Kamishna
Jenerali wa Jeshi la Magereza, John Casmir Minja(kushoto) akifunua
kitambaa kwenye jiwe la msingi kuashilia uzinduzi rasmi wa “Duty Free
Shop” ya Magereza Mkoani Tabora leo februari 28, 2015. Kamishna Jenerali
Minja amesema kuwa Huduma hiyo itatolewa pia kwa Maafisa na Askari wa
Vyombo vyote vya Ulinzi na Usalama Mkoani Tabora(kulia) ni Mwenyekiti
Mtendaji wa Kampuni ya Transit Military Shop, Bw. Sadrudin Virji. Kamishna
Jenerali wa Jeshi la Magereza, John Casmir Minja(kushoto) akiangalia
bidhaa mbalimbali zinazouzwa katika “Duty Free Shop” ya Magereza Mkoani
Tabora mara tu baada ya uzinduzi rasmi leo februari 28, 2015 katika
Viwanja vya Gereza Kuu Uyui, Tabora. Muonekano
wa Jengo la “Duty Free Shop” ya Magereza Mkoani Tabora ambalo
limzunduliwa leo februari 28, 2015 na Kamishna Jenerali wa Jeshi la
Magereza, John Casmir Minja(hayupo pichani)
Baadhi
ya Maafisa na Askari wa Jeshi la Magereza wakifuatilia kwa makini
hotuba ya Mgeni rasmi katika uzinduzi rasmi wa “Duty Free Shop” ya
Magereza Mkoani Tabora. Kikundi
cha ngoma za asili ambacho kinaundwa na Maafisa wa Jeshi la Magereza
Mkoani Tabora kikitumbuiza katika hafla ya “Duty Free Shop” ya Magereza
Mkoani Tabora. Kamishna
Jenerali wa Jeshi la Magereza, John Casmir Minja(katikati) akiwa katika
picha ya pamoja na Kamati ya Ulinzi na Usalama Mkoa wa Tabora(wa pili
kulia) ni RPC Tabora, ACP Suzani Kaganda(wa kwanza kulia) ni Mkuu wa
Magereza Mkoani Shinyanga, SACP. Anet Laurent(wa pili kushoto) ni Mkuu
wa Magereza Mkoani Tabora, SACP. Rajab Mbilo(wa tatu kushoto) ni
Mwenyekiti Mtendaji wa Kampuni ya Transit Military Shop, Bw. Sadrudin
Virji(wa tatu kulia) ni Katibu Tawala Mkoani Tabora, Bi. Kudra
Mwinyimvua(Picha zote na Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza).
No comments:
Post a Comment