Pages

KAPIPI TV

Tuesday, May 28, 2013

TATHMINI YA MIKUTANO YA CHADEMA NA CCM MKOANI TABORA...!!!!

Naibu katibu mkuu wa CHADEMA  Bw.Zitto Kabwe na Katibu wa CCM mkoa wa Tabora Bw.Idd Ame,Kwa nyakati tofauti na kwa mikutano miwili tofauti eneo la Stendi ya zamani ya mabasi mjini Tabora wakizungumza na kumwaga sera kwa wananchi wa mjini Tabora.    

Monday, May 27, 2013

KATIBU MKUU WA CCM ABDULRAHMAN KINANA AWASILI IRINGA KWA ZIARA YA SIKU SABA

DSC 5858 7c6e5
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana na Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye wakisalimia baadhi ya viongozi, baada ya kuwasili Uwanja wa Ndege wa Iringa asubuhi hii, kwa ajili ya kuanza ziara ya siku saba, mkoani Njombe. Kushoto ni Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Iringa, Joyce Msambatavangu
DSC 5861 961ae
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akiwa na viongozi wa mkoa wa Iringa. Nyuma ni Nape Nape naye akiwa na wenyeji
DSC 5863 20f77
Kinana akisaini kitabu cha wageni Uwanja wa Ndege wa Iringa baada ya kuwasili uwanjani hapo asubuhi hii. Kulia ni Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Iringa, Joyce Msavatavangu
PICHA NA:BASHIR NKOROMO

KIKONGWE ANUSURIKA KUUAWA KWA KUTUHUMIWA MCHAWI -TABORA MWANZAROAD

Bibi kizee  mmoja anayefahamika kwa jina la Binti Ally anayeishi eneo la mpakani Tambukareli amenusurika kuuawa na watu waliodai kuwa bibi huyo ni mchawi. Umati mkubwa ukiwa na dhana potofu juu ya kikongwe huyo ulijikuta unamuandama  kiasi cha kushindwa kujua nini cha kufanya zaidi kusubiri atendewe kile walichokusudia watu hao ambao walionekana kuzomea na hata kumwagia mchanga bibi huyo.   

Kikongwe huyo Binti Ally akiwa yupo chini ya ulinzi mahali ambapo imedaiwa kuwa eti alikwenda kufanya shughuli za kuwanga na hatimaye kushindwa kuondoka baada ya kunaswa na mtego mkali wa zindiko la nyumba hiyo huko eneo la Tambukareli.


OMBAOMBA ANAYEDAI HANA MKONO MMOJA APATA KIPIGO!!!

"Amefanya utapeli kwa muda mrefu,watu wamemgundua na kumuaibisha vibaya"

Omba omba tapeli anayejifanya hana  mikono akikamatwa na  wananchi  baada ya  kukimbia

Hapa  akibanwa  kuonyesha  mikono yake  yote  miwili
Wananchi eneo la Miyomboni  wakiwa  wamembana omba omba  huyu tapeli kuonyesha  mikono yake  yote
'' Huwa  unasema wewe  ni  mlemavu  huna mkono mmoja   hii nini ....nyosha  juu  watu waone utapeli  wako"

Hapa  ni  kipigo  kikiendelea
Tapeli  huyo akitaka  kujinasua  kutoka  mikono ya  wananchi  wenye hasira  kali
Hapa  baada ya  kupata upenyo akivaa nguo  zake
Hapa  akiwa ameachiwa  na kuanza kutimua mbio
Baada ya  kuchezea kichapo  tapeli huyo  sasa anajaribu  kuficha aibu
OMBA OMBA ALIYEIGIZA MLEMAVU WA MIGUU NA MIKONO AKIWA KATIKA KAZI ZAKE ZA KUOMBAOMBA
Huyu ni omba omba anayeigiza kutokuwa na mkono mmoja na mguu akiwa ameka eneo la M.R akisubiri kuomba chochote kutoka kwa wapita njia leo
Hapa akisubiri msaada kutoka kwa wasamaria wema leo
Hapa akitimua mbio kukwepa kamera ya mtandao huu leo


AMA Kweli  mwisho  wa  utapeli ni aibu  kubwa na   wahenga walinena   kuwa ukistaajabu ya mussa utayaona ya filauni leo kwa  wakazi  wa Miyomboni mjini Iringa wamepata  kushuhudia  kituko cha mwaka  baada ya watu  waliochoka  kuvumilia vitendo vya  kitapeli  vinavyofanywa mzee  mmoha ambae amekuwa akiigiza ni mlemavu asiye na mguu mmoja na mkono mmoja.
Tapeli  huyo  mbali ya  kuumbuliwa kwa  kutakiwa  kuonyesha miguu  yake  yote  pamoja na mikono  yake  yote  bado amepata  kuchezea  kichapo  kiasi cha  kunusurika  kuuwawa na wananchi  hao wenye hasira  kali.
Tukio la mzee  huyo  kubainika kama ni tapeli kwa mara  ya kwanza  mtandao huu wa www.francisgodwin.blogspot.com na www.matukiodaima.com ndio ulipata  kufichua siri  hiyo ya omba omba  huyo kuwa si omba omba kutokana na kumnasa akijiweka mfano  wa mlemavu .
Kutokana na kufichuliwa kwa  siri  hiyo ya  kujiigiza  kuwa ni  omba omba mlemavu wananchi wamekuwa  wakimtimua kila kona anayokaa tapeli huyo na  kumtimua  mbio kabla ya leo wananchi hao kuamua  kumkimbiza  kutoka eneo la Hazina  Ndogo  hadi miyomboni na kuanza  kumpa  kichapo hadi alipoamua kuonyesha viungo  vyote kuwa  si mlemavu
Tapeli  huyo mbali ya  kujifanya ni mlemavu  wa  viungo  wakati mwingine huwa anajifanya  ni mtu asiyeongea (bubu) asiye na viungo kama  mikono na miguu ila wakati mwingine akijifanya ni hana mguu  mmoja na  kuwaomba  watu fedha za matibabu .

Hata hivyo baada ya mmoja kati ya wananchi kufika eneo hilo alionyesha kufichua mbinu hiyo chafu ya mzee huyo kujifanya ni mlemavu wakati asubuhi alikutana maeneo akiwa mzima wa afya njema na katika kumhoji zaidi ndipo kamera ya mtandao huu ilipoamua kufanya kazi yake ya kunasa kituko hicho na ndipo mzee huyo alipoanza kuongea kwa sauti vizuri tofauti na alivyokuwa akijifanya kuwa hawezi kuongea kabisa (bubu)

Wakati mabishano yakiendelea eneo hilo ghafla mzee huyo alisimama kwa miguu yake yote miwili pamoja na awali kujifanya ni mlemavu asiye na mguu mmoja ila baada ya watu kutaka apigwe picha ndipo mzee huyo alipoanza kutimua mbio huku ulemavu aliokuwa nao akiusahau hapo  kutokana na  kichapo alichokipata  na kuumizwa  vibaya usoni .
Hata  hivyo  inasemekana  mzee  huyo  amekuwa akiadhibuwa katika maeneo mbali  mbali kutokana na mbinu yake ya  kufuru anayoifanya  kuwa ni mlemavu  wakati si mlemavu na  kuwa ni heri kuomba kama mtu mwenye matatizo ya  kiuchumi kuliko  kuwaigiza  walemavu na  kuwa iwapo atarudia na  kukutwa akifanya  hivyo watamvunja kweli mkono ili kuwa mlemavu walisema  wananchi hao ambao hata hivyo mtandao huu uliwaomba kufanya  hivyo .
Aidha  anadaiwa chanzo cha  kichapo  cha  leo kwa mzee  huyo tapeli ni mmoja kati ya  mpenzi  wake ambae  alikuwa amemsusa na  kuhamia kwa mpenzi mwingine  kuueleza umma kuwa  huyo ni tapeli na yeye ni mpenzi  wake ambae anamtambua kuwa na miguu yote,mikono na si bubu kama anavyoigiza jambo lililopelekea  wananchi kufanya udadisi .
Kabla kufukuzwa na kuchezea  kichapo tapeli huyo alifukuzwa  eneo ambalo alikuwa amekaa barabara eneo la Santona na kutoka kuondoka haraka na mmoja kati ya  vijana  wanaofanya kazi ya kusafisha na kushona  viatu na kupuuza na ndipo mtiti ulipoanza.
Baadhi ya wananchi wameuomba uongozi wa Manispaa ya Iringa kuwabana omba omba hao ambao wamekuwa wakidanganya watu kuwa wao ni walemavu kumbe ni wazima na kutaka kuwepo kwa utaratibu maalum wa watu kuomba misaada.

MAAFISA WA JESHI LA MAGEREZA KUPATIWA MAFUNZO


polis3 e8582
Mkuu wa Jeshi la Magereza nchini Namibia, Kamishna Jenerali Evaristus Shikongo akiijaribu moja ya silaha inayotumika kwa ajili ya kutuliza ghasia wakati wowote inapotokea ndani na nje ya gereza

polis4 7e52b
Askari wa Kikosi Maalum cha Kutuliza Ghasia Magerezani, wakimuonesha mbinu za kupambana na adui pasipo kutumia silaha Mkuu wa Jeshi la Magereza nchini Namibia,

polis5 1e862
Mkuu wa Chuo cha Maafisa Magereza Ukonga, ACP Mbaraka Semwanza akitoa taarifa fupi ya chuo hicho kwa Mkuu wa Jeshi la Magereza nchini Namibia, Kamishna Jenerali Evaristus Shikongo (katikati). Kushoto aliyekaa ni Kamishna wa Sheria na Utawala wa Jeshi la Magereza, Dk Juma Malewa, kulia ni Kamishna wa Fedha na Utawala, Gaston Sanga, anayefuata ni Kamishna wa Rasilimali Watu, Fedha na Utawala wa Jeshi la Magereza nchini Namibia, Clementine Feris. Picha na Felix Mwagara.

polis 1 3a368
Mkuu wa Jeshi la Magereza nchini, Kamishna Jenerali John Minja (kushoto) na Mkuu wa Jeshi la Magereza nchini Namibia, Kamishna Jenerali Evaristus Shikongo wakionyesha taarifa ya makubaliano waliyosaini.

Sunday, May 26, 2013

MKUTANO WA CCM TABORA,CHADEMA WACHEZEA KICHAPO,KEJELI NA ZOMEAZOMEA VYATAWALA!!

Mmoja kati ya watu wanaodaiwa kuwa ni wafuasi wa Chadema ambaye alipigwa na kujeruhiwa na vijana Green Guard wa CCM  wakati wa fujo zilizojitokeza katika mkutano wa hadhara wa CCM uliofanyika kwenye viwanja vya Stend ya zamani mjini Tabora.
Katibu wa CCM mkoa wa Tabora Bw.Idd Ame akizungumza na wananchi  katika mkutano wa hadhara ambapo katibu huyo alikuwa akinadi Sera za CCM.
Mmoja kati ya makada wa CCM wilaya ya Tabora mjini alikuwa akisikiliza kwa makini hotuba za baadhi ya viongozi wa CCM  katika mkutano huo wa hadhara.

Meya wa manispaa ya Tabora Bw.Ghulam Dewij akielezea utekelezaji wa Ilani ya CCM na mafanikio yaliyopatikana tangu serikali ya awamu ya nne kuingia madarakani ambapo kwa manispaa ya Tabora utekelezaji huo umeleta mabadiliko makubwa.
Mjumbe wa NEC Bw.John Mchele naye alipata fursa ya kuzungumza na wananchi  ambapo aliwataka kutokihama CCM kutokana na baadhi ya kauli za wanasiasa wanao kikejeli na kukichafua chama hicho.
 Askari Polisi Tabora akiwaangalia kwa hasira baadhi ya vijana wanaodaiwa kuwa ni Green Guard ambao walikuwa wakimsurubu kijana huyo anayedaiwa kuwa ni wa Chadema katika vurugu zilizojitokeza baada ya zomeazomea wakati wa mkutano wa CCM Tabora mjini.

Na (mwandishi wetu).

VIONGOZI WA CCM TABORA WAZOMEWA MKUTANONI.

CHAMA mapinduzi (CCM),na baadhi ya viongozi wake,kwa mara ya kwanza
jana walijikuta kwenye wakati mgumu baada ya kukumbwa na
“zomeazomea”toka kwa wanannchi kwenye mkutano wa hadhara.

Tukio la kuzomewa kwa viongozi wa wilaya na mkoa lilijiri kwenye
mkutano wa hadhara ambao ulifanyika kwenye viwanja vya stendi ya
mabasi zamani ambapo CCM ilikuwa ikifanya mkutano wake.

Mkutano huo wa hadhara unafanyika baada ya CHADEMA ikiongozwa na naibu
katibu mkuu wake,Zitto Kabwe, kufanya mkutano eneo hilo na kutamka
wabunge wa CCM Tabora hawawatendei haki wapigakura wao na  CHADEMA
watapiga kambi Tabora kuwatetea wananchi kwenye haki zao.

Hatua hiyo iliwafanya CCM nao kuja na badhi ya viongozi akiwemo mbunge
wa jimbo la Tabora mjini Aden Rage kujibu mapigo.

Dalili za zomeazomea zilianza mapema kwani baadhi ya wananchi walianza
vicheko na kejeli kwa viongozi wa CCM huku wengine wakisikika na
kutamka hawataki majigambo,matusi bali wanataka barabara za lami
Tabora-Nzega,Tabora-Urambo na ile ya Itigi-Tabora na wengine 'Peoples
Power'.

Wakati katibu wa CCM mkoa wa Tabora Idd Ame,akimwaga sera
zake,wananchi wachache waliokusanyika kwenye mkutano huo walianza
kuzomea kila katibu huyo alipokuwa akikikejeli chama demokrasia na
maendeleo,(CHADEMA).

“Ndugu zangu wananchi hebu angalieni mnavyodanganywa hivi hawa CHADEMA
wanajigamba kujenga barabara wakati wao siyo watoaji wa fedha na
kwamba fedha zinatolewa na serikali ya CCM siyo hao CHADEMA wanafiki
waongo.”alisema Ame.

Wakati katibu huyo akiendelea ma sera zake huku akikejeli na kufikia
kutamka mtu anakuja anaacha jimbo lake Kigoma kuja Tabora kuwafundisha
siasa huu ni ‘upumbavu’ kabisa.

Baada ya katibu huyo kutamka maneno hayo ndipo wananchi walipoanza
kuzomea kwa nguvu na kudai wanantaka sera za siyo matuzi huku wengine
wakisema nyie CCM waongo siku zote mlikuwa wapi kuja kufanya mikutano
hadi CHADEMA waje.

Aidha zomea zomea ilizidi ambapo katibu wa CCM mkoa wa
Tabora,alipoendelea kutamka kuwa endeleeni na huo ujinga wenu hapa
tutaumizana hapa hali ambayo ilizidisha hasira za wananchi huku nao
wakijibu mapigo kuwa sawa tu tuumizane tumechoka na ahadi zenu za
uongo.

“Hapa tuko kamili endeleeni kuzomea tu……..tutaumizana kwelikweli hapa
msifikiri hatuwezi na tutawashitaki viongozi wa CHADEMA Tabora kwa
kutufanyia fujo kwenye mkutano wetu.”

Wakati katibu huyo akitamka hayo,mjumbe wa NEC John Mchele alitoka
jukwaani na kwenda kumnong`oneza katibu huyo aachane na hayo amwage
sera tu.

Baada ya hapo ndipo ilizuka fujo kubwa huku Green Gurd wa CCM
wakitembeza mkong`oto kwa baadhi ya wananchi ambao walikuwa
wakionyesha ishara ya vema ikiwa ni alama ya CHADEMA na tafrani hiyo
ilidumu kwa dakika 20 hivi na ndipo askari polisi walipoongezwa na
mkutano kuendelea.

Baada ya vurugu kutulia huku wananchi wengine wakiondoka, mbunge
Tabora mjini Aden Rage alipopanda jukwaani ni kuongea na
wananchi,ambapo alitoa sh milioni 68 kwa kata kumi za manispaa hiyo,na
kila kata ilikabidhiwa hundi yake kwa ajili ya miradi  ikiwemo ujenzi
wa vyoo,umaliziaji nyumba za walimu na madarasa.

Aidha mbunge huyo alikabidhi chama wanedesha bodaboda pikipiki mbili
na kutoa ahadi ya kuendelea kuchangia misaada.

Katika hatua nyingine mwenyekiti wa CCM tabora mjini Moshi Abdurahaman
Nkonkota alilaani jeshi la polisi kuwa hawataki kulinda mikutano ya
CCM hadi wanafanyiwa vurugu.

Tutalipeleka lalamiko hili ngazi za juu kuwa askari polisi huwa
hawafiki kwenye mikutano ya CCM.” Alisema.






WAREMBO WA SHINDANO LA REDD'S MISS TABORA WATEMBELEA TABORA REST HOUSE

Warembo wakipozi na mdhamini wa shindano la REDD'S MISS TABORA 2013 Bw.Humud Nassor mmiliki wa TABORA REST HOUSE na kampuni la SUPER SONIC.

Nyumba hizi waweza pumzika na familia, rafiki, pia kwa wale wafanyao kazi za maofisi. Panakidhi haja zote za nyumbani. NYUMBA ZINAPATIKANA UZUNGUNI
Warembo wakiwasili eneo hilo la nyumba za kupumzikia (TABORA REST HOUSE)
Warembo wakizunguka kuangalia mahadhi mbalimbali ya makazi hayo waliyokaribishwa kwaajili ya kuweka kambi
wakipozi ndani ya nyumba hizo za kupumzikia
wakikatiza toka upande mmoja wa nyumba hadi mwingine
kuna mazingira mazuri ya kuvutia ambapo ukiwepo huwezi boreka
warembo wakibembea
moja ya kivutio maji yakitiririka kwa namna ya pekee
Mmiliki wa Tabora Rest House Bw. Humud Nassor
---------------------------------------------------------------------------------
SHINDANO LIKIWA LIMEBAKIZA SIKU CHACHE KUFANYIKA HAPO TAREHE 31 MAY, 2013 KATIKA UKUMBI WA FRANKMAN PALACE.
HUKU MSANII MKALI OMMY DIMPOZI KWA POZI KUSHUSHA MVUA YA BURUDANI NA KIPAZA SAUTI KUBURUZWA VILIVYO NA MKALI WA VICHEKESHO BAMBO a.k.a KISHTOBE.
---------------------------------------------------------------------------------
JIPATIE TIKETI YAKO MAPEMA KATIKA MAENEO YAFUATAYO
BAGENZI NETWORK TRADERS 0754-416724, ALOY SON 0715-103054, GAMALO PUB, CLUB ROYAL ENTERTAINMENTS 0754-666620/ 0713666624
---------------------------------------------------------------------------------
(PICHA: www.aloyson.com)

Wednesday, May 22, 2013

VURUGU MTWARA:-JENGO LA CCM LACHOMWA!!!

