Pages

KAPIPI TV

Friday, July 31, 2015

MSIMU MPYA WA KANDANDA NDANI YA DSTV KUTIMUA VUMBI WIKI IJAYO

IMG_0388
Meneja Uhusiano wa Kampuni ya Multichoice Tanzania, Barbara Kambogi, akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa utambulisho wa msimu mpya wa kandanda kwa wateja wa DStv jana jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Afisa Masoko wa Multichoice Tanzania, Furaha Samalu na kulia ni Meneja Mwendeshaji wa Multichoice Tanzania, Ronald Baraka Shelukindo.(Picha zote na Zainul Mzige wa modewjiblog).
IMG_0397
Meneja Uendeshaji wa Multichoice Tanzania, Ronald Baraka Shelukindo, akijibu maswali ya waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusiana na huduma za DStv. Kushoto ni Meneja Uhusiano wa Kampuni ya Multichoice Tanzania, Barbara Kambogi.
IMG_0422
Afisa Masoko wa Multichoice Tanzania, Furaha Samalu, akielezea huduma za kuunganishwa kwa wateja wapya wa DStv, ambapo ving'amuzi pamoja na dishi vinapatikana kwa gharama nafuu kabisa ya Sh.99,000/- kwa mawakala wote wa DStv nchini.
IMG_0443
Meneja Uhusiano wa Kampuni ya Multichoice Tanzania, Barbara Kambogi (wa pili kushoto) akikabidhi zawadi ya begi kwa mwandishi wa habari, Joseph Michael baada ya kuchezesha droo kwa waandishi waliohudhuria mkutano huo. Wanaoshuhudia kushoto ni Afisa Masoko wa Multichoice Tanzania, Furaha Samalu na kulia ni Meneja Uendeshaji wa Multichoice Tanzania, Ronald Baraka Shelukindo.
IMG_0454
Furaha Samalu na Barbara Kambogi wakikabidhi zawadi ya begi Super Sport kwa mpiga picha wa ITV, Abdallah Kaniki aliyeibuka mshindi katika droo iliyochezeshwa na Multichoice Tanzania wakati wa mkutano na waandishi wa habari. Kulia Meneja Uendeshaji wa Multichoice Tanzania, Ronald Baraka Shelukindo.
IMG_0458
Meneja Uhusiano wa Kampuni ya Multichoice Tanzania, Barbara Kambogi akikabidhi zawadi ya T-shirts kwa mwandishi wa habari wa gazeti la Mwananchi, Imani Makongoro.
IMG_0419
Baadhi ya waandishi wa habari waliohudhuria mkutano huo uliofanyika jijini Dar es Salaam.
Na Andrew Chale, modewjiblog
Msimu mpya wa Soka 2015/16, unatarajia kuanza rasmi Jumapili ijayo kwa kushuhudia ligi mbalimbali Duniani zikichezwa na kurushwa moja kwa moja kupitia SuperSport ambayo imejipanga kukuletea burudani kabambe kwa mashabiki wa soka barani Afrika.
Meneja uendeshaji wa Multichoice Tanzania , Ronald Baraka Shelukindo mapema jana akizungumza na vyombo vya habari amebainisha kuwa, Wateja wa DStv wakae tayari msimu huu kwenye Ulimwengu wa Mabingwa ambapo timu mbalimbali zimejiimalisha katika kuakikisha zinatwaa ubingwa.
“Ligi ya mwaka zitakuwa za kasi na kuvutia kwa kila timu. Barcelona wanajiandaa kutawala dunia kwa mara nyingine, huku Manchester United wanahitaji kurudisha kiti chao cha Ubingwa Uingereza. Jose Mourinho analenga kuhakikisha Chelsea inabaki juu, wakati huo huo , Hispania inajiandaa kuhakikisha wanashinda kwa mara ya tatu kombe la Euro 2016.” Ameeleza Baraka Shelukindo.
Ameogeza kuwa, Watazamaji wa SuperSport watakuwa na nafasi ya kipekee kushuhudia mechi kwenye ubora wa HD, ikiwa ni pamoja na michuano ya Ligi Kuu ya Uingereza (EPL) , Ligi ya Hispania (La Liga) , Ligi ya Mabingwa wa Ulaya(UEFA) na Ligi ndogo ya Ulaya ( Europa) ,mechi za FIFA za kirafiki za kimataifa na Klabu Bingwa ya Dunia , Kombe la Ujerumani , Kombe la Mfalme Hispania (Copa Del Rey) , Kombe la FA na zaidi.
Kwa upande wake, Meneja Uhusiano wa Multichoice Tanzania, Barbara Kambogi anaeleza kuwa, Katika msimu huu , Ulimwengu wa Mabingwa itakuwa ikionyesha mechi zaidi ya 900 za kimataifa. Wateja wa DStv Compact Plus wataweza kufurahia baadhi ya mechi zaidi ya 450 ‘live’, huku Wateja wa DStv Premium watazawadiwa mechi zote ‘Live’ zitakazorushwa katika chaneli zote za SuperSport .
“Kuanzia msimu huu na kuendelea, vituko vyote vya Ligi Kuu ya Uingereza vitakuwa vikiletwa kwenu kupitia SuperSport 5 ( SS5 ) inayopatikana kwenye kifurushi cha Premium. SS5 sasa itakuwa ni nyumba ya soka la Afrika kwa ligi kuu ya Uingereza huku ikijumuisha mechi 3 ‘Live’ kila Jumamosi na Jumapili. Kuambatana na mechi kutakuwa na vipindi maalum vya soka kama PLTV Kick Off, Match Day Live, Fan Zone, Saturday/Sunday Review, Football Today, Classic Matches, Netbusters na Mech za Wiki” Amebainisha Barbara Kambogi.
Moto wa La Liga utawashwa ndani ya SuperSport 3 ( SS3 ). Chaneli hii itakuwa inakuletea mechi hadi tatu za ligi ya Hispania ‘ Live’ kwa siku ya Jumamosi na Jumapili . Wateja wa DStv Premium na Compact Plus watapata nafasi ya kuangalia mechi za michuano ya Kombe la mashindano Uingereza ndani ya SS3 sambamba na mechi za Jumamosi mchana za Ligi kuu ya Uingereza , mbadala wa mechi inayorushwa ndani ya SS5, pamoja na Ratiba zote za Jumatatu usiku na vipindi vya mahojiano vya studio.
Pamoja na Mechi za ‘Live’ ndani ya SS3 , itakuwa inakuonyesha vipindi muhimu vya shoo za magazeti , yanayojiri ndani ya La Liga, pamoja na vipindi maalum vya ligi za soka . Makombe yote ya mpira wa miguu, Mabingwa wa Ulaya na Ligi ya Europa, Kombe la FA , Kombe la Mfalme Hispania (Copa Del Rey), Kombe la Ujerumani , Euro 2016 na mechi za kirafiki za kimataifa zitaendelea kutapatikana kwenye SS3 .
Kwa habari zaidi za michezo na ratiba za mechi kwenye SS5 na SS3, tafadhali tembelea www.supersport.com

No comments: