Waziri wa mashauri ya kigeni nchini
Ufaransa Laurent Fabius ameelezea hisia za baadhi ya nchi za ulaya dhidi
ya suala la uhamiji kuwa sawa na sakata.
Amezilaumu nchi za ulaya hasusan zilizo mashariki mwa ulaya kwa kukataa kuwaruhusu wahamiaji.
Bwana
Fabius aliiilaumu Hungary kwq kujenga ua ulio na lengo la kuzuia watu
wanaowasili wakipitia nchini Serbia akisema kuwa hatua hiyo haiendi sawa
na maadili ya ulaya.
Ufaransa imejiunga na Uingezea pamoja na na
Ujerumani katika kuitisha mkutano wa dharura na mawaziri wa nchi za
ulaya kutafuta njia za kukabiliana idadi ya wahamiaji inayozidi
kuongezeka. Chanzo:-BBC Swahili
No comments:
Post a Comment