Mtwara4 803f9
Habari zilizotufikia muda huu zinaripoti kwamba hali sio nzuri huko Mtwara, kwa ufupi hali ni tete na hakuna amani, mabomu ya machozi yanarindima muda huu na huduma zote za kijamii zimefunngwa hakuna usafiri, masoko, maduka na bar zote zimefungwa, daladala, Taxi na Bodaboda hazifanyi kazi. Kwa ujumla kinachoendelea ni mapambano makali kati ya Jeshi la polisi na wananchi wenye hasira wanaopinga vikali kuendelea kwa mchakato wa gesi ilihali nchi ikiwa haina sera inayosimamia nishati hiyo.
Kufuatia Kambi ya Upinzani kuukataa mpango wa serikali wa ujenzi wa bomba la gesi kutoka Mtwara Mpaka Dar es salaam ilihali Waziri wa Nishati akisoma hotuba yake.



 
 Jengo la Ofisi ya CCM saba saba limechomwa moto. 
Lodge/Hotel (Shengena) inayoaminika kwamba ndiyo waliyofikia Askari wa Jeshi la Polisi (FFU) kutoka mikoa ya jirani kwaajili ya operation inayoendelea imechomwa moto.
 
Nyumba kadhaa  za watumishi  wa Serikali  zimechomwa  maeneo ya Shangani. (habari haijathibitishwa rasmi)  
Ni magari ya FFU ndio yaliyopo barabarani nayo yanapata wakati mgumu kupita kwasababu ya mawe na magogo makubwa yaliyowekwa na Wananchi. 
 Hili linaendelea wakati bajeti ya nishati na madini ikiendelea kujadiliwa muda huu Bungeni. 
 

HALI NI TETE MTWARA LEO TANGU ASUBUHI,SAKATA LA GESI...!!!!


leo ntwara tangu asubuhi kila huduma imefungwa watu wapo kimakundi makundi wanasikiliza bunge hasa bajeti ya wizara ya nishati na madini,ni magari ya ffu tu ndio yapo barabarani nayo hupata wakati mgumu kupita kwasababu ya mawe na magogo yaliyowekwa na vijana,baadhi ya watu kadhaa wamechukuliwa na askari eti kwakuwa walipita jirani na gari yao,askari wengi waliokuja si wa hapa ntwara wengi wametoka Masasi na Lindi.


Kauli mbiu ya huku kwa sasa - "gesi haitoki hata kwa bomba la peni"


MORE UPDATES
MATAIRI KILA KONA YA MJI YAMECHOMWA BARABARANI POLISI NA ZIMA MOTO NDIO WANAKAZI YA KUZIMA NA KUFUKUZA RAIA

TAYARI NYUMBA KADHAA ZA WATUMISHI WA SERIKARI ZIMETIWA KIBERITI MAENEO YA SHANGANI
Click image for larger version. 

Name: NTWARA2.JPG 
Views: 0 
Size: 105.8 KB 
ID: 94735

MMOJA WA WAMILIKI WA JAMII FORUMS APATA AJALI MBAYA NZEGA



Nina habari za kusikitisha za Maxence Melo kapata ajali mbaya ya gari katika barabara kuu iendayo Mwanza kilometa chache kutoka Nzega mjini.

Msemaji wa Jamiiforums, Mike Mushi, amesema hali ya Maxence kwa sasa si mbaya sana na walikimbizwa katika hospitali ya Rufani ya Bugando kwa matibabu na uchunguzi zaidi.


Pamoja na Maxence alikuwapo ndugu yake mmoja ambaye naye amejeruhiwa vibaya na wote wamekimbizwa Bugando. Maxence na mwenzake walikua njiani kuelekea mkoani Kagera na gari walilokua wakisafiria (pichani) limeharibika vibaya.


Mwenyezi Mungu awawekee wepesi wa kupata nafuu haraka.