Pages

KAPIPI TV

Thursday, February 13, 2014

WANANCHI MANISPAA YA TABORA WAITAKA BIMA YA AFYA KUSIMAMIA KWA MAKINI TIKA

Afisa Udhibiti Ubora Dr.Wilbroad Rawile akitoa ufafanuzi kuhusu mpango wa Tiba kwa kadi maarufu TIKA kwa wakazi wa mtaa wa Liwale manispaa ya Tabora wakati wa kukusanya maoni ya wananchi kuhusu mpango huo ambao unampa fursa mwananchi atakaye jiunga na kuchangia atapata huduma za afya kwa urahisi ambapo atachangia kiasi cha shilingi elfu kumi kwa kila mwaka.
Afisa kutoka CHF makao makuu jijini Dar-es-salaam Bw.Salvatory Okumu akielezea manufaa ya mpango wa TIKA unaosimamiwa na Mfuko wa taifa wa Bima ya Afya nchini NHIF ambapo kwa manispaa ya Tabora utaanza utekelezaji wake hivi karibuni.
Mwanasheria wa halmashauri ya manispaa ya Tabora akisoma mbele ya wananchi kuhusu utaratibu wa kisheria utakaosimamia mpango wa TIKA na kuwaletea wananchi manufaa wakati watakapokuwa wakihitaji huduma za Afya kwa kutumia kadi ambapo mpango huo unatajwa kuwa utasaidia kuwaondolea usumbufu wananchi watakaojiunga.
Baadhi ya Wananchi wakisikiliza kwa makini katika mkutano wa ukusanyaji wa maoni kuhusu TIKA.
Bi.Rehema Migira mmoja kati ya wakazi wa mtaa wa Liwali mjini Tabora akiuliza na kutaka ufafanuzi kuhusu mpango wa TIKA ambao unataraji kuanza kutekelezwa mjini Tabora ambapo kila mwananchi atachangia kiasi cha shilingi elfu kumi kwa mwaka ili aweze kupata huduma za matibabu pasipo usumbufu,Rehema pia alishauri mpango huo kusimamiwa kwa makini ili uwe suluhisho la malalamiko dhidi ya wahudumu wa afya yanayojitokeza katika hospitali mbalimbali.
Mkutano wa ukusanyaji maoni ya TIKA
Mmoja kati ya wananchi kata ya Gongoni Aakisikiliza kwa makini ujumbe kutoka kwa maafisa wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya A fya wakati wa ukusanyaji maoni kuhusu mpango wa TIKA ambapo wananchi walionekana kuukubali zaidi.






No comments: