Pages

KAPIPI TV

Tuesday, June 4, 2013

MWILI WA MANGWEA UMEWASILI DAR-TANZANIA

Mwili wa Marehemu Albert Mangwea aliyefariki dunia May 28 huko Johannesburg leo umeingia Dar es salaam na kupelekwa moja kwa moja hospitali ya Muhimbili, umati wa watu  umefika uwanja wa ndege kushuhudia na kumpokea Ngwea.




 


 


NAPE AFUNGUA KAMPENI ZA UDIWANI SENGEREMA

13 e75cb
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Taifa, Nape Nnauye akihutubia wakazi wa kata ya Nyampulukano, Sengerema wakati wa ufunguzi wa kampeni za udiwani




"MUNDE AWAPIGA TAFU BODABODA TABORA,WENYEWE WAMTAJA KUWA NI JEMBE"

Mbunge wa Jimbo la Sengerema Bw.William Ngereja akikabidhi pikipiki kwa Mwenyekiti wa Chama cha Waendesha Bodaboda mkoa wa Tabora Bw.Amiri Kipusi zilizotolewa msaada kwa Chama hicho na Mbunge wa Vitimaalum(CCM)Bi.Munde Tambwe ikiwa ni hatua ya kutekeleza ahadi  yake juu ya kuwasaidia vijana wa mkoa wa Tabora katika kuwainua kiuchumi.
Mbunge wa vitimaalum kupitia Chama cha Mapinduzi mkoa wa Tabora Bi.Munde Tambwe akizungumzia dhamira yake katika kuwainua vijana pasipo kubagua itikadi za vyama ambapo Mbunge huyo kwasasa limekuwa kimbilio la vijana wa hapa mjini Tabora  na hasa Waendesha Bodaboda ambao hadi sasa wameendelea kukiri kuwa ni mkombozi wao
Mjumbe wa NEC kutoka mkoa wa Tabora Bw.John Mchele,katikati ni Mbunge wa Jimbo la Sengerema na mjumbe wa NEC Mheshimiwa  William Ngeleja


 Na Mwandishi Wetu,Tabora.
Mbunge wa Jimbo la Sengerema Bw.William Ngeleja amewatahadharisha waendesha Bodaboda nchini kutokubali kutumiwa na wanasiasa kwa manufaa yao binafsi na kwamba kufanya hivyo watajikuta wanapoteza muelekeo wa maisha kutokana na kuyumbishwa kila kukicha.

Bw.Ngeleja aliyasema hayo mwishoni mwa wiki mjini Tabora wakati wa semina ya kukiimarisha Chama cha Mapinduzi kwa wenyeviti,makatibu tawi na kata na baadaye  kukabidhi msaada wa Pikipiki kwa Chama cha Waendesha Bodaboda mkoa wa Tabora iliyotolewa na Mbunge wa vitimaalum(CCM) mkoani humo Bi.Munde Tambwe.
Alisema kwa siku za hivi karibuni imeshuhudiwa makundi ya waendesha Bodaboda hapa nchini wamekuwa wakitumiwa na wanasiasa kwenye misafara ya maandamano mbalimbali ikiwa ni sehemu ya wanasiasa  hao kujiongezea umaarufu na hata wengine kuwatumia kama chanzo cha vurugu kwa kigezo cha kudai haki.

Kupitia Vyama vyao vya  Waendesha Bodaboda Ngeleja aliwaasa kutumia  fursa hiyo kama sehemu ya kujiimarisha kiuchumi badala ya kutumiwa na wanasiasa kama mtaji katika maandamano yao ambayo kwa hatua za mwisho huwa ni vurugu na mapambano na vyombo vinavyolinda usalama wa raia na mali zao.

"Kwa mfano wenzetu wa upinzani wamewaona nyinyi ni Chambo au mtaji wa kutafuta umaarufu na mwisho wa siku wanawatelekezeni mkiwa hamna la kufanya na pia tumeshuhudia wenzenu wengi katika mikoa mbalimbali wanapata matatizo kwa ajili ya hawa wanasiasa wasiolitakia mema taifa,naomba muwaepuke jamani sio watu wazuri hao"alisisitiza Ngereja.

Akizungumzia dhamira ya kutoa  msaada wa pikipiki hiyo yenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni mbili kwa Chama cha Waendesha Bodaboda mkoani Tabora,Mbunge wa vitimaalum mkoani humo Bi.Munde Tambwe alisema ni moja ya ahadi aliyoitoa  baada ya uongozi wa Chama hicho kumuomba awasaidie katika mradi wao waliouanzisha kwa siku za hivi karibuni.

Munde alisema amekuwa bega kwa bega  na uongozi wa Chama hicho cha Waendesha Bodaboda  katika kukabiliana na changamoto mbalimbali zinazowakabili na kwamba mapema aliwashauri kuanzisha mradi wa pikipiki zao wenyewe badala ya kuwa na pikipiki za watu wengine ambao wanawaajiri kwa kupata ujira usiokidhi mahitaji yao.

Aidha Munde alisema katika makabidhiano ya msaada huo kuwa anaiomba Serikali kuwaangalia kwa jicho la huruma vijana hao wanaoendesha Bodaboda kuwafutia kabisa kodi wanayotozwa kwani bado hawajawa na uwezo kutokana na kujitafutia riziki za kila siku ambazo alidai kuwa bado hazijakidhi hata mahitaji ya kawaida ya binadamu.

Kwaupande wake Mwenyekiti wa Chama cha Waendesha Bodaboda mkoani hapa Amir Kipusi alitumia fursa hiyo kutoa shukrani kwa Mbunge huyo huku akiomba wadau wengine kujitokeza kuwasaidia kufanikisha mradi wao ambao bado wanahitaji kupata pikipiki zaidi ya 20.    

Monday, June 3, 2013

ALEX NTONGE ATETA JAMBO NA MISS TABORA 2013 ANNASTAZIA DONALD...!!!

Mhasibu wa Mamlaka ya maji safi na Maji taka mjini Tabora  Tuwasa,  Alex Ntonge  akiwa  pamoja na Redds Miss Tabora 2013 Annastazia Donald.

Sunday, June 2, 2013

"MZEE YUSUPH HOI KWA MASHABIKI TABORA,WALIJIANDAA KWA SHOW YAKE KAMA SIKUKUU"

Mmoja kati ya mashabiki wa muziki wa Taarabu mkoani Tabora aliyefahamika kwa jina moja tu la Tausi ambaye ni mkazi wa Tabora mjini akiwa ukumbi wa Frankman Hotel ambapo Jahazi Modern Taarabu chini ya uongozi wake Mfalme Mzee Yusuph.

Wadau wa mtandao huu nao hawakukosa wakiwa na Apolo Ndali kijana maarufu hapa mkoani Tabora.
 Gwiji la muziki wa taarabu nchini ambaye pia ni mkurugenzi wa bendi Jahazi Modern taarabu maarufu Mzee Yusuph akiwa jukwaani katika ukumbi wa Frankman Tabora mjini akiwafurahia mashabiki wake.
Deo mmoja wa mashabiki wa taarabu akiwa na warembo wawili ambao walihudhuria katika show ya Mzee Yusuph iliyoandaliwa na Kitumbo Security Guard.












Saturday, June 1, 2013

VITUKO MBELE YA WABUNGE KATIKA SHINDANO LA MISS TABORA

Mmoja wa washabiki wa muziki wa kizazi kipya ambaye alivaa vazi lililochangia kudondosha hata heshima yake ambaye alipanda jukwaani kumkumbatia  msanii  maarufu nchini Ommy Dimpoz  wakati alipokuwa akitoa burudani katika mashindano ya Redds Miss Tabora.
Mbunge wa Jimbo la Sengerema  Bw.William Ngereja akiwa na Diwani wa kata ya Kitete manispaa ya Tabora Bw.Daniel Mhina ambaye alikuwa MC katika onesho hilo lililofanyika katika ukumbi wa Frankman Hotel mjini Tabora.
Ommy Dimpoz akitokwa na machozi wakati akitumbuiza jukwaani alipofikia hatua ya kumkumbuka marehemu msanii  maarufu Mangwea.
Ommy Dimpoz alionesha kukubalika zaidi katika onesho hilo
Mbunge Ngereja akiwa na mbunge wa vitimaalum mkoani Tabora wakijaribu kucheza kwa pamoja muziki uliokuwa ukiimbwa na Ommy Dimpoz.






ANNASTAZIA DONALD NDIYE MISS TABORA 2013

Redds Miss Tabora 2013 Annastazia Donald(19)ambaye ni mwanafunzi wa Theofil Kisanji University,kushoto ni mshindi wa pili katika kinyang'anyiro hicho  Sabrina Juma(18) kutoka chuo cha African Utalii na mshindi wa tatu ni Cornecia Cossei(21)kutoka chuo cha Utumishi wa Umma Tabora. 
Warembo baada ya kutangazwa na kupatiwa zawadi zao katika shindano lililofanyika ukumbi wa Frankman Hotel mjini Tabora
Redds Miss Tabora 2013 Annastazia  Donald akiwa  katika vazi la ufukweni ambalo lilionesha kuwa kivutio kikubwa mbali na umahili wake wa kujiamini wakati wa kujibu maswali jambo ambalo lilichangia kumletea ushindi.
Mshindi wa pili katika mashindano hayo Sabrina Juma akiwa katika vazi la jioni
Mbunge wa Jimbo la Sengerma Bw.William Ngereja akikabidhi zawadi kwa mshindi wa kwanza katika mashindano ya uermbo yaliyofanyika
Warembo wakipita jukwaani kila mmoja akionesha uwezo wake mbele umati mkubwa wa wakazi wa Tabora waliofurika kushuhudia shindano hilo.







Friday, May 31, 2013

MWAKASAKA AKUSUDIA KUIBUA VIPAJI VYA VIJANA KATIKA MICHEZO TABORA

Mjumbe wa kamati ya uchumi na Fedha jumuiya ya Wazazi mkoa wa Tabora ambaye pia ni Mwanasheria ya kujitegemea Bw.Emmanuel Mwakasaka akikabidhi vifaa vya michezo Jezi na mipira kwa Jumuiya ya Umoja wa Vijana kata ya Kiloleni manispaa ya Tabora kwa ajili ya kusaidia kuibua vipaji vya vijana katika Soka,Vifaa hivyo vilipokelewa na Meya wa Manispaa ya Tabora Bw.Ghulam Dewij.
Bw.Emmanuel Mwakasaka Kada wa CCM



Wednesday, May 29, 2013

MJENGWA AIBIWA CAMERA NA SIMU,CHUMBA KILIPULIZIWA SUMU YA USINGIZI,WEZI WALISHIRIKIANA NA WALINZI

6 444e6
Ndugu zangu,
Usiku wa kuamkia leo nimepatwa na bahati mbaya ya kuibiwa  kamera  ( Pichani) na simu yangu aina ya Samsung Galaxy S4. Vyote hivyo ni kama jembe na nyundo zangu.
Ilikuwaje? Nilifika Msamvu nikitokea Iringa jana jioni. Baada ya mlo wa usiku nikaingia chumbani kwangu mahali nilipofikia. Nikafanya kazi mpaka saa tano na nusu. Nilitaka nilale mapema kwa kujiandaa kwa safari ya alfajiri ya leo kuwahi Dar kwenye mikutano ya kazi.

Kabla alarm yangu haijalia ya saa kumi na nusu alfajiri nikaamshwa na sauti za watu wanaume wawili wakiongea nje ya dirisha langu. Nilipochungulia nje dirishani nikaelewa  kuwa kuna wizi umetokea.  Watu wale wakaondoka ghafla. Walikuwa ni walinzi. Kisha wakarudi baada ya dakika kumi na kuniambia kuwa " Bwana Mjengwa umeibiwa!" Jambo ambalo nilishalibaini mwenyewe.

Kwamba sikuibiwa kamera na simu tu, na wallet yangu pia iliyokuwa na kiasi cha fedha ndani yake. Bahati nzuri wezi wale walichukua fedha na kuniachia wallet ikiwa na vyote muhimu ikwamo kadi za benki na hata kitambulisho changu cha Mpiga Kura.

Inavyoonekana, wezi wale wali spray chumba changu na kunifanya nilale muda wote wakifanya uhalifu wao. Maana, kawaida yangu hushtuka haraka kwa milio ya ajabu usiku na hata mwanga wa tochi. Na ajabu ya wizi waliofanya chumbani kwangu, walifanya hivyo hivyo kwenye chumba cha ndugu yangu Daniel Londo, mkewe na mtoto wa mwaka mmoja na nusu.  Walitumia mti na kutengeneza kitu kama ndoano. Inaonekana waliweka gundi pia kwenye ndoano ile, kisha wakapenyeza dirishani.

Tunashuku kuwa wezi walishirikiana na walinzi wawili wa usiku mahali hapo nilipofikia. Leo asubuhi, mimi na Daniel Londo tumeripoti tukio hilo Kituo Kikuu Cha Polisi, Morogoro.
Ndugu zangu,

Hapo Morogoro katika pitapita zenu huenda mnaweza kumwona anayeuza mtaani kamera aina  ya Canon D35,  yaweza kuwa kamera ya Mwenyekiti wenu, na simu pia, niliyoitaja hapo juu.

Maggid,
Dar es Salaam
0754 678 252

JE,HUU NI UTUMIKISHWAJI KWA WATOTO?

Mtoto akiwa amebeba mtoto mwenzake hatua ambayo imezoeleka katika jamii na haionekani kama ni sehemu ya utumikishwaji wa watoto eneo la majumbani.