Na Magreth Magosso,Kigoma
ZAIDI ya shilingi milioni 100 zinatumika katika mradi wa
kupima ramani ya wilaya mpya ya Buhigwe iliopo Mkoa wa Kigoma kwa ajili ya kuvutia
uwekezaji wa ndani na nje ya wilaya hiyo kwa nia ya kuboresha huduma za
wananchi husika.
Mbali na hilo wilaya imeingia mkataba na shirika la nyumba
taifa(NHC) kigoma kujenga nyumba 30 ambapo nyumba 20 zitanunuliwa na
halmashauri ya buhigwe na nyingine 10 zitakuwa ruksa kwa wananchi kununua .
Akielezea hilo juzi wilayani
humo Mkurugenzi wa halmashauri husika Simon
Mumbee alisema hivi sasa wana adha kubwa ya ukosefu wa huduma ya nishati,huduma
za kibenki ,maduka ya madawa muhimu,nyumba za kulala wageni ,migahawa na
miundombinu ya barabara ,ambapo wanatumia darasa moja la shule ya msingi
buhigwe kama sehemu ya ofisi.
Alisema kwa mujibu wa meneja wa mradi wa umeme vijijini
buhigwe ni moja ya wilaya itakayoondokana na adha ya nishati hiyo ifikapo Machi
,mwaka huu hali itakayosaidia wawekezaji wa ndani na nje ya hapo kuwekeza
huduma za kijamii .
Hivyo halmashauri hutumia gharama kubwa kwenda kasulu
kuchapa makaratasi mbnayohitajika kiofisi ambapo mradi wa upimaji na nishati ukiimarika wanaomba serikali husika
iwajibike kupitia bajeti ili wajenge majengo ya
ofisi.
Naye Mkuu wa wilaya ya Buhigwe Julius Gishuli alisema
changamoto kubwa ilikuwa katika upimaji wa viwanja ambapo imechangia halmashauri ishindwe
kuboresha huduma za msingi kwa wananchi hali inayochangia wilaya kukosa mvuto kwa
uwekezaji.
No comments:
Post a Comment