Picha kutoka maktaba ya KAPIPIJhabari.COM |
Na Magreth Magosso,Kigoma
KITUO cha kulea Watoto yatima na waliotelekezwa Cha Matyazo kilichopo halmashauri ya Wilaya ya
Kigoma Mkoa wa Kigoma,kimeitaka Wizara ya Ustawi wa Jamii iwajibike kujibu barua
za maombi za wananchi wanaohitaji kuwaasili watoto waliovuka umri wa miaka miwili.
Kauli hiyo inatokana na
Changamoto kubwa ya wanafamilia waliowapeleka watoto wachanga yatima na waliotelekezwa
kuwasusa pindi watimizapo umri huo kwa mujibu wa lengo la ulezi wa kituo
hicho,ambacho kwa sasa kinakabiliwa na ukosefu wa fedha za kuhimilili matunzo
ya vichanga hivyo.
Mbali na hilo wameziomba Asasi za
kiraia na Serikali hususani tasisi za kifedha na za mawasiliano ziwajibike kutoa sehemu za faida za mapato
katika uchangiaji wa kulea watoto wachanga ambao wanamahitaji maalum ambapo
inahitajika fedha nyingi ili kuwahudumia katika tiba,elimu, chakula,mavazi na
motisha kwa wahudumu wa ulezi huo
.
Akifafanua hilo juzi kituoni hapo
kwenye upokeaji wa msaada wa vifaa mbalimbali kutoka kwa Dawati la Jinsia
kigoma Mlezi wa kituo hicho Mary Leonard akiri kituo kuzidiwa uwezo wa watoto
,kutokana na familia kuiachia kituo watoto waliovuka sifa ya kuwepo hapo.
“kituo kina uwezo wa kulea watoto
60 lakini tuna watoto 65 mmoja ana miaka tisa naishi naye nyumbani walezi namba
za simu hazipatikani hawataki kuwachukua,wizara husika ilipelekewa barua sita
za maombi ya kuwachukua watoto sita wakaishi nao majibu hakuna tukiuliza kwa
kamishna mkuu anadai amesaini barua lakini kituoni hazijafika” alidai Leonard.
Kwa upande wa Mkaguzi wa kituo
hicho Sister Andrea Lehmann alisema awali wahisani kutoka Nchi ya Jerumani iliendesha kituo hicho,ambapo
mwaka juzi waliondoka na kuiachia halmashauri husika,ambapo mahitaji makubwa ni
tiba kwa watoto wenye mabukizi ya Virusi vya ukimwi,mdomo wa sungura na mwenye
kichwa kikubwa na fedha za usafiri wa
kuwafikisha CCBRT kupata tiba kwa wakati.
Lehmann alisema kitendo cha kuwatembelea
watoto ni faraja kwa walezi wa kitu hicho na kuwatia moyo kwa huduma wanayotoa naina
h waa kusihi mradi wa kutoa huduma ya midomo ya sungura na vichwa vikubwa
wakiangalie kwa jicho la tatu kituo hicho ambacho kina watoto watoto hao wasio
na hatia ya kuwa katika hali hiyo,wakatihuohuo watoto hutumia kilo 100 za
maziwa kwa mwezi.
Akikabidhi msaada huo Kamanda wa Polisi wa hapa Jafari Mohamed alisema watoto wana mahitaji makubwa kutokana
na uhalisia wa ulezi wa watoto wachanga ambao wanahitaji maziwa,sabuni mahususi
za kuogeshewa na kufua,mafuta,madawa kutokana na watoto waliowengi kusumbuliwa
na vipele na vidonda.
Naye
Kaimu mwenyekiti wa dawati
hilo Consolata Kashumba alisema wametumia kiasi cha shilingi milioni 1.5
kununua blanketi 16,kilo 6 ya sabuni ya unga,mafuta ya kupaka robo
katoni,nguo ,nepi dazeni mbili,mchele ,ngano na mharagwe kiasi tuvifaa
ambavyo vitawasaidia kwa siku chache na kuomba kila idara ya
serikali na binafsi za hapo zisaidie watoto yatima
katika vituo husika.
No comments:
Post a Comment