Mwandishi wa habari wa Channelten mkoa wa Morogoro Jimmy Mengele akiwasilisha majadiliano ya vikundi katika mafunzo hayo ya siku tatu mkoani Singida. |
Allan Mtana mwandishi wa habari wa gazeti la Majira mkoani Tabora akiwasilisha moja kati ya hoja walizojadiliana katika mafunzo hayo |
Na, Mwandishi wetu, Singida
WAANDISHI wa habari hapa nchini wametakiwa kuandika kwa wingi habari za matukio yanayohusu ukatili wa kijinsia unaofanyiwa wanawake ikiwemo udhalilishaji..
Wito huo umetolewa jana na Mwandishi wa habari wa siku nyibgi Jamila Rahma katika mafunzo ya siku tatu kwa waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali kutoka mikoa ya Tabora, Morogoro, Dodoma na Singida inayofanyikakatika hotel ya Aqua mjini hapa.
Mafunzo hayo yaliyoandaliwa na TAMWA katika mada yake Jamila alisema uandishi wa habari za kijinsia ni muhimu sana katika jamii kwa sababu unachangia kumwinua mwanamke mahali popote alipo kwa namna moja ama nyingine hivyo akawataka wanahabari hao kuandika habari zinazoibua
mambo mbalimbali yanayohusu wanawake pasipo kuwadhalilisha.
“ Jinsia inasaidia sana kuleta maendeleo katika jamii hivyo tambueni kwamba wanawake wengi wanahitaji kuinuliwa kwani wengi wao wanakabiliwa na changamoto nyingi za ukatili wa kijinsia hivyo kwa kutumia kalamu zenu mnaweza kuwainua au kuwadidimiza kabisa’, alisema.
Jamiola amewaasa wanahabari kuandika habari nyingi zenye kuibua matendo ya unyanyasaji wanayofanyiwa wanawake na kuzipeleke kwenye shindano la uandishi wa habari za kijamii.
Aliongeza kuwa kufanya hivyo watakuwa waameisaidia TAMWA na watajisikia vizuri sana mtakapopata tuzo kwa kuandika habari zinazofichua vitendo vya namna hiyo, aliongeza.
Katika semina hiyo washiriki wote waliweza kuainisha matukio mbalimbali ya ukatili wa kijinsia yanayojiri katika mikoa yao ambapo kwa ujumla walibainisha baadhi ya vitendo hivyo kuwa ni pamoja na ubakaji na ulawiti kwa watoto wadogo, ubakaji mabinti na wanawake, ukeketaji, vipigo kwa wanandoa, mimba na ndoa za utotoni na kuendekeza mazoea ya mfumo dume katika maamuzi.
Walitaja matukio mengine kuwa ni wanawake walio wengi kuendelea kunyimwa haki za kumiliki mali ikiwemo kukosa haki za kurithi mali za waume zao punde wenzi wao hao wanapofariki dunia, ukatili wa majumbani na manyanyaso katika migogoro ya wakulima na wafugaji.
Akitoa mfano wa unyanyasaji wanaofanyiwa wanawake, Mwezeshaji wa mafunzo hayo Deodatus Balile alisema katika takwimu za umiliki wa ardhi kati ya hati 817,000 zilizotolewa hapa nchini wanawake wanaomiliki hati za ardhi ni chini ya 3000.
No comments:
Post a Comment