wanashikiliwa na jeshi la polisi kitengo cha dawati la jinsia kwa mahojiano zaidi.


chanzo. ....Jamii Forum

Saturday, April 13, 2013

NJIA MBADALA YA KULEA MTOTO HII HAPA!!!

Wakati mwingine shughuli zinapokuwa zikimzidi mzazi,njia hii hutumika kulea mtoto kwa muda ili mambo mengine pia yaende kwa wakati uliopangwa. 

Friday, April 12, 2013

ALIYEIGIZA FILAMU YA THE PASSION OF CHRIST, MAMBO SI MAZURI HOLLYWOOD

Taarifa hii ni kwa hisani ya Gospel Kitaa...

Haya msomaji wetu wa Gospel Kitaa karibu katika kipengele chetu cha ''KWA TAARIFA YAKO'' ambacho kinakujia kila siku za alhamisi ndani ya GK kikiwa na lengo la kukupatia habari ambayo iliwahi kutukia lakini yawezekana huijui pia yawezekana ilitukia ukawa unaijua lakini GK ikawa imesahau mahali au kuna sehemu haina usahihi utapata fursa ya kusahihisha kwa kuweka comment yako chini kabisa kwenye habari husika. Karibu


Leo katika kipengele chetu ni kwamba mwigizaji wa Hollywood aliyeigiza filamu ya "The Passion of Christ" ambayo ilipokewa kwa hisia tofauti ikiwemo watu kuripotiwa kufariki dunia mara walipoitazama na baadhi ya Wayahudi kuiponda namna walivyoigizwa, bwana Jim Caviezel amesema tangu aigize filamu hiyo mambo yake hayako sawa ndani ya mji wa Hollywood kutokana na kutopewa tenda za kutosha za ugizaji na kwamba hata zinapokuja sehemu anayotakiwa kuigiza haziendani na utaalamu au kiwango chak

Jim ambaye ni Mkristo Mkatoliki pamoja na mkewe, amesema licha ya filamu hiyo kuuza zaidi ya nakala milioni 400 lakini mambo si shwari kwake kwakuwa hapewi tena nafasi ya kuigiza lakini amesema alishapewa onyo na muongozaji wa filamu hiyo Mel Gibson ambaye alimwambia uamuzi wake wa kutaka kuigiza nafasi ya Yesu katika filamu hiyo utamfanya kutoigiza tena katika Hollywood na kufikia tamati ya uigizaji wake,muigizaji huyo alimjibu akisema kila mmoja atabeba msalaba wake, kwasababu anakiamini kile anachotaka kukifanya hivyo kila mmoja abebe msalaba wake lasivyo uzito wake utatudondokea wenyewe tusipoibeba kwahiyo achana na hayo twende tufanye kazi.

Aidha mwigizaji huyo amekiri kuwa alijua fika kwamba kuigiza nafasi ya Yesu katika filamu hiyo ilikuwa ni kuiweka uigizaji wake matatani lakini hakujali hilo na kuamua kuigiza huku muongozaji wake bwana Gibson amewahi kushutumiwa na watu mbalimbali kuhusu mwenendo wake ikiwemo suala la ulevi jambo ambalo Jim amesema watu waache kuhukumu kama wameona Gibson ni mtenda dhambi jambo wanalotakiwa kufanya ni kumuombea ili aache nasio kumuhukumu. Ameongeza kwamba imani yake ndio muongozo wake binafsi na katika utaalamu wake katika uigizaji.

Jim akipata maelezo kutoka kwa Mel Gibson wakati wakirekodi filamu hiyo.
KWA TAARIFA YAKO tangu kutoka kwa filamu hiyo mwaka 2004 hadi leo hii mwigizaji huyo ameigiza katika tamthilia na filamu nyingine ambazo hata hivyo kwa mtazamo wmingine ni kwamba labda angepata kazi nyingi zaidi. Lakini hata hivyo mwigizaji huyo ametoa kazi yake mwenyewe ya sauti hivi karibuni aliyoipa jina "Words of Promise" Ikiwa ni biblia waliyoweka kwa njia ya sauti akiwashirikisha waigizaji wenzake. Hata hivyo licha ya mambo ya uigizaji Hollywood kutokuwa kama alivyotegemea lakini kwasasa anaonekana kukaza msuli zaidi katika utumishi wa kidini kwakuzungumza kwenye makongamano na mambo mengineyo... Kwahiyo hakijaharibika kitu

TFF YAMPIGA FAINI KOCHA WA RHINO KWA VITENDO VYA KISHIRIKINA

KAMATI ya Ligi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imempiga faini ya sh. 400,000 na kumfungia mechi sita Kocha wa Rhino Rangers, Renatus Shija kwa kushiriki vitendo vinavyoashiria imani za ushirikina na kumdhihaki mwamuzi kwenye mechi za Ligi Daraja la Kwanza (FDL).

Adhabu hizo zimetolewa kwa mujibu wa kifungu cha 31(1)(a) na (b) cha Kanuni za FDL ambapo Kocha huyo aliyeipandisha daraja Rhino Rangers kucheza Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) alifanya vitendo hivyo kwenye mechi mbili tofauti.

Mechi hizo ni kati ya Kanembwa JKT na Rhino Rangers iliyochezwa Februari 23 mwaka huu Uwanja wa Lake Tanganyika mjini Kigoma, na ile kati ya Rhino Rangers na Morani iliyochezwa Machi 17 mwaka huu Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi mjini Tabora.

Pia klabu ya Rhino Rangers imepigwa faini ya sh. 200,000 kutokana na Polisi Wanajeshi- MP kuwapiga walinzi milangoni kwenye mechi hiyo dhidi ya Kanembwa JKT ili kupisha washabiki wa timu hiyo waingie bure uwanjani.

Mchezaji wa timu ya Pamba ya Mwanza, Leonard Nahole amepigwa faini ya sh. 200,000 na kufungiwa mechi nne baada ya kumrushia chupa ya maji mwamuzi kwa madai amependelea kwenye mechi dhidi ya Polisi Tabora iliyochezwa Machi 16 mwaka huu.

Nao wachezaji Joseph Mapalala, Yohana Mirobo, Noel Makunja, Mkome Pastory na Rudenzi Kilinga wa Polisi Mara wamepigwa faini ya sh. 200,000 kila mmoja na kufungiwa mechi tatu kwa kufanya vitendo vinavyoshiria ushirikina na kumkimbiza mwamuzi kwenye mechi dhidi ya Morani iliyochezwa Machi 9 mwaka huu. 

Adhabu za wachezaji hao ni kwa mujibu wa kifungu cha 27(1)(g) cha Kanuni za FDL.
Klabu ya Villa Squad imepigwa faini ya sh. 150,000 kwa kuchelewa uwanjani kwenye mechi yake dhidi ya Ashanti United wakati Majimaji imepigwa faini ya sh. 200,000 kutokana na washabiki wake kufanya vurugu kwenye mechi dhidi ya Mbeya City iliyochezwa Uwanja wa Majimaji.

Vilevile Msimamizi wa Uwanja wa Majimaji aliyetambulika kwa jina moja la Mapunda aliwatukana waamuzi kwenye mechi hiyo, na suala lake litafikishwa kwenye Kamati ya Nidhamu ya TFF kwa ajili ya hatua za kinidhamu.

Pia uongozi wa Uwanja wa Mafinga unaotumiwa na timu ya daraja la kwanza ya Kurugenzi umetakiwa kuufanyia marekebisho, vinginevyo hautatumika kwa mechi za FDL msimu ujao.

MKUTANO WA WAANDISHI WA HABARI
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kesho (Aprili 11 mwaka huu) litakuwa na Mkutano na Waandishi wa Habari. Mkutano huo utafanyika saa 5 asubuhi kwenye ofisi za TFF.
Boniface Wambura
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)

Friday, April 5, 2013

WANAFUNZI 1605 WA KIDATO CHA KWANZA URAMBO ‘HAWAJARIPOTI SHULENI’

Na Allan Ntana, Urambo
JUMLA ya wanafunzi 1605 kati ya 4604 waliochaguliwa kujiunga kidato cha kwanza mwaka huu katika wilaya ya Urambo, mkoani Tabora, wameshindwa kuripoti katika shule za sekondari walizopangiwa kwa ajili ya kuanza masomo licha ya kupewa muda wa kutosha kuripoti katika shule hizo.
Hayo yalibainishwa jana na ofisa elimu (taaluma) anayeshughulikia elimu ya sekondari wilayani  Urambo, Grace Nghambi Monge, katika taarifa iliyoandaliwa na idara hiyo ikionyesha idadi halisi ya wanafunzi walioingia kidato cha kwanza mwaka huu, ambapo taarifa hiyo inaonyesha kwamba wanafunzi 1605 sawa na 35%  ya waliotakiwa kuingia sekondari hawajaripoti.
Nghambi alieleza kuwa kati ya wanafunzi hao 1605 wavulana ni 800 na wasichana ni 805, na walioripoti mpaka sasa hivi ni 2989 sawa na 65% tu ambapo wavulana ni 1713 na wasichana ni 1276, aliongeza kuwa idadi hiyo ya watoto walioshindwa kuripoti ni kubwa sana ukilinganisha na mikakati waliyokuwa wamejiwekea.
Nghambi alibainisha sababu zilizochangia wanafunzi hao kushindwa kuripoti shuleni kuwa ni baadhi yao kuolewa mapema, kukosa ada na mahitaji muhimu yanayotakiwa shuleni ikiwemo sare  za shule, madaftari, kalamu na kadharika, na hii inatokana na umaskini wa wazazi walio wengi katika wilaya hii ambao unawafanya kuwa na mwamko mdogo katika suala la elimu.   
Nghambi aliongeza kuwa mambo mengine yaliyochangia kutoripoti ni kitendo cha wazazi kuwatumikisha watoto wao katika shughuli za kilimo hasa tumbaku na wazazi wengine kuwazuia watoto wao kuendelea na masomo kwa kisingizio cha kupoteza nguvu kazi katika kilimo hicho.
Aidha Nghambi aliongeza kuwa watoto wengine hususani wale wanaotoka katika jamii ya wafugaji wameshindwa kuripoti sekondari kwa sababu ya kuhamahama kwa wazazi wao kwa ajili ya kutafuta malisho ya mifugo yao, jambo linalowafanya kuishi umbali mrefu na mahali shule ilipo.
Akizungumzia mikakati ya kupambana na changamoto hizo, Nghambi alisema kwamba halmashauri ya wilaya hiyo imekusudia kuwasaka na kuwafungulia mashtaka wazazi wote waliowazuia watoto wao kujiunga na wenzao sambamba na kuwaelimisha wazazi hao juu ya umuhimu wa kumsomesha mtoto na madhara ya kumkosesha haki hiyo ya msingi.
Aidha, halmashauri hiyo pia imekusudia kuongeza nyumba za waalimu na hosteli za wanafunzi kwa baadhi ya shule ili kupunguza kero ya umbali mrefu uliopo kati ya shule na makazi ya watu.
Naye Coleta Hassan, ambaye ni Ofisa elimu idara ya msingi, akizungumzia mikakati iliyowekwa na halmashauri hiyo katika suala la kuboresha elimu, alisema kuwa wamekusudia kukarabati madarasa, ofisi, nyumba za waalimu, ikiwa ni pamoja na kuhamasisha wazazi  kuchangia chakula ili kuanzisha utaratibu wa kuwapatia chakula cha mchana wanafunzi wote wanapokuwa shuleni.

MWANAFUNZI WA DARASA LA SITA AUAWA AKICHUNGA NG’OMBE-SIKONGE

Na Allan Ntana, Sikonge

MTOTO mwenye umri wa miaka 14, aitwaye Ngwege Ngoroma Paul, mwanafunzi
wa darasa la sita katika shule ya msingi Songambele, mkazi wa kijiji
cha Mtakuja wilayani Sikonge, mkoani Tabora, ameuawa na kisha mwili
wake kuchomwa moto na watu wasiofahamika baada ya kumpora ng`ombe
aliokuwa akichunga.

Akitoa taarifa hiyo kwa waandishi wa habari, diwani wa kata ya
Kiloleli, Bonifasi Mtani, alisema tukio hilo lilitokea wiki iliyopita
tarehe 25 machi, mwaka huu majira ya saa nne asubuhi.

Mtani aliongeza kuwa mtoto huyo alifikwa na mauti baada ya kwenda
kuchunga Ng`ombe 13 mali ya baba yake mzazi Ngoroma Paul Ngwengwe
(36).

Diwani huyo alisema kuwa baada ya mtoto huyo kwenda machungoni na
kukaa huko hadi majira ya saa kumi na mbili za jioni, alikutana na
watu wanne ambao inaonyesha kuwa walimnyonga hadi kufa na kisha
wakamchoma moto na kutokomea na ng`ombe wote kusikojulikana.

Aidha aliongeza kuwa kutokana na msako uliofanyika, baada ya siku nne
kupita, ng`ombe hao walipatikana katika kijiji kilichoko kwenye msitu
wa hifadhi ya Impembapasi, wilayani humo, wakiwa wanaswagwa na watu
wanne ambao hawakutambulika majina yao majira ya saa 11:00 jioni.

“Baadhi ya wananchi waliweka mitego sehemu mbalimbali za barabara na
misitu ndipo walipofanikiwa kuona kundi hilo la ng’ombe na watu wanne
wasiofahamika waliokuwa na mifugo hiyo walitimua mbio kuingia msituni
na kuwaacha ng`ombe hao.” alisema diwani huyo.

Diwani huyo aliongeza kuwa tukio hilo liliripotiwa kituo cha polisi na
upepelezi unaendelea, lakini akatoa wito kwa wazazi na walezi kuacha
tabia ya kuwatumikisha watoto ama wanafunzi katika kazi za kuchunga
mifugo na kazi ngumu za mashambani kwani kazi hizo zinawanyima haki
yao ya kupata elimu.

“Natoa wito kwa wazazi na walezi wote kuacha tabia ya kuwatumia
wanafunzi au watoto wadogo kuchunga mifugo kwani inahatarisha maisha
yao kama hili la kuuawa na kuporwa mifugo au kuliwa na wanyama wakali
na hili ni tukio la pili kwa kipindi cha mwaka huu tu.

MCHUNGAJI AINGIA KWENYE UTAPELI,ASHIRIKIANA NA MAKAHABA

Video hii ni kwa hisani ya Ntv