Pages

KAPIPI TV

Tuesday, October 21, 2014

GAIDI MKUU WA ULIPUAJI WA MABOMU AUAWA NA POLISI ARUSHA


1
Kamanda wa Polisi mkoa wa Arusha, Liberatus Sabas.
Kiongozi wa  matukio ya ulipuaji wa mabomu na umwagiaji tindikali viongozi wa dini aliyejulikana kwa jina la Yahaya Hassani Omary ameuwawa na jeshi la polisi wakati alivyokuwa akijaribu kukimbia.

Akithitisha kutokea kwa tukio hilo kamanda wa polisi mkoani Arusha, Liberatus Sabas, alisema kuwa tukio hilo limetokea  October 19 majira ya saa tano na nusu  katika barabara ya Babati mkoani Arusha wakati alipokuwa akijaribu kuwakimbia polisi.

Alisema kuwa mtuhumiwa huyo wa ugaidi alishikiliwa wiki mbili zilizopita  huko mkoani Morogoro  mara baada ya kutafutwa kwa muda mrefu na hapo jana alikuwa akipelekwa wilayani Kondoa mkoani Dodoma  kwa ajili ya kwenda kuonyesha sehemu ambazo alikuwa ameficha mabomu mengine.

“mtuhumiwa huyu alikuwa anasakwa kwa muda mrefu bila mafanikio kwani alikuwa hakai sehemu moja ila jeshi la polisi huko mkoani Morogoro lilimkamata wiki mbili zilizopita na baada ya kufanyia mahojiano alisema ameficha mabomu mengine huko Kondoa na juzi alikuwa akipelekwa kuonyesha ndipo alipotumia triki zake ambazo amefundishwa za ugaidi kwa kupiga judo na kutaka kuwakimbia askari ndio akapigwa risasi mbili”,  alisema Sabas.

Kamanda Sabas, alitoa wito kwa wananchi kuendelea kuwafichua waovu  ili kuwaza kuteketeza matukio ya uhalifu. Habari kwa hisani ya woindeshizza blog

No comments: