Pages

KAPIPI TV

Monday, August 25, 2014

NRA YAMTAKA ZITTO ATIMIZE AHADI KABLA YA KUHAMIA CHAMA CHA ACT-KIGOMA

Na Magreth  Magosso,Kigoma

KATIBU  wa Itikadi na Uenezi Taifa  Chama cha NRA Hamis Kiswaga  amemtaka Mbunge wa Jimbo la Kigoma Kaskazini  Zitto Kabwe arudi Jimboni kwake kutimiza ahadi  wa ujenzi wa kipande cha  Barabara cha Mwandiga Sokoni , gari aina ya Fuso  na Boti la abiria katika maeneo husika kabla ya kuhamia Chama cha ACT.
 
Pia amewaonya wananchi waache kuchgua kiongozi kwa  mapenzi na utashi binafsi wa mtu na kuwasihi wachague  kwa kupima uwajibikaji wenye kukidhi matakwa ya wengi katika jimbo husika.

Kiswaga alisema  katika vijiji kumi na moja  vya jimbo lake vinakabiliwa na adha ya maji safi  katika kijiji cha mwandiga,bitale kiganza,kibingo,kihinga,simbo,msimba,kizenga  na nyamhoza ambapo jamii  inachangia maji ya mto mngonya na ng`ombe.
 
Ahadi hizo alitoa katika kampeni ya mwaka 2010  na kusisitizia katika kikao cha kamati ya kijiji  cha mwandiga kilichoketi  machi, 27,2013 mbele ya mwenyekiti Yususph Kikunku ,baada ya  kubaini baadhi ya raia hawako pamoja nae hali inayodaiwa  kulihama jimbo 2015 pasipo  kutimiza ahadi hizo.
 
Kiswaga alisema  mbunge huyo anatumia watu wachache kufanikisha  kuficha mapungufu ya uwajibikaji katika adha za jamii  na hatimaye kutimkia chama cha ACT katika sura ya kudai anaonewa chama kilichompa jina(Chadema) .
 
Hivyo wanasiasa waliowengi watachomwa moto,kutokana na kutafunwa na  dhambi ya kuuza utu wa  wananachi waliowaamini  kwa kushindwa  kuwaletea maendeleo  na kuondoa adha zinazowakabili  ili kuboresha ustawi wa jamii husika.
 
  Wabunge wa hapa hutumia majukwaa ya siasa kudai wanasomesha wanafunzi ili hali ni uongo ukweli fedha hizo ni za serikali kuu kupitia mifuko ya majimbo kwa lengo la kusaidia familia zenye sintofahamu ya maisha.
 
Mwenyekiti wa kitongoji cha mwandiga  sokoni Ramadhan  Omari alipohojiwa ahadi za mbunge huyo kijijini hapo  alisema ni kweli na kudai mtendaji wa kijiji cha mwandiga alipima  barabara hiyo kwa kutumia koleo na alipata mita 124 na walimpa mrejesho .
 
Alitoa kiasi cha shilingi 20,000 kwa mtendaji ikiwa ni kazi ya upimaji wa barabara ya njia panda mwandiga  sokoni na alipoambiwa ili kumaliza adha ya maji jimboni anatakiwa atoe milioni Nnne ili kununua vipuliza  maji vitano.
 
Alisema jibu la Zitto alisema atafanya hivyo,endapo mto mngonya utakauka na anadhihilisha kulihama jimbo hilo 2015 kutokana na matendo yake kwa  kushukuru  wakazi wa kigoma mjini  baadala  ya wakazi wa jimboni kwake  ambao walimwezesha .
 
Mtandao huu metonywa kuwa,sababu kuu ya mbunge huyo  kuweka mazingira ya kutetea  jimbo la kigoma mjini  2015 ni  wananchi  kuchoshwa na ukaidi wa kushindwa  kutatua  adha na hatma ya ahadi sanjari na kutowezesha vijana na ajira za ujasiliamali katika miradi yenye tija kwao.

No comments: