Pages

KAPIPI TV

Wednesday, February 12, 2014

NHIF WAANZA KUKUSANYA MAONI KWA WANANCHI KUHUSU MPANGO WA TIBA KWA KADI MANISPAA YA TABORA

Meneja wa Bima ya Afya kanda Bw.Emmanuel Adina akizungumza na wananchi wa kata ya Kabila wakati wa ukusanyaji wa maoni kwa wananchi kuhusu mpango wa tiba kwa kadi maarufu TIKA ambao utampatia fursa mwananchi katika kila Kaya kupata huduma ya matibabu hospitalini mpango ambao kila mwananchi atachangia kiasi cha shilingi elfu kumi kwa mwaka.

Baadhi ya wakazi wa vijiji mbalimbali vya Kata ya Ndevelwa wakisikiliza kwa makini maelezo kuhusu mpango wa TIKA yaliyokuwa yakitolewa na maafisa kutoka Bima ya Afya NHIF wakati wa kukusanya maoni juu ya mpango huo wa hiari.
Diwani wa Kata ya Ndevelwa Bw.Suleiman Maganga akizungumza na wakazi wa Ndevelwa ambapo aliwataka kuukubali mpango wa Tiba kwa Kadi ambapo kila mwananchi atakayechangia atafaidia kupata huduma za matibabu kwa mwaka mzima akichangia kiasi cha shilingi elfu kumi.
Wananchi wa kata ya Mtendeni eneo la Kidatu nao walipata fursa ya kusikiliza na kutoa maoni yao kuhusu mpango huo wa kupata huduma ya matibabu kwa kadi ambapo wameonesha mwamko wa kuukubali mpango huo huku wakiushauri mfuko wa Taifa wa Bima ya A fya kuusimamia kwa makini ili uweze kuleta tija kwa wananchi ambao kwa kipindi kirefu waliowengi wamekuwa wakilalamikia huduma za afya zinazotolewa katika hospitali,zahanati na vituo vya afya vinavyomilikiwa na Serikali.
Wakazi wa kata ya Malolo wake kwa waume,vijana kwa wazee wakiwasikiliza maafisa wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya  NHIF ambao walipita kukusanya maoni ya wananchi kuhusu mpango wa tiba kwa kadi. 
Wakazi wa kata ya Isevya eneo la Bombamzinga wakimsikiliza Afisa udhibiti ubora Dr.Wilbroad Rawile wakati wa ukusanyaji wa maoni kuhusu mpango wa tiba kwa kadi manispaa ya Tabora ambapo wananchi waliowengi wameonesha kuukubali mpango huo ambao kila mwananchi atachangia kwa hiari shilingi elfu kumi kwa mwaka ili aweze kupata matibabu pindi anapougua.







No comments: