Wednesday, June 19, 2013
MWANDISHI WA HABARI WA CHANNELTEN CHARLES HILILA AFARIKI DUNIA
Tuesday, June 18, 2013
KADA WA CCM EMMANUEL MWAKASAKA AOKOA MAISHA YA MWANACHAMA WA CHADEMA
![]() |
| Mmoja kati ya waliokuwa viongozi wa Chadema wakikabidhi bendera na kadi zao na kujiunga na CCM. |
![]() |
| Mwenyekiti wa jumuiya ya Umoja wa vijana wa CCM wilaya ya Tabora mjini akionesha bendera ya Chadema iliyorudishwa na viongozi wa Chadema. |
Monday, June 17, 2013
MGAMBO WAWAKAMATA CHANGUDOA SINZA
MACHANGUDOA WANAOFANYA BIASHARA YAO SINZA WAKAMATWA-KUMRADHI KWA UKALI WA PICHA.

Mgambo wa jiji la Dar es Salaam wakiwa katika zoezi la kuwakamata Madada wanaofanya biashara ya kuuza miili yao wajulikanao kama Machangudoa katika eneo la Sinza. Picha mbalimbali zikionyesha namna walivyokuwa wakipakiwa ndani ya Gari tayari kwa kupelekwa katika vyombo vya sheria.
Sunday, June 16, 2013
WAUMINI WA DINI YA KIKRISTO WACHANGIA UJENZI WA MSIKITI WA MUHAAJIRINA TABORA,MWAKASAKA ATOA ZAIDI YA SHILINGI MIL.MOJA
![]() |
| Jengo la Msikiti wa Muhaajirina |
![]() |
| Sheikh wa wilaya ya Tabora Sheikh Ramadhani Rashidi akimpongeza Bw.Emmanuel Mwakasaka baada ya kupokea mchango wake wa shilingi mil.moja |
![]() |
| Baadhi ya kinamama wa Kiislamu wakiwa katika sherehe hizo za Maulid |
JITIHADA ZA MKUU WA MKOA TABORA ZAANZA KUWANUFAISHA VIJANA
Na Mwandishi wetu, Sikonge
JITIHADA
za mkuu wa mkoa wa Tabora Bi. Fatma Mwassa kuhakikisha mkoa huo unakuwa
na kituo cha kisasa cha mafunzo ya ujasiriamali kwa vijana ili
kuboresha maisha yao zimeanza kuzaa matunda baada ya kituo hicho kuanza
kutoa mafunzo mbalimbali kwa vijana kutoka maeneo mbalimbali katika
wilaya ya Sikonge mkoani humo.
Hayo
yalibainishwa jana katika ziara maalumu iliyofanywa na mkuu huyo wa
mkoa akiambatana na watendaji wakuu wa serikali ya mkoa na halmashauri
ya wilaya ya Sikonge walipotembelea kituo hicho na kushiriki kazi mbali
mbali pamoja na vijana walioko katika kambi hiyo.
Katika
ziara hiyo Bi. Mwassa na wasaidizi wake walishuhudia shughuli
mbalimbali zilizofanywa na vijana hao kwa ustadi mkubwa katika kituo
hicho ikiwemo ubunifu wa kutengeneza vitu mbalimbali, utengenezaji na
utundikaji wa mizinga ya nyuki, ujenzi wa mabanda ya kufugia nyuki,
ufyatuaji matofali aina ya ‘interlock’, bustani za mboga mboga katika
mtindo wa ‘green-house’, useremala na mengineyo.
Akiwa
katika kituo hicho ambacho kutokana na umaarufu wake vijana hao
wamekipa jina la ‘TULU GREEN CITY’, Mwassa alisema kuwa mpaka sasa
vijana hao wamefanya mambo makubwa kwa mda mfupi jambo linaloashiria mwanzo mzuri huku akiwapongeza wataalamu wote wanaowasaidia vijana hao.
Aidha,
Mwassa aliongeza kuwa vitu vyote vitakavyotengenezwa na vijana hao
vitakuwa vikiuzwa kwa watu mbalimbali ikiwemo halmashauri zote za mkoa
huo ili kuwanufaisha zaidi vijana hao na kwa kuanzia tayari tumeshapokea
oda toka sehemu mbalimbali za kununua matofali hayo na vifaa vingine
vitakuwa vikiuzwa katika maonesho ya kibiashara.
Aidha , Mwassa alibainisha kuwa Tanzania tumeamua kuingia kwenye mfumo wa matokeo makubwa sasa unaojulikana kwa jina la ‘BIG RESULTS NOW’ lengo
likiwa kuwapa vijana ujuzi katika nyanja mbalimbali ili wawe chachu ya
maendeleo kupitia uzalishaji na utengenezaji wa bidhaa kadhaa wa kadha
sambamba na kuwafundisha vijana wenzao.
Mwassa
alibainisha kuwa nguvu kazi ya vijana hao imeanza kuiva, kazi
zinafanyika kwa uhakika na matumaini juu ya vijana hao ni makubwa, na
kuongeza kuwa kuanzia mwezi Desemba mwaka huu wanatarajia kuanza
ufugaji, kilimo cha mtama, alizeti, viazi vitamu, mbogamboga na mazao
mengine yanayostahimili ukame sambamba na ujenzi wa jengo la utawala na
karakana.
‘Hii
ni fursa muhimu sana kwa vijana wetu wasiipoteze, naomba wana Tabora
waniunge mkono ili ndoto zangu za maendeleo kwa vijana na mkoa kwa
ujumla zitimie na hatimaye tubadilishe uzalishaji katika mkoa huu’,
alisema.
Akizungumza
na waandishi wa habari katika kituo hicho, Mwenyekiti wa halmashauri ya
wilaya ya Sikonge Robert Kamoga, alipongeza wazo la kuanzishwa kituo
hicho katika wilaya hiyo na kubainisha kuwa kero za ajira kwa vijana
sasa zitapungua kwa sababu vijana hao watajiajiri wenyewe na kuajiri
vijana wenzao, hivyo akatoa wito kwa jamii kutembelea kituo hicho ili
kujifunza.
Naye
Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Sikonge Shedrack
Mhagama, alisema kuwa wamedhamiria kuwawezesha vijana kupata ujuzi
utakaowawezesha kutengeneza ajira zao wenyewe ili kujiongezea kipato
kupitia uzalishaji mali, ufugaji wa ng’ombe, mbuzi na kuku, kilimo na
ujenzi, hivyo akawashauri wazazi wawaruhusu vijana wao wajiunge na kituo
hicho.
Vijana
walioko katika kituo hicho Remi Alisemi (22) na Raymond Peter (23)
wakizungumza mbele ya mkuu wa mkoa, walitoa shukrani zao kwa kuanzishwa
kijiji hicho cha mfano na kusema kuwa kimekuwa mkombozi wa maisha yao
kwani awali walikuwa wazururaji tu huku wengine wakiwa wavuta bangi,
vibaka, wabwia unga na hawakuwa na ujuzi wowote ule tofauti na walivyo
sasa.
SERIKALI YAPONGEZA MRADI WA PROSPER
Na Juma kapipi - Kaliua
SERIKALI
wilayani Kaliua imepongeza jitihada za kutokomeza
utumikishwaji watoto wadogo katika mashamba ya tumbaku na kazi za
nyumbani zinazofanywa na mradi wa PROPSER kwa kuwa tatizo hilo limekuwa
kikwazo kikubwa kwa watoto waliowengi mkoani Tabora kutopata fursa ya kwenda shule.
Pongezi
hizo zimetololewa na mkuu wa wilaya ya Kaliua, Savery Maketta, katika
kilele cha maadhimisho ya siku ya kupinga utumikishwaji watoto duniani iliyofanyika juzi
katika kijiji cha Igwisi wilayani hapa ambapo pamoja na mambo mengine alisifu jitihada
mbalimbali zinazoendelea kufanywa na taasisi ya Winrock International
kupitia mradi wake wa PROSPER unaotekelezwa katika mkoa wa Tabora.
Akizungumza
katika sherehe hiyo iliyohudhuria na wanakijiji kutoka vijiji vya
Igwisi, Nsimbo, Mahalaja na Mpandamlowoka, mkuu wa wilaya kupitia
mwakilishi wake, Josephati Brown, ambaye ni Afisa Tarafa wa wilaya ya Kaliua
alisema kuwa mradi wa PROSPER umekuwa mkombozi kwa maelfu ya watoto
mkoani Tabora kwani jitihada zake za kuendelea kupinga kila namna ya
utumikishwaji zimezaa matunda.
Mkuu
huyo wa wilaya alisema kuwa wimbi la watoto wa mitaani limeendelea
kuongezeka kwa kasi kubwa katika maeneo mbalimbali hapa nchini huku
watoto hao wakitumikishwa katika kazi za nyumbani,mifugo na mashambani kwa ujira mdogo, jambo linalohitaji kupingwa vikali na serikali, wazazi, taasisi na wadau wote wa maendeleo.
Aidha
mkuu huyo alisema jitihada zinazofanywa na taasisi hii zimefanikiwa
kurejesha watoto zaidi ya 1500 shuleni baada ya wazazi wao kushindwa ambapo
kati yao 600 wamepewa mahitaji yote ya shule na wanaendelea na masomo
na wengine wapatao 850 wamesajiliwa katika mpango maalumu wa elimu baada ya muda wa masomo na michezo.
Akisoma
taarifa fupi katika maadhimisho hayo Mkurugenzi mtendaji wa Mradi wa
PROSPER, Mary Kibogoya alisema kuwa kwa kipindi cha mwaka 2012 kupitia
mradi huo, watoto
zaidi ya 2194 wavulana wakiwa 1164 na wasichana 1030 wameondolewa katika
utumikishwaji huo uliokuwa ukifanywa na wazazi na walezi ambao hawaoni
faida ya
kuwapeleka watoto wao shule na badala yake huwatumikisha katika mashamba
ya
tumbaku.
Alifafanua
kuwa mradi wa PROSPER ambao unatekelezwa katika vijiji 20 unafadhiliwa
na Umoja wa wadau wa zao la tumbaku Duniani ELCT na kutekelezwa na asasi
tatu za Winrock International,TDFT na TAWLAE ambapo unalenga kuzuia na
kuwatoa watoto 7,800 kwenye utumikishwaji katika mashamba ya tumbaku.
‘Hatari
za kuacha watoto wazagae mitaani ni kubwa, na mradi huu umekuwa na
juhudi nyingi za kuokoa maisha ya watoto hao katika wilaya za Sikonge na
Urambo hapa mkoani Tabora , lakini nasikitika kwamba baadhi ya wazazi waliowengi bado hawajabadilika, naomba ieleweke wazi kwamba suala la kupeleka watoto shule ni la lazima na si ombi’, alisema.
Awali, wakisoma risala yao katika sherehe hiyo, watoto
wa shule za misingi waliiomba serikali, wazazi na taasisi zinginezo
zisaidie kukomesha aina zote za utumikishwa wa watoto hapa nchini kwani
wanapoteza haki yao ya msingi ya kupata elimu na hivyo kuzidi
kutumikishwa au kubakia kuwa ombaomba mitaani.
BOMU LALIPULIWA KWENYE MKUTANO WA CHADEMA ARUSHA,WATU KADHAA WAHOFIWA KUFA.
WAFUASI NA MASHABIKI WA CHADEMA KATIKA MKUTANO WA KUFUNGA KAMPENI ZA UDIWANI SOWETO JIJINI ARUSHA .
WATU wawili wanahofiwa kupoteza maisha na wengine kujeruhiwa kutokana na
mlipuko wa bomu lililolipuka kwenye mkutano wa CHADEMA katika eneo la Soweto,
kata ya Kaloleni jijini Arusha, wakati wa kufunga kamp
eni za uchaguzi wa
madiwani katika maeneo ya jiji hilo.Waliojeruhiwa wamekimbizwa katika hosp
itali ya Seliani na Mount Meru.
Bomu hilo linaelezwa kuwa lilitupwa kwenye mkusanyiko wa watu, lilipuka mwendo wa saa kumi na mbili na robo jioni wakati mkutano huo ulipokuwa umekwisha na shughuli ya kukusanya michango ikiendelea.
Viongozi wa juu wa CHADEMA, Freeman Mbowe na Godbless Lema walikuwepo na wameendelea kuwepo kwenye eneo baada ya mlipuko huo.
Polisi wapo katika eneo hilo wakijitahidi kutuliza ghasia lakini inasemekana upo upinzani mkubwa kutoka kwa wananchi wanaojaribu kuwafukuza, hali iliyowalazimu kupiga mabomu ya machozi na kukamata watu kadhaa wakiwemo viongozi wa CHADEMA.
ILANI: Baadhi ya picha zilizopachikwa hapo huenda zikagusa hisia ya mtizamaji, tafadhali ikiwa huwezi kuvumilia kuona damu usibofye tarakimu zilizopo hapo chini kufungua picha zinazofuatia.
CHANZO http://mwanahabariuswazi.blogspot.com

SEHEMU YA UMATI WA WAFUASI WA CHADEMA KATIKA MKUTANO HUO.
WAHANGA WA TUKIO HILO
DAMU
WANANCHI WAKIANGALIA DAMU ILIYOMWAGIKA KUTOKA KWA WAHANGA HAO.
DAMU SAMBAMBA NA KANDAMBILI
WANANCHI WAKIANGALIA DAMU ILIYOMWAGIKA KUTOKA KWA WAHANGA HAO.
DAMU SAMBAMBA NA KANDAMBILI
GARI LIKIWA LIMEHARIBIWASaturday, June 15, 2013
MUNDE AWAKOMBOA MAKATIBU U.W.T TABORA MJINI,ATOA MSAADA WA BAISKELI ZENYE THAMANI YA SH.MIL.3.75
"MARUFUKU KUWATUMIKISHA WATOTO KWENYE MASHAMBA YA TUMBAKU"-SERIKALI KALIUA
![]() |
| Baadhi ya watoto wa Shule ya msingi Igwisi ilyopo kijiji cha Igwisi wilayani Kaliua mkoani Tabora wakiandamana wakati wa maadhimisho ya siku ya kupinga ajira mbaya kwa watoto. |
![]() |
| Hawa ni miongoni mwa watoto ambao hawajapata fursa ya kupata elimu ya msingi ambao wanaishi katika kijiji cha Igwisi wilayani Kaliua. |
![]() |
| Watoto katika maadhimisho hayo waliimba nyimbo zilizohamasisha jamii kupambana na tatizo la ajira mbaya kwa watoto kwenye mashamba ya tumbaku. |
Friday, June 14, 2013
MSANII WA BONGO FLEVA MKOANI TABORA "MAN FLEY"SASA ANAKUBALIKA KWA KAZI ZAKE
POLISI ZANZIBAR NA VIKOSI VYA SMZ KUFANYA MATEMBEZI YA AMANI
Jeshi la Polisi Zanzibar Jumamosi Juni 15, 2013 litafanya matembezi (Route March) ya pamoja kati yake na Askari wa Vikosi vya SMZ.
Kamishna
wa Polisi Zanzibar CP Mussa Ali Mussa, ameyataja makundi mengine
yatakayoshiriki kwenye matembezi hayo kuwa ni pamoja na , Vikundi vya
Mazoezi ya Viungo pamoja na Vikundi vya Ulinzi Shirikishi.
Amesema
matembezi hayo ambayo yataanza saa 12.00 alfajiri siku hiyo, yataanzia
kwenye Viwanja ya Polisi Ziwani na kuishia nje ya Uwanja wa Michezo wa
Amani saa 3.00 asubuhi.
Kamishna
Mussa amesema matembezi hayo yenye sura ya amani yatapokelewa na Mkuu
wa Mkoa wa Mjini Maghari Unguja Bw. Abdallah Mwinyi Khamisi na washiriki
wake watatoka katika mikoa mitatu ya Unguja.
Katika
taarifa yake kwa vyombo vya Habari, Kamishna Mussa amewaomba wananchi
wa mji wa Zanzibar na Viunga vyake wameombwa kufika nje ya Uwanja wa
Amani kuanzia saa 2.00 asubuhi ili kupata ujumbe utakaotolewa siku hiyo.
Viongozi mbalimbali kutoka Vyombo vya Ulinzi na Usalama Zanzibar watahudhuria katika mapokezi hayo.
Aidha
Waandishi kutoka vyombo mbalimbali wa Habari, wameombwa kuhudhuria ili
kusaidia kutoa elimu kwa umma juu ya yale yote yatakayoelekezwa kwa
manufaa ya Taifa letu.
IMETOLEWA NA INSP. MOHAMMED MHINA, AFISA HABARI MKUU WA JESHI LA POLISI ZANZIBAR.
0715 886488, 0784 886488, 0767 886488
Monday, June 10, 2013
NZEGA BINGWA WA SOKA MASHINDANO YA UMITASHUMTA TABORA
POLISI TABORA WAKAMATA BANGI YENYE THAMANI YA SHILINGI MIL.68
Thursday, June 6, 2013
TUHUMA ZA UBAKAJI ZAMPONZA!!!

Mtu alie
sadikika kumbaka mtoto wa umri wa miaka nane mkazi wa manispaa ya
Iringa, akipokea kichapo toka kwa wananchi wenye hasira huku
akisindikizwa kituo cha Polisi .
Tuesday, June 4, 2013
WATOTO TABORA WAPATA SEHEMU YA BURUDANI "AMOUR CHILDREN PARK IPO KILOLENI JIRANI NA GODOWN LA TFC"
Amour Children Park ipo eneo Kiloleni nyuma ya Godown la TFC,hapa watoto wanapata burudani za aina mbalimbali na huku wakiwa katika mazingira salama kabisa,
Huduma ya burudani zote hizi zinatolewa kila Ijumaa,Jumamosi na Ijumaa lakini pia kwa mtu yeyote anayetaka kusheherekea siku ya kuzaliwa kwake anakaribishwa na atalipia gharama nafuu kabisa.































