Bibi Joha Maganga mmoja kati ya watu walioathirika na janga la mvua kubwa ya upepo mkali iliyonyesha katika kijiji cha Tumbi manispaa ya Tabora akiangalia namna ambavyo wanachama wa CCM Tabora mjini walivyojitokeza kuchangia nguvu zao kusaidia watu waliokumbwa na janga hilo lililotokea usiku wa mkesha wa krismas.Wanachama hawa wa CCM wakiongozwa na Mwenyekiti wa chama hicho wilaya ya Tabora mjini Bw.Moshi Nkonkota waliamua kumjengea bibi huyo nyumba ya kudumu kwa kutumia tofali za kuchoma na saruji. |
No comments:
Post a Comment